YOHANA
3:1-6 JE NI WEWE?
“Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake
Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2Huyo alimjia usiku, akamwambia Rabi,
twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa MUNGU; kwa maana hakuna mtu awzaye
kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa MUNGU yu pamoja naye. 3YESU
akajibu akamwambia, Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi
kuuona ufalme wa MUNGU. 4Nikodemo akamwambia, awezaje mtu kuzaliwa,
akiwa ni mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5YESU
akajibu, amin, amin nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa ROHO, hawezi
kuingia ufalme wa MUNGU. 6Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na
kilichozaliwa kwa ROHO ni ROHO. 7Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia,
hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote wa mataifa yote,
ambao mmeumbwa na MUNGU na pia unafanana nay eye kwa sura na mfano wake. Amenituma
mwanae wa pekee kwenu nyie niwaeleze ukweli na kuwaonyesha njia ya kweli ili
kila atakayeifuata ataurithi ufalme wa MUNGU na kila atakaye kaza shingo
kukataa kumrejea MUNGU aokoke ataurithi ufalme wa shetani ambapo mahali peke ni
jehanamu alipoandaliwa yeye na malaika zake na wanadamu waliomkataa YESU WA
NAZARETI. Amenituma mengi ni kwa ajili yako wewe unayetafuta njia ya ukweli ya
mbinguni ili siku moja na wewe ukakae na YESU mahali alipo na yeye . Ameniambia
niwaeleze mbatizwe watu wote yaani mzaliwe mara ya pili kama alivyozaliwa yeye
mara ya pili ili mfike mbinguni, kinyume cha hapo, kama haujazaliwa mara ya
pili hakika hautaenda mbinguni huo ndio ukweli. Wengi wakristo mnadanganyika
mpaka sasa mnajiita wakristo lakini hamjazaliwa mara ya pili. Nitaelezea jinsi
inavyotakiwa ili uzaliwe mara ya pili.
Kwanza mwanadamu anazaliwa kimwili na baadaye anaonekana
mwili halisi (huku ndiko kuzaliwa mara ya kwanza) na kuzaliwa mara ya pili
lazima uwe mtu mzima na una akili zako hapa unazaliwa kiroho hivyo hauhitaji
kurudi tena tumboni mwa mama yako na pia haiwezekani urudi tena kwenye tumbo la
mama yako. Jinsi ya kuzaliwa mara ya pili ni unabatizwa katika maji mengi
yanayotembea kama vile YESU alivyobatizwa katika mto Yordani. Na unapozaliwa
mara ya pili ni tendo la imani, ukubali peke yako wewe mhusika na uamue kutoka
moyoni mwako ukiwa unayo akili timamu kama vile YESU alivyokuwa na akili timamu
na akaonyesha njia ifuatwe ambayo ndiyo sahihi. Tazama Nikodemo yeye alikuwa ni
mtumishi katika masinagogi (leo hii ndio wanaitwa watumishi, wachungaji,
waalimu, mtume, nabii, wazee wa kanisa, shemasi, maaskofu).
Nikodemo alimuamini YESU kuwa ni mwana wa MUNGU lakini
alikuwa hajazaliwa mara ya pili na hakujua ukweli, mpaka pale alipoelezwa na
YESU ya kuwa mpaka uzaliwe mara ya pili ndio utaurithi ufalme wa MUNGU.
Nikodemo alishangaa, hivi ndivyo ilivyo hata sasa manikodemo ni wengi
hawajazaliwa mara ya pili na wanahubiri makanisani katika ulimwengu wote wakati
hata wao hawaendi mbinguni. Na kama mtu anakuhubiria habari za ufalme wa
mbinguni wakati yeye mwenyewe haendi, sababu hajazaliwa mara ya pili je hauoni
huku ni kuwapotosha watu waangamie roho
zao na hauoni hawa ni viongozi vipofu? Na hata waumini wao wamekuwa vipofu?
Rudi katika neno, linasemaje? Je ni biblia gani wanayoitumia? Jibu ni ya
shetani ndio watu hawazaliwi mara ya pili ili wasiurithi ufalme wa MUNGU na
kama hawajazaliwa mara ya pili basi ni wazi na ni kweli bila kubisha makanisa
hayo ni ya miungu na yesu wa uongo na mpinga kristo. Na je kama ni mtumishi na
unahubiri kanisani halafu wewe peke yako hauendi mbinguni je hauoni utadaiwa
hizo roho na MUNGU? Na kama ulikuwa haujui sasa amua ukazaliwe mara ya pili na
utoke huko sababu huko ni mahali feki na ni mahali pa gereza la kuwahifadhi
wanadamu wasimjue YESU ili akija katika unaykuo watu wabakie hapo hapo sababu
hawajazaliwa mara ya pili, kama ulikuwa hauelewi sasa elewa na utapona roho
yako. Makanisa mengi zaidi siyo ya MUNGU WA KWELI bali ni ya miungu.
