Pages

Thursday, September 18, 2014

NINI MAANA YA CHRISTMAS TREE? JE UNAJUA NI KUABUDU MIUNGU??
















BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI, ambaye kupitia yeye ndio tunapata siku ya Krismasi ambayo watu husherekea kukumbuka kuzaliwa kwake mwana huyu wa MUNGU  aliye hai na aliye maarufu kupitia manabii wote waliopita na maarufu kupita viumbe vyote na ndiye MWANA WA PEKEE wa MUNGU.

Leo nitaelezea maana ya mti wa Krismasi, unayo maana gani na pia nitaelezea kuhusu mti unaoitwa (Christmas Tree) hauna uhusiano na siku aliyozaliwa YESU kabisa bali mti huu unao uhusiano na miungu iliyoitwa Tammuz. Kama nilivyoelezea katika makala ya Nabii Hebron uisome kuhusu Father Christmas (neno) huyo ni mzimu wa mtu aliyeitwa Santa Claus ila usome utaelewa vizuri na wewe utaachana na kuweka midoli katika siku ya Christmas, badala ya kuiita hiyo siku ni ya YESU peke yake, mbinu za shetani kuivuruga hii siku ya Christmas na kuwapiga wanadamu upofu wajijue kama wanamsherekea YESU siku hiyo. Shetani aliwateka wakristo wa enzi hizo ambao ni wana dini wakaamua katika siku hiyo maarufu ambayo ni kukumbuka kuzaliwa kwa YESU WA NAZARETI, na kumtukuza MUNGU aliye hai, shetani akawashika wanadamu fahamu zao katika siku hiyo wakaweka mti na mti ukaitwa mti wa Christmas. Na siri ya mti huu, zamani wapagani waliamini miungu wa mimea na ndio waliamini ndiye mungu wao, sasa wakamuingiza huyo mungu wao wakampamba katika tarehe hiyo ya Christmas ili kuiteka hiyo siku asiabudiwe MUNGU wa kweli na kila anayeweka mti huo wa Krismasi hadi leo ajielewe  anaupanda ufalme wa Babeli katika moyo wake na anatekwa katika ulimwengu wa roho  anakuwa anampamba mungu Tammuzi au mungu mimea pasipokujua.

Asili ya mti uitwe jina la Christmas tree ilianza Europe, France na Germany, katika biblia hakuna neno mti wa Krismasi, na cha ajabu katika ulimwengu wote watu wanapigwa upofu waliookoka, wapagani, watu wa dini hawaijui siri hii na hata wakiijua hawasemi ukweli wazi wazi ili watu wapone roho zao. Amenituma niwaeleze ukweli peupe peupe. Anayetaka apone atapona, anayekaza shingo majibu atayapata. Huu mti unaoitwa Christmas tree nataka muelewe kwanza haina ushirikaa kabisa na siku hiyo ya kuzaliwa BWANA YESU WA NAZARETI, ila lengo la mti huo ni niungi inayoitwa Tammuz (miungu ya mimea ambayo watu waliamini ile rangi ya kijani ina nguvu katika mimea enzi hizo) hivyo pasipo kumjua MUNGU wa kweli wakaona eti aliyemzaa YESU ndie miungu ya mimea, wakati ukifikiria wewe peke yako utaona mti hauwezi kumzaa mtu, hata kumuuumba, bali mti unatawaliwa na wanadamu kama viumbe vingine. Na pia Christmas tree siyo ishara ya kuzaliwa kwa YESU bali ni ishara ya Ashera au mhimili wa miungu ya Tammuz, na shetani alitumia mbinu kubwa mpaka akauteka ulimwengu na hadi leo watu badala ya kumpokea YESU na kufurahia katika mioyo yao wanatekwa na shetani katika ulimwengu wa roho  kila aliye na huo mti iwe nyumbani, kanisani, ofisini, hotelini anakuwa amaemuabudu mungu Tammuz, na siku hiyo unakuwa umejiimarisha kwa mungu Tammuz pasipo kujua. Ila wachawi wanajua na viongozi wa freemason, wanajua na watumishi wa uongo wanajua kabisa, wanafurahia mpigwe upofu mfe roho.

