BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote ambao tayari ambao
tayari mmezaliwa mara ya pili kiroho na hata wale ambao hawajazaliwa mara ya
pili kiroho katika mpango aliouleta YESU. Lengo langu ni mfunguke sababu
yamkini haujui au hauelewi kuwa bado haujazaliwa mara ya pili au unaona upo
sawa na ni kiumbe kipya na kumbe bado wewe ni kiumbe kile kile cha mwili na bado
asili ya dhambi ipo ndani yako. Zaidi soma katika makala ya Nabii Hebron, soma
la KUZALIWA MARA YA PILI nimeelezea
vizuri na natumanini utaelewa na utafunguka zaidi na roho yako ipone.
Watumishi wanaozalisha watu kwa njia ya uongo au upotofu, au
kwa njia za formula ya miungu au mungu asiyejulikana, na ambaye makao yake yeye
ni jehanamu na ni mpinga kristo, watumishi hawa utawajua katika tendo lao la
kubatiza, utaona ni ubatizo ambao haupo katika biblia (ubatizo wa mungu
asiyejulikana na wa yesu wa uongo ili kukulaghai wewe uone umezaliwa tayari
kiroho na umeondolewa dhambi kumbe umepigwa upofu. Hawa ni manesi wa shetani
ambao ndani yao ipo roho ya mpinga kristo na kumpinga MUNGU na kuharibu neno la
MUNGU na kulichanganya na uongo. Kibinadamu anayezalisha hospitalini anafuata
kanuni za kuzalisha na endapo atakosea au kufuata kanuni tofauti mtoto atakufa,
na pia kiroho mtu ili azaliwe kiroho zipo kanuni zake na amezileta MUNGU yeye
zitumike ili aweze kuzaliwa mara ya pili kiroho, na ikiwa ni tofauti basi mtu
huyo anapozalishwa kiroho kwa kanuni ambazo sizo za MUNGU mtu huyo anawaua
kiroho na anakufa bali kimwili anaonekana anatembea. Ili uelewe amekufa kiroho,
utaona anajiita ni mkristo wa kanisani anaenda lakini hajaokoka, anatenda
dhambi, ni mlevi, ana wake wengi, waume wengi na yupo kwenye dini bado badala
ya kuiga mfano wa Nikodemo katika dini akamfuate YESU sababu katika dini ni
mahali pa dhambi na watu hawajijui na hawaendi mbinguni wamepigwa upofu sababu
hawazaliwi mara ya pili kwa kufuata kanuni alizozianzisha MUNGU ili zifuatwe
ndipo mtu ataweza kuzaliwa mara ya pili kiroho. Watu wengi wamezaliwa mara ya
pili katika wrong formula na matokeo yake hawaendi mbinguni, ubatizo wao imekuwa
ni kama vile mtu amejitupa katika maji kama vile bata au chura kasha akatoka
akakauka.
JINSI
YA KUELEWA MKUNGA FEKI WA KIROHO.
·
Kwanza anazalisha watu kwa mara ya pili watoto
wadogo badala ya watu wazima, na anatumia maji ya kikombe na pia kumwekea
msimamizi mwanamke au mwanume ndio mashahidi wako ukikua wanakuelezea badala ya
kukubali ukiwa na akili yako uone kwa macho yako, peke yako na uokoke.
·
Atakubatiza kwa jina lake anachanganya na la
YESU.
·
Anakubatizia katika kisima ndani ya kanisa au
nje badala ya mtoni katika kijito cha utakaso maji yanayotembea kama vile
Yordani.
·
Atakuchaji pesa za malipo ya ubatizo.
·
Yeye mwenyewe amebatizwa ubatizo wa maji ya
kikombe (amekufa kiroho) hivyo na wewe anaiua roho yako.
·
Mtumishi ambaye amejiita, anatafuta pesa, kanisa
linalofanya biashara na kuchangisha pesa, hapo ni mortuary ya kiroho.
·
Mtumishi ambaye hajaokoka na kuitwa na MUNGU na
ni mchawi na ni freemason.
·
Watumishi wanaovaa kofia wakati wa kubatiza au
kuhubiri (1 Wakorintho 11:7-8).
·
Watumishi wenye huduma tofauti na zile tano
alizozianzisha YESU halafu wakazipa wengine majina yao na vyeo vyao.
·
Watumishi wanaozini na waumini, wanyang’anyi wa
mali za waumini, wanaofanya mazingaumbwe, mfano misukule, kutoa watu vitu
vinavyoonekana katika mwili wa binadamu mfano mawe, misumari, sigara na
vinginevyo vyote hayo ni mapepo.
·
Watumishi wanaovaa misalaba, kuabudu misalaba
(hawa ni waabudu sanamu na mtu uelewe kama haujui ukitenda hayo uelewe umetekwa
nafsi yako badala ya kumuabudu MUNGU aliye hai unakuwa unaabudu miungu na wewe
binadau pasipo kujua unakuwa na wewe umeabudu miungu wakati unampenda MUNGU,
funguka sasa.
Yapo mengi zaidi, soma kitabu cha Nabii Hebron cha UBATIZO
WA KWELI KWA WATU WOTE, utapata soma na utapona na wewe uendelee kusema kweli
na watumie watu kila mahali ili watu waponywe na watoke katika mikono ya
shetani. Na zaidi watumishi wa jinsi hii fuatilia mienendo yao na matendo yao
ndio yatakupa picha ya uwazi haya nimekufunulia katika mwili ili uelewe kwa
urahisi. Hawa siyo wazalishaji wa watu katika roho kwa mara ya pili bali ni
waangamizaji wa roho za watu katika roho. Kama vile mkunga wa kibinadamu
anapokuwa anazalisha bila kujua mtoto anatokea wapi badala ya sehemu yake yeye
anatafuta mtoto azaliwe katika kisigino cha mguu, je mtoto atazaliwa kupitia
katika kisigino? Jibu haiwezekani milele.
Basi ndivyo ilivyo wengi hawajazaliwa mara ya pili mpaka
sasa sababu ya formula ya elimu ya wanadamu badala ya elimu ya MUNGU ambaye
yeye peke yake ndiye anayemzaa mtu kiroho mara ya pili na yeye anao manesi wake
aliowateua kufanya kazi hiyo yaani watumishi wa kweli na anaowajua yeye, siyo
waliojiita, siyo wanaotafuta pesa, wachawi, waliomsaliti.
NOTE:
Uwe makini jichunguze, angalia usije ukawa unapoteza muda
miaka yote ukifikiri utaenda mbinguni na umezaliwa mara ya pili, kumbe bado
dakika hii haujazaliwa kiroho kikweli. Amua ubatizwe mara moja zaidi karibu
katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, uje ubatizwe uzaliwe
mara ya pili na katika huko ulipo haijalishi utatengwa na dini wewe furahi sababu
umekuwa nuru hauna giza (dhambi ya asili hivyo watakuona siyo mwenzao na wewe
waeleze bye bye naenda mbinguni.
BWANA YESU naomba unisamehe, uniokoe, unifungue akili na
roho yangu ili nizaliwe upya mara ya pili, uniongoze kwa mtumishi uliyemteua
ili nizaliwe kikweli sawa sawa na mpango wako, uniandike jina langu katika
kitabu chako cha uzima wa milele, niishike njia yako ya mbinguni na roho wako
aniongoze siku zote. Amen.
NABII HEBRON.