Ujumbe huu ambao nawaeleza ni YESU WA NAZARETI ndiye
aliyenionyesha na mimi nikawaona kwa macho yangu, japo inatisha ila
nitawaelezea kwa kifupi na sababu ya mimi kuonyeshwa ni ili niwaeleze ulimwengu
wote wajirekebishe na wamrejee YESU WA KWELI na siyo wa uongo na kuzifuatia
hadithi za uongo na elimu ya uongo katika makanisa yote. SOMA 2 Timotheo 4:
1-4.
Mnamo 2013 BWANA YESU alinichukua akanionyesha picha ya
kuzimu jinsi ilivyo halisi na waliopo huko ambao wanasubiri hukumu na mlango
wao kwenda mbinguni umeshafungwa. Niliona ofisi za kuzimu na serikali zake, kwa
vitengo mbali mbali, ila nitaelezea kwa kitengo cha kanisa cha kuzimu. Ipo
wizara ya kanisa la kuzimu na ndiyo inayowapa watumishi wa kipepo nguvu za
miujiza ya shetani na kuwapa vyeo kwa kufananisha na huduma tano za kanisa.
Shetani amecopy kila kitu na yeye akawaita wa kwake wachungaji, manabii,
mitume, waalimu, wainjilisti. Ila wewe kwa macho yako ya nyama ya kibinadamu
hauwezi kuwajua maana hata mimi Hebron sikuweza kuwajua miaka yote mpaka
aliponifundisha YESU mwenyewe, maana mimi kazi yake ananifundisha yeye peke
yake, na wala sijaenda chuo chochote cha kibinadamu katika ulimwengu huu.
Ilipofika wakati wa kunionyesha watumishi waliopo kuzimu
niliona ni mamilioni ya watu, nikamuuliza YESU hawa si watumishi wako mbona
wapo huku badala ya paradiso. Akaniambia, mwanangu Hebron nimeamua nikuonyeshe
uyaone na wewe, nilikuisha kueleza katika siku za mwanzo 2010 nilipokutana na
wewe tukiwa wawili tu, nilikuambia nataka mwili wako tu nipeleke injili yangu
mimi peke yangu nitaishi ndani yako. Hao niliowatuma wamenisaliti mimi wameamua
kumfuata shetani, ila hapa ulimwenguni kimwili hunitaja kwa midomo yao ila
ndani ya mioyo yao ni mbwa mwitu. Mimi niliwaita watumishi wachache tu na siyo
wengi kama inavyoonekana katika ulimwengu huu. Wengi wamejiita, wanajifanya,
wanatafuta pesa, wengine ni wa kanisa la kuzimu. 98% ya watumishi wote
ulimwengu huu siyo watumishi wangu mimi YESU WA NAZARETI ni watumishi wa kristo
wa uongo.
Akanionyesha mmoja wa waanzilishi wa dini katika ulimwengu
huu na alikuwa amefungwa mnyororo mkubwa katika kiuno kwenye mhimili wa chuma,
nikamuangalia kwenye paji la uso wake nikaona jina lake Martin Luther,
nikashtuka maana mimi kwa akili zangu nilijua atakuwa paradiso. Akaniambia,
usiogope, nikamuuliza YESU huyu anafanya nini huku na ni mtumishi wako,
akaniambia, Hebron huyu sijamuita anitumikie na wala hata katika kitabu cha
listi ya watumishi waliotoka kwangu huyu hayupo, wala sijamtuma. Niliogopa
zaidi, akaniambia huyu amefanyika kuwa geti la kuwazuia watoto wangu wasije
mbinguni akianzisha dini yake ambayo mimi sijamtuma na kama sijamtuma ujue yupo
aliyemtuma, akampa maneno yake na uwezo wa kufanikisha kusudi hilo. Akaniambia,
Martin Luther ningekuwa ni mimi nimemtuma angelitenda Neno langu. Akaniambia,
Hebron, ubatizo wa maji ya kikombe umetoka kwa MUNGU? Nikajibu hapana,
akaniambia hilo ni moja uelewe, alichokianzisha siyo Neno langu, pili mimi
nilionyesha njia nikiwa mtoto mdogo nilibarikiwa tu na nilipokuwa mtu mzima
ndiyo nilibatizwa, ila yeye ametenda kinyume na ubatizo wangu. Akaniambia, mimi
sijaruhusu sadaka ya ahadi na collect, akanimabia sadaka ya ahadi ni agano kati
ya mtu na Martin Luther ya kuwa wewe ni wa Martin Luther na mtu siyo wa kwangu.
