Nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye hai na
ndiye aliye mwana wa MUNGU wa pekee na mpaka sasa hajatokea kama yeye na
hatatokea mwingine zaidi yake. Siku ya Pasaka 20.04.2014 aliniambia Hebron
najua leo mnasherekea siku ya ushindi ambayo mnakumbuka nilipoteswa na kuzikwa
na nikafufuka ili muwe huru. Akaniambia nakutuma kwa watu wote na mataifa yote
uwaeleze kila mtu abatizwe ubatizo wa maji mengi kama nilivyobatizwa mimi
katika maji yanayotembea, na pia waokoke na kuishi katika utakatifu siku zote,
mimi nakaribia kurudi nitakuja kuwachukua wale tu waliobatizwa kwa ubatizo
niliobatizwa mimi ambao ndiyo ubatizo wa MUNGU ambao pia ndiyo Yohana
alianzisha hapa ulimwenguni na mimi YESU nilibatizwa hivyo hivyo, pia
nitawachukua waliookoka na kuishi maisha matakatifu peke yake.
Kwa hiyo kila mtu ajichunguze je haya mambo matatu
umeyatimiza? Na je unaishi katika maisha matakatifu? Au umeokoka na bado unatenda
dhambi? Haitakiwi uwe na doa lolote huu ndio ukweli na usidanganyike ukifa
utaombewa ndio uende mbinguni, wakati wako ndio huu wewe uliye hai na MUNGU
huwasikiliza walio hai sababu yeye ni MUNGU aliye hai, na kama ni MUNGU aliye
hai basi yeye siyo MUNGU wa wafu. Msitende dhambi, jitengeni na tabia za dunia
hii. Akaniambia yeye alikufa msalabani
na aliubeba msalaba ili wewe usibebeshwe tena msalaba! Watu wote msibebe
msalaba maana YESU alishabeba, unapobeba unakuwa unampinga yeye neno lake. Hata
mashingoni msivae wala kutembeza katika eneo lolote MSALABA SIYO YESU. Mnatakiwa
mumuinue YESU na jina lake na ukuu wake peke yake, ila watu wanainua misalaba
kitu ambacho ndicho kilicho muulia YESU; huko ni kumuinua shetani na hata
kaburi lake haupaswi kuliinua maana kaburi lake alilozikiwa siyo MUNGU, wala
msalaba siyo MUNGU.
Hapa ndipo shetani alipo wateke wanadamu fahamu zao
wakajiona wapo salama katika nuru, kumbe wapo katika giza la shetani. Ibada za
misalaba, kubeba misalaba shingoni na kuibusu huu ni upofu ulioletwa na shetani
ili watu wasiliinue jina la YESU na badala yake fahamu zao na akili zao
zikatekwa katika vifaa vilivyomuulia YESU na kuzikwa! Kama ni mwanadamu mwenye
akili timamu hata ukifikiria utajiona unakosa kubwa la kumkufuru ROHO
MTAKATIFU. Kwanza imeandikwa msiabudu chochote wala kuisujudia
kilichotengenezwa na mwanadamu pia hata alivyoviumba MUNGU, ikiwemo nyota, mwezi na vinginevyo. Tazama
sasa utaona ulivyotekwa na shetani, ondokeni huko mkatengwe na uovu maana mahali
penye sheria hizo ni mahali pa muovu shetani au mpinga kristo.
