MAHOJIANO: KUPITIA YOU TUBE.
JINSI NABII HEBRON ALIVYOITIKISA KUZIMU
NA KUMTOA ALIYE KUWA NGAZI YA TATU TOKA UFALME WA SHETANI
SEHEMU YA
3.
MTUME: Karibu tena katika kipindi cha Nabii Hebron wa Kanisa la YESU NI BWANA NA MOKOZI WA MATAIFA
YOTE. Somo ambalo nitakuwa nikifundisha
kupitia ushuhuda ambapo nipo na Isaya, ambaye alikuwa anaitwa Maxwel sasa
anaitwa Isaya, ambaye yeye alikuwa huko kuzimu na YESU alinituma nikamtoa huko,
kwa hiyo nitaendelea leo katika mahojiano mengine tena. Ili kwamba, kuweza
kuwafungua macho mjue ni nini mbinu za shetani na mjue mnatoka huko na mpone
msidanganyike . Ameen!!
Mtume: Karibu sana Isaya..
Isaya: Asante , BWANA YESU asifiwe, kwa jina naitwa Isaya ambaye jina langu la mwanzo
nilikuwa nikiitwa Maxwel ni mtoto ambaye nabii alikuwa akinielezea, lakini kwa
sasa hivi sipo tena katika huo ufalme, nimeokoka nampenda Bwana YESU na
ninamtukuza na ninacho penda kuwaambia labda, ndugu zangu msije mkakubali tena
kukaa kwa shetani kwa sababu mmeshaujua ukweli tayari. Mnatakiwa kumfuata
MUNGU, kwa sababu shetani ni mbaya .
Na baada ya MUNGU kuona shetani
anatamba ovyo ndio mana akaamua kumshusha Mtume na Nabii Hebon hapa duniani.
Kwa hiyo watu wasimuone mtume
na nabii Hebron kuwa ni mtu wa kawaida, na tusiwe na mazoea na MUNGU,
tunatakiwa kumuogopa MUNGU,kumuogopa Bwana YESU na pia madhabahu yake takatifu
tuiheshimu na pia Mtume na Nabii tusimzoee tusimuone ni mtu wa kawaida.
Mtume: Sasa si watu wataniogopa aisee…. Hehehe!!
Mtume: BWANA YESU asifiwe,
aaa.. sasa siku ya leo kuna maswali ambayo nitakuuliza machache, japo mimi
nayajua lakini ili tuweze kuwafundisha, ndugu watazamaji na watoto wa MUNGU,
ambao wanamjua MUNGU ili warejee kwa YESU na watoto wa MUNGU kile alichonituma YESU ni kuhakikisha kwamba
wewe unamjua MUNGU , unaokoka nunakuwa mtoto wake ili kwamba usipelekwe huko
ambako shetani alishaandaa kwa ajili yako wewe
na mwingine lakini ipo neema ya MUNGU leo , utaenda kutubu na kuambatana na mimi tuungane na YESU , utapona. Bwana YESU
asifiwe,
Sasa siku ya leo Isaya
nitakuuliza japo mimi nina yajua lakini ni kwa faida ya kuwafundisha wana wa
MUNGU amen!!..
Mtume; eee, Katika ofisi yako uliyokuwa nayo,wakati
napambana na joka kuu na lusifa , nikitafuta yale mafail, nilielelezwa wewe
ndie mwenye mafail ya dunia nzima.. sasa
embu tuelezee kwa ufupi hayo mafail yalikuwa na nini na nini ulikuwa navyo..
Isaya: BWANA YESU
asifiwe..
Mtume: Ameen..
Isaya: Yale mafail yalkuwa na baadhi ya majina ya
wale waliokwenda kinyume na amri za MUNGU
na kila rekodi ya kila kitu kilichofanyika hapa duniani katika yale
mafail, na pia kazi yake ilikuwa ni kurekodi kazi za kule kuzimu, kitu ambacho
labda kimefanyika siku nzima na kwa masaa.
Na yale mafaili yalikuwa yana
majina ya watu wa shetani ambao wapo
katika kile kitabu cha shetani ambacho ni kitabu cha hukumu na yalikuwa yana
mambo mengi sana.
Mtume: Lakini hayo mafaili kwa nini shetani na joka
kuu walikukabidhi wewe hayo mafaili
yote ya serekali ya kuzimu ambayo kwa
sasa hivi nimekwisha yachukua?
