Katika ulimwengu huu tunao ubatizo
wa kweli ambao uliletwa na Yohana ambaye ndiye aliyetumwa na MUNGU kuanzisha
huduma ya ubatizo kutoka kwa MUNGU. Na ubatizo huu ni ubatizo pia aliobatizwa
YESU WA NAZARETI, ukisoma katika kitabu cha Mathayo 3: 13-17 inaelezea vizuri
kabisa. Neno ubatizo ina maana kuzamishwa katika maji tena mwili wote na
ubatizwe kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU. Ukisoma biblia yote utaona
ni ubatizo wa maji mengi peke yake tu ndio ubatizo uliotokea kwa MUNGU na unaelezea maelezo yake jinsi ipasavyo watu
wabatizwe na hata katika injili ya Mathayo 28: 18-20 YESU anawaeleza wanafunzi
wake na ukisoma katika injili ya Ufunuo wa Yohana 22: 18-20 ole wake atakayeongeza
maneno ya unabii wa kitabu hiki au kupunguza hakika sehemu yake ya uzima
itaondolewa na MUNGU.
Watumishi wengi na makanisa,
madhehebu mengi katika ulimwengu wote wameongeza maneno yao katika injili na
wengine wanayapunguza ili kuficha maana ya Neno la MUNGU. Hawa wote hii ni
picha halisi tokea hapa ulimwenguni tayari sehemu yao ya uzima haipo wala
safari yao siyo ya mbinguni bali ni safari ya jehanamu. MUNGU anaangalia Neno
lake, haijalishi sehemu nyingine wanafuata biblia na sehemu nyingine wanabadilisha.
MUNGU siyo wa michanganyo, yeye ni MUNGU mkuu (ALPHA NA OMEGA). Wewe mwanadamu
ni nani hata umchanganye MUNGU? TUBU, kuchanganya Neno la MUNGU na uongo ni
kumtukana MUNGU na kumdharau. Nawaeleza wazi watu wote mnaolibadili Neno la
MUNGU au kulipunguza wote mmemtukana MUNGU, na yeye MUNGU 2013 alisema na mimi
akaniambia mimi ni MUNGU wala zaidi hayupo na hatakuwepo. Kama mimi sina mwanzo
wala mwisho, je Hebron kwa nini wanadamu wananitukana? Nikanyamaza kimya maana
nilijua wametumia lugha chafu kama vile watu katika ulimwengu huu wakitukanana
wenyewe kwa wenyewe, akaniambia siyo maana alijua ninawaza nini, kutokana na
alivyoniuliza. Akaniambia hata wewe Hebron, ukienda kinyume na Neno langu
utakuwa umenitukana, niliogopa, akaniambia waeleze watu warejee kwangu na njia
ya YESU WA NAZARETI atakayewafikisha kwangu. Watu wote wanaobatiza ubatizo
ambao sijaagiza mimi hao wananitukana au kuvunja sheria zangu.
Nitaelezea kwa kifupi mpaka
katika makala nyingine. Hayo yote ni MUNGU ndiye anayenifundisha ili niukomboe
ulimwengu, yeye yupo ndani yangu. Sasa enyi watu wote huu ni wakati wa kujua
kweli yake maana wapo watu wa matabaka mawili. Wapo wanaompenda MUNGU na wapo
wanaomchukia kabisa, ila wanampenda lusifa. Na lusifa na yeye anao ubatizo wake
(Namba 666) ile unaingia katika paji la uso katika roho na ubatizo wa lusifa
(freemason) au mpinga kristo ni huu. Unabatizwa ubatizo wa maji ya kikombe
kichwani tu na ubatizo mwingine wa freemason ni ubatizo wa maji mengi ila ni ya
kisima, hayatembei, na ubatizo mwingine wa freemason ni ubatizo wa kubatizwa
kwa jina la mchungaji haijalishi ni ubatizo wa maji mengi huo ni ubatizo wa
freemason. Ili uwe mkristo ni lazima uokoke na ubatizwe ubatizo wa maji mengi
(SOMA KITABU CHA UBATIZO WA KWELI KWA ULIMENGU WOTE CHA NABII HEBRON) inaelezea
kwa undani na utaelewa na hakuna cha kubisha kitakuweka huru. Sasa shetani
anazo trick nyingi na amelipiga kanisa upofu kabisa sababu watumishi
wamemsaliti wakayapokea ya shetani badala ya kutenda maneno ya MUNGU. Wewe
mwenyewe kibinadamu unajua ubatizo wa kweli ni wa Yohana wa maji mengi. Sasa
huu ubatizo wa maji ya kikombe nikuulize upo katika Neno la MUNGU? Jibu haupo
(haya ndiye maneno ya shetani sasa).
