Pages

Friday, January 10, 2025

JANUARY MPAKA DESEMBA HAYO NI MAJINA YA MIUNGU


JANUARI MPAKA DESEMBA HAYO NI MAJINA YA MIUNGU.
 
BWANA YESU ASIFIWE!
Zimebaki siku chache mpaka mwisho wa mwaka na tunakwenda kupokea mwaka mpya. Napenda kukufundisha kwamba ni vizuri kujua inawezekana ukawa unapokea miungu katika mwaka mpya pasipokujua au kujua, na hili ni jambo limefanyika miaka nenda rudi watu wanapokea miungu badala ya MUNGU haijalishi ameokoka, haijalishi ni mpagani, haijalishi ni mkristo haijalishi ni muislam, kwa kujua na kutokujua wanakuwa wanapokea miungu. 
Aliyeanzisha mwaka ni MUNGU na aliyeanzisha siku ni MUNGU, lakini kuna siku za miungu pia. Ukisoma kitabu cha Mwanzo 1:1-5 utaona MUNGU akaifanya siku na ukiendelea kusoma biblia utaona siku ya kwanza MUNGU aliumba mbingu na nchi, siku ya pili alifanya nini, siku ya tatu akafanya nini, siku ya nne akafanya nini, siku ya tano akafanya nini, siku ya sita akafanya nini, haya yote yapo kwenye kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza. Lakini kuna jambo ambalo limefanyika kwa kujua au kutokujua ambao ni mpango wa shetani mtu anaweza kupokea wiki kwa kuanza na Jumatatu. MUNGU hajaita Jumatatu wala hajaita Monday ameiita "siku ya kwanza" inapokuwa Jumatatu ina maana mtu anasema mungu Jumatatu; kuna mungu Jumanne, kuna mungu Jumatano, kuna mungu Alhamisi, kuna mungu Ijumaa, kuna mungu Jumamosi na kuna mungu Jumapili na hata katika Biblia haijaandikwa Jumapili imeandikwa "siku ya Saba". Hii yote ni kumfanya mwanadamu anapozikiri hizo siku anakuwa amemnyanyua mungu kwa jina ya hiyo siku mfano: Jumatatu, Jumanne au Jumatano, hapo kuna utukufu huyu mungu Jumatatu, Jumanne, Jumatano anaichukua katika siku yako na kufanikiwa kwako kwa siku hizo itakuwa kwa shida sana au utafanikiwa kwa neema ya MUNGU.
 KUMBUKUMBU LA TORATI 15:1, 14:28, 11:11-12
 