Akaniambia hivi watu wanatakiwa waitwe kwa jina langu au kwa
jina la mtumishi? Nikamjibu wanatakiwa waitwe wakristo, sasa kwa nini hawa
wanajiita ni wakristo halafu wanajiita kwa dhehebu la aliyelianzisha? Akaniambia
ukijiita kwa jina la aliyeanzisha dhehebu ina maana wewe ni wake na mimi YESU
sikupati wewe na hata ule mwisho nikija nitakuja kuwachukua wale waliookoka na
ni watakatifu tu ndiyo nitakaowachukua, ila kila aliye kinyume uwaeleze watu
wote na kwa mataifa yote sitamchukua mimi YESU sipo kinyume na BABA yangu letu
ni moja. Waeleze mimi sijaanzisha madhehebu wala dini. Dini na madhehebu
yalikuwepo hata kabla yangu mimi YESU kuja kimwili ulimwenguni. Na kazi ya dini
siku zote ni kubadilisha Neno la MUNGU na kuweka uongo ndani yake, kama ilivyo
ubatizo wa uongo, ubarikio wa uongo, hayo yote ni maneno ya shetani
yaliyoingizwa katika makanisa ili kuwapiga watu upofu wapotee kama ilivyo sasa.
Nimekufunulia siri hii na wewe uwaeleze watu wote na mimi
ninaangalia kila anayeusoma ujumbe au kuusikia asipotii haya ajue na yeye
ataungana na Martin Luther katika mateso milele. Akasema kwa hasira kweli, OLE
wao na hao waliopo hai katika ulimwengu wanaobadilisha Neno langu na
kusimamisha mizizi ya shetani ndani ya mioyo yao, waeleze na wao mahali pao ni
kuzimu. Ila wapo ambao hawajui Neno langu na wengine wanajua kabisa wanafanya
makusudi. Waeleze wanirejee mimi wafuate njia zangu, kinyume na hapo Jehanamu
inawahusu. Nikamuuliza mbona Martin anajulikana ni mtu maarufu katika
ulimwengu? Akaniambia, kwa MUNGU ni haki peke yake na utakatifu, ghafla
akanionyesha watu maarufu waliokufa wakiwemo maraisi, wafalme mbali mbali
akiwemo Herode, matajiri maarufu, akaniambia angalia na hao wapo wapi?
Akanimabia hawakuwa watakatifu na hawakuokoka. Akaniambia pando ambalo mimi
sikulipanda nitaling’oa na kulichoma moto liteketee, mafundisho ambayo
hayajatoka kwangu na kila aliyeanzisha watu wakayafuata hao wote mahali pao ni
jehanamu, na wote wanaoendeleza mafundisho ya uongo watajumuika nao hapa hapa
kuzimu. Akaniambia, ujumbe wangu uufikishe tena haraka, nikasema ndiyo BABA,
nami nawaeleza watu wote jamani okokeni kikweli, kuzimu kuna mateso
yasiyoelezeka na Malaika Gabriel yupo makini kuchukua roho itokayo kwa mtu
wakati wa kufa anaipeleka kwenye matendo yake, kama ni matendo ya giza ni
kuzimu unasubiri jehanamu, kama ni mtakatifu utakaa paradiso ukisubiri ule
mwisho ila hauteseki unakula raha.
Akanimabia, waeleze mtu anapokata roho tu ndiyo mwisho wake
anapelekwa kule alichokipanda ndicho atakachovuna. Ila watu wameletewa
mafundisho ya uongo wakifa wataombewa ili wapokelewe, akanieleza, waeleze hao
wote ni waongo ndani yao ipo roho ya mpinga kristo ili kuwazubaisha watu
wasinijue mimi YESU na wasifike nilipo mimi. Waeleze mataifa yote wanirejee,
muda wangu umekaribia kurudi kwa mara ya pili, ila watu wengi ni wa shetani.
Makao nimeshayatengeneza kama nilivyoahidi naenda kuwatengenezea makao, ila
haya makao hayana watu wa kukaa, waeleze watakaokuja kwenye makao niliyoyaandaa
ni wale walio wangu tu. WAMEOKOKA NA WATAKATIFU 100%. Wengi watalia na kusaga
meno maana nitawaambia sikujui sikujui, sababu ya matendo yao. Na zaidi YESU
akaniambia madhehebu na dini siyo matawi yake ni matawi ya shetani na kila tawi
ambalo silo lake yeye hulikataa. Akaniambia ndiyo maana Martin Luther yupo huku
kuzimu sababu siyo tawi langu, niliogopa zaidi maana sikuyaelewa haya, waeleze
atakayesikia atapona atakayepinga na yeye ule mwisho wake ataungana nao na
kufungwa minyororo kuzimu.
SALA YA TOBA:
YESU WA NAZARETI NAOMBA UNISAMEHE UNIANDIKE KATIKA KITABU
CHAKO CHA UZIMA WA MILELE, UNIONGOZE MILELE NISIPOTEE, AMEN.
NABII HEBRON.