Ubatizo huu ni agano la kikombe cha shetani, ubatizo huu ni
kifungo cha kuwapeleka watu kwa sheyani, kivipi? Fuatilia Makala ya Nabii
Hebron na somo hili pia.
Neno ubatizo maana yake (baptize) ni kuzamisha. Na inavyoitwa
ni ubatizo wa kikombe au kumwagiwa maji kichwani tayari huko sipo kuzamishwa
kabisa. Hivyo msidanganyike watu wote ambao mnampenda MUNGU na hamjui kuwa
mnapotezwa na shetani bila kujua au kujua kabisa unaenda kinyume na biblia.
Nikuulize swali, neno ubatizo ni nini? Jibu ni kuzamishwa, sasa hauoni huu ni
uongo mkubwa kabisa, eti mtu anamwagiwa maji kichwani halafu anasema katika
maji, swali, je amezamishwa? Jibu hajazamishwa. Hata mimi nilimwagiwa maji
hivyo hivyo sababu hata wazazi wangu hawakujua maana ya ubatizo japo na wao
walimwagiwa maji kichwani wakadanganywa wamebatizwa, kumbe hawajazamishwa na
bado ni wenye dhambi haujazamishwa katika maji. Na umeshajiuliza ni kwa nini
makanisa yanayojiita kwa jina la Kristo yaliyo mengi katika ulimwengu wote
wanawamwagia watu maji kichwani tuu badala ya kuwazamisha katika maji? Na je
hawaoni dictionary na kusoma hili neno ubatizo ni nini? Na kwa nini
wanawadanganya watu wamebatizwa na kuoshwa dhambi zao wakati hawajazamishwa
katika maji mwili wote kama vile YESU alivyoonyesha njia, je hiyo ndiyo njia ya
YESU? Jibu siyo, na kama siyo je ni njia ya nani? Jibu ni ya Joka Kuu.
Enyi mataifa yote, amenituma YESU WA NAZARETI niwaeleze
ukweli ili mpone roho zenu sababu shetani na mpinga kristo wamewapiga upofu
mabilioni ya watu wakajiona ni wakristo na tayari wameoshwa dhambi zao katika
miili yao yaani dhambi ya asili na kumbe mpaka sasa bado kile ambaye
hajabatizwa katika ubatizo wa maji mengi tena yanayotembea bado anayo dhambi ya
asili na kama mpaka sasa unayo dhambi hiyo haijalishi unajiita mkristo na ni
mzee wa kanisa, mchungaji au yeyote Yule, mjielewe mnayo dhambi ya asili
inawashikilia na bila kubatizwa ( kuzamishwa mwili wote) dhambi ipo juu yako
bado hata kama hautendi dhambi kwa sasa, ila ipo ile ya asili na
usipobatizwa kwa maji mengi hiyo dhambi
ya asili itakuwa ni bango kwako wewe usiingie mbinguni na MUNGU ni mwenye haki
ataangalia matendo yako.
Katika kitabu cha 1 Wakorintho 12:13 (inasema hivi, kwa
maana katika roho mmoja sisi sote tulibatizw kuwa mwili mmoja, kwamba tu
Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote
tulinyweshwa Roho mmoja. Hapa nakuonyehsa ukweli na kukufungua akili yako. Neno
hili lipo tofauti na ubatizo wa kikombe, kwanza ni tofauti na ule wa YESU na
pili ukiwa unayo dosari moja tu basi ni tayari umevurugika na hiyo hata roho
siyo ROHO MTAKATIFU bali ni roho mchafu. Na ikiwa sasa mwili haujazamishwa
katika maji ina maana siyo mwili mmoja na wa YESU kabisa sababu ili uugane na
wa YESU ni lazima uzamishwe kama vile YESU alivyoonyesha. Sasa mpaka hapa
mmepata ukweli, ila zaidi usome kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE,
kilichoandikwa na Nabii Hebron kitabu hicho kitakuweka huru na utapona,
utabatizwa na utakuwa mwili mmoja na YESU, badala ya kuwa mwili mmoja na joka
kuu, sababu umeyafuata yake kwa mafundisho ya uongo, tafuta katika biblia
hautaona ubatizo wa kumwagiwa maji kichwani bali katika biblia ya shetani ili
akuunganishe uwe mwili mmoja na yeye lazima ushiriki ubatizo feki (kumwagiwa
maji kichwani unakuwa unaunganishwa na joka kuu uwe mwili mmoja, na kama ndio
hivyo swali je mwili wako ukiwa umeunganishwa na joka kuu je huo mwili utaenda
mbinguni? Jibu unalo, utaenda alipo yeye. Swali je mtu wa jinsi hiyo je ni
mkristo? Na je anayohaki ya kuitwa mkristo? Jibu hana sababu ni hizi zifuatazo
kwanza hajawa mwili mmoja na YESU, pili hana ROHO MTAKATIFU, tatu hana mpango
wa kwenda mbinguni, nne yupo katika kifungo, amepigwa upofu. Amenituma YESU
niwaeleze ukweli watu wanapotezwa na huku ndiko kutekwa na shetani. Sasa uelewe
ukikaza shingo hiyo ni juu yako ila nakusihii urejee ili uwe mkristo na mwana
wa YESU badala ya joka kuu.
Point ya pili (Marko 16: 15-16) ; “akawaambia, enendeni
ulimwengu mwote, mkaihubiri injili ya kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa
ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Hapa neno linasema ukweli na linakushuhudia
wewe, YESU alitoa amri kwa wanafunzi wake waende ulimwenguni pote waihubiri
injili na kuwabatiza watu na siyo kuwamwagia watu maji kichwani hapo uelewe
vizuri. Na akasema kila mtu ambaye hatabatizwa (kuzamishwa) atahukumiwa. Je mpaka
sasa watoto wa MUNGU ni wengi wameshahukumiwa au wapo katika list ya kuhukumiwa.
