Pages

Thursday, January 30, 2014

KUZIKWA NA MSALABA NI LAANA NA UNAZIKWA NA VIFUNGO VYA SHETANI.
KUVAA MSALABA NI LAANA (DHAMBI)
KUBUSU MSALABA NI LAANA (DHAMBI)


IBADA YA KUTEMBEZA MSALABA NI LAANA

Ndugu msomaji wa makala ya Mtume na Nabii Hebron karibu tena katika shule ya mbinguni kutoka kwa BWANA YESU WA NAZARETI maana haya yalikuwa yamefichwa ila kwa neema yake MUNGU aliye hai na aliyewaumba wanadamu wote na vitu vyote. Amenituma kuukomboa ulimwengu kutoka kwa shetani, maana watu wamekuwa upande wa shetani wengi pasipo kujijua ila viongozi wa makanisa wao wanajua kabisa wamekuwa watumishi wa shetani kwa ajili ya kuangamiza roho za wana wa MUNGU wakitumia jina la mwana wake wa pekee yaani YESU WA NAZARETI. Amenituma kwa kila mtu na mimi nimemtii MUNGU kama YESU alivyomtii BABA yake, wala hakusikiliza maneno ya Mafarisayo ya kumkatisha tamaa, alisimamia lile kusudi tu la BABA yake na mimi Hebron ndivyo hivyo hivyo, siangalii lolote ni kusudi lake tu mpaka ulimwengu umrudie MUNGU na shetani apate hasara na MUNGU utukufu wake uwe juu milele na milele.

Mambo mengi ninayowafundisha ni tayari yalishageuzwa na kuwa kinyume na ilivyoandikwa katika biblia na kupewa elimu ya kugeuzwa neno la MUNGU na ukiwa tu ni tofauti na neno katika biblia, ndugu msomaji ujijue tayari umetekwa na shetani, wewe siyo wa YESU WA NAZARETI wewe ni wa yesu wa uongo, na wewe umefanyika kuwa mtoto wa kristo wa uongo na baba yako ni shetani ambaye ndiye mungu wa uongo.



NINI MAANA YA MSALABA

Msalaba ni ishara inayotokana na mistari miwili kuungana (). Asili ya msalaba ni katika nchi za  Wajemi na Misri katika miaka ya zamani. Misalaba hii ilitumika katika kuwaua watu waliokuwa na makosa au waliolaaniwa. Msalaba ulitumika kama kitanzi cha kuhukumia mwanadamu ili afe asiwepo aishi tena katika dunia hii. Msalaba ni mti (Matendo Ya Mitume 5: 30), msalaba ni mti ambao Wayahudi walimhukumia pia YESU japo pia ilitumika kuuliwa watu mbali mbali na YESU yeye hakuwa ni wa kwanza kuuliwa kupitia msalaba (Matendo Ya Mitume 10: 39). Neno la MUNGU linazidi kujithibitisha pia ya kuwa msalaba ni mti (Matendo Ya Mitume 13: 29). Hivyo YESU alitundikwa katika mti mpaka akafa ili kubeba mateso yetu na kukombolewa katika laana ya dhambi, na sisi tusije bebeshwa tena msalaba yeye alibeba badala yetu ili tuokolewe na alipochoka kubeba msalaba yupo mwanadamu aliyeitwa Simoni alimsaidia, na kitendo cha Simoni kubeba msalaba maana yake yeye mwanadamu alibeba badala yetu sisi, hivyo haitupasi kubeba tena msalaba, maana msalaba siyo kitu kitakatifu ni kitu cha kuulia wanadamu asiishi tena.

Muda na siku siyo nyingi nilipokuwa nasema na MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo kama vile na wewe uongeavyo na mzazi wako ana kwa ana. Alinieleza mambo mengi ambayo mengine ni yangu kama mimi Hebron tu na mengine ni namna ya kuwatoa wanadamu katika vifungo vya shetani. Na katika jambo limojawapo MUNGU alilonieleza, mimi mwenyewe niliogopa sana. Akaniambia Hebron mwanangu, hivi ni kwa nini wanadamu wanaabudu msalaba? Wanabeba misalaba vifuani mwao na pia katika shingo zao na pete zao? Sikuwa na jibu. Akaniambia hivi ndivyo wanadamu walivyopotea wengine wakijua kabisa ni makosa kuabudu misalaba na hata pia kufanya ibada ya misalaba ila wamekaza shingo zao. Na wengine hawajui ukweli wanapotoshwa. Akasema, mwanangu YESU yeye yupo mbinguni, yeye haishi katika misalaba ya aina yeyote ile, yeye hayupo katika mbao tena, na alipokuwa hapa ulimwenguni hakuruhusu watu waabudu misalaba au waivae misalaba. Watu wengi wanavaa misalaba wakijua mimi nipo katika misalaba. Mwanangu YESU hayupo katika misalaba, na wote mnaojibebesha misalaba iwe ni shingoni, kifuani au kjichora nembo ya msalaba mahali popote au hata majoho yenye alama ya misumari, akaniambia waeleze waache kama wanataka kupona roho zao. Ina maana wanaoivaa hiyo misalaba wanachukuliwa katika ulimwengu wa roho wanapelekwwa Golgota ya shetani na wanasulubishwa na mapepo ya Kiyahudi tena. Hivyo maisha yao wao wanakuwa ni wasulubishwa wa shetani na roho zao zinauwawa katika ulimwengu wa roho.