MWAKA
MUNGU anaujua mwaka na Biblia inautambua mwaka na miungu pia inatambua mwaka lakini ina miaka yao. BWANA YESU ASIFIWE! Mwaka unapoanza unaanza na jambo jipya na kuna mwanzo mpaka mwisho wa mwaka. Mwaka unasiku 365, na MUNGU ni wa ajabu sana alishakwisha waandaa wanadamu kwa kuweka hivyo vitu ndani ya mwanadamu akijua kuwa wakati ukifika nitamtumia huyu au huyu. BWANA YESU ASIFIWE, Tunafahamu nchi ya Misri, ni nchi ambayo MUNGU aliiandaa kwa ajili ya vitu vingi; Musa alitoka pale, YESU alihifadhiwa pale kwa muda akarudi, kina Yoshua na Yeremia na hata Yakobo walikuwa kule na pia elimu ya utaalamu ya ujenzi kama Pyramid, architects, engineers kwa kiwango kikubwa walitoka Misri na hata mpaka sasa ni maarufu katika eneo hilo. Nikirudi kwenye neno husika hapo juu MUNGU hakusema mwezi wa Januari alisema mwezi wa kwanza, mwezi wa pili, mwezi wa tatu. Watu wengi wanausubiri Januari, sasa Januari ni jina la mungu anayeitwa Janus; mungu wa Kirumi, Februari anaitwa Februa ni mungu wa utakaso wa Kirumi, Machi anaitwa Mars ni mungu wa vita ambaye ni mungu wa miungu ya vita wa kwao ambaye alikua anatumiwa na watu wao zamani, Aprili anaitwa Apru ambaye ni mungu wa upendo wa kiungu, Mei anaitwa Maia ni mungu wa mzunguko wa anga ambaye alikuwa anakaa katika milima ya atlas ana jicho la mbele na ya nyuma kwa hiyo anaona kila mahali, mambo ya Warumi haya. Mnapoita hii miezi kwa majina yake ina maana miungu inaendelea kutukuzwa na wanaendelea kuishika miezi husika. Juni anaitwa Juno ni aina ya mungu mkuu, Julai anaitwa Julius Ceasar ni aina ya mungu, Agosti chanzo chake cha kuitwa Agosti ni Agusto huyu alikuwa ni mtoto wa mfalme wa kumlelea kwa hiyo akaitwa jina la kumbukumbu, Septemba ambaye ni mwezi wa tisa kwa kilatin inaitwa Septem na ina maana saba, bado tumedanganywa siyo mwezi wa tisa.
Tumeambiwa kuwa Oktoba ni wa kumi, Oktoba kwa kilatini siyo kumi ni nane unaona mdanganyo huu, Novemba wa kumi na moja ila sivyo Novemba kwa kilatini ni tisa, Desemba ni kumi kwa Kilatini. Haya majina yote ni miungu. Ukiangalia kalenda zote na diary zimeandikwa majina ya miungu. Kalenda zinatakiwa ziandikwe mwezi wa kwanza, mwezi wa pili, mwezi wa tatu, mwezi wa nne, mwezi wa tano, mwezi wa sita, mwezi wa saba, mwezi wa nane, mwezi wa tisa, mwezi wa kumi, mwezi wa kumi na moja, mwezi wa kumi na mbili kwa lugha zote. Unapotumia hayo majina ya miungu unaendelea kushikiliwa na kukamatwa maana wana uhalali kwa njia hiyo ya kutamka majina yao. Ni mipango ambayo shetani alipanga sana na kuificha. Mwisho wa mwaka watu wanafanya mambo ya matambiko sana na ni huyu mungu Desemba anasaidia katika vitengo hivyo katika ulimwengu wa roho. Kuna wakati fulani MUNGU alikuwa ananituma mahali, akamtuma malaika Gabriel akaniambia "nimetumwa na BABA MUNGU kutoka mbinguni, tarehe fulani mwezi fulani uende nchi fulani kwa majira ya nchi yako majira ya Afrika mashariki"; siku ya tatu siku ya pili, hajawahi kuniambia Wednesday (Jumatano) au Tuesday (Jumanne). MUNGU hajaumba Jumatatu, MUNGU hajaumba jumanne, hakuziita Tuesday (Jumanne) au Wednesday (Jumatano) wala Saturday (Jumamosi) au hata Sunday (Jumapili). MUNGU hata YESU hajawahi kuniambia Uwahi kanisani Ibada kanisani Jumapili ananiambia "Siku ya Bwana uitakase siku ya saba" ilikuwa inanichanganya muda mrefu; akaniambia "Nakufundisha Hebron, dunia imepinduliwa!" sasa ukija ukakuta mambo niliyokuandikia leo kama Desemba ni kumi unaambiwa ni kumi na mbili, nani aliyewaloga enyi Wagalati, aliyewaloga dunia? Kwa hiyo unaposema hayo majina yote, hayo ni majina ya miungu. Hii dunia ukisema ukweli kuna wengine wanachukia wanasema "anasema nini?" kwa hiyo nikuche ufe? Kama wewe hutaki ukweli wako wanaopenda ukweli na watapona. Biblia inasema kila kitu kwa wakati wake na majira yake. Tuje kwenye habari ya saa (majira); saba ndo inaitwa saa moja, saa nane inaitwa saa mbili, saa tisa inaitwa saa tatu BWANA YESU ASIFIWE, Kumi inaitwa saa nne; hata kwa Kingereza kumi ni ten kwa jina lake. MUNGU anajua muda wake na wakati wake kwa saa, dakika na muda.
Tunajua MUNGU siku yake moja ni miaka 1000 usije ukafikiri kwanza ni hizi siku saba za umbaji sivyo; katika siku moja miaka 1000 MUNGU aliumba vitu vingi sana usione kuna wadudu, miti, majani; hizi ni habari njema nakufudnisha wewe. Leo hii hakuna mwanadamu aliyemaliza siku moja ya MUNGU wanakufa katika masaa, nasema hivyo jwa sababu kama siku moja ni miaka 1000 na wewe una miaka 20 si sekunde au dakika hizo umekufa. Unakwenda kumaliza mwaka hakikisha unakwenda kupokea mwaka kwa kukataa kabisa kusema Januari ndo maana Januari inaanza na ugumu, shida, unampenda MUNGU ila unapokea mwaka na Januari ni miungu umeipokea, unchokikiri kwa kinywa chako ndivyo ilivyo, sema naupokea mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu mpaka wa kumi na mbili na kumshukuru MUNGU, lakini mambo ya kusema Janus, Januari, Februa siyo sahihi ni kukataa hiyo miungu. Malango ya shetani yameanda Januari jini, Januari miungu yote hayo ili kuhakikisha wamekamata siku za MUNGU, hawajaumba kitu hao wote ni feki na katika kukiri na kufuata hiyo miezi unaweza jikuta unaishi maisha feki kwa kusema mambo ya Februari, Machi na ndo maana kuna mambo hayatokei na mambo huyapati, hao Februari na Machi wanapambana katika ulimwengu wa roho, uendelee kuifuta pale ulipotaja hayo majina katika ulimwengu wa roho hata ukizitaja zisifanye kazi katika ulimwengu wa roho na kuzimwagia damu ya YESU katika ulimwengu wa roho. Badilisha usemi wa hayo majina katika maombi hayo, moe MUNGU haki yake, sababu MUNGU husimama katika haki yake. Shetani aliiba vitu vingi vya umbaji wa MUNGU na kuvibadilisha mpaka kwenye siku, masaa wewe unaambiwa saa sita ni kumi na mbili?! ukirudi kwa Kirumi wao moja ni moja hata kwenye maandishi ya majira (zile saa za Kirumi I,II,III n.k) ila mifumo ya Freemason inakufanya uende nyuma ya wakati wako, nyuma na miezi yako na shughuli zako, endelea kuwanyanganya kwa maombi ukikiri kuwa hiyo miezi haina mamalaka na maisha yako na vitu vyako na kumkabidhi BWANA YESU amiliki na kutawala maisha yako kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa kumi na mbili; hivyo wale wachawi au wanga wanaokutafuta kwa siku ya Jumatatu au Jumamosi au mwezi wa Januari au Agosti hawakuoni wala kukupata.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE, NISAMEHE PALE AMBAPO NILITAJA MAJINA YA miungu BADALA YA KUTAJA MAJINA SAWA SAWA NA UMBAJI WAKO, NINAOMBA UNIFUTIE HAYO MASHTAKA HAKIKA NIMEJIFUNZA NA SITARUDIA TENA. NAOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU NA KULIANDIKA JINA LANGU KWENYE KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE. ASANTE BWANA YESU. NAKUPENDA SANA.
 
PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.