Na je umeshajiuliza ni kwa nini lazima mtu azaliwe mara ya
pili ndio uende mbinguni? Soma masomo haya na ubishi utakwisha 1 Wakorintho
15:50…, Yohana 3:6, Mathayo1: 18-25. Watu ni lazima wazaliwe mara ya pili
sababu kila mwanadamu anayezaliwa lazima azaliwe na dhambi ya asili ambayo
unarithi kutoka kwa wazazi wetu, na pia mwili imetokana na udongo na hivyo
itarudi kwa udongo, sasa ili uzaliwe mara ya pili ni ubatizwe ubatizo wa maji
mengi ukiwa mtu mzima, unapozaliwa mara ya pili unaondolewa ile dhambi ya asili
na unavuliwa sura ya asili, unavalishwa sura ya mbinguni ambayo ni sura ya YESU
(Adamu wa pili) na tendo hili ni la roho yako na mbinguni hauwezi kwenda kama
bado haujazaliwa mara ya pili. Zaidi soma kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA WATU
WOTE (Nabii Hebron Kisamo) utaelewa vizuri na utaona jinsi mamilioni ya watu
mpaka sasa hawajijui ya kuwa hawaendi mbinguni. Sababu ya kina Nikodemo wa siku
hizi (watumishi wasiomjua MUNGU wa kweli).
Tendo tu la kutozaliwa mara ya pili katika makanisa pamoja na
watumishi hii ni dalili tosha wanamtumikia mungu wasiomjua (mungu wa uongo)
haijalishi wanalitaja jina la YESU (YESU alishasema watawadanganya wengi
wakitumia jina langu) hata sasa angalia je maneno ya YESU hayajatimia? Watu wote
ambao hawajazaliwa mara ya pili bado wanayo dhambi ya asili na hakuna mwenye
dhambi ambaye atakayeingia mbinguni. Jichunguze je hauna hiyo dhambi? Zaidi shetani
akabadilisha formula ya kuzalisha watu kiroho mara ya pili, wakristo wengi
badala ya kubatizwa wakiwa watu wazima na akili zao, sasa wakizaliwa tu
wanamwagiwa maji kichwani wanaambiwa wameshazaliwa mara ya pili. Nawaeleza watu
wote unapobatizwa kwa maji ya kichwani, maji ya kisima, au kwa jina la
mchungaji, nawaeleza mnakuwa mmebatizwa au kuzaliwa mara ya pili ili muurithi
ufalme wa shetani na hili limefanyika ili kuwapiga upofu watu waridhike tayari
tendo hilo la kuzaliwa mara ya pili limefanyika kwao. Swali je ulipobatizwa
uliona, ulikubali, uliamini, ulishaokoka? Jibu ulilonalo ni taarifa tu uliopewa
ulivyokuwa mtu mzima. Na ukifuatilia kitabu kitakatifu biblia utaona utaratibu
wa mtu kuzaliwa mara ya pili, lazima aamini, akubali, aone kwa macho yake. Ikiwa
ni kinyume ujue mpaka sasa haujazaliwa mara ya pili na mbinguni hauendi (hivyo
ndivyo kanisa lilivyotekwa na shetani unapokea mafundisho ya uongo na uongo ukapokewa
na watumishi na waumini na wanaposhiriki tu wanakuwa wanaongozwa na miungu na
siyo MUNGU mtakatifu na kibinadamu nitaelezea mfano wa mkunga anayezalisha
hospitalini au nyumbani, siku zote wanafuata formula ya kuzalisha , wanajua mtoto
anatokea katika eneo Fulani na kudeal nalo mpaka mtoto azaliwe na aonekane. Hata
kiroho formula ni hivyo hivyo tu ambazo zimeonyeshwa na MUNGU zifuatwe ndipo
mtu atazaliwa mara ya pili kiroho.
