BWANA YESU ASIFIWE! Nawasalimia kwa jina la YESU WA NAZARETI
aliye hai na ndiye aliye Kristo wa kweli, leo ninafundisha kuhusu ukristo ni
nini? Na wokovu ni nini? Maana watu wengi katika ulimwengu wote wanapigwa upofu
na shetani wakajiita wao ni wakritso bila kuokoka. Amenituma niwaeleze ukweli
wake maana anajua wengi mnampenda na pia wapo wasiompenda yeye, amenituma
niwaeleze ukweli kuhusu yeye YESU WA NAZARETI na jinsi ipasavyo mtu akamilike
ili awe mkristo kamili na siyo mkristo mpagani. Ameniambia yeye alipokuja hapa
ulimwenguni yaani yeye Kristo alitumwa na BABA yake awaletee wanadamu wokovu na
wokovu mtaingia tu pale kwa yule atakayemkubali kwa kumkiri kwa kinywa chake
kama ndiye BWANA NA MWOKOZI kwa kufuata yale aliyoyaleta katika ulimwengu huu.
Ukisoma katika kitabu cha Yohana 3:16 inasema kwa maana
jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu hata akamtuma mwana wa pekee ili kila mtu
amuaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Na ukisoma katika kitabu cha
Warumi 10: 9-10 bila kumkiri YESU hakuna wokovu, bila kumkiri YESU hakuna
ukristo. Sasa shetani na yeye anajua wokovu ndio nini na sababu anajua wokovu
ndio ukristo wa kweli. Yeye akayateka makanisa na kuwanyima wasiokoke bali
wajiite tu wao ni wakristo. Unatakiwa ujiulize katika akili yako je YESU
alileta jina lake tu au MUNGU alimtuma aulete wokovu? Na atakayemkiri ndiye
atakaye okoka.
Makanisa yametekwa na shetani 98% katika ulimwengu wote
yamekuwa siyo makanisa ya YESU KRISTO wa kweli. Sababu hayana wokovu na hata
viongozi wao hawajaokoka. Sasa kama makanisa yaliyopo katika ulimwengu huu
yaliyo mengi hayakiri wokovu bali yanatumia jina la YESU kujiita wakristo. Nawaeleza
mfunguke makanisa yote katika ulimwengu huu ambayo watu hawaokoki hayo siyo
makanisa ya Kristo wa kweli, sababu kama yangekuwa ni ya kristo wa kweli lazima
yangekuwa na wokovu na siyo litrugia au sheria. Ila uelewe yapo makanisa
yanayoona yapo sahihi mbele za MUNGU kumbe yapo sahihi kwa kristo wa uongo. Kristo
wa kweli yeye alileta wokovu na uzima, ila kristo wa uongo yeye alileta jina
lake tu na hana wokovu, sasa embu fungukeni mataifa yote. Je mfano anarudi leo
hii je wanaojiita wao ni wakristo na hawajaokoka wataenda mbinguni? Jibu ni
hapana, na je jiulize hivi hao wote waliofariki na wakajiita wao ni wakristo na
hawajaokoka je wanaenda paradiso? Jibu unalo sasa hao wote wapo kuzimu sababu hawakuokoka
bali waliongozwa vibaya kwa kufuata mapokeo yaliyo elimu ya wanadamu na ndivyo
ilivyo leo hii YESU anao wakristo waliokoka 2% katika ulimwengu wote hiyo 98%
ipo chini ya kristo wa uongo na inawezekana na wewe ni mmoja wapo na haujielewi
na unaona wewe ni mkristo safi na unahaki ya kuwa mkristo, fungukeni enyi
wanadamu mimi Hebron nilipotumwa na YESU na alionieleza ni mengi ila
aliponieleza watumishi wamemsaliti sikuelewa vizuri ila aliendelea kunifundisha
mpaka nikamuelewa maana katika ulimwengu huu hata mimi sijawahi kuona mwalimu
anayefundisha kama YESU na unaelewa vizuri.
