Kila mtu anajua kuwa YESU WA NAZARETI ni mwana wa MUNGU wa
pekee na hakuna mwana mwingine wa pekee kutoka kwa MUNGU katika ulimwengu huu na
yeye ndiye mkombozi wa pekee zaidi yake hakuna wote ni waongo na zaidi
alitabiriwa atazaliwa na atakufa na kufufuka na kupaa na ikatokea. Na sasa
tunasubiri Neno la MUNGU litimie kwa kurudi mara ya pili ambao ndiyo mwisho. Katika
ulimwengu huu wapo watu wanaosulubishwa msalabani eti wanajitolea kila mwaka
wasulubishwe badala ya YESU, na wanaokubali kusulubishwa wanaona wanatenda
vyema kabisa ila nawaeleza watu mnaojisulubisha badala ya YESU wote mmemkufuru
MUNGU. Kwa kufanya hivyo ina maana unalipinga Neno la MUNGU, aliposema kwa
kupigwa kwake sisi sote tumepona.
Pili haijaruhusiwa katika Neno la MUNGU eti wanadamu
wasulubishwe badala ya YESU, wakati MUNGU alimtoa mwanae aliyempenda aje atufie
sisi msalabani ili tupone. Sasa jiulize huyu mwanadamu anayesulubishwa
msalabani yeye anasulubishwa kwa ajili ya nani tena? Jibu hakuna, anajitesa
bure na zaidi amezidi kumkosea MUNGU na kupinga Neno La MUNGU au kulibadilisha
Neno la MUNGU. Na zaidi YESU kusulubiwa ilikuwa ni ahadi ya MUNGU. Je hawa
wanadamu wanaosulubiwa wakati wa Pasaka kwa niaba ya YESU je, ni ahadi ya
MUNGU? Jibu siyo. Na kama siyo ahadi ya MUNGU ya nini kumkufuru MUNGU? Kama ulikuwa
hauelewi tubu sasa na uache.
NABII HEBRON.