Sasa kiroho formula alizozileta MUNGU zimetupiliwa mbali
watu wakachukua za shetani, sasa formula ya shetani je itakuzaa wewe kiroho na
kukuondolea dhambi? Jibu unalo. Huu ni wakati wako sasa na ufanye maamuzi kama
kweli unayo nia ya kweli ya kwenda mbinguni. Uzaliwe mara ya pili na uangalie
pia anayekubatiza, sababu kama huyo mtu anayetumika kukuzalisha mara ya pili kama
yeye amejiita, anajifanya, ni mtumishi wa mshahara na yeye hajazaliwa mara ya
pili au ni mchawi, anafanya biashara; michango, benki, mlevi, mzinzi, muabudu
sanamu, au amemsaliti MUNGU, au ni freemason au anaongozwa na mizimu, mfanya
mazingaumbwe, au hata MUNGU hamjui ila yeye anajifanyia tu wala hajatumwa na
MUNGU nakueleza ukweli bado utakuwa haujazaliwa mara ya pili sababu ROHO
MTAKATIFU hayupo ndani yake ni roho myingie na hapa mabilioni ya watu wanapigwa
upofu. Aliponionyesha YESU niliona watu ambao idadi yake sikuwa na hesabu ni
umati ambao unawea ukajaa urefu wa kilomita 100 kwa urefu na upana, wakiwemo
waliookoka na wamebatizwa kwa maji mengi lakini kumbe wamezaliwa feki na
hawajui ukweli hii ni wan chi zote na mabara yote. Unayejiita mkristo
haukamiliki kama haujaokoka, kuzaliwa mara ya pili ukiwa mtu mzima. Iwe ni
waumini na watumishi. Mfano halisi nimeelezea habari za Nikodemo, tazama hata
Paulo alibatizwa mara ya pili akabadilika, nawasihi mfunguke mkatae uongo MUNGU
anawaoenda watu ndio sababu aliandaa njia njema ya watu wazaliwe mara ya pili
na shetani hapendi kabisa watu wazaliwe mara ya pili sababu anajua pendo lake
la dhambi litaondoka ndani yako na hata kupata. Haijalishi unaenda kanisani
kila jumapili kama haujazaliwa mara ya pili mbinguni hauendi kabisa na kama
unasali katika kanisa ambalo linabatiza ubatizo wa kikombe uelewe hapo ni
pangoni au shimoni pa kuzika roho zenu, na hapo hakuna njia ya mbinguni ni
jehanamu wala halipeleki mtu mbinguni sababu watu hawazaliwi mara ya pili
kiroho. Haijalishi wewe ni tajiri namba moja wa ulimwengu wote, iwe ni mfalme,
ni Rais wa dunia yote ni mtu maarufu wa aina yeyote au ni maskini au haujasoma,
unajulikana, kama haujazaliwa mara ya pili nakueleza kwa mamlaka aliyonipa YESU
WA NAZARETI ili watu waujue ukweli wapone roho zao, kama haujazaliwa mara ya
pili mbinguni hautaenda na utajijua kabisa kuanzia sasa kama unaenda mbinguni
au hauendi, chunguza ubatizo wako, na uishi maisha matakatifu ya kumpendeza
MUNGU.
NOTE:
Hii ni story ya kweli kabisa mimi nilikuwa Driver guide
katika nchi ya Tanzania, niliacha pale nilipokutana na YESU ana kwa ana
Serengeti 2010. Nilikutana na kutembeza wageni karibu mataifa yote na mabara
yote. Nitaelezea niliyokuwa naongea na baadhi ya wazungu (European, American,
Indian, Chinese na wengineo wengi) walikuwa wananiambia hakuna MUNGU, wewe
tumia akili yako usome, sisi hatuendi kanisani makanisa wanaenda wazee tu. Niliendelea
kuwaombea sababu nilishangaa na wakati huo nilikua bado ni mchanga simjui YESU
vizuri, lakini nilipokuja kuingia katika kazi yake nilikumbuka maneno waliyonieleza,
kwa kweli sikuwalaamu kabisa niliona wapo sawa, sababu huko walipo walishachoka
na kudanganywa na kupotosha na waligundua watumishi ni waongo na wakakata tamaa
ni bora wawepo hivyo hivyo. Ila nawasihi nyie niliokuwa nawapeleka safari na
wengine wote mlio kata tamaa sasa mrejeeni YESU, ni kweli mlidanganywa na YESU
anawapenda. Amenituma kwenu mnaosema hakuna MUNGU, njooni kwake leo mtamuona
MUNGU. Ni kweli mliondoka sababu YESU alikataliwa na watumishi na wao wakamleta
yesu wa uongo wa miungu, na nyie mlishtuka, ni wajanja. Sasa leo nawakaribisha
kwa YESU WA NAZARETI niliye naye ndani yangu. Useme BWANA YESU naomba unisamehe
dhambi zangu, narejea kwako uniongoze wewe hadi kwa MUNGU WA KWELI, sababu
tuliona hakuna MUNGU kumbe upo. Karibu ndani yangu, uniandike jina langu katika
kitabu chako cha uzima wa milele, miungu siwataki tena na uniongoze ili niweze
kuzaliwa mara ya pili, ili niweze kuurithi ufalme wako na mimi. Amen.
Ujumbe huu watumie na wengine kwa njia yeyote utainuliwa na
utakuwa unamfurahisha YESU.
NABII HEBRON.