Ndugu
msomaji wa makala ya Nabii Hebron au unaweza kuiita makala ya YESU WA NAZARETI,
aliye kufa na kufufuka na sasa yupo mbinguni kwa BABA yake. Mimi jina langu
linatumika tuu kwa sababu ni mimi ndiye ninayekufikishia ujumbe huu. Ila
yaliyomo ndani ya makala ni jinsi anavyonieleza na mimi ndipo hukufikishia
ujumbe wake kwa mataifa yote na watu wake ili wapone na wajue ukweli wa MUNGU
na siyo uongo wa shetani aliouingiza katika wanadamu ili wasiwe wakristo
halisi, bali ni wakristo wa uongo. Na ujanja aliyotumia shetani, anajua watu
wengi wanampenda YESU na hawampendi yeye. Hii ni sababu jina la YESU
linalothamani, lingekuwa halina uthamani watu wasingeukimbilia ukristo.
Sasa
alichokifanya hapa ili awateke wanadamu na hata wakijiona wao ni wakristo
halali na kumbe ni wakristo feki. Shetani alianzisha ubatizo wake wa kikombe
(maji ya kumwagiwa kichwani tuu na siyo kuzama kwenye maji kama yeye alivyotii
akabatizwa na Yohana mbatizaji. Soma (Yohana 3: 13- 16), ni ubatizo uliotoka
kwa MUNGU aliye hai ndiyo maana unabatizwa kwa jina la BABA, MWANA NA ROHO
MTAKATIFU. Sasa tendo hili likiwa tofauti na lile la MUNGU alilomtuma Yohana
aje afanye kwa njia ya maji mengi tayari hapo ni kumuasi MUNGU na kuvunja
sheria zake alizozihakikisha akipiga muhuri ya kuwa (NDIZO TU).
Nitatoa
mfano katika ulimwengu huu umeshajiuliza swali Je? Ni kwa nini bunge likitunga
sheria hata kama wamezipitisha muda huo hazianzi kutumika mpaka Rais wa nchi
azikubali na kusaini na kupiga muhuri. Na endapo hatazisaini sheria hizo hakika
hazitatumika na serikali hiyo. Je? Unaelewa mpaka sasa? Sasa nakurudisha katika
biblia ambayo ndiyo katiba ya mkristo ambayo maneno yake ameyahakikisha MFALME
WA WAFALME yaani MUNGU ili watu wote waifuate na akasema kisiongezwe neno
lolote wala kupunguzwa akasema na OLE WAKE yule atakaye vuruga au kufanya
tofauti (Ufunuo Wa Yohana 22: 18-19).
Sasa
katiba ya MUNGU imevunjwa na baadhi ya wanadamu wenye kiburi cha kumdharau
MUNGU. Na wengine wamevunja au kushiriki bila kujua; sababu hawaijui kweli, ila
leo utaijua kweli nayo itakuweka huru. Na ujumbe huu ni kwa ajili ya ulimwengu
wote na mataifa yote.
Tarehe
15.11.2013 muda wa saa tisa mchana kwa saa za Afrika mashariki, nilikuwa katika
ibada katika kanisa langu. Kabla sijaanza kuhubiri akaja mbele yangu,
akaniambia, Hebron wafundishe watu wote wanijue mimi na wasiangamie. Kazi ya
kanisa imeharibika, kanisa limenikataa ndani ya mioyo yao ila kwa midomo yao
hunitaja tuu wala mimi sipo nao, sababu mimi na BABA yangu na ROHO MTAKATIFU
tunaliangalia Neno La MUNGU tuu kama lilivyo, likiwa tofauti tayari hilo silo
Neno La MUNGU aliye hai. Neno lake halibadilishwi ameshalihakikisha na vifungu
vyote. Niliogopa! Akaniangalia machoni akaniambia USIOGOPE. Haya niliyokueleza
waeleze watu wote nawataka wawe watoto wangu yaani wafuasi halisi wa mimi YESU
WA NAZARETI na niliye pia BABA yako.
Akaniambia
nipo na wewe katika ibada na Malaika na Serikali yote ya mbinguni tumekuja
kushiriki pamoja na wewe na kanisa lako ulilokabiziwa na BABA, uliongoze mpaka
ule mwisho wa ulimwengu huu au maana nyingine mpaka ujio wangu mimi mara ya
pili kuja kimwili; akamaliza, akaniacha, nikatafakari nikiwa nimekaa kwenye
kiti japo muda huo kanisa walikuwa wanaimba na kumsifu MUNGU, ila wao
hakujifunua kwao ili wamwone. Na mengi aliniambia ila sitayaandika hapa.
