Enyi mataifa nawasihi mrejeeni MUNGU wa kweli na muokoke na
kuishi maisha matakatifu ambayo ndilo kusudi la MUNGU, na ukitenda wema na
kuokoka kikweli hakika hautaenda kuzimu baada ya wewe kufariki. Wakati wako
ndio huu sasa, ukishakufa basi hauna nafasi tena ya kutubu sababu roho yako
itapokelewa kuzimu, maana mtu apandacho ndicho avunacho. Usidanganyike utaombewa
ukifa, mabilioni ya watu mbali mbali waliokufa tayari wapo kuzimu yamkini hata
ndugu zako.
Nilichoonyeshwa na YESU WA NAZARETI na nikapiga hesabu ya
kibinadamu nikakuta kila familia katika watu waliokufa katika kila familia 97%
wapo kuzimu. Nilianza kwa kuangalia katika familia yangu, wengi waliokufa
nimewaona kuzimu na walikuwa ni wakristo. Nikaangalia baadhi sehemu mbali mbali
mambo ni hayo hayo tu. Niliogopa sana, akaniambia YESU nilitaka uyaone haya
halafu ujue jinsi watu wanavyovunwa na shetani. Akaniambia MUNGU ni wa haki
haangalii umaarufu wako, yeye anaangalia wokovu tu na utakatifu maana hivyo
ndivyo alivyowaamrisha na alinituma mimi na nikaja hapa ulimwenguni nikaulete
wokovu ambao ndiyo njia ya uzima. Akaniambia MUNGU hana dini yeyote, dini zote
siyo yeye amezianzisha ni wanadamu kwa akili zao. Akanionyesha mbinguni sikuona
majina ya madhehebu yeyote ambayo yapo hapa ulimwenguni, niliona wokovu na
utakatifu peke yake.
Akanionyesha viongozi wote waasisi wa madhehebu yote sura
zao na kwa majina yao wamefungwa minyororo wanasubiri ule mwisho wa dunia
wachomwe moto, niliogopa. Akaniambia Hebron, usiogope hawa wote sijawatuma mimi
kuanzisha haya madhehebu, kumbuka hata mimi nilivyokuja hapa ulimwenguni
niliyakuta, angekuwa ni BABA yangu kayaamrisha yeye asingenituma mimi nije
katika ulimwengu huu tena. Akaniambia hawa ndio wamefanyika kuanzisha matawi ya
shetani wakitumia jina langu na kulibadilisha Neno la MUNGU na watu wakawaamini
nakuwafuata na kushiriki uongo. Nilizidi kuogopa sana, maana sikuyajua hayo, na
katika dhehebu nililokuwa mshirika tokea kuzaliwa kwangu, nikamuona huyo muasisi
na cha ajabu hapa duniani watu wanamsifu na wanasema tufuate nyayo zake, kumbe
wanafuata alipo na yeye. Akaniambia madhehebu na dini zilianzishwa na shetani.
MUNGU hana dini yeye aliamrisha wokovu na utakatifu peke
yake kupitia mimi YESU ambaye ndiye njia ya uzima ili kila atakayenifuata
atafika nilipo mimi, na hao wasionifuata mahali pao ni hapo ulipopaona. Akaniambia
nenda uwakomboe watu na mataifa yote na uwaeleze ukweli na mimi nipo na wewe,
muda wangu umekaribia kuja nahitaji uwalete watu wengi Kaanani katika nchi ya
Ahadi. Nitaeleza kwa ufupi maana ni mambo ya kutisha na jinsi watu
wanavyoteseka kuzimu wanatumikishwa mateso ambayo hapa ulimwenguni hakuna. Na vyakula
wanavyokula kuzimu ni nyama za watu waliokufa ambao hawajaokoka kikweli na
ambao hawajaokoka kabisa, ndiyo chakula chao. Na hutumia mafuvu ya vichwa vya
watu kama sahani za kuwekea chakula.
WALIOPO
KUZIMU
1.
Wanajimu wote waliokufa na waganga wa kienyeji,
washirikina.
2.
Viongozi wote waasisi wa dini zote na madhehebu.
3.
Maaskofu, Wachungaji, Mapadre, Mashehe, Maimamu,
PAPA wote waliofariki, Wainjilisti, Waalimu, Manabii, Mitume maarufu katika
ulimwengu huu kwa majina yao waliokufa. Na watu wote wa nchi zote waliokufa
bila kuokoka na kuishi maisha matakatifu wote wapo wanateseka.
