Pages

Friday, May 16, 2014

NINI MAANA YA KUJITWIKA MSALABA

LUKA 9:23

Neno la MUNGU linasema hivi, akawaambia wote, mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku anifuate. Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron YESU WA NAZARETI anawapenda watu wote wa mataifa yote anawataka mumrejee yeye amenituma niwaeleze habari njema na usije ukafikiria habari hizi za neno lake mimi nimesomea katika chuo cha hapa ulimwenguni wala sina hata degree ya elimu ya biblia wala cheti chochote cha chuo chochote, katika ulimwengu huu.

Yeye kwa mara ya kwanza 2010 nilipokutana naye mimi Hebron na YESU tukiwa wawili tu, akaniambia nakufundisha na wewe ukawafundishe mataifa yote kweli yangu na ulinyooshe neno langu pale lilipopindishwa au kubadilishwa sababu kila anayefuata maneno tofauti na mimi tayari amepotea na hii ni sababu watumishi wa shetani wanaojiita watumishi katika makanisa wanawapoteza watu ili wasije kwangu, ila uwaeleze na uwaeleze makao ni tayari atakayekusikiliza na kuyatenda hayo unayowaeleza watapona roho zao, ila watakao pinga jehanamu inawasubiri. Haya ni maneno ya YESU WA NAZARETI ambaye mnasikia habari zake na katika vitabu vya nyaraka takatifu, ila mimi nimepata neema hata ya kuongea naye kibinadamu. Sasa zaidi endelea kusoma makala yangu na pia karibu katika kanisa langu ambalo ameniweka nilisimamie ambalo ndilo kanisa la ulimwengu wote na kwa watu wote ili awaponye, awafungulie njia ya mbinguni ambayo watu walifungiwa na kutekwa na shetani wasimjue YESU wa kweli.

Ndugu msomaji sasa naelezea maana ya kubeba msalaba aliyosema YESU na jinsi inavyotakiwa. YESU alivyosema kila mtu aubebe msalaba wake ndipo ataweza kumfuata, YESU alimaanisha kila siku hakikisha umeubeba wokovu na wokovu ndio mzigo aliokuletea na aliuleta kwa ajili ya watu wote watakaomuamini yeye na kumkubali. Ila shetani amewapiga upofu watu sasa wanabeba misalaba kifuani na shingoni kila siku badala ya kuupokea wokovu aliouleta, shetani amebadilisha kwa ujanja ili awatese wana wa MUNGU. Kwanza haitakiwi mtu yeyote abebe msalaba tena sababu YESU aliposulubiwa pale msalabani tusibebeshwe tena mizigo na zaidi Simoni Mkirene alipomsaidia YESU kubeba msalaba aliubeba kwa niaba yetu sisi watu wote katika uliwmengu, na zaidi ukibeba msalaba unakuwa unapelekwa na wewe katika golgota katika uliwengu wa roho na wewe unahukumiwa na mapepo ya kiyahudi.

Sasa shetani na mpinga kristo walichokifanya hapa kuwateka watu fahamu zao wakatae kuokoka na wakubali kubebeshwa msalaba. Kumbuka katika makala ya Nabii Hebron nimeshafundisha habari ya msalaba, kuwa msalaba siyo alama ya mkristo, alama ya mkristo ni wokovu tu na siyo kitu kingine. Sasa fungukeni na msibebe misalaba tena, ila beba wokovu ndani ya mioyo yenu kila siku na mtamuona YESU. Kubeba msalaba ni kujilaani au nikujiandaa katika ulimwengu wa roho kuteswa na shetani.

SALA YA TOBA:

BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE UANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA, NIVUE MISALABA NILIYOVAA PASIPOKUJUA AU KUELEWA NA WEWE YESU UJAE NDANI YANGU NIWEZE KUKUFUATA KILA SIKU NA NIURITHI UFALME WA MILELE. AMEN.

NABII HEBRON.