Mfano halisi, tazama hata kifo cha Petro na yeye alipigiliwa msalabani akafa na waliomuua ni Waroma, hivyo shetani alibuni mbinu ya kuhakikisha atawapata tu Wakristo, akatumia upofu wa misalaba. Sasa zamani ilikuwa kimwili unahukumiwa ufe ila sasa ni kiroho. Msalaba siyo kitu kitakatifu ni kitu cha kuulia roho za wanadamu wasimuone MUNGU. Ila kanisa lililotekwa na shetani ndilo limekumbatia msalaba yaani laana ya kifo cha kiroho. Hivyo mahali popote palipo na msalaba ujue ni mahali pa laana na kuulia roho za wana wa MUNGU katika ulimwengu wa roho. Na pia MUNGU akaniambia Hebron, umeshaelewa kuhusu msalaba ni nini lengo, sasa hii ni siri nimekufichulia uwafundishe watu wote wa ulimwengu huu nauwaeleze nawapenda, wale watakaonirejea mimi na kutubu watapona ila akaniambia siyo wote (hayo mengine hajaniruhusu niyaseme).

Akasema kama msalaba ungekuwa unanguvu zangu basi hata mwanangu YESU alipozikwa angezikwa na msalaba. Akaniambia Hebron, uwaeleze watu wote kuhusu msalaba, waeleze msalaba ni kifungo cha shetani anachojiwekea mwanadamu kama yeye tayari amejilaani na shetani anasimamisha bango kwao na mimi MUNGU ni wa haki, naona kweli wamekubali misalaba yaani vifungo na wengine hata wakazikwa juu ya makaburi yao unawekwa msalaba (yaani kifungo) au kwa maana nyingine huyo aliyekufa amesulubiwa. Hivyo watu hata miili yao inakuwa na laana. Akaniambia, mwanangu YESU alionyesha njia kila kitu, ili wanadamu wote waige njia zake (Yohana 14: 6) “YESU akamwambia, mimi ndimi njia ya kweli na uzima, mtu haji kwa BABA bila kwa njia ya mimi.” Hivi ndugu msomaji umeshajiulizaga wewe katika akili yako kwa nini YESU anajiita yeye ndiye njia ya uzima na kweli. Ina maana yeye alionyesha kweli na ili ufike mbinguni umfuate yeye na kweli tupu pamoja na njia yake. Tazama MUNGU alijua hata wanadamu watakaokufa, akaonyesha njia jinsi wazikwe, maziko ya YESU ndio pendezo la MUNGU. YESU hakuzikwa na msalaba (kifungo) na ndiyo maana alifufuka sababu hakuwa na kifungo cha shetani katika lile kaburi lake. Sasa tafuta hata katika biblia haijaruhusu watu wazikwe na misalaba, hata kubeba msalaba haijaruhusu. Na zaidi watu wanaweka misalaba mpaka manyumbani mwao ina maana wamejiwekea kifo chao tayari kuhukumiwa.

Mnaotaka kuzikwa bila kifungo usikubali kuzikwa na msalaba, huu ni ujumbe kwa mataifa yote, fuata mfano wa YESU. Au nikuulize swali je wewe unapenda uzikwe tofauti na YESU alivyozikwa na akasema tuifuate njia yake? Jibu, hautaki kabisa, ila nakufungua uzidi kuelewa jinsi kanisa lilivyotekwa na shetani.

