Safari ya mbinguni ni maandalizi ya kupata ticket au visa ya
kwenda mbinguni, visa hiyo ni YESU WA NAZARETI peke yake tu yeye ndiye njia ya
uzima na ukweli ya kumfikisha mtu mbinguni katika neno la MUNGU yaani biblia. Pia
imeandikwa ni YESU peke yake ndiye njia ya uzima na ukweli (Yohana 14:6), au maana
nyingine katika safari hauwezi kuingia katika ndege au basi bila ticket. Ukiingia
kwenye basi unaulizwa ticket yako uliyokata na kama hauna hushushwa na kuachwa
hivyo hivyo, na kwenda mbinguni bila kuwa na YESU WA NAZARETI tena wa kweli
yaani yeye ndiye ticket original hauendi. Na ukiwa na ticket feki ya YESU pia
utashushwa na kuachwa sawa sawa na vile vile kimwili ukiwa na ticket feki ya
basi fulani utakapoitoa utakataliwa utaambiwa hiyo ni feki na unaachwa.
Ukisoma katika kitabu cha Ezra 8:21, inasema “Ndipo
nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili upate kijinyeyekeza mbele za
MUNGU, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa
ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.” Hii inamaana kuwa njia iliyonyooka watu wanaitafuta iliyo salama
maana pia zipo njia za uongo au ramani
za uongo zikitoa direction ya safari ya mbinguni na kumbe ni wrong direction.
Ndugu msomaji, funguka ufahamu wako sasa ili ujue njia iliyo
sahihi na ticket za salama za kwenda mbinguni pakuzipata. Katika safari ya
mbinguni ticket original hupatikana kwa watumishi aliowaita YESU na siyo
waliojiita au kutamani tu kufanya pasipo yeye kuwatuma. Ni sawa sawa katika
basi, ili upate ticket original utamuona agent au wakala wa basi hilo original
ndiye atakayekupatia ticket sahihi, ukienda tofauti na wakala asiyejulikana au
tajiri huyo atakupatia ticket feki na muda wa basi kuondoka wakati wa ukaguzi
wakiangalia ticket yako, wakiikuta siyo original yao watakushusha na kukuacha
na pesa umeshatapeliwa.
Kama watu ilivyo kimwili wanayokatiwaga ticket feki sehemu
mbali mbali katika miji mbali mbali, hubakia kulia na basi limeondoka. Watu wengi
wanafikiria wanaenda mbinguni. Nilipokuwa ninaongea na YESU WA NAZARETI katika
maongezi yangu mimi na yeye na kunifundisha, akanielezea kuhusu ticket feki za
mbinguni na original. Sasa nakuja katika kanisa, watumishi 98% all over the
world is fake, agent of the wrong Jesus, utaniuliza kivipi? Nitaelezea sababu
chache ambazo utazichunguza kimwili;
·
Watumishi wote walio freemason member (angalia
kwa internet).
·
Watumishi wote wanaobatiza ubatizo ambao haupo
kwa biblia na hata katika kisima, na pia kubatiza kwa kutumia majina yao (huo
ndio ufeki na hayo mnayashiriki mkijua ndio ticket za mbinguni na kumbe siyo,
hayo siyo maelezo yaliyopo kutoka kwa mwenye kuandaa safari hiyo yaani YESU WA
NAZARETI. Soma katiba yake hayo hayapo, onyo hao ni feki wakala ni wezi
wanaotumiwa na shetani kuiba roho za wana wa MUNGU kwa kuwapa ticket za kwenda
kuzimu badala ya mbinguni. Watu wengi hata wengi waliokufa wanajuta na kusaga
meno, muda mwingi walioupoteza makanisani mpaka kifo hawakupewa ticket original
bali ni feki.
Kivipi? Mtumishi wa jinsi hiyo hata ile
sala ya toba anayokuongoza haipokelewi kwa sababu yeye siyo wakala wake
haijalishi anatumia jina la YESU.
·
YESU aliye njia ya uzima na ukweli mawakala wake
yaani watumishi ndio wakataji wa ticket za watu kwenda mbinguni, mtumishi yeyote
anyefanya maombi kwa pesa ujue huyo ni fake agent, kubusu misalaba ni fake
agent maana hayo maelezo ya kuruhusu hayo yafanyike siyo ya YESU WA NAZARETI ni
ya yesu wa uongo na ukiambatana na yeye na wewe unakuwa mwana wa uongo. Ufunguke
ufahamu wako ili uipate ticket original ya YESU WA NAZARETI. Sasa hivi 98% ya
watumishi wote katika ulimwengu wote ni fake, na hii inaonyesha picha halisi
jinsi walivyowapa watu wengi ticket feki na hawaendi mbinguni.
·
Mtumishi yeyote anayetoa stika zake na kuipiga
saini yake halafu anawaambia watu inayo nguvu za MUNGU, huyo ni feki. Amekupa hirizi
pasipo wewe kujua na hali yako itakua mbaya siku zote mpaka ufunguliwe na
uichome. Hata stika zenye mikono ya watumishi zitupe, kupitia ile mikono ya
stika zao inaiba uchumi wako, unaenda kwao. Au nieleze kirahisi ni jini chuma
ulete.
·
Mtumishi anayechangisha pesa za harambee, au
kukopa benki pesa kwa ajili ya kujenga kanisa, hayo yote siyo maelekezo ya
mwenye ticket original ya mbinguni ni maelekezo ya mawakala feki ambao
hajawaita wala kuwatuma bali kazi yao ni wizi tu wa mali za wana wa MUNGU. Kama
ilivyo kimwili mawakala feki wa mabasi huchukua pesa na kukupa ticket feki na
kukuacha umechanganyikiwa, haujijui, hivyo ndivyo ilivyo wakristo 98% katika
ulimwengu hawaendi mbinguni pasipokujua.
Leo funguka, toka huko utajuta
ule mwisho, kanisa limetekwa na shetani, na shetani amewatumia hawa hawa
mawakala wake kuwapofusha watu wasubiri safari njema ya mbinguni. Siku ile YESU
atakuambia sikujui sikujui wewe, ataangalia moyoni mwako je? Aliyekuongoza sala
ya toba ni wakala wake? Ataangalia, akikuta ni safi utaenda, akikuta ni feki
utatupwa motoni milele. SOMA VITABU VYA NABII HEBRON JINSI KANISA LILIVYOTEKWA
NA SHETANI, MKRISTO USIKUBALI KUWA MPUMBAVU, na watu wote katika ulimwengu huu
msikubali kuwa wapumbavu mbele za MUNGU, muwe wajanja kama alivyo YESU. Chunguzeni
ticket zenu, waliowaongoza sala za toba na mikao yao je inafanana na toba za
YESU, ukikuta tofauti ujue umeangamia. Fanya haraka utafute mtumishi wa kweli
aliye na YESU wa kweli akuongoze sala ya toba iingie ndani ya moyo wako tena
original.
NOTE:
YESU anasema anawapenda wale
wote wamtafutao kwa bidii na hakika watamuona, ila 98% all over the world bado
hawajamuona yeye, je? Ni wewe? Jichunguze.
NABII HEBRON.