Isaya : Ni kwa sababu
walifikiri kwamba mimi sitatoka tena kule..
Mtume : MMh..
Isaya: Na walishaniamini kwamba ile kazi naiweza
lakini mpango wa MUNGU nimetoka pasipo
wao wenyewe kuamini nimetokaje.
Mtume: kwa hiyo kuzimu yote ..siri zote hata joka
kuu hana tena, yote yapo katika yale mafaili niliyayachukua na BWANA YESU ?
Isaya: Ndiyo.
Mtume: Sasa watoto wa MUNGU nawaambia ni wakati wa
kufunguka! Hapa ipo neema ambayo mwana wa MUNGU anawaelezea….
Bwana YESU asifiwe!!.
Aaa nakuuliza ni namna gani
hizi roho saba za shetani zinafanya kazi? Maana hata katika kanisa kuna roho
saba lakini shetani nae anaroho saba na manabii wa uongo nao pia wana roho
saba.. karibu..
Isaya; Hizo roho saba !
Mtume: Mmh..
Isaya: Kazi yake inakuwa ni kuwapa manabii pamoja
na mapepo na kundi la majini kule kuzimu kwa
hiyo hapa ni kuwapulizia pumzi ya
uhai kila siku. Nabii anapokuwa kule kuzimu
anapokuwa anapata zile roho saba, kufa kwake inakuwa .. labda
inakuwa tabu kidogo..
Mtume: Inakuwa hafi?
Isaya: Ndiyo.
Mtume; Lakini toka nimebomoa nini tena kinaendelea…?
Isaya : Hakuna kitu.
Mtume: Bwana YESU asifiwe..
Isaya: Amen.
Mtume: Mmh.. tutaendelea katika jambo lingine..
Mtume: Je, unamfahamu mtu aliyepo kuzimu anayeitwa
amakuta?
Isaya: Ndiyo.
Mtume: Embu tuelezee..
Isaya: Amakuta ni jinni kule
kuzimu, na amakuta kitu anachokifanya ni kupotosha watu yeye pamoja na
kusimamia majini mengine, huko kuzimu na ndote zote za uongo duniani na pia
anakitengo chake kingine ambacho alipewa
na shetani ambaye ni lusifa, lakini kile kitengo nilikuwa sikifahamu kwa sababu
sihusiki nacho.
Mtume: kwa hiyo kwenye upande
wa injili kama vile unavyoambiwa sadaka
zisiandikwe majina, yeye anawaambia waandike majina, batiza ubatizo wa maji
mengi ametoa ubatizo wa maji mengi ambayo ni kinyume na MUNGU . Bwana YESU
asifiwe.
Mtume; Nitakuuliza, je, unaweza
elezea njia ya shetani ambayo anaipitia peke yake?
Isaya; ndiyo
Mtume: Embu elezea..
Isaya: njia ambayo shetani anapita ni njia ambayo ipo
katika kijiji chake kinachoitwa freemason village, ile njia ipo ardhi ya
million mia nane daraja la nne. Ndiyo njia ambayo yeye anaitumia kwenda katika
kazi zake na kufanya mambo yake yeye mwenyewe.
Mtume. Na unaweza kuelezea njia
ya joka kuu anayo pitia yeye peke yake?
Isaya : Njia joka kuu anayoipitia ni ardhi ya mwisho kabisa ya milioni mia nane na pia yeye
anapita daraja la sita.
Mtume. Daraja la sita?
Isaya: ndiyo.
Mtume: Na unaweza kuelezea na njia yako ilikuwa ya
wapi?
Isaya: Bwana YESU asifiwe.
Mtume: Amen.
Isaya: Njia yangu ilikuwa ardhi ya million mia nane
daraja la tano.
Mtume: Je, unafahamu mti wenye
matawi saba uliopo kwa joka kuu na kazi zake ambazo ndizo roho saba?
Isaya; Ndio
Mtume. Na ukoje huo mti embu
elezea sababu watazamaji na wasikilizaji wangependa kuelewa kwa sababu walizoea
kusoma tu, joka kuu itakuwa hivi mara vile, lakini kuna neema ya kumjua mpaka
sura amen!!.
Isaya; Bwana YESU asifiwe huo mti ni mkubwa sana
labda tuseme ni kama Tanzania nzima.
Mtume: Mmm..