Ni wengi idadi ni mabilioni ya watu na swali lingine jiulize je hao
wanaowamwagia watu maji kichwani je ndio agizo alilolituma YESU watu wamwagiwe
maji kichwani na je hauoni hawa ni waongo na siyo watumishi wa YESU wa kweli,
sababu ya kwanza ya kimwili ambayo
inakupa ushahidi live live wao wanamwagia maji na je kumwagia maji kichwani kwa
nini waite ni kitendo cha kuzamishwa? Hapa chunguza maana ya tendo hili,
utapata jibu siyo wanafunzi wa YESU wa kweli. Alifanyalo mwanafunzi ndilo
alilofundishwa mwalimu wake, sasa ni mwalimu YESU WA NAZARETI kafundisha
kumwagia maji kichwani badala ya kuzamishwa mwili wote? Na je neno ubatizo ni
kumwagiwa maji kichwani? Jibu ni uongo mtupu.
Point nyingine (Matendo 22:16); neno linasema “basi sasa,
unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake.” Hii ina maana
kila anayebatizwa lazima awe mtu mzima na aamue na imani yake asimame
katika maji yanayotembea azamishwe ndipo dhambi zake zitaondoka kwa kupitia
jina la YESU. Sasa angalia neno lilivyopindishwa na maajenti wa shetani, na
kuwafanya watu mpaka sasa wanayo dhambi ya asili na hawaendi mbinguni,
wakajidanganya wajimuagie maji kichwani. Sasa swali je umezamishwa mwili? Jibu siyo
hapo hakuna ujanja wala ubishi, sasa amua ubatizwe ili uoshwe dhambi zako. Sababu
bado unazo dhambi za asili na haujawa mwili mmoja na YESU WA NAZARETI, bado
mwili wako upo na mwili wa asili wenye dhambi na unaomuunganiko na shetani.
Point nyingine (Wakolosai 2:12) “mkazikwa pamoja naye katika
ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za MUNGU
aliyemfufua katika wafu.” Hapa utaona neno lipo wazi utakapozikwa katika maji
yanayotembea utakuwa umeunganishwa na YESU alipokufa na akafufuka, hii ni roho
yako ndiyo itafufuka, hivyo mpaka sasa haujabatizwa ubatizo wa maji mengi
ninaoelezea hapa ujijue bado ni mfu, pili ujijue siyo mwili mmoja na YESU WA
NAZARETI, sasa fanya uamuzi ubatizwe ili uwe mwili mmoja na wanafunzi wake YESU
WA NAZARETI. Hizi ni point za kikweli za kukufungua ujielewe, sasa nakuja
katika kipengele cha kiroho niliyoyakuta kuzimu na kuona kwa shetani anacho
kikombe chake ambacho ni cha kumwagia watu maji na kupitia mpinga kristo na
kikombe hicho anakiunganisha na kile kikombe ambacho mtu anamwagiwa macho maji
halafu anaambiwa amebatizwa, sasa maana ya kikombe hicho kila anayebatizwa
ubatizo wa kikombe anakuwa amewekwa katika agano la kikombe chake joka kuu
hivyo mtu anaingizwa katika agano na shetani either kwa kujua na idadi kubwa
hawajui huko ndiko kutekwa na shetani na unakuwa mwili mmoja sasa na yesu wa
uongo, halafu huku ulimwenguni wewe unajiona upo sawa kumbe ulishatekwa tokea
umezaliwa, na kule kuzimu ndipo unapokuwepo na wewe sababu ya agano la kikombe
au beseni lilitumika kukumwagia maji kanisani, hapo tayari unakuwa umejimaliza
usiende mbinguni.
Na mamilioni ya wakristo hawajaenda mbinguni walishakufa na
miili yao ndio chakula cha mashetani, sababu hiyo miili ina uhusiano na mwili
wa shetani, bali miili ambayo ni ya watu ambao walikufa na wamekuwa mwili mmoja
na YESU, walibatizwa ubatizo wa maji mengi na wakaishi maisha matakatifu miili
yao hailiwi kabisa wala kuguswa sababu roho inakuwa ipo mbinguni na ulinzi wa
malaika. Bali hii ya ubatizo wa kikombe, ubatizo wa maji ya kisima, kubatizwa
kwa jina la mchungaji, miili hiyo ni chakula cha mashetani na majini na roho
zao zipo kwa joka kuu ambapo ndipo asili ya ubatizo wa kikombe. Hivyo nawaeleza
mkatae msije mkawa nyama za mwili wake utakapokufa na roho yako isibakie kwa
mashetani.
Nilishangaa sana mara ya kwanza YESU aliponieleza nenda kwa
mataifa yote waeleze habari za ubatizo wangu na wabatizwe upya ili wapone roho
zao, ila siku zilivyozidi akinifundisha yeye mwenyewe mengi na sasa na wewe
unajifunza, chukua hatua karibu uje ubatizwe katika kanisa la YESU NI BWANA NA
MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, utubu umrejee MUNGU, neema yake inasema na wewe sasa,
na usikubali udanganywe na kufundishwa uongo. Elimu ya kweli ndio ya YESU,
ikiwa imebadilishwa hiyo ni elimu ya uongo na asili yake ni baba wa uongo
shetani.
BWANA YESU WA NAZARETI naomba unisamehe, nashukuru kwa
kunifungua ufahamu naomba uniokoe na uniandike jina langu katika kitabu chako
cha uzima, simtaki tena lusifa na elimu ya uongo. Naomba uniongoze mahali
ambapo wewe upo ili unioshe dhambi zangu katika mwili na unifufue tena. Amen.
NABII HEBRON.