HAPPY
PASSOVER 2018
HERI YA
PASAKA 2018
Siku ya kukumbuka kufufuka kwake BWANA wetu na mwokozi wa
maisha yetu kwa wanadamu wote, kwa wale ambao watamuamini na kuokoka na kuishi
katika maisha matakatifu hao wataurithi ufalme wa mbinguni na siku moja
atawapokea mahali pa paradiso alipo yeye. Zaidi napenda kukumbushia kwa
ulimwengu wote wamrudie YESU watubu na kuokoka YESU anarudi wakati wowote na
akirudi akikuta haujaokoka kwa kweli hatakuchukua utabakia katika mateso na
Jehanamu sababu Jehanamu imeandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake
pamoja na wale wanadamu wote ambao
watakataa kuokoka, kumpokea YESU. Basi YESU aliniambia niwaeleze na yeye atawakataa
siku ile mbele ya BABA yake, hivyo wakati huu ni wa neema.
Kipindi cha pasaka ni kwa ajili ya ukombozi wa wanadamu
lakini cha ajabu hata binadamu hawa wengi sana hawataki wokovu wanabakia
kujiita wakristo jina tu, yaani hawaokoki, hawamkiri na kufuata njia zake, watu
hao jehanamu ndio sehemu yao, sasa rejea kwake ipo siku utayakumbuka maneno
haya na neema itakuwa imeshapita, milango imefungwa hata ukitubu hausikiki
tena.
Napenda mkumbuke kuwa pasaka haiitwi Easter haya ni makosa
makubwa zaidi soma katika blog hii nimeelezea kuhusu neno Easter ni nini. Easter
ni mungu wa kike aina ya sungura. Sisi wakristo hatupaswi kumsherekea yeye na
katika biblia hakuna neno easter ndio pasaka bali pasaka ni pasaka na kwa
kingereza ni Passover. Hata waisraeli wenyewe hawasemi Happy easter wanasema Happy
Passover.
Muepuke chachu ya Mafarisayo ujumbe mkuu aliouacha YESU.
Nawatakia Pasaka njema, Happy Passover.
APOSTLE
HEBRON.
