By Nabii
Hebron.
Nawasalimu kwa jina la mwenyezi MUNGU aliye hai na siyo mungu
mfu ambaye hajulikani na wala hajaumba chochote na hana chochote katika
ulimwengu huu. MUNGU wa kweli ndiye BABA yake YESU WA NAZARETI, ambaye alikufa
na kufufuka na katika ule mwisho ndiye MUNGU aliyemchagua kuja kuuhukumu
ulimwengu na kwa jina lingine wanamwita Nabii Issa.
Leo tena ninawajulisha yale yatakayotokea Tanzania Bara
2014, kama nilivyokwisha kuwaeleza miaka miwili iliyopita mtaona mabadiliko
katika uchumi, gesi itapatikana, na madini yatarudishwa kwa wananchi wa nchi hii
na baadhi ya Mawaziri watatolewa katika uongozi wa serikali hii na mmeyaona
yametimia na mengine mengi aliyonieleza YESU kuhusu kuiinua nchi hii sasa inajulikana
zaidi, maana ilikuwa imefungwa kipepo na watu wenye nia mbaya kuhusu nchi hii.
Tokea 2012 nchi hii MUNGU ameishika kwa mikono yake mwenyewe
na ataibadilisha kila siku apendavyo yeye na akaniambia Tanzania ndiyo Eden ya
sasa. Viongozi wote wenye nia mbaya katika serikali hii na hata katika vyama
vya siasa hawatadumu watajikuta kila wakati wakiondolewa katika uongozi na
kukataliwa na Bunge, wananchi, na ni MUNGU ndiye afanyaye hayo nab ado ataendelea.
Naelezea machache tu ambayo ameniruhusu niyaseme, hayo mengine mpaka kwa wakati
wake.
Na pia bandari ya Dar Es Salaam itakuwa ndiyo bandari bora
na kubwa kuliko zote kwa upande wa bahari ya Afrika mashariki mwa Bara la
Afrika. Ndege tayari shirika limefufuka la ATC, RELI na pia mafuta ya petrol yapo
Tanzania tena mengi sana, ila mpaka atakapotaka YESU ndipo yataonekana ili
Watanzania wenyewe wafaidike, na siyo wezi wasio na nia njema katika nchi hii.
Nchi hii sasa hivi, kila kiongozi katika eneo lolote atende
haki, na asitumie uchawi. Endapo atakuwa kinyume na haya niliyoeleza hata dumu
katika kazi atatolewa, na mwaka huu 2014 uovu utafichuliwa zaidi na ni YESU
mwenyewe ndiye afanyaye hayo.
·
Upande wa Mawaziri bado wengi watatolewa tena. Mtakapo
yaona msiogope mjue ni YESU yupo kazini kuitengeneza nchi.
·
Watumishi waliomsaliti YESU wataporomoka mpaka
zero.
·
Watumishi wanaotumia nguvu za shetani watakufa vifo
vibaya kimwili.
·
Watumishi wanaouza madawa ya kulevya watajisema
wazi wazi na Usalama wa Taifa MUNGU amewainua sana, watafanya kazi nzuri sana,
na mtasikia ni mengi yalikuwa hayajulikani watayakamata, wataongozwa na YESU
tena pasipo wao kujua. Hawatalogeka, hongeka, danganyika.
·
Mwaka 2015 katika uchaguzi viongozi wengi
watalia machozi maana hawatapata tena nafasi katika nchi hii ya kuiongoza, na
wote watakaotumia uchawi hawatapata nafasi na hata wakiiba kura, hawataishi.
·
Pesa zilizoibiwa za nchi hii zilizopo huko
katika nchi za nje zitarejeshwa nchini, MUNGU ndiye atakaye yafanya hayo yote
wala hakuna kitakacho pingika, akisema niamesema.
NOTE:
Yapo mengi sana katika nchi hii na mengine yatakuwa ni
mabaya zaidi kwa jinsi wanavyochelewa kutii ujumbe wake na taarifa wanazo. Kwa sababu ya viongozi kukaza shingo ngumu
kumtii MUNGU na ujumbe wake kwa ajili ya nchi hii. Muonapo hayo yakitokea
msiogope mjue ni MUNGU mwenyewe, ila wakitii ujumbe wake kila kitu kitakuwa
salama. Maneno haya nimeelezwa na MUNGU peke yake na mimi nayaandika kama
alivyonieleza, namtii BABA yangu na MUNGU wangu. Na mengine nitayatoa kila
akiniruhusu maana ujumbe huu siyo kutoka kwa Nabii Hebron, ni MUNGU mwenyewe.
SOMA website ya Prophet Hebron www.prophethebron.blogspot.com na pia angalia video
za Prophet Hebron kwenye YouTube.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
NABII HEBRON.