 Haya wengine wanasema kaburi la mkristo alama yake ni msalaba? Ndugu msomaji hivi alama au ishara ya YESU ni msalaba? Jibu, siyo, na kama msalaba ndiyo ingekuwa ndiyo ishara ya YESU basi hata biblia tusingeisoma kila mtu angejitengenezea misalaba then kwisha. Na zaidi tunajua YESU yu hai, je misalaba inayo uhai? Inapumua? Misalaba ni sanamu, ukisoma katika kitabu cha (2 Wakorintho 6: 14-16, 18) neno linasema tena pana mapatano gani kati ya hekalu la MUNGU na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la MUNGU aliye hai, kama MUNGU alivyosema ya kwamba, nitakaa ndani yao na kati yao nitatembea na nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo tokeni kati yao mkatengwe nao asema BWANA. Msiguse kitu kilicho kichafu nami nitawakaribisha nitakuwa BABA kwenu nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na kike. Hapa pia unaona neno linasema ninyi ni hekalu nitakaa ndani yenu siyo nje yenu.

Sasa hebu ona hapa misalaba inaabudiwa nje inafanywa ndiye MUNGU je hamjaangamia sasa au kupotea? Toka huko umrejee MUNGU wa kweli, yeye hayupo katika misalaba 100%, haya ni mapokeo ya shetani aliyoyapitishia kwa watumishi waliomuasi MUNGU ili kuja kutufundisha uongo wa shetani na ndiyo maana misalaba inaabudiwa katika ulimwengu huu. Nawafungua fahamu zenu, ameniambia MUNGU wote mnaovaa misalaba, hata kwenye kuiweka makanisani na kufanya ibada za misalaba; ni mnamtukuza shetani pasipo nyie kujua, sasa funguka.

Na watumishi wengine katika nyumba zao wamejenga misalaba na makaburi. Misalaba hiyo inayomaana kubwa hapo kwake, ndipo anapotengenezea vifungo vya kuwafunga wana wa MUNGU wafe roho zao, na yeye anajijua anachokifanya. Na zaidi biblia inasema tumwabudu yeye katika roho tu, sasa kimwili tu utaona hii misalaba siyo kiroho tena.

Hivi mmeshajiuliza kwa nini makanisa ya wokovu mengi hayaweki misalaba makanisani? Wao walijua hiyo siri ila hawakuelewa mengine kama ya kuzika na misalaba. Misalaba ingekuwa ina nguvu za YESU nakueleza makaburini wachawi wasingekanyaga kuloga au kufukua maiti wale nyama. Misalaba ingekua ina nguvu za YESU ingekuwaga hailiwi na mchwa au ianguke. Na ingekua na nguvu za YESU nakueleza kila anayeivaaga mapepo yasingemgusa wala matatizo yeyote yale. Na cha ajabu mamia ya watu ninaowaombea wakija kanisani kwangu kumtafuta MUNGU 100% ndiyo wenye mapepo mengi yanawatoka na mengine yanagoma kutoka mpaka uondoe vitu vyao yaani hiyo misalaba, ndiyo mapepo na ndiyo vifungo vyao.

Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron ufunguke na uwajulishe wengine watapona na watapona roho zao na kuachana kabisa na ibada hizo ni machukizo kwa MUNGU na wote wanaoshiriki wanajitenga na MUNGU, sasa angalia ni muda gani haukujua ukweli na ulipotea kwa shetani.

Jambo lingine ni kuhusu mwili wa BWANA, pia unawekewa alama ya msalaba ina maana unapokula tayari na wewe umekula laana na vifungo vya shetani vimekaa mpaka kwenye akili. Tazama aliye njia ya uzima na kweli YESU alipokuwa akiumega mkate (ile chapati) je ilichorwa msalaba katikati yake? Jibu, hakuna, kama yeye alionyesha njia na katika ule mkate haikuchorwa msalaba, je nyie watumishi huo msalaba umeruhusiwa na nani? Jibu siyo YESU ni shetani. Hivyo inavyoitwa chakula cha BWANA ina misalaba hiyo ni chakula cha kujifunga kiroho uhukumiwe na matokeo yake utashangaa mtu ameshiriki lakini anayo mapepo yaani roho wa shetani, magonjwa, na afya mbaya hata kimwili, hii ina maanisha unaula msalaba, mti au laana au unazidi kujifunga uwe mbali na MUNGU na zaidi mwili wako unakuwa siyo hekalu la MUNGU tena, bali ni hekalu la shetani.
Hivyo ndivyo elimu ya Neno la MUNGU ilivyobadilishwa ili wanadamu wasimuone MUNGU milele, haijalishi utakula na utamtaja YESU. Hiyo ni feki, tafuta kwenye biblia hakuna maagizo hayo. Hii ni dunia nzima 98% shetani ameliteka kanisa na watu hawajijui, MUNGU amenituma niwaeleze ukweli na niwafundishe kweli yake mumrejee yeye, maana kwa njia hiyo tayari mmeshatengwa na MUNGU na hamtamuona pasipo kuacha na kuokoka.