Akaniambia hivyo
ndivyo watu wanafarijiwa kwa uongo kwa maneno ya kukataliwa kuokoka na
wakiambiwa mimi ndivyo nilivyo. Akaniambia waeleze watu wote wanaotaka kuja
mbinguni mahali nilipo mimi, wapokee kile nilichokileta yaani wokovu peke yake
ndio uzima wa milele na mtu ili anipokee mimi cha kwanza apokee wokovu aokoke,
anapookoka ndipo mimi naingia ndani yake na yeye anaitwa mwanafunzi wa Kristo
aliye hai, na pia akisha okoka aishi maisha matakatifu, na atimize misingi ya wokovu,
ubatizo wa maji mengi na siyo ya kikombe au ya maji ya kisima. Ifanywe kama
nilivyofanya mimi nilipoonyesha njia na pia ubatizwe kwa jina langu tu na siyo
la mchungaji au mtu yeyote yule. Hapo utakuwa mkristo maana aliye mkristo
lazima afanane na mimi kiimani na kimatendo. Sasa watu wengi wanajiita wakristo
lakini hawafanani na mimi kiimani wala kimatendo.
Sasa mpaka sasa umepata picha ili uwe mkristo ni lazima
uokoke na kama haujaokoka wewe siyo mkristo. Nina nukuu maneno alionieleza YESU
kwa kinywa chake, nilirudisha fahamu zangu katika picha halisi ya ulimwengu huu
nilisikia kulia sababu mabilioni ya watu wanajiita ni wakristo wanadanganywa
kwa kupewa mafundisho ya mpinga kristo ili waangamie wasiende mbinguni na
ndivyo ilivyo sasa leo uokoke ili uwe mkristo kamili, na zaidi hayo makanisa
yote ambayo hayakubali watu waokoke hayo yote siyo matawi ya YESU wa kweli
haijalishi wanalitaja jina lake. Alisema YESU msiziamini kila roho bali
zijaribuni, utazijaribu kwa matendo. Sasa kwanza kwa nini hawataki tendo la
wokovu, na pia hata makanisa yao why yanaitwa ya dini? Je YESU alileta makanisa
ya dini? Jibu siyo, YESU alileta wokovu ambalo ndilo kanisa la wokovu sasa watu
wanang’ang’ania makanisa yale ambayo YESU aliyakutaga enzi zile na wakakataa
kutoka huko na kulifuata kanisa la wokovu, ambapo pasipo wokovu hauna haki ya
kwenda mbinguni na huo ndio ukweli 100%. Na shetani bado hakuchoka akajua watu
wanajua wokovu ni kitu cha thamani sana na wokovu ndio ukristo, akayateka makanisa
baadhi ya wokovu na akawaita watumishi ambao ndio watumishi wanaofundisha uongo
katika makanisa yanayojiita makanisa ya wokovu na watu wapo pale wakijua
wanakutana na YESU wa kweli kumbe wanaenda tena kukutana na shetani pasipo
kujua alichokifanya.
