Ufunuo wa Yohana 20:1-3
“1kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni,
mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2Akamshika
yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na shetani, akamfunga miaka
elfu. 3Akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake,
asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo
yapasa afunguliwe muda mchache.”
BWANA YESU ASIFIWE, nitawaeleza kwa ufupi jinsi sura ya joka
kuu ilivyo, maana nilimuona kwa macho yangu tarehe 5.11.2012 muda saa sita ya
usiku. Nilichukuliwa na serikali ya mbinguni pamoja na Malaika Mikaeli ambaye
ndiye malaika mkuu wa vita, nilichukuliwa katika uliwengu wa roho nilivyokuwa
naomba japo nilipewa taarifa kutoka mbinguni taarifa ambaye Malaika Gabriel
alikuja kunijulisha akaniambia leo saa sita ya usiku itakapogonga saa sita
kamili uwe katika maombi na baadhi ya watumishi wangu, akaniambia atakamatwa
joka kuu leo, basi ilipofika muda huo katika maombi, alishuka malaika mkuu na
funguo (Mikaeli) ukakamatwa na mamilioni na nililiona kwa macho yangu, ilikuwa
ni vita ambavyo sijawahi kuona tokea kuzaliwa kwangu au kuisikia jinsi malaika
wa MUNGU walivyopigana mpaka akashikwa, na kuamuriwa aiteme dunia aliyoimeza
katika ulimwengu wa roho na vingine
ambavyo sijaruhusiwa kutaja bado. Na kuanzia tarehe 5.11.2012 ndipo ilianza ile
miaka elfu moja. Sasa watu wengi wanafikiria atakuja malaika kimwili watamuona amkamate
joka kuu, hapana. Vita vyetu ni katika ulimwengu wa roho na tayari sasa tupo
katika miaka 1000, na mtaona ufalme wa mpinga kristo ukibomoka kila siku, na
watumishi waliokuwa wanatumia nguvu za giza wataporomoka sababu hawana pa
kupatia msaada tena.
Mnapoyaona msishangae, mengine mtasikia ni manabii na watu
waliwaamini, lakini watapatwa na aibu nanyi myaonapo muelewe haya niwaelezayo
mimi Nabii Hebron. Joka kuu sura yake ipo hivi, ni joka likubwa na sura ya uso
wake inafanana na mtu bali katika kichwa chake kuna magamba na anavichwa saba,
na katika mkia anayo kucha kubwa. Mpendwa msomaji inatisha sipendi kuendelea
zaidi, ila mpaka hapo umeijua sura yake. Naifahamu sababu nilimuona na nilishuhudia
akifungwa na mimi nilitumika kwa neema ya MUNGU na nilimpiga. Huyu ndie
kiongozi au baba wa miungu yote, wachawi, wapinga kristo, lusifa, amjini,
mapepo na lengo lake ni kuhakikisha hakuna mtu ataenda kwa YESU. Amewawekea
watu mioyo migumu wasiokoke, kama haujaokoka uelewe ni joka kuu anakushikilia
hadi sasa, na YESU akija utabakia kwake. Karibu uokoke sasa, sema BWANA YESU
naomba unisamehe dhambi zangu zote, nitoe katika mikono ya joka kuu, uniandike
jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, uniongoze wewe, najikabidhi
kwako YESU WA NAZARETI. Amen.
NOTE:
Nakufunika kwa damu ya YESU WA NAZARETI.
NABII HEBRON.