Isaya: Na ule mti kazi yake pia
ni kutoa hizo roho kwa wale manabii pamoja na wale wote walioenda kinyume na
MUNGU kule kuzimu.
Pia kazi yake ni kutoa zile
roho ambazo manabii na wale wote walioenda kinyume na amri za MUNGU ambao wapo
kule kuzimu.
Na ule mti unahusika na unaushirika
na mapepo ambayo yanaruka duniani kila siku kwa muda wa saa sita usiku. Yanaporuka yale mapepo yanaachilia zile roho
za ule mti.
Kwa hiyo labda inaweza kupita
Tanzania na kuziacha zile roho mkoa Fulani au Kenya zinaacha sehemu Fulani na p
engine popote pale.
Na pia ule mti ulikuwa una
ndege, ambayo ilikuwa inaitwa “air force one.”
Mtume: Ukubwa wake hiyo ndege ni kama kiasi gani?
Isaya: Ni kama Arusha nzima,
Mtume: Ndege moja?
Isaya: Ndiyo. Ile ndege pia inahusika katika kitengo cha
ule mti cha kuachilia zile roho huku duniani kwa sababu yale mapepo yanaanza
kazi saa sita yanapumzika siku ya kwanza, siku ya pili inaingia ile ndege
inaachilia zile roho saba.
Mtume: Mmm.. Ndugu watazamaji
mmeshaelewa ni kwa nini watu wanafanya dhambi wana ugua, ni kwa sababu ilikuwepo ndege ambayo inamwaga roho za
dhambi, ndiyo ndege kama alivyokuwa anatuelezea hapa ambayo kwa sasa imesha
tunguliwa na watu ni wakati wa kuja kwa YESU sasa na watu waliookoka sasa
watakwenda kusimama imara kwa Yule wanayempenda BWANA YESU , Ameen!
Mtume: Jambo lingine nitapenda kukuuliza, hebu
nieleze , kwa sababu ulikuwa mkuu wa kitengo
hiki na hayo makanisa ya kichawi yaliyopo yanatumia jina la YESU, wewe
ndiwe kiongozi na kuwapa nguvu na kuwapa
pesa na kama ulivyowapa dola wale waliopo Tanzania, wenye mabenk embu naomba
uelezee ndugu wasikilizaji na watazamaji, kwa nini makanisa mengine yanakuwa na
picha ya msalaba, halafu yana alama ya dunia, halafu kuna nyoka kwenye msalaba; na watu hawajijui
wanaona wameokoka embu elezea maana yake ni nini?
Sasa unawaambiaje wasikilizaji
na wanadamu wanaompenda YESU kuhusu hii habari ya huyu nyoka.
Huyu nyooka ninachowaambia
ndugu watazamaji ni shetani, iweje leo kanisa la wokovu lina nyoka kwenye nembo yake? Hiyo nembo huyo
hapa ndiye aliyekuwa anatoa mashariti
,.. sawa , sawa ..
Mtume: Bwana YESU asifiwe
! Ni masharti aiweke pale ili hawa
washuke, wanaposhuka hapo… embu eleza
nini mnachokifanya katika kanisa.
Isaya: Unapoona ilea lama ya
nyoka ndiyo inayotukaribisha sisi kushuka katika hilo kanisa na tunapokuwa
tumeshuka tunashuka kwa kuongozana,
Mtume: Ki vipi?
Isaya: Mtu wa kwanza kushuka anakuwa ni joka kuu,
mtu wa pili kushuka anakuwa ni shetani ambaye ni lusifa na mtu wa tatu kushuka
alikuwa ni roho mtakatifu wa kuzimu ambaye ndiye niliye kuwa naitwa maxwel. Na tunaposhuka,
tunaenda kuchukua sadaka za watu, na wale watu tunachukua miili yao na pale
kanisani tunaacha kopi, na pia joka kuu anaenda kumeza watu wote waliokuwepo
katika hilo kanisa, na pia analimeza kanis azima, lusifa anaenda kuwaua watu
wote, na mimi nilikuwa nikienda kuchukua pesa za watu.
Isaya: BWANA YESU asifiwe,
Mtume: Ameen..
Isaya: Unapoona ile duara
inamaanisha ni dunia, ule msalaba,
unamaana yake maana ya kwanza ile ncha
ya kwanza iliyo simama juu ni joka kuu, ya kulia ni shetani ambaye ni lusifa,
ya kushoto ndiye maxwel ambaye ndiye nilikuwa mimi zamani kwa sasa hivi naitwa Isaya. Ile ya chini inamaanisha kuzimu nzima.