Pia watu wengi wanapoombea vyakula badala ya kumshukuru YESU, mtu anaweka alama ya msalaba halafu Amen, anakula chakula. Hiyo ni makosa inaonyesha hiyo ishara ya msalaba ndiyo YESU na unaabudu msalaba, kwa kufanya hivyo wewe chakula chako hakijabarikiwa na YESU 100% bali umekishirikisha hicho chakula na vifungo vya shetani na afya yako ifungike zaidi na kufunga riziki ya chakula kijacho kukipata, na ndiyo maana kwa njia hii njaa hazikomi katika familia na watu kupata milo kwa shida, hii ni sababu moja wapo, maana YESU angekibariki yeye nakueleza njaa kwako na kulala njaa ingekuwa ni historia. Tazama yeye alivyoiombea ile mikate na samaki 12 je iliongezeka au ilipungua? Jibu iliongezeka. Sasa alionyesha njia ya kuombea chakula, je yeye aliweka alama ya msalaba? Jibu siyo. Tafuta katika biblia yote hata wale wanafunzi wa YESU wa kwanza hawakuombea chakula kwa ishara ya msalaba. Hii ni ya MPINGA KRISTO.

Unakuta mtu kabla ya kuanza ibada mtumishi anataja nafungua ibada hii kwa jina la BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU, hiyo ni sawa ila anaharibu pale anapotumia mikono yake kufanya alama ya msalaba () yaani hapo mtumishi anamkufuru ROHO MTAKATIFU pia maana yeye siyo msalaba, wala MUNGU siyo msalaba, wala YESU siyo msalaba, hivyo inakuwa ni ibada ya kumkufuru ROHO MTAKATIFU. Na watumishi wengi hawajui wanachofanya wao walipelekwa vyuo vyao wakapokea elimu ya wanadamu na siyo ya mbinguni, na elimu ya wanadamu haikufikishi mbinguni.
Tafuta katika maisha ya YESU alipoomba hakutaja au kufanya alama yeyote ya msalaba, ni sababu msalaba ni laana na upo kwa ajili ya kuulia roho za wana wa MUNGU tu, na yeye hana  ushirika na msalaba na ndiyo maana mbinguni hakuna msalaba.

KAZI YA IBADA YA MSALABA

Katika biblia haijaruhusu ibada ya msalaba, ibada ya msalaba ni ibada ya kila anayeshiriki ibada hiyo anakwenda kujiangamisha na vifungo na mateso ya shetani na kujilaani, na katika msalaba ipo roho ya mauti. Msalaba unapelekwa nyumbani kwako na ikafanyika ibada hapo ina maana hiyo familia imeupokea na kukubali ya kuwa imelaaniwa na imeikubali dhambi hadharani na imeabudu sanamu, na mapepo ya mateso huwa na kibali (hivyo ndivyo watu baadhi yao sababu hawaujui ukweli ndivyo walivyopotea na mafunuo hayo ya msalaba na ibada hizi zimetoka kuzimu na muasisi wake ni mpinga kristo. (Ukishiriki ibada hiyo au katika kanisa lifanyayo hayo tayari na wewe roho ya mpinga kristo ipo na wewe. Toka huko uokoke upone roho yako).

VITU VYOTE VENYE ALAMA YA MSALABA

Vitu vyote hivyo vyenye alama ya msalaba ndani yake ipo roho ya mauti na laana, na katika ulimwengu wa roho inafanya kazi ya kuua roho zote ambazo zinawekewa misalaba either katika vyombo vya kushiriki divai, au pete za mikononi. Na mwenye pete yenye msalaba anayoivaa ina maana amefunga ndoa na vifungo na laana.

Kwenye vibao vya makanisa ule mchoro (†) ina maana ipo roho ya laana na vifungo vya shetani na inao uhalali katika kanisa  hilo kuwatesa waumini wao na hata ndani au nje msalaba ni alama ya hapo ni makutanio ya kuua roho za wana wa MUNGU na kuzisulubisha Golgota katika ulimwengu wa roho.