Kama huu ubatizo ni tofauti na
ule ubatizo wa Yohana tayari umekwenda kinyume na Neno la MUNGU, unalifuata
neno la shetani na ukalikubali hivyo na wewe unafanyika kuwa mwana wa shetani
au unakuwa na wewe ni freemason bila kujua na matokeo yake katika ule mwisho na
wewe unaingia jehanamu, maana akija YESU katika ule mwisho anakuja kuwachukua
wale walio wake, ni alama yake atakayoiangalia, ni ubatizo wake yaani chapa
yake ambayo ndiyo Yohana alimbatizia pia YESU. Kama ukiwa na ubatizo tofauti na
wa Yohana hatakuchukua na pia hata waliokufa kama hawajabatizwa ubatizo wa maji
mengi habari ya mbinguni na hiyo waisahau. Na katika ulimwengu huu na mataifa
yote wakristo wengi wanapinga jambo la freemason na hawataki kabisa ila pia
wapo wanaoitaka na kuupenda ufreemason.
Naelezea kwa hawa wanaompenda
YESU na hawajijui kumbe na wao tayari ni freemason bila kujua. Kama unabatizwa
ubatizo tofauti na YESU, tayari na wewe unayochapa ya freemason (666). 98% all
over the world shetani ameliteka kanisa, na YESU amenitoa katika kazi yangu ya
professional driver nikiwa Serengeti,
akaniambia nautaka mwili wako niupeleke ujumbe wangu na niukomboe ulimwengu
maana watu wanaona wapo sawa na kumbe tayari shetani amewateka, sasa jichunguze
kama na wewe siyo freemason, tena bila kupenda, ukawekewa chapa ya 666, ukijua
ndiyo ubatizo wa kweli na ndiyo alama ya YESU WA NAZARETI na ndiyo alama ya
mkristo. Freemason wameliteka kanisa na wamejiekea mizizi na kuwafunga watu
akili zao wasielewe hata Neno lilivyo wazi la ubatizo, badala ya YESU kuwawekea
watu chapa zake sasa freemason ndiyo anayewekea chapa zake kwa wingi na
wakristo idadi 90% wanapigwa chapa ya freemason na namba 666, bila kujua na hao
watumishi wanaobatiza na kupiga chapa 666 ubatizo wa maji ya kichwa hawa ni
watenda kazi wa shetani japo wapo wanaofanya bila kujua sababu ya mapokeo. Ila
ili upone utoke huko na ukabatizwe kwa maji mengi ufutwe chapa ya freemason ili
uwe mkristo wa kweli.
NOTE:
Ø Chunguza
hata wewe mwenyewe na ujiulize ni kwa jinsi gani wakristo wengi wanabatizwa
tofauti na YESU. Hii ni sababu shetani ameliteka kanisa alishirikiana na roho
za watenda kazi wake freemason.
Ø Na kama
umebatizwa ubatizo tofauti ujitambue wewe ni freemason sio mkristo wa kweli.
Ø Freemason
wao wanamuamini shetani na wanamuona YESU ni mbaya na wanaamini eti YESU ndiye aliyemfitini
lusifa akafukuzwa mbinguni na MUNGU, wakati ukweli ni huu; Lusifa alitaka
ampindue MUNGU ndipo akatupwa na kutolewa mbinguni. Joka kuu ambaye ndiye baba
yake shetani. Sasa lengo la freemason ni kupinga Neno la MUNGU na kulibadilisha
ili wale wote watakaoamini au kuyafuata katika kanisa na wao wanaunganishwa na
freemason. Sababu wana uhalali maana umebatizwa tofauti na Neno la MUNGU. Ila
amua usiwe tena mfuasi wa freemason, ubatizwe ubatizo wa kweli, na kama mpaka
sasa haujabatizwa ubatizo wa maji mengi akija YESU au ukifa hauendi mbinguni.
Jichunguze, jibu unalo. Elimu
hii siyo kutoka katika akili yangu nimeelezwa na YESU WA NAZARETI. Anawapenda watu
msipotee, yatunze maneno haya ni uzima na uwaeleze na wengine. Soma zaidi blog
yangu na zaidi karibu katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA
YOTE. Ipo shule ya mbinguni.
NABII HEBRON.