Na Yule nyoka anayekuwa
anazunguka ndiye joka kuu ambaye anazunguka na kuitawala dunia ameimeza.
Mtume. Sasa ni kwa nini kanisa utakuta mchungaji
ameokoka lakini nembo yake ipo nyoka?
Isaya: Bwana YESU
asifiwe!
Mtume: Ameen..
Isaya: Unapoona hiyo nembo ya
nyoka , maana yake ni watoto wa joka kuu
wametawala katika hilo kanisa lake, na wanakuwa wanaachilia nguvu zao, toka
kuzimu katika hilo kanisa na pia wanaenda kuiba nafsi za wana wa MUNGU pamoja
na vitu vyao vyote .
Mtume; Wanaosali
mahali hapo?
Isaya; Ndiyo.
Mtume: Kwa hiyo watu kwenye
makanisa hayo iwe hawajaokoka au wameokoka, mbinguni hawaendi?
Isaya: Ndiyo.
Mtume. Na inakuwaje sasa unakuta anaitwa nabii,
mtume , mchungaji lakini anasema amepandishwa
na YESU eti mpaka mbinguni hii ni teckique gani wakati unasema hapa kuwa
alikuwa mtu wenu?
Isaya: kwanza anakuwa ni muongo
anakuwa anaongea kwa kinyume,
anamaanisha ameshaenda kuzimu. Na pia anapokuwa anasema yeye ni nabii wa Mungu
anamaanisha yeye ni nabii wa shetani na zile nguvu anazokuwa nazo ni mapepo
yanakuwa katika kanisa lake na anakuwa na mapepo ya utambuzi utakuta anakuambia
hivi na vile utoe pesa yako na unapoitoa pesa yako, tayari unakuwa
umeshajiandikisha kwenye kitabu cha kuzimu.
Mtume: Swali jingine
ulishanieleza japo nilikuwa najua, ulikuwa unawapa pesa , utashangaa kanisa
hapa duniani linanyanyuka kumbe wewe ndie zile bank zilizokuwa zinaendeshwa na
makanisa zilikuwa na maana gani?
Bwana YESU asifiwe embu naomba
utuelezee ni kwa nini wengine wanakuwa
na benk na ulishanieleza kwamba, japo nilikuwa najua ulikuwa unawapa pesa,
unashangaa kanisa linaendelea hapa duniani , utajiri hilo linaendelea
limenyanyuka, kumbe wewe ndie ulikuwa unawapa pesa. Embu elezea zile pesa
zilikuwa na maana gani?
Isaya: BWANA YESU
asifiwe!
Mtume: Ameen..
Isaya: zile benki zinapokuwa zinaongozwa na
makanisa, zinanakuwa ni pesa za kwenu nyie nyie waumini, mnatoa sadaka katika
lile kanisa, zile pesa zinakuwa zinapelekwa katika benki ya kuzimu, na kule
kuzimu nilikuwa nazibadili zile pesa,
nakuwa nawapa manabii zinakuwa inawapa wale manabii zile pesa zao na
kuwaambia wakajenge kitu Fulani, na mnapojenga, inakuwa hicho kitu wanajua
lazima kitakamata watu sehemu Fulani, na zile pesa pia zinakuwa ninyi wenyewe waumini
mnakuwa mmekwisha ingia agano pasipo nyie wenyewe kujielewa.
Mtume : Okey .. Jambo lingine ,
aa.. bank kuu ya shetani ambayo ni ya shetani, wewe ulikuwa ni partiner mmoja
wapo?
Isaya: Ndiyo
Mtume: na mlikuwa partiners wangapi katika benki ya kuzimu?
Isaya: Watatu
Mtume: ehee namba moja?
Isaya: Joka Kuu,
Mtume: namba mbili?
Isaya: Lusifa
Mtume; namba tatu?
Isaya: Maxwel
MTUME: Ambaye ndiye wewe hapo?
Isaya: ndiyo
Mtume; Sasa wewe ulikuwa director kule ee.. !! ulikuwa gavana? sasa
Isaya; nilikuwa gavana.
Mtume; Ulikuwa gavana na sasa
umetoka kule, embu nieleze namna gani ulikuwa unawapa pesa? Badhi yao
walikuwa wanakuja kuzitumia hapa duniani
Isaya: Bwana YESU asifiwe,
Mtume; Ameen..
