BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa
jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME na
pia aliye BABA YANGU NA MWOKOZI WANGU, yeye aliyeniokoa nay eye aliyeniita
nikamtumikie sawa sawa atakavyo ili kuwarejesha ulimwengu wote kwake, sababu
aliwatuma watumishi wachache nao wakamsaliti YESU na wengine wakajiunga na
freemason na wengine kuzimu nay eye YESU akawaacha. Kazi aliyonipa ni kubwa ila
nitaelezea leo kuhusu shetani alivyo, mimi nimempata bahati ya kumuona shetani
alivyo na nilimuona wakati nilikuwa na malaika wa serikali ya mbinguni.
Nimeamua kuwaelezea alivyo sababu kabla ya hapo hata mimi
nilikuwa sinjui alivyo, nikionyeshwa picha za ajabu na za aina aina, ila ukweli
hakuna kata picha moja ambaye ni ya kweli ambaye niliyoiona katika ulimwengu
huu. Hii ni neema ya YESU alipenda nimuone na nimshughulikie kuharibu ufalme
wake na bado naendelea mpaka atakaporudi YESU kuja kulinyakua kanisa lake. Shetani
ambaye anaitwa lusifa yeye sura yake alivyo nitaelezea at least upate picha. Yeye
yupo kama mwanadamu yupo uchi anayo mabawa mawili mgongoni kama vile ya malaika,
pia anaomkia mrefu katika sehemu zake za nyuma, pia mkono wa kushoto katika
kidole kidogo anaoukucha mrefu sana na pia katika macho yake, katika jicho lake
la kulia amepaka wanja kama vile unavyoona watu hapa ulimwenguni wanavyopaka
wanja katika macho ila shetani yeye anapaka katika jicho moja la kulia.
Ni jitu la kutisha kama hauna YESU wa kweli. Natumaini mnapata
ukweli halisi, mimi Hebron namfahamu vizuri ndio sababu haniwezi na hatakaa
aniweze, nitaendelea kuangamiza majeshi yake na kazi zake zote, sawa sawa na
nilivyotumwa na YESU WA NAZARETI pamoja na MUNGU aliyeniumba. Shetani huyu
lengo lake akuteke wewe na wengine wasiende mbinguni ili wakachomwe nae. Na wewe
okoka sasa, usije ukakutana naye huko alipo akakuteka.
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote
nilizosababishiwa na shetani adui yako. Namkataa sasa hivi, naja kwako YESU
uniokoe, nitoe katika mikono yake, niwepo katika mikono yako, na katika kitabu
cha ufalme wako. Shetani sikutaki kuanzia sasa YESU WA NAZARETI niongoze, mimi
ni mali yako sasa. Amen.
NOTE:
Kama haujaokoka mpaka sasa uelewe wewe ni mali ya shetani. Ili
uwe mwana wa YESU kiri hiyo sala ya toba hapo juu.
Nakufunika kwa damu ya YESU WA NAZARETI aliye hai.
NABII HEBRON.