4.
Wanamziki wote waliokufaga walioimba nyimbo za
kidunia hawaendagi mbinguni; mpaka waokoke na waache kuimba hiyo miziki wakiwa
hai, haijalishi wanajiita wakristo.
Kila mtu anayeimba miziki ya kidunia au kuicheza au hata
ukienda disko, unapoimba hizo nyimbo unakuwa unamtukuza aina ya mungu anayeitwa
mziki. Yupo mungu mziki na ndiye anayewapa wanadamu nyimbo ili waziimbe na
wanapoziimba wanakuwa wanamtukuza yeye, na hivyo kuwafanya wanadamu wote
wanaoimba miziki ya kidunia watu hao wanakuwa wapo chini ya mungu wa kuzimu na
anacho kibali kabisa ya kuwachukua kuzimu maana wanamtukuza yeye kama mungu
wao, ila wanamziki hawajui haya yamefichika, YESU kanifunulia niwaeleze mpone.
Ukisikia sikia, ukikaza shingo ukifa utawafuata wengine
waliokufaga wote. Baadhi ya wanamziki maarufu waliyopo kuzimu na wanateseka
mpaka sasa yupo Bob Marley, Lucky Dube, Pepe Kale, Kanumba na wengine wengi
maarufu wapo wanateseka mateso yasioelezeka, ni maelfu ya wanamziki, na hata
hawa waliopo duniani majina yao yapo kuzimu wanasubiriwa wakifa tu waende
mahali yalipo majina yao. Pia waigizaji wa sinema maarufu wapo, wachezaji
maarufu wapo na wote waimbaji wa miziki ya injili wanaotumia uchawi au nguvu za
giza.
Wapo mawaziri, wabunge, viongozi mbali mbali wa nchi mbali
mbali na watu maarufu waliokufa.
AFRIKA
1.
Mawaziri wote wakuu waliokufaga wapo kuzimu
wanateseka.
2.
Maraisi tokea 1949-2014, hakuna aliyeenda
Paradiso wapo kuzimu wanateseka, wanatumikishwa na wanalia lakini msaada
hakuna, wanafanyishwa kazi ngumu, wanachapwa bakora.
AMERICA, EUROPE, ASIA na mengine yote hali ni hivyo hivyo na
inavyoonyesha walifikiri starehe walizokuwa nazo hapa ulimwenguni wakifa
wataenda nazo wakamsahau Mwenyezi MUNGU na kumrejea yeye. Na wengine hata sijui
majina yao ila ni sura zao wapo pamoja katika kundi la mateso. Yupo OSAMA,
HITLER, IDDI AMINI, GADAFFI, SADAMU HUSSEIN, SAVIMBI na sababu wengine sijui
majina yao niliona nchi zao inatimia 99% ya wote viongozi waliofariki tokea
ulimwengu uumbwe wapo kuzimu hata Farao wa Misri yupo kuzimu.
NOTE:
Nawasihi watu wote wa ulimwengu huu mrejeeni YESU WA
NAZARETI yeye ndiye tiketi salama, na uhakikishe unampata YESU wa kweli maana
hata waliopo kuzimu walikuwa na yesu ambaye ni wa uongo na ndiyo maana
wanateseka. Yapo majeneza ya shetani katika ulimwengu wa roho yanawinda
wanadamu ili wakupate, na salama yako ni wokovu tu na utakatifu wa ukweli. Ni mabilioni
ya watu wanavunwa na shetani kila siku, kila saa, je na wewe upo wapi? Uwe mjanja
uokoke, waliopo kuzimu hawakuwa wajanja walipokuwa hapa ulimwenguni, ndiyo
maana wamenaswa katika huo mtego. Mpokee YESU usikamatike na uwe makini
usimpokee yesu wa uongo anakaa katika watumishi wa pesa, michango, harambee,
ubatizo wa maji ya kikombe, masanamu, umchunguze anayekuongoza matendo yake.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NAJIKABIDHI
KWAKO, UNIANDIKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHAKO CHA UZIMA, MIMI SIMTAKI SHETANI
TENA, MIMI NI MALI YAKO. AMEN.
NABII HEBRON.