Ubatizo huu unaofanya watu wengi waone wamebatizwa yaani
kuzamishwa kama vile YESU alivyoamuru lakini matokeo yake ni feki bado mtu
anakuwa hajabatizwa kabisa, sababu ya kwanza maji hayatembei (siyo kijito cha
utakaso) na pili hairuhusiwi kabisa kujenga kisima, halafu ubatizwe hapo tayari
umelibadilisha neno la MUNGU na shetani anamwekea MUNGU bango la mashtaka hawa
siyo wakristo ni mwili mmoja na mimi shetani kivipi endelea kufuatilia
mafundisho ya Nabii Hebron yanayosema ukweli na uwazi mtupu ili kuwaongoza
mataifa yote wamjue MUNGU wa kweli na siku moja wafike mbinguni ambapo mwanae
alienda kuandaa makao na hata sasa makao yapo tayari ila hayana watu
watakaoenda ni kidogo sana mpaka ni aibu hata kutaji idadi hiyo kwa siku ya leo,
na ndio ninaogeza bidii kuwafundisha ili anayekubali na kubadilika apate makao
mbinguni.
YESU alibatizwa katika mto unaotembea maji kijito cha
utakaso na katika tendo la ubatizo ni la asili kutoka kwa MUNGU kwa kupitia
umbaji wake wa asili mfano Jordan river, mto ulikuwa na asili ya MUNGU peke
yake. Hivyo swimming pool, kisima, hivi havina uhalisi wa MUNGU bali vina uhalisi
wa kazi za binadamu,mpaka hapa uelewe, kama ulibatizwa
ubatizo wa jinsi hii ujijue bado mpaka sasa unayo dhambi ya asili na siyo
mkristo, haijalishi unajiita mkristo na umeokoka, wokovu wako ni bure sababu
kinachokuunganisha wewe uwe mwili mmoja na YESU ni ubatizo wa maji mengi
yanayotembea. Na ujanja huu aliutumia joka kuu ili kuwapiga upofu watu waliokoka
wakiri sala ya toba na katika kumalizia swala la kuunganishwa kuwa mwili mmoja
akawatega na mafunuo tofauti ya kujijengea visima.
Ila katika kufundisha yeye aliyonituma YESU WA NAZARETI
alinipeleka kuzimu akanionyesha kila kitu ambacho shetani anawategea watu ili
wasiende mbinguni. Maana ya kila kisima kwanza kinachimbwa kinaenda chini, huko
chini ni kuzimu hivyo mtu unapoingizwa katika kisima hicho linachoelekea chini
kama vile shimo unakuwa unavuliwa vitu vyako vyote vinaenda kuzimu na unabakia
empty kama vile boksi tupu. Hii ni njia ya shetani kuwateka watu kwa ubatizo
wake kwa maji mengi. Pili na visima vyote ambavyo vimejengwa ndani ya kanisa, kisima
hicho linatumiwa na shetani kama njia yake ya kufikia madhabahuni na ndiyo
sababu kisima linachimbwa kuelekea chini. Utajiuliza mbona mto mto ni mrefu na
unaweza ukazama unaelekea chini. Mto tofauti yake hauna mwisho na mto ni umbaji
wa MUNGU peke yake (soma makala ya Nabii Hebron somo la ubatizo wa kikombe)
nimeelezea utaona tofauti hapo. Hivyo hapo tayari ni feki, na pia wapo
wachungaji ambao hapa ulimwenguni watu wanafikiri ni watumishi wa MUNGU wa
kweli kumbe ni washetani. Ile huduma na nguvu anazopewa na shetani lazima afuate
ubatizo wa kisima hayo ni masharti ili kuwapeleka watu kwa shetani, hapa
ulimwenguni mtaona anahubiri biblia na ana onya dhambi, ila katika ulimwengu wa
roho ni kinyume na mafundisho mnayoyasikiliza na kuyapokea yanawaua kiroho
pasipo kujua. Sasa uelewe, mimi nasema ukweli na kweli itawaweka watu huru,
imeandikwa atakayeongeza maneno ya kitabu cha MUNGU atahukumiwa au kuyapunguza.
Sasa hiki kisima, swimming pool, tenki je hazijaongezwa kutoka katika biblia ya
shetani, vikatae upone, ubatizwe upya.
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu, uniandike katika
kitabu chako cha uzima, uniongoze nibatizwe upya, maana nilidanganywa, asante
kwa kujua ukweli wako, nishike mkono. Amen.
NABII HEBRON.