Anarudi YESU, tazama hata kipindi cha kina Nuhu alitumwa na
akayasema tubuni, acheni uovu, wakamcheka wakamtukana na kumuona
amechanganyikiwa, nawaeleza tena hivi ndivyo itakavyo kuwa katika KIAMA
nawasihi OKOKENI moto ni mkubwa wa jehanamu aliotengenezewa shetani na wale
watakaofuata matendo ya shetani (dhambi). Ukibatizwa ubatizo tofauti na
aliobatizwa YESU ujue unayo dhambi, usipookoka ujue unayo dhambi tayari maana
ameagiza watu wote waokoke na kumpokea yeye. Usipoishi maisha matakatifu ujue
ni dhambi. Mimi Hebron mwanzoni sikuyaelewa haya ila aliendelea kunifundisha na
mimi nawaeleza ili mpone maana hakuna mwalimu zaidi ya YESU WA NAZARETI na pia
uelewe pia ukiona mafundisho tofauti na neno la MUNGU aliye hai uelewe pia
mafundisho hayo yanatokea kwa yesu wa
kuzimu ambaye ndiye yesu wa uongo hivyo anaingia ndani ya watumishi akawapatia
elimu yake ya uongo na wakaisambaza katika makanisa mengi katika ulimwengu huu
na watu wakaipokea ile elimu ya uongo. Mfano rahisi elimu ya ubatizo wa maji ya
kikombe, tafuta katika biblia yote haupo na kama haupo sasa unatoka wapi? Jibu,
unatoka katika kitabu cha yesu wa uongo na watu wote waliobatizwa ubatizo wa
kikombe hataenda hata mmoja, sawa sawa na alivyonieleza YESU peke yake, na wewe
uwaeleze watu hata uwaforwadie watu ili wapone roho zao na zaidi usome katika
kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE, nilichokiandika mimi Nabii
Hebron, ingia katika blog na website www.prophethebron.org
utalisoma na pia vipo katika kanisa langu.
Haya ndiye maneno ya MUNGU aliye hai na yapo kwa ajili ya
wanadamu wote ila shetani amewavuna mamilioni na kuwajazia elimu ya uongo. Yeye
ndiye njia ya ukweli na uzima sasa ndio ukweli wa YESU wa ubatizo unaoufuata au
unaompinga na kufuata ubatizo wa uongo? Fuata aliyoagiza peke yake tena
lisibadilishwe (Ufunuo 22: 18-19) onyo atakayeongeza au kupunguza atahukumiwa
na wote wanaoshiriki maneno ya uongo nao njia ni moja, na hao wote wanaobatiza ubatizo
tofauti na alioagiza YESU hao wanaongozwa na mpinga kristo na mwalimu wao ni
yesu wa uongo, wala YESU WA NAZARETI hawatambui wala kuwajua. Nawaeleza muelewe
hata ukibatizwa katika kisima au ukabatizwa kwa jina la mchungaji ujijue umetekwa
na shetani na pia huyo mchungaji amekuteka wewe na wewe ni mtumwa wake milele
na hautamuona YESU milele bali utamuona yesu wa uongo maana umekubali maneno
yake ya uongo yakakaa ndani yako hivyo anaouhalali wa kukutawala sababu ndani
yako umewekewa na wengi hawajui ukweli huu, nawasihii tubuni leo hii.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU MIMI NINA DHAMBI NAOMBA UNISAMEHE UNIANDIKE
KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WEWE YESU WA NAZARETI UWE BABA YANGU MILELE.
NIPONYE, NIONGOZE WEWE PEKE YAKO KWANZIA SASA, NIFUNGUE FAHAMU ZANGU NIKUJUE
WEWE. AMEN.
NOTE:
Soma makala na vitabu katika blog yangu hakika utakua
kiroho, na kama hakuna kanisa la kweli mahali ulipo wewe uwe unasoma vitabu
nilivyoviandika, na pia uwe unasikiliza mahubiri kwa njia ya YouTube ambayo
nimeyahubiri mimi, na usome katika home page ya website uangalie vipindi vya
television na redio ujue muda wake uwe unasikiliza na mimi naendelea kuwaombea.
Na wote mliopo nchi za nje nawakaribisha kanisani kwangu uje uponywe na ukutane
na YESU, zaidi upige simu utaelekezwa jinsi ya kufika au utume email utajibiwa.
Nawatakia wokovu ndani yenu.
NABII HEBRON.