Pages

Saturday, May 17, 2014

MIUJIZA YA MUNGU WA KWELI IPO HIVI….!!!
MIUJIZA YA SHETANI IPO HIVI….!!!
KWA MAKANISA NA WATUMISHI.

Kwanza kabisa natumaini watu wengi mtafunguka zaidi maana hili jambo la miujiza  limekuwa likiwatesa watu wengi na kushindwa  kutofautisha ipi ni ya MUNGU wa kweli na ipi ni ya shetani maana miujiza hiyo inatendeka makanisa sehemu mbali mbali na watu wanashindwa kutofautisha na pia katika makanisa mengine hakuna miujiza kabisa.

MIUJIZA

Miujiza ni nguvu za MUNGU au maajabu yanayotendeka kupitia mtumishi wa kweli na pia katika miujiza hii ipo ya shetani pia kama nilivyokuisha kusema, miujiza ni nguvu sasa hapa ndipo pa kuelewa, maana hata miujiza ya shetani ndio nguvu zake au maajabu ayatendayo. YESU alisema msiziamini kila roho bali zichunguzeni kama zimetoka kwa MUNGU aliye hai. Sasa uelewe vizuri, ukiona mtumishi anatenda miujiza ujue yeye yupo karibu na MUNGU sasa pia lazima uelewe hata anayetumia nguvu za giza na yeye yupo karibu na mungu wake ambao ndiyo miungu. Ila uelewe sasa kupitia neno lake MUNGU wa kweli, nimekupa bure, toa bure, naeleza katika habari ya miujiza inayotolewa na watumishi waliokaribu na MUNGU, miujiza hiyo hawakudai pesa, wala hawajisifu ni wao wamefanya, wanamrudishia MUNGU utukufu, na miujiza ya MUNGU wa kweli siyo ya kununua kwa anayetendewa jambo au kufunguliwa, ni bure.

Ila kwa miujiza ya kipepo mtumishi lazima adai pesa maana usipotoa yule mungu wake ambaye maneno yake katika biblia yake ya shetani yeye hatoi bure. Na zaidi haponyi ila anakuongezea pepo lingine juu yake halafu linalipooza lilikuwapo halafu baada ya muda shida ipo pale pale au hali yako inazidi kuwa mbaya zaidi. Sasa ukiona miujiza yote inayotendeka lazima mtumishi adai pesa au sadaka za kukufungua ndugu ufunguke sasa hiyo nguvu aliyo nayo ni ya maagano ya kipepo na ndiyo hao manabii wa uongo sasa umepata jibu. Hata ukikuta kanisa lina benki au biashara na miujiza inatendeka elewa siyo ROHO wa MUNGU yupo hapo bali ni mapepo, hata akichangisha pesa kanisani, elewa huyo anatenda miujiza kutoka kwa nguvu za shetani.

Na jambo lingine katika makanisa, ilitakiwa makanisa yote kupitia mtumishi hao watumike kutenda miujiza, lakini ni cha ajabu siku hizi hakuna miujiza ni sababu hao watumishi hawapo karibu na MUNGU na pia wengi wanajiita na wanatafuta pesa na watumishi wa jinsi hii hata wamtafute MUNGU hawatamuona sababu yeye hawajui wala hajaweka utumishi ndani yao bali wengi wamejiingiza kwa kupenda kufanya kwa ajili ya mshahara. Na hii ni shetani sababu YESU alisema mtatenda makubwa na msingi ya kuzimu haitawaweza sasa ukiona kanisani hakuna miujiza ya MUNGU uelewe kanisa hilo limeshafungwa na kutekwa na shetani na hata kuhani, na zaidi mpaka litekwe na shetani ina maana watumishi hao hawapokaribu na MUNGU katika mioyo yao ila kwa nje wanajionyesha wako na MUNGU, YESU alisema watu hawa wananiheshimu kwa midomo bali mioyo yao ni mbwa mwitu. Na madhara wale wote wanaosali katika kanisa lisilo na miujiza na wao wanakuwa wapo mbali na MUNGU, na ibada zote ni feki mnajichosha.

Karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE mtapona na zaidi soma makala ya Nabii Hebron moja baada ya moja hakika utafunguka na utaona nuru.


NABII HEBRON.