Ndugu
msomaji, ninakusalimu katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI ambaye ni mwokozi
wa maisha yangu na ulimwengu wote. Mimi naitwa Nancy Hebron na kwa neema yake
amenichagua kueneza injili yake kupitia Huduma yake; HUDUMA YA YESU NI BWANA na
MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRYchini ya uongozi wa Mtume na
Nabii Hebron.
YESU
aliponiita kufanya kazi yake, sikuamini, niliona ni utani. Nilijiangalia jinsi
nilivyo; mchafu, muovu, nimejaa dhambi na Je? YESU angetaka kunitumia mimi kwa
kusudi gani, kwa sababu gani, nani angenisikiliza mimi hata ningemhubiria kuhusu
YESU?! Na kwa nini mimi na sio mwingine? Nilijiuliza maswali mengi sana. Lakini
kama neno lake kwenye Isaya 55:8 inavyosema “Mawazo yetu sio mawazo yake na
njia zetu sio njia zake.”
YESU
alinijua jinsi nilivyo na akaniambia nisiogope kwa kuwa yeye ndiye alinichagua
na angenibadilisha na kunitumia kuwa mfano kwa vijana na wanawake dunia nzima.
Aliniambia nisiangalie umri wangu kwa kuwa angenitumia kama vile alivyomtumia
Yeremia.
Mwanzo
ilikuwa ngumu sana kukubali kile alichoniambia kwa kuwa nilijidharau na kuona
isingewezekana, na hapo ndipo nilikosea kwa kuwa kazi yake haifanyiki kwa nguvu
zetu bali kwa nguvu zake ndani yetu. Na madhara ya kujidharau kwangu ilichukua
muda kufanya maamuzi. Nilijiambia nitaomba nimalizane na dunia ndipo
nimtumikie.
Ndugu
msomaji, usidanganyike, hakuna kitu kama kumalizana na dunia, muda na wakati ni
sasa, YESU anarudi na Je? Atakukuta wapi? Duniani au Ulimwenguni?
Basi,
alishaniita mtumishi wake lakini bado nilikua mbishi. Nilitaka kuishi kote
kote. Niwe kwa YESU na pia duniani. Huo ulikuwa ni upumbavu, na wale ambao
hawamjui au hawamkubali YESU ndio wanaisha katika upumbavu na mimi nilikuwa
bado nimejaa upumbavu. Nikawa nasua sua kwa muda, nilikuwa vuguvugu. Niliishi
maisha mawili tofauti kwa kuwa ujana wangu na matamanio yangu yalikuwa
yananipumbaza sana.
Ndipo
siku moja nikafungua neno la Ufunuo 3: 15-16
“Nayajua
matendo yako, ya kuwa hu baridi au moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au
moto. Basi kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto nitakutapika
utoke katika kinywa changu.”
Niliogopa
sana, na ndipo ubishi wote uliisha, japo nilikuwa na kasoro zangu nilikuwa na
hofu ya MUNGU na sikutaka kumkosea.
Japo
ilikuwa ngumu YESU alinisaidia kufanya maamuzi, kuacha dunia na mambo yake na
kuishi ulimwenguni kwa YESU. YESU KRISTO WA NAZARETI ni mweza yote,
na ukijiachia kwake yote yanawezekana, hata kutoka duniani. Na kupitia makala hii ninapenda kusema zaidi na vijana, ili wajue kuwa dunia haina lolote, kwa
YESU ndio mambo yote, na ninamwomba MUNGU ukimaliza kusoma makala hii utafanya
maamuzi kuja kwa YESU full.
DUNIA NI NINI, NA ULIMWENGU NI NINI?
Dunia
na Ulimwengu zipo mahali pamoja lakini ni vitu viwili tofauti au ni sehemu moja
lakini ni tofauti, Kivipi basi?
Dunia
ni pahali ambapo shetani anatawala na yeye ndiye kiongozi, na wale ambao
hawajamkubali YESU ndio wako chini yake, na yeye ndiye mungu wao, haijalishi
kama wewe ni mkristo, kama haujaokoka shetani ndio kiongozi wako, na dunia ni
muunganiko moja kwa moja na kuzimu.
Unaweza
kujiuliza inakuaje shetani ndio kiongozi wa dunia na MUNGU aliumba vyote. MUNGU
aliumba ulimwengu na sio dunia. Wale ambao wameokoka na kumwamini
YESU, wanafwata na kuishi katika sheria na amri zake ndiyo wanaishi
ulimwenguni.
