Namshukuru MUNGU
kwa kunipa kibali cha kuandika Ujumbe huu, juu ya Viongozi wa Kanisa ,
kwa sababu Viongozi wamepewa Jukumu la
kusimamia waumini ili wasipotee, lakini cha kushangaza wameacha maagizo
waliopewa na Mwanzilishi wa Kanisa ambaye ni YESU KRISTO WA NAZARETI,
wakakimbilia mambo ya dunia, kama Kutafuta pesa.
Nitaeleza kuhusu
kiongozi wa Kanisa ni nani?
Kiongozi wa kanisa
ni Mtumishi wa MUNGU aliyechaguliwa kwa kusudi la kuongoza kanisa, ambalo ni
waumini, ili watoto wa MUNGU waweze kwenda Mbinguni.
Kiongozi wa kanisa
ni pamoja na Wachungaji, Maaskofu, Wainjilisti
na Waalimu.YESU amewapa kazi ya kuwaongoza watoto wake ili waurithi
ufalme wa mbinguni. Lakini sasa hivi ni kinyume. Viongozi ndio wamekuwa
kisababisho cha waumini kulia, kuhangaika na kuteseka wakati baba yao
aliyewaumba yupo. Wao ndio chanzo kikubwa kanisa kuteseka na waumuini wakaona
kama BABA yao aliye mbinguni hayupo, sasa hivi yuko Karibu kurudi, viongozi
wanaofanya mambo ya dunia watahukumiwa. Waliiacha misingi aliyoiweka YESU KRISTO
WA NAZARETI na kufuata mambo ya dunia kama yafuatayo:-
- Kuchangisha pesa makanisani, (Harambee)
- Kubatiza ubatizo wa beseni, ndoa
za shida na Raha
- Kufanya minada makanisani, sikukuu
za Mavuno
- Nyumba na Magari ya kifahari
- Wamejiunga na Vyama vya Freemason.
Na ukisoma kwenye
kitabu cha waraka wa kwanza kwa Timotheo 3:1-7
inaeleza kwamba Askofu au Mtumishi anatakiwa awe mtii, awe na mke mmoja,
asiwe mwenye kupenda pesa, awe mpole kiasi, awe mnyenyekevu, awe mwenye
kusikiliza watu, asiwe na majivuno, lakini mambo yamebadilika, kiongozi ndiye
mwenye kuoa wake wengi, ndiye mwenye kufanya minada makanisani na baadhi yao
wanamagari ya kifahari na hizo pesa wanazipata kwenye sadaka za waumini.
Unakuta kwenye kanisa kuna sadaka nyingi wakati sadaka ni Fungu la kumi na
shukurani basi, na pia ukipenda kumtolea
MUNGU kwa hiyari yako.
Viongozi wa kanisa
wameacha kufundisha mambo ambayo YESU anayoyataka, wao wanafanya kinyume , viongozi
wa kanisa wamejihusisha na kuuza madawa
ya kulevya, wanafungisha ndoa za mashoga, wanazini na waumini, wanatapeli watu
pesa zao na magari yao, eti anakuambia njoo nikutolee unabii kumbe anataka pesa
zako. Watumishi wamekuwa wachawi, washirikina kuliko hata waganga wa kienyeji,
Hivi kweli ndio mambo ambayo YESU amewatuma? Jibu ni hapana. Viongozi mnaofanya hivyo; Ole iko juu yenu
sasa hivi.
Inasikitisha sana
viongozi wamemuacha MUNGU na kutumia Majini Muhubiri ili kuwakamata watu walete
pesa makanisani. Hii ni aibu kubwa sana. YESU hapendi kabisa na hukumu iko juu
yao. Viongozi wamesabisha waumini wawe Masikini wa kiroho na kimwili, Watu
wanahangaika kumtafuta YESU wa kweli lakini viongozi wanawapotosha. Viongozi wa
kanisa wamesababisha waumini kutangatanga na kukosa mwelekeo.
Viongozi wamekuwa
wakichangisha pesa kama vile:-
Harambee ya
kujenga makanisa, kuchangisa pesa ya kufanya mikutano ya Injili, wakati
wanatakiwa hawa viongozi wamuombe MUNGU
ili awaletee watu wa kujenga Makanisa na sio kuchangisha waumini, watu wanalia tuu PESA PESA, Ibada siku hizi
zimekuwa za kutiana Moyo. Unakwenda Kanisani Kuanzia January mpaka December hauoni
majibu yako, Viongozi hawa wametumwa kutafuta Pesa au kuponya Roho za Watu?
Siku hizi Mikutano ya injili ni kutapeli watu hamna udhihirisho wowote. Wewe
mwana wa MUNGU unayesoma Makala hii ukiona michango makanisani ondoka
ukamtafute YESU wa kweli hao viongozi wanatafuta pesa tuu. Mbona wao wana magari
ya kifahari wakati wewe nyumbani hata centi hauna, wao ndio
wanakuchuna wewe
tu, funguka ufahamu mwana wa MUNGU mbona
na wewe hawakuombei ili na wewe upate vitu kama wao walivyonavyo.
