BY
NABII HEBRON.
Kuhusu visiwa vya Zanzibar ambayo ni sehemu moja wapo ya
nchi ya Tanzania. Kisiwa hiki ni tajiri sana ila utajiri wake ulikuwa umeibiwa
na uthamani wake na pia maisha ya watu waliopo. Mwanzo wa tarehe 8.1.2014 MUNGU
ameikomboa Zanzibar sasa ipo mikononi mwake na amerejesha uthamani wa Zanzibar
na utajiri wake na maendeleo yake na ya watu wake. Mtaona mabadiliko makubwa
sana kiuchumi, kielimu, na hata katika viwanja vya ndege. Mashirika mengi ya
ndege kutoka nchi mbali mbali yatakuja na wageni wataongezeka zaidi. Uoto wa
asili yaani mimea itastawi zaidi, na samaki soko litakuwa kubwa, wananchi watajituma
sana kufanya kazi.
Katika serikali Mawaziri baadhi wataondolewa katika nafasi
hizo, na pia katika bandari baadhi ya watumishi wataondolewa sababu kuna vitu
vitafichuliwa. Uchawi haufanyi kazi tena katika kisiwa cha Zanzibar, waliozoea
sasa mwisho umeshafika, ni MUNGU ndiye atakayeyafanya hayo yote na tayari
ameshaanza kazi hiyo na atawatumia watu hao hao na kuwaongoza.
Madawa ya kulevya hayatapita tena katika airport na
bandarini, MUNGU mwenyewe atafanya njia akiwa na YESU WA NAZARETI (Nabii Issa).
Tanzania Bara nilishawaeleza yote yametokea na sasa ni wakati wa Zanzibar
kuinuliwa juu, mtashangaa mabadiliko makubwa sana. Na pia mafuta ya petrol yapo
ila yatapatikana pale wananchi wakijielewa maana wapo wanayo yamendea na waibe
faida yote. Utajiri huu ni kwa ajili ya wananchi au watu aliowaumba MUNGU
mahali hapo na siyo kwa wageni.
Mwaka 2015 viongozi wengi waliopo madarakani katika uchaguzi
watalia machozi (hawatapata tena nafasi na watakaotumia uchawi) MUNGU
atasimamia uchaguzi huu na atawaongoza watu aliyewaumba yeye wawachague wale
watakao mtegemea yeye tu.
Zaidi soma katika blog ya Prophet Hebron www.prophethebron.blogspot.com
na pia Prophet Hebron YouTube.
Uovu na ufisadi utafichuliwa kila mara katika maeneo yote na
watasemana, myaonapo msiogope, mjue ndiye mwenyezi MUNGU yupo kazini. Hata pesa
zilizoibiwa zikapelekwa nje ya nchi zitarejeshwa.
·
Bunge litakuwa kali sana, na MUNGU atawatumia
watasema kweli bila kuogopa wala kusua sua.
·
Meli zitaongezeka.
·
Wananchi watajenga mahoteli makubwa yakitalii.
·
Biashara halali zitainuka na nchi nyingi
zitaanza kwenda kufanya shopping Zanzibar kama ilivyo watu wanaenda Dubai au
China. Hayo yote ni YESU WA NAZARETI ayafanya. Na Rais MUNGU atamuongoza wala
hakuna atakayeweza kumyumbisha na atamlinda yeye peke yake.
·
Kuhusu kuvunjika muugano hilo halitakaa litokee
milele ndivyo alivyonieleza MUNGU, na wanaotaka muungano uvunjike ni bora
wakalime au kufanya biashara maana watapata faida. Ila kuhusu kuvunja muungano
ni wanajisumbua akili zao, haya amenieleza yeye aliyeiumba Zanzibar na dunia
yote, na Zanzibar ni sehemu moja ya Edeni ya sasa.
NOTE:
Ujumbe huu nimepewa mimi Nabii Hebron na MUNGU mwenyewe
tarehe 8.1.2014, ndipo Zanzibar aliifungua upya na kuibariki na kuitoa mikononi
mwa wakoloni walioiba uthamani wake na kwa watu wengine wenye nia mbaya.
Zanzibar sasa siyo ile ya zamani ni mpya imeinuliwa juu na ipo mikononi mwake
sasa.
MUNGU IBARIKI ZANZIBAR
NABII HEBRON WA KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE.