Mataifa yote nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye
hai na ambaye yeye ndie atakayekuja kukamilisha tendo la mwisho wa dunia. Kama
nilivyokwisha eleza ya kuwa lengo alilonituma YESU kwa mataifa yote ni
waonyeshe njia ya kweli ili alipo yeye na wewe ufike na mwingine. Sababu sasa
hivi hali ya injili ya neno la MUNGU limechanganywa na uongo na kubadilishwa
ili watu watakapoamini uongo na kuufuata wasimuone MUNGU na wasiende mbinguni.
Soma hili ninalowaandikia mataifa yote, ni mambo niliyofundishwa na YESU yeye
ambaye ndiye kweli usije ukaona ni mimi Hebron, hapana, ni YESU ndani yangu
aliyekasirika kwa nini watumishi wanawadanganya watu ya kuwa wanaijua siku ya
mwisho wa dunia, wakiwemo wana sayansi na wanajimu?
Biblia inasema katika kitabu cha Mathayo 24:3 “hata
alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa
faragha, wakisema, tuambie mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya
kuja kwako, nay a mwisho wa dunia?” Hapa utaona wanafunzi waliuliza mambo
mawili la kwanza ni kuja kwa YESU mara ya kwanza (unyakuo) na pili baada ya
unyakup itapita miaka saba ya dhiki kuu ndio itatokea lile tendo la mwisho wa
dunia. Sasa nataka mfunguke ufahamu
mataifa yote sababu mpaka sasa watumishi wanawadanganya watu eti kuwa sasa hivi
tunasubiri mwisho wa dunia wakati ni uongo.
Kwanza ili ujue ni uongo kwanza unyakuo bado haujatokea,
hili litakuwa ni tendo la kunyakuliwa watakatifu (watu waliookoka tu na
kuzaliwa mara ya pili kwa maji mengi) na litafanyika kama vile mwezi baada ya
unyakuo wale watakaobaki ni wenye dhambi peke yake wataiona dhiki kuu hii
itakuwa ni miaka saba na hii haitakuwa siri katika ule mwisho wa dunia (Mathayo
24: 29-31) itakuwa ni wakati wa hukumu. Sasa watu wanadanganywa eti wajiandae
na mwisho wa dunia badala ya kujiandaa na unyakuo kwanza. Nikuulize swali ni
biblia gani wanayoisema ambayo inasema ni mwisho wa dunia unakuja kwanza?
Badala ya unyakuo ambao ndio ujio wa kwanza wa YESU. Mimi nawasihi watu wote
zaidi mjiandae kwa unyakuo sasa sababu ni wakati wowote hii ni siri ya MUNGU
peke yake itakuwa ni lini na mwaka gani, mwezi gani ni yeye anajua peke yake.
Sasa wanadamu wamekuwa ni waongo hata wanajaribu kusema
wanajua ni miaka gani na ni lini mwisho wa dunia? Nawatangazia hao watu ni
waongo tena wanamkufuru ROHO MTAKATIFU na kuwapotosha watu wasijiandae na
unyakuo sasa. Ukikuta mtumishi anaelezea au kuhubiri habari za mwisho wa dunia
ni lini na anajua uelewe huyo ni MUONGO, anapotosha watu ndani yake ipo roho ya
mpinga kristo na wengine hawajielewi wanaiga mapokeo ya elimu ya wanadamu
pasipokujua. Watumishi hao wanakuandaa wewe ushiriki dhiki kii na usinyakuliwe
na ndio sababu wao badala ya kuona unyakuo kwanza wao wanaona dhiki kuu,
watashiriki na watakaa hapa hapa kipindi cha dhiki kuu na wateseke na kuteswa
na mpinga kristo na watabakia hapa wanasubiri hukumu ile siku ya mwisho.
Natumaini unanielewa vizuri kuwa huu ni wakati wa unyakuo
sawa sawa na katiba ya MUNGU isemavyo, kisha itakuwa dhiki kuu, halafu ndio
mwisho wa ulimwengu. Haya yaliyotabiriwa vita, magonjwa haya yote yanaashiria
dalili za kuja mwana wa MUNGU YESU WA NAZARETI kuja kulinyakua kanisa lake kwa
mara ya kwanza kasha atakapilinyakua atapaa nao kwa miaka saba, hata wale
waliokufa katika BWANA watafufuka wapae na kumlaki YESU mawinguni. Na wale
ambao watakuwa wamekufa na dhambi watafufuka waishi tena kipindi hicho kitakuwa
ni cha last game kama ukishinda hautahukumiwa. Na kama itakuwa ni kipindi cha dhiki
hivi unaweza ukavumilia sababu utaambiwa ukimkiri YESU unakatwa mkono, sikio,
miguu lakini haufi sababu mauti itafungwa. Je wewe upo tayari ubakie katika
dhiki kuu? Kusubiria ule mwisho wa dunia? Jibu unapona, utoke, unyakuliwe, amua
sasa uokoke na uyatoe mafikirio hayo katika moyo wako na kusubiria mwisho wa
dunia badala ya unyakuo, kama hautaki unyakuliwe na YESU ujue mateso ya dhiki
kuu yatakuhusu na je utaweza kuyavumilia? Jibu hautaweza.