Sasa katika makanisa ya kipentekoste katika ulimwengu wote
shetani akaingia ndani yao watumishi wakaanza kufungua makanisa wakisema ni ya
wokovu kumbe siyo kweli ni mahali pa kuwatesea wanadamu na kuwapiga upofu waamini
hapo ndipo wanafika salama, kumbe ndio njia ya jehanamu. Makanisa ya wokovu leo
hii watumishi wengi ndio freemason, ndio waganga wa kienyeji, ndio wafanya
mazingaumbwe, ndio wanaowabatiza watu kwa majina yao, ndio wanaobtiza ubatizo
wa maji ya kisima, ndiyo yanayowafungia ndoa watu kwa agano la shida, ndiyo
yanayofanya nyumba ya MUNGU kuwa sehemu ya biashara na ufisadi. Chunguza huko
ulipo utapata picha ya kweli, sasa na makanisa ya jinsi hii pamoja na watumishi ambao ndio viongozi hao pia siyo
wakristo wa kweli, uchunguze Neno la MUNGU je kinaruhusu hayo? Na ukiona kanisa
la wokovu pia lipo katika mambo ya kifisadi na kutoa huduma kwa pesa, uelewe
hapo hayupo mwokozi YESU na siyo tawi lake bali ni tawi la shetani. Toka huko
muombe MUNGU atakuongoza na kama hakuna pa kwenda wewe endelea kusoma makala ya
Nabii Hebron na vitabu, MUNGU atakutunza na nitaendelea kukuombea maana hata
sasa najua mpo maelfu katika uliwmengu mlio ujua ukweli wa YESU amewafungua fahamu
zenu na hamtaki kurudia matapishi tena, bali mnataka wokovu safi siyo wokovu
feki au wokovu wa kifafa. Na baada ya kuokoka hakikisha unailinda wokovu wako,
maana shetani hapendi mtu aokoke, akiokoka tu anajua tayari huyo ni mkristo wa
kweli wala simpati sasa kazi ni kwako wewe ambaye unaujua ukweli huu ya kuwa
hauwezi ukajiita mkristo bila ya wewe kuokoka sasa chunguza ni wangapi
wanaojiita ni wakristo na hawajaokoka? Ni mamilioni shetani anafurahia atakuwa
nao jehanamu.
NOTE:
SALA YA TOBA
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU NA LEO HII
UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE NAOMBA UNIOKOE NA
KUNIOKOA KWAKO NI MIMI KUUPOKEA WOKOVU TU NA SIYO KINGINE, UNILINDE, UNIONGOZE,
NIFUNGUE NIKUJUE WEWE KRISTO WA KWELI NA NIWE MFUASI WAKO. AMEN.
Baada ya kuokoka sasa wewe ni mkristo, na usiabudu mahali
popote ambapo siyo kanisa la wokovu, na kanisa hata la wokovu ukikuta tu tayari
ni michango na kutafuta pesa ondoka maana hakuna tena wokovu imekuwa ni dini,
na hii ndio njia ya shetani aliyotumia pia kuyateka makanisa ya wokovu na kama
yametekwa uelewe hayo tayari siyo tena makanisa ya wokovu haya yamekuwa
makanisa ya dini tu. Na pia muwe makini katika makanisa yote ya wokovu, ukiona
kuna bendera ya aina yeyote sasa ufunguke hizo bendera zinazo maana yake na ni
maagano ya kuzimu hata ikiwekwa ya nchi. Mimi nakueleza uelewe, hizo bendera
zinakuwa na majini na pia ni ishara ya ufalme wa giza unatawala hapo na ndio
unaotenda kazi na siyo MUNGU sasa uelewe. Na unaweza ukadanganywa eti zinapokaa
kanisani ni tunaziombea hizo nchi. Rudi katika neno imeandikwa hata katika
nyumba ya MUNGU kisiwekwe kitu chochote kwa ishara yeyote, inapokuwa hivyo hiyo
ni sanamu. Na pia imeandikwa katika nyumba ya MUNGU ni mahali pa sala tu, na
pia imeandikwa ya Kaisari mpe Kaisari na ya MUNGU mpe MUNGU. Na zaidi endelea
kusoma makala yangu utaendelea kujua mengi na kuponywa roho yako na pia karibu
katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, ili uupokee wokovu
wa kweli kutoka kwake mwenyewe. Na ukamilike uwe mkristo sasa wa kweli,
ubadilike.
Wote nawasii sana muokoke leo hii na ndipo utakuwa mkristo
na kama hujaokoka uelewe mpaka sasa wewe siyo mkristo, iwe ni askofu, mchungaji
au mtumishi unayeona unafanya kazi ya kanisa elewa unamfanyia shetani ambaye
ndiye kristo wa uongo. Soma Mathayo 23: 1-37, huu ndio ukweli.
SWALI: umeshajua wewe upo katika kundi gani la ukristo?
Je ni
ukristo wa kweli?
Je ni
ukristo wa kipagani?
OKOKA
SASA ILI UWE MKRISTO.
NABII HEBRON.