Isaya; Mimi kama mimi binafsi
nilikuwa nikitoa pesa kulingana na mtu kazi aliyokuwa ameifanya, kama mtu
amefanya kazi nzuri ambayo shetani amemtuma aifanye anapokuwa ameifanya ile
kazi sawasawa kama inavyotakiwa huwa nampa pesa lakini kama ameifanya kitu
ambayo haijatakiwa ifanywe ,. Hapati kitu.
Mtume: ni pesa za namna gani mlikuwa mnawapa?
Isaya; Dola.
Mtume: na hizi dola? Haziwezi
kuwa fake huku duniani?
Isaya: Haziwezi.
Mtume; Zinakuwa ni
original? Sasa bwana governer wa bank ya
kuzimu enzi hiyo ambayo banki hiyo ilikuwa ni ya joka kuu, lusifa na maxwel bank
sindio?
Isaya: ndiyo
Mtume: ni nini sasa kinaendelea? Pesa watapata wapi?
Isaya: Bwana YESU asifiwe,
Mtume: amen
Isaya; Kwanza katika ile bank
pesa hakuna tena, ile bank ilishalipuliwa na hata manabii wa uongo
wameshaporomoka kiuchumi, na pia ile bank kwa sasa hakuna pesa yeyote
inayoingia wala kutoka.
Mtume: ni kwa nini?
Isaya: ni kwa sababu ile bank
imeshalipuliwa haifanyi kazi tena.
Mtume: Ililipuliwa Lini?
Isaya: ililipuliwa wiki
iliyopita.
Mtume: ilikuwaje?
Isaya: Bwana YESU asifiwe?
Mtume: amen
Isaya: Na hiyo bank ililipuliwa
mwaka 2014 mwezi wa kumi wiki iliyopita
Mtume; Tarehe ngapi?
Unaikumbuka
Isaya: tarehe siikumbuki, na
aliyeilipua ni Mtume na Nabii Hebron peke yake.
Mtume: Sasa ni nini
kinachoendelea kama benki imelipuliwa?
Isaya: hakuna tena uchumi
kuzimu wala hakuna tena pesa.
Mtume: Ndugu wasikilizaji hata
vipo baadhi ya vyama vya siasa vilitegemea kuchukua pesa kuzimu, kule wapo
waliokuwa wanapiga kampeni zile za urais, ubunge walikuwa wana mwaga pesa. Na
watangazia hakuna pesa za kumwaga tena na uchaguzi kuanzia 2015 hakuna
atakayetumia uchawi atakaye fanikiwa.
Bwana YESU asifiwe!
Mtume: Kuna kitovu ambacho cha wokovu wa uongo
utaweza kuelezea mana katika dunia hii utasikia mtu anasema lakini huyu
hajaokoka wokovu wake ni wa uongo.. sasa shetani ndugu wasikilizaji na
watazamaji naye alikuwa na kitengo chake cha wokovu lakini makao yake yalikuwa Sri lanka na bwana mkubwa zamani sasa hivi
mtoto wa YESu embu tuelezee hicho kitovu kilichokuwepo Srilanka
kilichowekwa na shetani na kazi zilizokuwa kinafanya.
Isaya: Bwana YESU asifiwe,
Mtume; amen
Isaya; Kile kitengo kilikuwa
kinafanya kazi ya kuingiza roho za uovu duniani. Na pia kilikuwa na ushirika na
joka kuu pamoja na majini na mapepo kule kuzimu.
Kwa hiyo kitu kilikuwa kinafanya
kilikuwa kinaingiza wokovu wa uongo siku hadi siku na ule wokovu..
Mtume: Mmmh..
Isaya; Na ule wokovu wa undio kama hivyo, ubatizo
wa kikombe na maubarikio haya ya watu wazima na mambo mengine ambayo hayo ni
dhambi.
Mtume: Ee.. Unaweza kuelezea
watoto wa MUNGU na wana wa MUNGU kwa nini watumishi wana vaa nguo zenye nembo,
mfano jumlisha, mzunguko, njiwa , mkuki, kondoo kwa sababu mimi YESU
alishanifundisha nilipokuwa kule kuzimu japokuwa hayafanyi kazi tena.
Na unaweza kuniambia, nembo
zake mlikuwa mnazifanyia nini? Na je? Hizo nembo ni mpango wa MUNGU au shetani?
