Nilipoonyeshwa kitengo kingine cha shetani niliwaona malaika
zake wakimsifu na kumuabudu wakishirikiana na serikali yote ya shetani nyimbo
ambazo wao wanasema ni roho mtakatifu wao akiwaingia mapepo ambaye ndiye roho
mchafu akiwaingia kwa nguvu wakati wakimsujudia shetani na joka kuu.
Joka kuu huwavuvia nguvu zake ameiga kama vile watu
wanavyoshukiwa na ROHO MTAKATIFU wanaanza kunena kwa lugha, na joka kuu
huwavuvia nguvu zake na wao huanza kuimba RAP, kama vile huku ulimwenguni watu
wanavyoimba miziki ya RAP ni hivyo hivyo, na wanadamu wanaoimba RAP na wenyewe
wamevuviwa nguvu kutoka kuzimu wanaanza kufoka foka, na wanapoziimba
mnaunganishwa na wakati wa sifa za kuzimu, na asili ya RAP music ni kuzimu na
wote wanaoimba nyimbo hizo mapepo ya roho mchafu yanawaingia na kuwapa mafunuo
wa miziki hiyo na kuwakamata vijana wa leo. Kama ilivyo sasa badala ya vijana kujazwa
nguvu za ROHO MTAKATIFU vijana wengi wanajazwa nguvu za roho mchafu kupitia
hizo nyimbo za RAP na kila muimbaji anapewa uwezo wake tofauti na mwenzake kwa
jinsi alivyoshukiwa na hiyo nguvu ya roho mchafu.
Mziki wa RAP umebuniwa na kutumwa ulimwenguni ili kuwakamata
vijana wasimpokee ROHO MTAKATIFU na shetani anausambaza kwa speed zaidi na hata
watu wengine uuita mziki wa kizazi kipya (kwenye ulimwengu wa roho ni mziki wa
kizazi cha nyoka) yaani shetani. Madhara ya nyimbo hizi kila mwanamziki
anayeimba RAP jina lake lipo katika ufalme wa shetani na anayeimba nyimbo hizo
yeye ni agent wa shetani ili kuhakikisha watu hawampokei ROHO MTAKATIFU ili
wapone roho zao bali wampokee roho mchafu ili wafe roho zao na matendo ya uovu
yazidi kufanywa. RAP ni uovu mtupu na kujitenga na MUNGU, ila kama mlikuwa
hamjui eleweni na muwaeleze na wenzenu. Mnapoimba nyimbo hizo mnaunganishwa na
kipindi cha kumuabudu shetani na unatekwa bila kujua, ila wapo wanaoimba nyimbo
hizo na ni maarufu sana katika ulimwengu huu wao huenda kabisa kuzimu na kupewa
hizi nyimbo na lusifa na wengi wao ni wanachama wa freemason.
NOTE:
Kama unataka kupona wacha kuimba miziki yeyote ya kidunia na
zaidi utashangaa na makanisani wameanza kuimba nyimbo kwa mitindo ya RAP eti
wanasema wanaenda na wakati. Mmepotea na nyie mmeunganishwa na kuzimu na ndiyo
maana makanisa mengi shetani ameyatawala, ni sababu ya nyimbo za kidunia
wanaiga. Na jambo lingine watumishi waimbaji wanatumia nguvu za giza wengi sana
90%. Wanapokuja kuziimba katika makanisa wanaunganisha makanisa na kuzimu
pasipo hata watu kujua. Muwe makini na mumkatae shetani na yeye atawakimbia.
NABII HEBRON.