Pages

Tuesday, November 5, 2019

WALIOALIKWA HARUSINI


BWANA YESU ASIFIWE!

SHALOM watu wote. Karibuni katika elimu ya Neno la MUNGU ili kuwafunulia ukweliwa Neno lilivyo kama MUNGU wetu alivyo mkweli na siyo mwongo. Katika somo hilinapenda kuelezea kwanza maana ya harusi. Kibinadamu harusi inajulikana ni shereheya watu wawili wanapo sheherekea kuwa mwili mmoja yaani kama vile baba na mamakuwa mume na mke, ila harusi ninayoongelea hapa kama ilivyoandikwa katika kitabucha Mathayo 25:1 na kuendelea katika Neno la MUNGU, hii ni harusi ya walioalikwakwenda Mbinguni kusheherekea ushindi wa milele na kustarehe na BWANA YESUmilele mbinguni. Napenda kuwajulisha watu wote ya kuwa YESU wa Nazaretiameshawaalika watu wapokee kadi za mwaliko, ambayo kadi hiyo ni wokovu kumkiriYESU awe ndio Bwana wako na mwokozi wako. Unapomkiri anakuandika jina lako,anakuwa tayari ameshakualika kwenda mbinguni, ila unapokataa kuokoka ujieleweunakataa kwenda mbinguni wazi wazi, kwa hiyo usije ukajuta siku ile ya hukumuutachomwa moto.

Nawasihi mzitupe kadi za harusi ya shetani, najua watu wengi watajiuliza je mimi sinahiyo kadi au kusema sizijui. Nataka nikueleze siyo kadi za kimwili ni kadi za kirohoambazo ni kumkiri YESU, uokoke na tena uongozwe sala ya toba na mtumishianayeongozwa na Roho wa kweli na siyo anayeongozwa na roho ya unyang'anyi aukuwatoza watu pesa ndio awaombee. Napenda muelewe hata huyo hana Roho wakweli kutoka mbinguni (zijaribu hizo roho). Roho wa kweli wa MUNGU hutoa bure,huponya bure. Kwa wale wanaoenda au walioenda kwa waganga watawasikiawakisema mungu anasema leta malipo kiasi fulani ndio akufanyie jambo lako, sasanapenda muelewe hata roho ya uongo imeingia katika makanisa mengi duniani na kwabaadhi ya watumishi katika ulimwengu wote. Wapo ambao ni wachungaji huwawanaenda kuzinunua hizo roho kwa shetani ili wapate pesa wakitumia jina la YESU,hao shauri yao, moto wa jehanamu unawasubiria na tayari majina yao yapo katikaorodha ya kuchomwa, ingawaje wanahubiri na wana makanisa, iwe ni Nabii, Mtume,Mchungaji, Mwinjilisti, Mwalimu, Shemasi, Askofu sehemu yao ni katika ziwa la motokwa sababu wametumika kusambaza kadi za shetani na kuwapa watu ili wakatae zaYESU.

YESU amenituma niwakaribishe watu wote wa nchi zote kukaribia kwenda mbingunikwa kuokoka, mkatae kadi za shetani na za mpinga kristo. Kuwa mkristo wa jina tuhalafu usiokoke hapo umedanganywa, ili uwe mkristo ni lazima uokoke umkiri YESU nauishi maisha matakatifu, siyo kujiita mkristo halafu bado ni mchawi, unafanya dhambi,na hutaki kuokoka. Unatakiwa ujielewe ni upendo gani alionao MUNGU kutualikambinguni na ukaishi milele. Akamtoa mwanae wa pekee awe ni kadi yetu ili tumpokee,ila watu wengi ni wanafiki kwa YESU wanajiita ni wafuasi wake lakini ukimwambia mtuaokoke anakataa anasema yeye bado ni wa shetani, tayari katika ulimwengu wa rohoanayo kadi ya jehanamu pasipokujua au kwa kujua, ila unapookoka unapewa kadi ya
kwenda mbinguni na Roho Mtakatifu. Sasa uitunze kadi yako, yaani wokovu wakomaana adui hatakupenda kwa sababu umekataa mwaliko wa kuchomwa pamoja nayeye. Na jambo la ajabu unaweza kukuta kanisa linamtaja YESU lakini ukiokoka ukiwakatika kanisa hilo wanakutenga eti umepotea. Nakutia moyo mwana wa Munguhaujapotea bali umetoka njia ya jehanamu, ila waliopo hapo wao ndio wapo kwenye njiaya jehanamu kabisa na katika hiyo madhabahu kuna roho ya kuzimu inayoongoza hapoau roho ya mpinga kristo ndio inaliongoza hilo kanisa, ndio maana inachukia kwasababu unapookoka unakuwa umevunja agano la kwenda kuchomwa moto. Nakusihiwewe uliyeokoka jipe moyo, songa mbele kwa maana utasheherekea milele mbinguni.Injili inahubiriwa sana ila ipo inayochanganywa na uongo, hii ya uongo hata ukiongozwasala ya toba napenda kukujulisha katika njia hizo bado haujaipokea kadi ya mbingunikwa sababu wanaongozwa na roho ya uongo au mpinga kristo. Wapo wanaotumiauchawi kuhubiri na hawa ndio wengi sana wanafikia 90% katika ulimwengu wote ila siyorahisi kujua mpaka uwe una macho ya rohoni au kwa Neema ya MUNGU akujulishekwa sababu watu hao wamepewa nguvu ya kujificha wasijulikane na watu, haijalishiwatawadai watu pesa za maombezi, kuwabatiza watu kwa majina yao, kufanya miujuzaya kichawi na wakisoma biblia na wengine wakijiita wao ni YESU au MUNGU.Sasa kwa neema ya YESU amenijulisha ili niwajulishe watu ukweli ili waende mbinguni.Kataeni kualikwa kwenda jehanamu, kataeni kadi zao, mjitenge nao kiroho hata kimwili,usishirikiane nao kabisa kwa sababu roho yako itapotea kwenda gizani kwa sababuinakuwa imepewa kadi ya mwaliko wa kwenda kuchomwa moto. Shetani amewapawatu roho ya kiburi sana, watu hawataki kuokoka na wengine wanajaribu hata kusemakabisa kuwa hakuna MUNGU, tubu haraka kabisa na mkaribie YESU upokee kadi yamwaliko wa kwenda mbinguni.

Sema, BWANA YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote, nakataa kadi yajehanamu, naiteketeza kwa Damu ya YESU, nimejua kumbe kama sijaokoka kumbeninayo kadi ya kwenda jehenamu na mimi sitaki kuchomwa moto. Nakupokea YESUuwe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu, asante kwa kadi ya kuingia mbinguni,nitaitunza siku zote, nikijua kuna ile siku ya mwisho, Malaika na serikali yako mbinguniwataniuliza kadi iko wapi, niwezeshe niitunze siku zote. Amen.

ANGALIZO:Mbinguni hamna mtu atakayeweza kuzamia au kuingia bila kuokoka au kuingia kwakumtumia mtu aliyealikwa, HAPANA. Siku ile kila mtu ataulizwa peke yake, heri ujuesasa na kuelewe. Karibu sana katika sherehe ya harusi ya kumsubiri BWANA YESUambaye ni mpendwa wetu, ambaye muda wowote atakuja, uwe tayari.

PROPHET HEBRON.