JINSI SHETANI AMEWADANGANYA VIJANA NA KUWASHIKILIA DUNIANI?
2
YOHANA 1:7
“Kwa
maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa YESU KRISTO yuaja
katika mwili. Huyo ndiye Yule mdanganyifu na mpinga KRISTO.”
Mdanganyifu
ni nani basi?
Mdanganyifu
ni mzinzi, mlevi, mvuta sigara na bangi, muongo, msengenyaji, mwenye tamaa,
muaji, mwabudu sanamu, mwizi, anapenda pesa na vyeo, mshirikina, wasio na
heshima, wana kiburi na kujua na mmenginevyo, kwa kifupi wadanganyifu ni wale
wenye tabia za shetani.
Dunia
ni mahali pa giza, mahali ambapo vijana wengi wanakaa kwa kuwa wanaogopa kuitwa
washamba. Shetani amewaekea ugumu kwenye mioyo yao ili waone kuwa wokovu ni
ushamba na wazee tu ndiyo wanaokokaga. Siwalaumu vijana kwa kuwa hata mimi
kabla ya kumjua YESU nilikuwa na waza hivyo.
Kwa
nini lakini? ni kwa sababu makanisa yapo duniani na sio ulimwenguni. Na
makanisa hayo yanagandamiza na kudanganya wana wa MUNGU, kuwanyag’anya mali zao
na pesa zao, na kuwaacha na nuksi, balaa na mikosi. Nilikuwa nikimwangalia
mwana wa MUNGU nilikuwa sioni udhihirisho wa YESU ndani yake au mabadiliko. Mtu
aliyeokoka ndiyo alikuwa amechakaa, hajipendi tena na ukimwangalia unawaza tu
kuwa nikiokoka nitafanana kama huyu na nitakuwa maskini, na ndicho
kinachowakimbiza vijana wasije kwa YESU. Lakini haya yote ni kwa sababu kanisa
lipo duniani kwa shetani na siyo ulimwenguni kwa YESU.
Njia
nyingine shetani amehakikisha anavijana wengi duniani ni kupitia nyumba za
starehe; disko, casino. Disko na casino ni muunganiko moja kwa moja na kuzimu.
Ukiwa kwenye hizo nyumba unashiriki kila kitu na shetani na watoto wake, na
malaika zake (majini na mapepo). Na kila ukiwa humo, majini na mapepo yanakuvaa
na wewe unakuwa na tabia kama zao, uovu, uchafu na mara nyingi unajikuta
unafanya mambo ya uchafu hata kama haupendi kwa kuwa wameshakuvaa na
wanakuendesha jinsi wanavyotaka. Kwa hivyo unazidi kuwa mlevi, mzinzi, mvuta
sigara na bangi hata kuwa mshiriki wa madawa ya kulevya. Shetani anakugaragaza
kwa kuwa wewe ni wa kwake na anauhalali na wewe.
Ukisikiliza
miziki wanaopiga disko, kupitia hizo nyimbo shetani anakamata ufahamu wako na
kukuendesha jinsi anavyotaka, akisema lolote au akitaka ufanye lolote utafanya
kwa kuwa yeye ndiye kiongozi wako na hauna nguvu ya kukataa.
Kwenye
casino, jinsi shetani anahakikisha amekukamata. Unapeleka pesa zako, na
ukishaanza kucheza michezo yao, uthamani wa pesa zako zinapelekwa kuzimu na
kupitia hizo pesa shetani anakumiliki na kukuwekea jini chuma ulete. Unajikuta
kila wakati unataka kurudi huko hata kama unamaliza pesa zako zote huko, bado
unarudi tu, hata ukiishiwa unakopa, ili tu urudi kucheza kamari. Na jinsi
unavyo zidi kurudi na shetani anazidi kukushikilia.
Njia
nyingine ni kupitia mavazi ya Yezebeli na mapambo yake pia, shetani
amehakikisha anawaunganisha vijana na kuzimu na kuwashikilia duniani.
Dunia
imejaa mashindano, majivuno. Ni mahali ambapo vijana wengi hawapo, wanatembea
na kuishi lakini nafsi zao zimeshikiliwa na kutumikishwa na shetani na ni mpaka
neema ya MUNGU iwafikie na kuwatoa huko.