Natumaini mpaka hapo at least umepata picha kiasi Fulani ila zaidi endelea kusoma makala ya Nabii Hebron utajifunza mambo mengi sana aliyonifundisha YESU na niwafundishe ili mpone. Madhara ya kuita mti au kitu chochote kiitwe ni Krismasi hiyo ni dhambi, na ni kumnyang’anya YESU happy birthday yake na kuipa miungu kama vile huu mti badala ya kuitwa mti tu ukaongezwa Christmas hapa ni kumkufuru MUNGU. Kama ulikuwa haujui tubu, usiweke miungu tena nyumbani kwako, hata katika kanisa, na kila mahali wanapoweka mti katika kanisa panakuwa ni mahali pa miungu siku hiyo na MUNGU wa kweli hashiriki katika kambi ya miungu. Je upo tayari kuweka miungu ya Tammuz kwa kuweka mti wa Krismasi? Na kumkana MUNGU aliye BABA yake YESU WA NAZARETI? Ambaye siku yake ya kukumbuka kuzaliwa imeingiliwa na kubadilishwa jina lake pasipo watu kujua. Yeye ni mfalme asiyefananishwa na kiumbe chochote wala kwa jina lolote lile, na ndiyo maana katika ulimwengu huu hakuna mtu anayestahili kuitwa YESU. Sasa muulize swali yeye anayejiita ni YESU, je alizaliwa na Maria? Na je alikufa na kufufuka? Na je yeye ndie atakayekuja kutunyakua katika unyakuo? Na je muulize mbona upo hapa ulimwenguni haujapaaga tokea enzi hizo? Na mbona haupo na wale wanafunzi wako hapa uliwenguni, tuonyeshe Petro na wenzake 11, jibu hana. Huyo ni feki ndani yake ni miungu inayojifananisha na YESU ili awadanganye watu kuwa yeye ndie na kumbe ni uongo.

Nataka muelewe injili ya kweli na siyo ya uongo na ukweli unachanganya, yaani nuru na giza, kitu chochote cha MUNGU halifai kufananishwa au kuitwa kwa jina lake, unapofananisha au ukaita ujue tayari umemkufuru MUNGU. Hata leo wakristo wengi wanamkufuru MUNGU pasipo kujua sababu ya mapokeo ya miungu mfano halisi ni tendo la kuweka mti wa Krismasi kanisani, nyumbani pako, wewe badala ya kumpamba YESU katika roho, sifa na kusujudu, unampamba mti halafu unaviita ndiyo siku kuu ya kuzaliwa YESU WA NAZARETI hapo umepotea kinachotokea katika ulimwengu wa roho unapandiwa roho za huo mti katika moyo wako na mambo ya miungu na ule mwisho unabakia kwenda jehanamu sababu utakuwa umevunja moja ya amri kumi, usivisujudie vitu, mheshimu MUNGU aliye muumba wako, usimfananishe na chochote kile, sasa huu mti haujafananishwa na YESU? Je haujavunja amri ya MUNGU? Tubu leo na uitupilie mbali wala usiweke kanisani wala popote kama kweli wewe hautaki kumkufuru MUNGU.

Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote naomba unisamehe niliabudu miungu ya mimea bila kujua au kwa kujua narudi kwako MUNGU WA KWELI nisamehe nioshe kwa damu ya mwanao YESU WA NAZARETI, najitenga na miungu yote, sishiriki tena kuita mti uitwe jina lla Christmas wala kuinunua, najitenga na mapokeo ya miti hiyo na maroho yote. Nisaidie nikuabudu wewe katika roho siku ya Christmas na siku zote nikusifu wewe peke yako. Amen.


NABII HEBRON.