Fimbo inayobebwa na kuhani yenye msalaba, fimbo hiyo ina maanisha katika ulimengu wa roho hiyo fimbo inayoongoza inayo roho ya vifungo na watu wote badala ya kuongozwa wapone kama vile fimbo ya Musa alipoinyoosha iliangamiza adui na mara nyingine ilipiga mwamba maji yakatoka. Sasa fimbo ya Musa haikuwa na msalaba na tafuta katika biblia hakuna mahali biblia imeruhusu fimbo iwekewe msalaba. Maana yake badala ya kuwalinda kondoo na kuwachunga fimbo hiyo inawalaani na kuwafungia vifungo katika ulimwengu wa roho na wasimuone YESU milele, hii ni siri ya mpinga Kristo. Ndiyo maana aliyeanzisha hayo alibuni njia na namna ya kuhakikisha ameumaliza ulimwengu wote. Na ukiona mtumishi yeyote anatumia fimbo yenye msalaba halafu alama ya kondoo ipo na fimbo imezungukia ina maana ni fimbo ya kufunga wana wa MUNGU wasimuone MUNGU. Ile roho ya upotofu ndiyo ipo ndani yake. Haya yote yalifanyika baada ya kuwaua wanafunzi wa YESU akiwemo Petro.

Vyombo vya sadaka venye msalaba, unapotoa sadaka yako hapo unajitolea ufungiwe uchumi wako na maisha yako na roho yako ilaaniwe na kazi zako.

Nguo zenye misalaba (watumishi) YESU hajaruhusu misalaba kanisani. Watumishi wanapovaa mavazi yenye misalaba, wanapigwa upofu, YESU haonekani inakuwa ni ibada ya sanamu full. Na hata wengine hawajui maana yake hawapendi kuabudu sanamu na tena wanafundishwa msiabudu sanamu ila wao wenyewe wanavaa sanamu ya msalaba, ibada hizo zote ni feki mbele za MUNGU na ameniambia niwaeleze mnaotaka kupona uamuzi upo juu yako, na ambaye hataki kupona roho yako jehanamu inakusubiri. Pia muelewe katika dunia hii wala mbinguni hakuna msalaba mtakatifu, sababu ipo kwa ajili ya kuulia roho za wana wa MUNGU na sehemu yeyote utakapoiona katika nyumba zinazoitwa kanisa ameniambia hayo siyo makanisa yake yanayoweka laana kwa wana wa MUNGU hivyo fanya maamuzi utoke huko, maana ujumbe alionipa YESU ni sababu anawapenda na hataki mpotee. Aliwatuma wengi wamekataa kusema ukweli huu wakamsaliti. Wamebakia kumtaja jina tu kwa midomo ila ndani yao hayupo na wao.

Hivi umeshajiuliza swali katika akili yako kwa nini hawatumii misalabba wakati wa kuzika maiti au miili ya watu? Hawa ni wajanja tokea awali watangulizi wao waliona misalaba mtu akikosa amepelekwa kutundikwa ameuwawa. Kibinadamu na wao wanajua msalaba ni kitu kibaya haileti picha nzuri tena, kumuekea udongo halafu alama ya msalaba kama yeye ni mkoseaji au anayo laana amekufa kabla ya kuhukumiwa kimwili sasa asulubiwe huko katika roho alipoenda. Hivyo ndivyo ilivyo mamilioni wamekufa ila roho zao zimefungiwa na shetani vifungo vya msalaba. Na mimi Hebron nawaeleza kama alivyonieleza yeye aliyekuumba. Kuzika mtu na msalaba ni kumhukumu yule aliyekufa katika ulimwengu wa roho, wala msalaba siyo alama ya YESU, ila msalaba ni laana au kifungo na anayefunga vifungo hivi ni shetani sasa fungukeni ulimwengu wote.

NOTE:

Ninajua mabilioni ya watu wote katika ulimwengu huu hakuna hata mmoja aliyejua kuhusu msalaba ni vifungo na pia haifai mtu kuzikwa na msalaba. Mimi pia Hebron sikuyajua hayo ni mpaka pale MUNGU aliponieleza, ambaye amenituma niukomboe ulimwengu wote kwa jinsi atakavyoniongoza yeye, utukufu wa kanisa la mwisho umesharejea, ni wakati wa YESU WA NAZARETI kuvuna na siyo shetani tena na ndivyo ilivyo. Serikali ya shetani kwa sasa imechanganyikiwa ni mapinduzi ya YESU WA NAZARETI anayafanya, na mpaka atakaporudi mliopotea mrudieni YESU WA KWELI maana watu wote ni MUNGU amewaumba, ila kinachomtenganisha mwanadamu na MUNGU ni dhambi ikiwamo hii misalaba. Imeletwa ili wanadamu waiabudu watengwe na MUNGU, leo nimekujulisha. Hakuna lolote kwenye misalaba ni wapinga Kristo, hata watumishi wanaovaa kifuani hawajui ilivyo ni dhambi, inamaanisha wamebeba laana na vifungo vya shetani katika vifua vyao ili kuvisambaza. Maneno haya nimeyatoa kama alivyonieleza MUNGU wala sijayabadili.
MUNGU AWAOKOE.


NABII HEBRON.