Hivi vitu mnavyoviona sasa katika ulimwengu huu haya ni
matayarisho ya dhiki kuu je na wewe unayataka? Matayarisho haya hayatawadhuru
wale ambao hawajamsaliti YESU WA NAZARETI na wameokoka, na msishangae hata
majengo yakianguka katika sehemu mbali mbali, ni dalili za mwanzo wa kuja kwa
mara ya kwanza YESU WA NAZARETI kulinyakua kanisa ambalo ni mtu aliyeokoka na
kuzaliwa mara ya pili. Hivyo kuanzia sasa penda kufuatilia habari za unyakuo
ili ukae vizuri na YESU akija akunyakue. Siyo vibaya kujua habari za mwisho wa
dunia ni vizuri kabisa ila ninachotaka kwenu mtoe mawazo yenu katika elimu ya
uongo mrejeshe katika elimu ya kweli ambayo ni unyakuo kwanza, na watakaobaki
na dhambi wajue mateso ya dhiki kuu atapambana nayo, ni baada ya kupita miaka
saba ndio sasa tendo la mwisho wa dunia litatokea, na watu kuchomwa katika ziwa
la milele.
Hao wote wanaotabiri na kusema mwisho wa dunia umefika au ni
mwaka Fulani au mwezi Fulani, waulize
swali je hivi YESU ameshanyakua wateule wake? Atabaki hana jibu, yeye ni muongo
na ndani yake ni roho ya unabii wa uongo ili afundishe uongo na kutabiri uongo
ili watakaoamini wawe wanatekwa fikra zao na fikra ikitekwa tu ujue YESU akija
unyakuo hakunyakui sababu wewe fikra zako na nafsi yako inasubiri dhiki kuu, na
hukumu. Sasa funguka leo na utubu na zaidi usome blog na masomo ya Nabii Hebron,
blog hii inaitwa kwa jina la Hebron kama kivuli, hii ni blog ya YESU WA
NAZARETI ajaye kulikomboa kanisa lake ili na wewe upone soma blog ya YESU
ambaye inaitwa kwa jina la Nabii Hebron basi utapona na utakuwa huru.
Nimewaeleza mara nyingi ulimwengu umetekwa na shetani hata
kanisa na watumishi utaona kabisa hawasemi ukweli idadi kubwa na kama hawasemi
ukweli uelewe wazi kabisa ni roho ya Nabii wa uongo ndio itendayo kazi,
ingekuwa ni roho ya kweli ya MUNGU angesema ni habari za unyakuo watu wajiandae
na kuokoka na utakatifu. Sasa hizi roho zidanganyazo zinafundisha kinyume eti
kwanza ni mwisho wa dunia, je unyakuo
utakuwa lini? Je neno la MUNGU ni uongo? Na je ni kwa nini YESU alisema kila
kitu kitapita bali kila neno lililoandikwa katika biblia lazima litimie. Je
hauoni YESU amepingwa na MUNGU amepingwa? Ila shetani anatukuzwa. Amenituma habari
njema msidanganyike na usitishwe hakuna anayejua siku wala mwaka atakao
linyakua kanisa lake YESU, bali akishalinyakua hapo itakuwa siyo siri tena
itapita miaka saba ya dhiki kuu ikiisha tu ndio YESU atakuja tena kulitimisha
tendo la mwisho wa dunia, wala siyo mtume yeyote, Nabii yeyote au chochote,
ameteuliwa YESU peke yake na yeye atawachukua watakatifu peke yake, na baada ya
unyakuo ndio dhiki kii itaanza. Wakati huo ataruhusiwa shetani atembee live
live na mpinga kristo na kazi ya mpinga kristo atakuwa anahakikisha tu wale
waliobaki na dhambi wmakatae YESU kabisa. Kutakuwa hakuna amani, itakuwa ni
serikali ya shetani inatenda kazi.
Nitaelezea kwa ufupi hayo mateso kwa mfano baadhi, ukisema
unaokoka au unampenda YESU, unaingizwa kwenye mafuta yanayochemka uchemke kama
samaki na haufi unateseka tu, ila ukimkataa YESU ndio unatolewa je utaweza
kuvumilia wakati huo? Jibu hapana. Utakatwa miguu, masikio, wengine watakatwa
viungo vya sehemu za siri zinang’olewa na upanga, wengine miguu yote itakatwa
na mikono na unabakia hapo chini hakuna msaada unabakia na maumivu miaka saba nab
ado utateswa kila siku, je enyi wanadamu utaweza kuyavumilia hayo? Au utachemshwa
kwenye maji ya moto kama vile mayai ya kuku na hautolewi mpaka umkane YESU, je
utaweza kuyavumilia kwa miaka saba? Amua leo uokoke na ukae katika utakatifu na
uishi maisha matakatifu yanayompendeza MUNGU ili MUNGU atakapomtuma mwanae YESU
WA NAZARETI aje kuwanyakua watoto ambao MUNGU amependezwa nao na wewe uwe mmoja
wapo. Nawaeleza hawa wanaowadanganya watu mwisho wa dunia ni siku Fulani,
wasipo tubu na kuokoka leo wajijue jehanamu inawahusu pamoja na dhiki kuu. Ila lazima
muelewe wengi wanaotabiri mwisho wa dunia ni lini hao ni wachawi, na siyo
watumishi wanaoongozwa na roho wa MUNGU ndio sababu hawakiri kweli kama neno
lisemavyo bali aliyepo ndani yao ni roho wa uongo ndio sababu wanatoa habari za
uongo.
Omba toba wewe ambaye una dhambi, BWANA YESU naomba
unisamehe dhambi zangu zote uniandike jina langu kwenye kitabu cha uzima wa
milele na uninyakue na mimi nisibakie katika dhiki kuu hapa duniani. Nibadilishe
fikra zangu niujue kuwa ni unyakuo wa YESU WA NAZARETI kwanza, na mimi
uninyakue YESU mwokozi wangu BWANA WA MATAIFA YOTE. Amen.
Karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA
YOTE, sikiliza vipindi vya television, radio na youtube. Fungua www.prophethebron.org utapata maelekezo
zaidi. Na pia ulipokwama tuandikie kwa email yetu tutakuombea na kukuelekeza.
YESU WA NAZARETI AKUBARIKI.
NABII HEBRON.