Isaya: Bwana YESU asifiwe..
Mtume; Amen,
Isaya: Nembo hizo sio mpango wa MUNGU, ni mpango wa
shetani. Kwanza ningependa kuelezea ukiona kanisa lina alama ya mkuki, anakuwa
anaua rohoa za wana wa MUNGU, wote mnakuwa tayari zimeshauliwa, na pia ile
njiwa ina maana roho mtakatifu ambaye ni roho mchafu wa kuzimu, ambaye ndiye
nilikuwa mimi kwa jina la maxwel.
Mtume: mmh..
Isaya: Na unapokuwa unaona kuna
alama moja mfano labda ekaristi katika ekaristi kuna kaalama kama cha kikombe
kilichowekwa chini, kile inamaana ni damu ya shetani pamoja na damu za wanadamu
wenzako. Kwa hiyo unapokuwa unakunywa
unakuwa umekunywa damu ya wanadamu wenzako pasipo wewe mwenyewe kujielewa. Na
pia kunai le kondoo ina maana watoto wa shetani ambaye ni baba wa kuzimu ambaye
ni joka kuu.
Watoto wake wanakuwa
wanashiriki mahali hapo na nyie pia mnaongozwa na watoto wa joka kuu.
Mtume: Bwana YESU asifiwe
Mtume: Sasa tunaingia katika
lengo lingine la sanamu, kwanza hizi zilizopo duniani zina maana gani?
Karibu!!
Isaya: Bwana YESU asifiwe,
Mtume: Ameen,
Isaya; Zile sanamu zilizowekwa duniani huko,
zimewekwa kwa ajili ya kuteka fahamu za watu, waone wanamuabudu bwana YESU
ambaye wanaweka picha za Yule Brian na kuna makanisa mengine unaweza ukasikia
wanasema YESU ameshuka tumemuona, anakuwa haja shuka YESU ni ule mzimu wa Brian
unakuwa unashuka mahali alipo kwa sababu hata mimi pia nilishashuka kwa mfano
wa sura ile ile.
Mtume: Sura hiyo hiyo
Isaya; Ndiyo.
Mtume: ulishuka katika nchi
gani? Usitaje sehemu
Isaya; Nilishuka, nchi ni
nyingi kama nchi tano hivi watu walikuwa wanasema yesu ameshuka
na kumbe wao bila kuelewa ni mimi.
Mtume: Kwa sura kabisa?
Isaya: ndiyo, nilikuwa nimekuja
duniani
Mtume: Ulishuka duniani watu
wakaona ni YESU kabisa? Ilikuwa ni nchi gani?
Isaya: Nilishuka Tanzania
Mtume: Sehemu gani Mkoa?
Isaya: Nilishuka mkoa wa Dar es
Salaam,
Mtume: Dar es salaam ni maeneo gani?
Isaya; Dar es salaam ilikuwa ni
maeneo ya mbezi pia maeneo ya temeke, na maeneo ya kunduchi.
Mtume: Ni katika makanisa pote
Isaya: Ndiyo.
Mtume; Na lengo ulivyoshuka
ilikuwa ni nini?
Isaya; Ndiyo mara ya kwanza
nimeshuka kuja kuiangalia dunia.
Mtume: Na lengo ulivyoshusha ilikuwa ni nini?
Isaya: Ndio mara ya kwanza
nimeshuka kuja kuiangalia dunia.
Mtume; Dunia..
Isaya: Ndiyo
Mtume: Aaha..na kwa nini ile sura ya YESU hamuwezi kuivaa
kabisa muiecti, na yenyewe?
Isaya: Haiwezekani.
Mtume: haiwezekani, kwa hiyo
watu wanavyo sema wamemuona YESU ni uongo, kumbe wamemuona Brian.
Hata mimi nimekwisha kuwaambia
watoto wa MUNGU sura ya YESU duniani hakuna picha yake wala hakuna kumbu kumbu
yake.
Bwana YESU asifiwe,
Lakini sasa tunapata shule na
kuelewa maana mambo yameharibika, ila YESU amenituma niwaeleze habari njema.
Mtume; Kwenye habari za sanamu
unakuta sanamu zipo kwenye mikoa, miji mbali mbali hizi zina maana gani kwenye
ulimwengu wa roho?