Viongozi wa kanisa
hawawathamini wale ambao hawana pesa wakifanya makosa huwatenga. Je? YESU
aliwatenga wenye Dhambi ? Jibu ni hapana, kwanini viongozi hawawaombei ili watu
watubu na wamrudie YESU.
Nyie viongozi
mnaofanya hivyo sasa YESU yuko kazini, mtaona mtashushwa mapaka ziro, YESU
amekasirika mmeacha kazi yake, mkaanza kutafuta Pesa badala ya kuhubiri injili.
Na YESU yupo kazini sasa kuwakomboa watoto wake, amewaona wanapata shida sana, wanahangaika,
na atawatoa wale viongozi wote waliomsaliti.
Viongozi wa kanisa wamefanya nchi hii iingie kwenye matatizo, ndio wanahujumu uchumi wa
Tanzania na kuwafanya watanzania wawe maskini, kwasababu wao wanatakiwa
waiombee nchi na taifa zima. Wao ndio wanatakiwa kuwaongoza wana wa MUNGU. Wamemkasirisha MUNGU hata
wakifanya mikutano ya kuombea nchi, MUNGU hawezi kuwasikiliza kwasababu
hawafuati mapenzi yake na sheria zake. YESU amewakataa kabisa mpaka watubu.
YESU amekasirika
amemwinua Mtumishi wake Mtume na Nabii Hebron Kuupindua ulimwengu huu uliotekwa
na Shetani 98%. Na amempaka mafuta ya kuongoza ili wana wa MUNGU wamrudie YESU.
Ukubali, usikubali yeye ndiye atakayewaongoza wana wa MUNGU ili wasipotee na wasipate shida
tena. MUNGU aliona hakuna ambaye anaweza kumwinua akamchagua yeye peke yake.
Kwa maana viongozi wote wa kanisa wanatafuta pesa tu, hawaponyi roho za watu. Tuliona
kwamba kanisani ni mahali pa kuponea kumbe ndio tunateseka na kuibiwa nyota na
viongozi wa kanisa. Jiulize twende wapi? Jibu twende kwa YESU KRISTO WA
NAZARETI ndio mahali sahihi Makanisa yamekuwa
hayafai kabisa ni bora ukae nyumbani, maana ukienda makanisani ni
michango mingi. Unakuta ibada moja inamichango minne. Funguka mwana wa MUNGU
usiibiwe tena.
Asilimia kubwa
viongozi ni vipofu hawaoni kabisa wamefuata mambo ya pesa, badala ya kuwafungua
wana wa MUNGU. Hii inatisha sana ukiona kiongozi mzinzi, mlevi na anafanya
mambo ambayo hayampendezi MUNGU. Unakata tamaa kabisa hata ya kwenda kanisani,
ni kwa sababu tu ya upofu wao, ni kweli MUNGU amewaacha kabisa, kama MUNGU
angekuwa yuko nao, watu wasingepata shida maana wapo viongozi wanowaombea,
badala yake wao ni kutafuta pesa. Ole,iko juu yao wanajijua na wapo tunawaona
kabisa.
Ndugu msomaji wa
makala hii mahali ulipo mwangalie YESU peke yake, yeye ndiye anaweza
kukufundisha na kukuelekeza, watumishi siku hizi wanatafuta pesa hawana muda na
wewe hata kukuombea ufanikiwe. YESU
hayupo makanisani, hawezi kuingia kwenye
mapango ya wanyang’anyi, sehemu wanazochangisha pesa. Mwenyewe ukiangalia kwa macho ya damu na nyama
walivyokuwa na utajiri na majumba ya kifahari. Hivi kweli kanisa la la YESU
linaweza kuwa na mabenki, mahoteli? Jibu ni hapana. Sasa ndio utajua kweli hawamtumikii
MUNGU. Kazi yao ni kutafuta pesa.
Ndugu msomaji
usirudi huko tena, ukikuta Viongozi wa kanisa wana batiza watoto Wadogo na maji
ya kikombe, kubariki watu wazima, huko YESU hayupo kabisa wewe tafuta kanisa la
YESU wa kweli ambalo halichangishi pesa, wala haliwaibii watu vitu vyao.
Viongozi wa kanisa wamefanya tumkosee MUNGU wetu kwa kutupeleka pabaya.
Omba MUNGU
akuonyeshe mahali sahihi pa kuabudu usirude tena huko . Mrudie YESU awe Bwana
na mwokozi wa maisha yako.
Ubarikiwe wewe
uliyesoma makala hii utafunguka utajua kweli viongozi wanatafuta pesa tu badala
ya kufanya kazi ya YESU aliyowaachia.
MWINJILISTI MARTHA
IMANI