BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA NAZARETI anawapenda watoto wa
MUNGU na anataka msipotezwe tena bali mpone roho zenu. Amenituma niwaonyeshe
njia ya kweli sababu shetani akiwatumia watumishi wake anawatumia kuwapoteza
watu ili wasimuone MUNGU na ile siku ya mwisho wakajumuike na yeye katika
motoila wewe utakayeelewa haya ninayokueleza na kubadilika utapona roho yako. Kwanza
kabisa nataka uelewe kuwa katika kanisa ni mahali pa sala peke yake na
hakiruhusiwi kitu chochote kuwekwa hii ni sababu MUNGU hachanganywi na chochote
na pia imeandikwa ya MUNGU mpe MUNGU na ya Kaisari mpe Kaisari.
Leo ninawafunulia siri za hizi bendera zinazowekwa katika
makanisa na watu wengi wakiziona wanafikiri wana nia njema na nchi hiyo, jibu
siyo. Ukiona katika kanisa lolote linaweka bendera ya nchi yake na mengine
utashangaa wanaweka bendera zaidi ya nchi nne au zaidi. Sasa nataka uelewe,
jambo la kwanza ujue unapoyaona hayo uelewe mtumishi au kuhani wa madhabahu
hiyo yeye siyo mtumishi aliyetoka kwa MUNGU bali ametoka kwa shetani haijalishi
analitaja jina la YESU. Hao ndio wale wakristo wa uongo. Hizi bendera ni
maagizo rasmi ambayo mtumishi aliyepewa nguvu na shetani na hupewa maagizo ya
kuteka hizo nchi ili watu wasimjue MUNGU wa kweli na pia kuharibu uchumi wa
hizo nchi na endapo mtumishi atakuwa amepanda cheo zaidi katika ufalme wa
shetani ndivyo atakavyopewa nchi nyingi zaidi azishughulikie na kuziteka katika
ulimwengu wa roho, siyo kwamba anajipangia tu aweke bendera, hapana! Ni amri
anayopewa na shetani na wengine utakuta wana makanisa katika mikoa mbali mbali,
hivyo badala ya kuweka ya nchi peke yake wanatengeneza zao binafsi zenye nembo
zao ili kuwateka watu wa mikoa hiyo na kuharibu uchumi wa mikoa hiyo na
kuwafunga watu wasiende mbinguni japo kibinadamu watu hawajielewi. Hii ni siri
ninayowafunulia watu wa MUNGU mpone roho zenu katika nchi zote na mataifa yote.
Hivyo basi sasa uelewe nini maana ya bendera kuwekwa
kanisani au bendera za nchi mbali mbali, hayo ni maagano ya shetani
anayoyaingiza na mtumishi ateke hizo nchi zisiende kumjua MUNGU. Hivyo uelewe
sasa ukitaka kupona roho yako huo ndio ukweli halisi, madhabahu ya jinsi hiyo
ni za maagano ya shetani na kama ni za maagano ya shetani basi hata wewe
muumini ujijue kuwa umeingizwa katika agano la kuwa mwana wa shetani pasipo
wewe kujua, funguka ufahamu, masikio na macho ya rohoni upone roho yako. Bendera
ni kwa ajili ya serikali za nchi peke yake. Utasema BWANA YESU naomba unisamehe
dhambi zangu zote, uniandike jina langu katika kitabu cha ufalme wako. Leo hii
nitoe katika kanisa lenye agano la bendera za nchi, niweke katika agano la damu
yako na uzima wako. Uniongoze nisitekwe tena na shetani na watumishi wake
kuanzia sasa najitoa sadaka kwako YESU WA NAZARETI. Amen.
NABII HEBRON.