Isaya: Sanamu pia kazi yake
unapokuwa umeiangalia ile sanamu unapogeuka nyuma unakuwa umeacha kila kitu
chako pale, unakuwa umeacha sura yako, maisha yako, uthamani wako pamoja na
vitu vyako vyote.
Kuzimu pia kuna sanamu ambazo
zina connection huku duniani hata ikiwa sanamu ya raisi yambunge au ya mtu
yeyote hata kama ni ya mtumishi unayvyoiangalia hiyo sanamu unakuwa unaacha
vitu vyako vyote katika ile sanamu wewe ukigeuka unakuwa unageuka boksi.
Mtume: Mmh.. kabla ya kumaliza
kuna baadhi wana picha wanaziabudu picha za watumishi,
Isaya: Bwana YESU asifiwe..
Mtume: Ameen
Isaya: Zile Kwanza ningependa
kuelezea katika upande wa stika zile stika maana yake?
Mtume; Stika zipi hizo?
Isaya: Kwa upande wa stika
ambazo zinakuwa zinatolewa makanisani. Zile stika unapokuwa unazichukua unakuwa
tayari umeshachukua kumbukumbu za shetani ambaye ni lusifa na joka kuu pamoja
na Yule roho mchafu wa kuzimu ambaye ni maxwel, unakuwa unawapeleka hao watu
nyumbani kwako na unapo wapeleka hao watu nyumbani kwako tayari umekwisha wapa
uhalali wa kushikilia kila kitu chako.
Mtume; mm..
Isaya: Kwa sababu hata huku
duniani labda kwa upande wa nyumba huwezi kuwa na nyumba ukiwa hauna hati, hata
mtu akiichukua ina maana hiyo nyumba sio ya kwako tena.
Hizo stika unapozichukua
ukaenda kubandika nyumbani kwako tayari unawapa hao watu watatu uhalali pamoja
na kuzimu nzima
Mtume; kwa hiyo na watu wengi
naona wanaweka kwenye magari kwa hiyo wamemkaribisha shetani?
Isaya: Ndiyo
Mtume; kwa hiyo hizo ni hati za
kumpa shetani mali yako na maisha yako? Lakini wao wanafikiri ni YESU
Isaya: ndiyo.
Mtume: Sasa niwaulize watoto wa
MUNGU, je, YESU anatoa stika? Imeandikwa mniabudu katika roho lakini usichukie
bali ufurahi, maana hizi ni habari njema alizonituma YESU WA NAZARETI, na siku
ya leo nakufundisha kwa namna nyingine upate kuelewa. BWANA YESU ASIFIWE, sasa
katika somo hili la shuhuda ambalo huyu ambaye nilikuwa namhoji, nafasi ya tatu
kutoka kwa shetani, huyu hakuna mwanadamu alikuwa anamweza, hakuna mchawi
anamweza. Huyu ndiye alikuwa anawapa mbinu zote, sasa YESU ni mjanja wa wajanja,
amenituma mimi mjanja, nimemkamata, na sasa hivi mnaoendelea kuwa na uchawi
mmeaibika YESU atainuliwa, huu ni wakati wa YESU WA NAZARETI peke yake
kuinuliwa na shetani hana mamlaka tena katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI.
Zaidi ingia katika website
yangu www.prophethebron.org, ingia katika
blog www.prophethebron.blogspot.com
utapata masomo mengi, na ingia katika YouTube ya prophet hebron utakuta vipindi
vingi na zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA
YOTE. Shida yeyote inayokusumbua karibu tena njoo bure bila hata pesa,
utafunguliwa ndio kazi YESU amenituma, BWANA YESU ASIFIWE. Na wengine wote
mnayo nyanyaswa na shetani wakati wa kunyanyaswa umekwisha,wakati wa
kudanganywa umekwisha, njoo usikilize ukweli na ukweli ukae ndani yako, watu
wamedanganyika sana kwa habari ya makanisa, lakini sasa leo nimekuja
kuwafundisha kwa njia hii japo mimi nilikuwa nayajua.
MUNGU WA IBRAHIM, MUNGU WA
ISAKA awabariki, awatunze, nawafunika kwa damu ya YESU. Tutaonana muda mwingine
wakati kama huu, karibuni sana katika siku za ibada mfunguliwe, mtukuze MUNGU,
muwe na amani enyi mataifa yote, msidanganyike tena mambo yameharibika, ndio
maana makanisa imemuacha MUNGU inatafuta pesa tu.