Ndugu
msomaji au wasomaji wanaopenda ukristo Je? Kwa nini unabatizwa ubatizo wa maji
ya kichwani halafu unajiita wewe ni mkristo halali? Nimekueleza ukweli, YESU
ameniambia watu wote na watakaoendelea na ubatizo huo, WAJIJUE WAO SIYO
WAKRISTO WA KWELI AU WAFUASI WANGU WALA SIYO TAWI LANGU, wala MUNGU siye
mkulima au mwanzilishi wa ubatizo huo wala Serikali ya Mbinguni. Na hata katika
biblia aliyoichagua yeye na akasema tuifuate hapo. Na kama haupo ina maana wote
waliobatizwa ubatizo huo wa kikombe wamewekewa pando lisilojulikana, na kama
halijulikani asili yake na wote walioshiriki pando hilo la shetani na wao ni
pando la shetani.
YESU
anarudi muda wowote ameniambia, waambie wanadamu wanirudie mimi na ile siku
wengi watalia na kusaga meno wakisema wao ni wakristo halafu nitawaambia
siwajui nyie, wote wanaojiita wakristo na wamebatizwa ubatizo wa maji ya
kikombe, hamtaenda mbinguni, huo ndio ukweli, na kama huamini ile siku ya mwisho utakumbuka maneno haya.
Nimekupa siri ili upone hata wanaobatiza ubatizo wa kikombe ameniambia hao siyo
watumishi wake 100%.
Yeye
hakufundisha wanafunzi wake ubatizo huo na aliwafundisha ili sisi tuige tufuate
mfano huo huo. Sasa, nikuulize swali, hivi hata kibinadamu Mwalimu
anavyokufundisha darasani kitu fulani si iliukijue na ukifanye hicho? Sasa,
anapotunga mtihani akakuuliza swali alilokufundisha ukajibu lingine tofauti je?
Atakupa vyema au tiki (√) au atakukata (X). Sababu ya kukupa X ni umekosea.
Turudi katika somo la ubatizo aliouamrisha na kufundisha hapa Mwalimu ni MUNGU
aliye hai na wanafunzi ni wanadamu. Je? MUNGU alifundisha ubatizo upi ufuatwe?
- Ubatizo wa maji ya kikombe? Jibu
siyo hivyo X
- Alifundisha ubatizo wa maji mengi
kwa watu wote kijito cha utakaso na alimtumia Yohana Mbatizaji kufundisha.
Ubatizo
ni kadi ya mwanachama au mfuasi wa YESU wa kweli na kadi original ni ubatizo wa
maji mengi yanayotembea katika kijito cha utakaso. Ila kadi feki ya fojari ya
wanachama au mfuasi wa YESU wa uongo (kuzimu) ni ubatizo wa kikombe. Mpaka hapo
unazidi kuelewa, sasa tupa hizo kadi feki za ukristo yaani ubatizo usiopo
katika biblia. Ukibatizwa na kuokoka kikweli kwa ubatizo wa maji mengi na uhame
kabisa hiyo kambi ya wakristo feki na uwafundishe na wengine ili wasiwe feki,
maana najua wengi hawapendi kuwa mkristo feki au siyo? Sasa umejijua vizuri na
usiwe mchoyo kumweleza na mwingine hata ikibidi mwambie aingie katika website
ya www.prophethebron.org na aingie
katika blog yangu atapona na wewe utabarikiwa sababu YESU atazidi kuwapata
wanachama hai na sio wafu.
Cha
ajabu baada ya kutafakari ujumbe huu kwa muda ya siku mbili zaidi na
nikiendelea kuomba. Nikapiga picha katika ulimwengu wote, nikaangalia jinsi
wakristo wanaojiita kwa jina lake wanaempenda wanapigwa upofu na kupewa kadi
feki pasipo wao kujijua. Na hii yote ilisababishwa na wamisionary walioleta
injili Afrika na katika mabara mengine hawakuleta injili ya kweli kama
ilivvyopangwa na MUNGU. Wakabadilisha, hii ndio injili ya mapokeo ya wanadamu!