JINSI YA KUTOKA DUNIANI NA KUISHI ULIMWENGUNI?
WAFILIPI
4:13
“Nayaweza
mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”
Ndugu
msomaji, kwanza ni vyema kujua hatuwezi jambo lolote bila uweza kutoka kwa
MUNGU. Kwake kuna vyote, kuna amani, furaha, kicheko, baraka, uponyaji, ufufuo
na WOKOVU.
Ndugu
msomaji, wokovu ni kwa neema yake, na ukisha mkiri YESU kama mwokozi
na mchungaji wako, mwachie maisha yako na moyo wako na yeye ndiye
atakubadilisha. Maisha ya utakatifu sio kitu cha siku moja bali siku hadi siku
YESU ndiye anakutengeneza na kukuimarisha kwa ajili ya utukufu wake. Anachukua
kisichofaa na kukitengeneza kwa ajili ya utukufu wake.
Basi,
kutoka duniani ni kwa njia ya kumkiri YESU, kuamini anaweza yote na kutii
sheria na amri zake. Kuishi maisha matakatifu. Kuabudu kanisa ambalo lipo
ulimwenguni na sio duniani; kanisa ambapo yeye yupo na wanafwata yale anayotaka
yeye. Mahali ambapo wanabatiza ubatizo wa Yohana, mahali ambapo wanamwabudu
yeye tu na siyo masanamu, mahali ambapo hawanyang’anyi pesa au mali zako,
mahali ambapo hawana sadaka zaidi ya fungu la kumi na sadaka ya shukurani,
mahali ambapo hawafanyi harambee, mahali ambapo kuna neno ambaye ni MUNGU, na
hilo neno likijaa ndani yako linakubadilisha siku hadi siku. Mahali ambapo kuna
nuru na udhihirisho wa YESU KRISTO WA NAZARETI.
YESU ANAWAPENDA VIJANA
1
YOHANA 2: 14
“…….
Nimewaandikia ninyi vijana kwa sababu mna nguvu na neno la MUNGU linakaa ndani
yenu, nanyi mmemshinda Yule mwovu.”
YESU
anawapenda vijana na anajua kuwa wakiamua kuja kwake wanaamua kabisa, na ndiyo
maana shetani na yeye anafanya juhudi zote kuwapoteza ili wasimjue YESU.
Kumpenda
YESU sio ushamba, bali ni ukombozi. Na heri uitwe mshamba wa YESU na kuurithi
ufalme wake, kuliko kumkataa na kuchomwa jehanamu.
Kama
YESU anajua kuwa unauwezo wa kumshinda shetani, wewe ni nani kutokuamini
unaweza kumshinda shetani?
YESU
anakuita leo, anakupenda na anataka uwe mtoto wake kwa kumkiri yeye kama
mwokozi wa maisha yako. Kama uko tayari, sema maneno haya;
“BWANA
YESU NIKO MBELE ZAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI. NINAOMBA REHEMA KWA KUWA NIMEENDA
KINYUME NA MAPENZI YAKO SIKU NYINGI. LEO NAMKATAA SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE NA
MAMBO YAKE YOTE. NINAOMBA UNITOE DUNIANI ILI NIWEZE KUISHI ULIMWENGUNI.
NINAKUKARIBISHA MAISHANI MWANGU NA MOYONI MWANGU. ANDIKA JINA LANGU KWENYE
KITABU CHAKO CHA UZIMA, NA UKIRUDI NIWEZE KUONDOKA NA WEWE NA KUURIITHI UFALME
WAKO. AMEN
Kuokoka
kwako ni agano kati yako na MUNGU wako, siyo lazima watu wengine wajue. YESU
atakubadilisha kwa muda na wakati unayompendeza yeye na watu watauona wokovu
wake kupitia matendo yako. Dunia haina starehe kama ulimwenguni kwa MUNGU BABA,
MWANA na ROHO MTAKATIFU, na siku ya leo umefanya maamuzi sahihi ya kumkiri
YESU. Usiogope mwana wa MUNGU, yeye sasa ni mchungaji wako na hautapungukiwa na
kitu.
MUNGU
WA IBRAHIM, ISAKA NA YAKOBO AKUBARIKI NA AKUHIFADHI.
MWALIMU
NANCY HEBRON KISAMO.