Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI, nitaelezea maana ya
mtumishi au mchungaji, Nabii, Mtume na wengineo wenye bendera zao binafsi ni
jinsi gani ni jinsi gani imefikia mpaka akawa na bendera yake binafsi hata
ukiona katika gari lake akitembea inapepea mbele ya gari lake na katika kanisa
lake pia mtaikuta imewekwa mlingoti au na kama anayomakanisani sehemu nyingine
hivyo hivyo ataziweka bendera nyingi kwa idadi ya makanisa yake. Bendera hizi
ambazo utaiona ni special kwa mambo yake, kwanza kabisa mpaka uone mtumishi
amekuwa na bendera yake uelewe amefikia kiwango kikubwa cha uchawi hivyo hupewa
bendera hiyo na joka kuu ili awe na serikali yake huko duniani na anapokuwa na
bendera hiyo anapewa mamlaka ya kuwateka waumini wake kwa nguvu za kipepo
pamoja na watumishi wake wa chini na anawapa utawala, yeye anakua ni mfalme kwa
upande wa shetani na majeshi ya shetani na mapepo huja kufanya kazi ya
kuwasaidia kuwateka watu fikra zao na kuwanyang’anya nyota na kuwapofusha watu
wasiende mbinguni.
Mahali pa namna hiyo nawaeleza ukweli halisi kama
nilivyoelezea katika makala ya Nabii Hebron katika somo la bendera, soma
utaelewa zaidi nini maana ya bendera kuwekwa makanisani. Ufalme wa MUNGU katika
ulimwengu huu hauna alama, ufalme wa MUNGU upo katika roho tu, na ndio maana
imeandikwa tunaenda katika roho na siyo katika mwili, bali ufalme wa shetani
unaonekana kimwili na ndio sababu watumishi wanaotumiwa na shetani na
wanapandishwa ngazi nyingine lazima hupewa bendera yake ili aanzishe serikali
yake. Ni kama vile kiongozi wa nchi yeyote sababu anashinda kura na kuteuliwa
kuwa kiongozi wa serikali lazima huwa na bendera yake kuashiria yeye ndie
kiongozi mkuu wa serikali hiyo (kwa upande wa serikali za Kaisari hiyo ni sawa
kabisa) ila kwa upande wa MUNGU hakuna kitu kama hicho cha mtumishi kuwa na
bendera yake binafsi katika gari au kanisa. Hayo yote niliona kuzimu na niliona
wanayopewa na lengo lao, akinipeleka YESU na
niliporudi ulimwenguni nikafunguka akili sababu hata mimi sikujua. Akaniambia,
hao wanawapoteza watoto wangu na watoto wangu hawajui, nenda uwafungue macho,
wahubirie wapone, waeleze mimi nilipokuwa hapo ulimwenguni nilionyehsa njia,
kama ingekuwa ni mpango wa MUNGU, basi mimi YESU ningekuwa wa kwanza kuweka
bendera katika punda au boti au katika gari la farasi. Mimi ndiye mfalme
waeleze hao wote siyo watumishi wangu ni watumishi wa ufalme wa joka kuu
amekuja kuupanda katika dunia, ni watumishi wa shetani na OLE wao wanaonitesea
watoto wangu na kulibadilisha neno la MUNGU. Mimi YESU sina ushirika nao kabisa
wala siwajui. Na mimi ninawafikishia ujumbe huo watu wote wa mataifa yote. Amua
sasa upone na umrejee YESU ili utolewe katika hiyo serikali ya shetani
iliyokuteka na wewe ukaona upo katika kanisa la YESU kumbe upo katika kanisa la
mpinga kristo.
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote asante kwa
kujua ukweli wako, niponye roho yangu, uniandike jina langu katika kitabu chako
cha uzima wa milele. ROHO MTAKATIFU uingie ndani yangu uniongoze peke yako. Amen.
NABII HEBRON.