Sasa nikuulize swali, Je? Wewe unataka injili
ya wanadamu au injili ya YESU? Jibu ni YESU WA NAZARETI. Sasa kwa nini watu
wanapewa injili za wanadamu badala ya injili ya YESU ya kweli? Sababu ni baada
ya wale mitume wa kwanza wa YESU kuondoka na wengine kuuwawa na wale wanafunzi
wa mitume walipokufa au kuuwawa, ndipo injili ikabadilishwa. Na sababu za hao
mitume kuuwawa mfano; Petro, hao waliomuua walimuua kwa sababu ili kuvunja
ukristo wa kweli na kuyaharibu au kuyakataa mafundisho ya ubatizo wa maji mengi
ile waliokataa. Ndiyo maana wakauwawa, hawa ndiyo majasiri ndiyo maana wapo
mbinguni wamekuwa ni moja wapo ya wazee 24 waliopo mbinguni kwa sasa.
Na
pia ukiangalia wale waliomuua Petro enzi hizo na wakaweka kaburi lake mpaka leo
hii, Je? Kama kweli wangekuwa wanamuenzi mtume Petro kwa yale aliyoyafundisha
wangebatizwa ubatizo wa maji mengi. Ila sababu walimuua ni ili wapoteze
kumbukumbu za mafundisho ya kweli ya ubatizo wa maji mengi na kuwafanya watu
wawe wakristo feki, ambao YESU ameniambia hawajui kabisa. Hata hao wanaotaja
majina ya watoto wa YESU yaani wale mitume wa kwanza, ingekuwa kweli wana
waheshimu au kuwapenda wangebatizwa
ubatizo wa maji mengi, ile ambayo walitumwa na YESU waineze katika ulimwengu
wote.
Nikuulize
swali, sasa je? Huu au hii injili ya ubatizo wa maji ya kikombe huku ndiko
kueneza injili ya kweli au ndiko kuua ukristo? Jibu, ndipo kuua ukristo.
Wanabatiza ubatizo tofauti na alioagiza YESU WA NAZARETI (Mathayo 18: 19-20)
“wabatizwe wawe wanafunzi wangu na mkiwafundisha kuyashika yale yaliyoyangu.”
Sasa ewe mwanadamu hapo watu wamepigwa chenga na shetani na leo hii ujue kama
unabatizwa ubatizo wa kikombe ujue shetani amekuweza na amekupiga chenga na
akakufunga goli yeye amekuwa mshindi kwako!
Fanya
zoezi upya, ubatizwe ubatizo wa maji mengi, hapo utakuwa MKRISTO HALISI.
Kinyume na hivyo jehanamu inakuhusu tokea hapa duniani, hiyo ni ticket ya
kuenda jehanamu hata kama unatoa sadaka, unasali sana, unaimba na kumsifu.
Mwenye chama siku akija atawachukua wale tu wanachama wenye kadi zake na awape
makao. Na hata sasa wote wote wanaokufa wakiwa wamebatizwa na kikombe wanaenda
jehanamu na nimewaona LIVE LIVE. Zile ibada za maziko ni imekuwa kama desturi
tena.
Na
waonye wale wanaosema wewe uliyekufa umetutangulia mbele za haki na sisi
tutakufuata. Laiti ungejua ungefuta hayo maneno, haujui kama ameenda mbinguni
au kuzimu. Kwa kinywa chako unajipatanisha na usichokijua na hiyo roho inakaa
ndani yako. Na mnavyosema mbele za haki, ni kweli, haki kweli kweli inafuatwa.
Siyo kama haki za hapa duniani, unaweza onewa, pendelewa, honga upate msaada.
Huko hakuna muda ni sasa na leo, maana hata kesho hujui kama utaishi; fanya
maamuzi.
(SOMA
KITABU CHA UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE CHA NABII HEBRON).
OKOKA
BWANA YESU WA NAZARETI
NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE UNIANDIKE KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA
MILELE NIBADILISHE NIWE MKRISTO WAKO WA KWELI, NIONGOZE NIBATIZWE UBATIZO WA KWELI. AMEN.
NOTE
Fanya
maamuzi haraka YESU WA NAZARETI anakuita uwe wake. Ukigoma ubatizo wake na
kukaa katika utakatifu hautamuona milele. Ila jehanamu ndiyo imeandaliwa
shetani na wanadamu watakao muasi YESU WA NAZARETI.
NABII
HEBRON