ANDIKO LENYE PUMZI YA MUNGU LINAFAA NA
ANDIKO LISILO NA PUMZI YA MUNGU HALIFAI!
BWANA YESU asifiwe, watu wote wa mataifa yote
mlioubwa na Mwenyezi MUNGU na aliyetupa Neno lake lenye pumzi ili tulifuate na
litufae katika wokovu wetu na ukristo wetu Mtakatifu. Ukisoma katika Kitabu cha 2 Timotheo 3:16-17, 16Kila andiko, lenye
pumzi ya MUNGU, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaongoza, na kwa
kuwabadilisha katika haki; 17ili
mtu wa MUNGU awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Utaona jinsi MUNGU alivyotupa andiko lenye pumzi
yake ili utakapolifuata upate kuwa mtu kamili na kukuongoza wewe ili upate
kufanikiwa na uwe na ushindi na uzima. Ninavyosema andiko lenye pumzi ya MUNGU
nina maanisha ni Neno la MUNGU kama lilivyoandikwa bila kuchanganywa na uongo,
yaani nuru na giza kutawala pamoja na kwa maana nyingine ni Neno la MUNGU kama
lilivyo bila kubadilishwa na ndio sababu akaonya lisiongezwe wala kupunguzwa
sababu alijua yale aliyoyaweka tayari yanatoka katika kinywa chake na hayo
yatakayo ongezwa hayajatoka katika kinywa chake, hivyo hayana uzima kwa viumbe
vyake na ikiwa hayajatoka katika kinywa chake hayana pumzi yake bali yana pumzi
ya mungu asiyejulikana na anayaingiza ili kuuwa roho za wanadamu ili hao
wanadamu wasifike mbele za MUNGU.
Nitaeleza mimi Nabii Hebron kwa ufupi baadhi ya mifano ya maandiko yenye
pumzi ya MUNGU na kisha yakabadilishwa na mpinga kristo na mawakala wake ili
kuwaongoza wanadamu na kuwatenganisha na Mwenyezi MUNGU kwa njia hiyo, hayo
hufanywa na baadhi ya watumishi ambao wana ushirika na shetani na kuagizwa
kuendeleza maandiko yenye pumzi ya shetani, mfano:
1. Ubatizo ni mmoja tu tena ni mtoni na ndio
alioagizwa Yohana na YESU; Yohana akafuata ubatizo uliotoka katika kinywa cha
MUNGU na ndio uliopo katika Biblia. Ubatizo mwingine wowote tofauti na huo
haujatoka kwenye kinywa cha MUNGU. Ubatizo
ambao hauna pumzi ya MUNGU ni wa kikombe, wa kisima, kubatizwa kwa jina
la mtumishi. Sasa cha kujiuliza ni kwa nini ulimwengu umepotezwa na kufuata
maandiko yasio na pumzi ya MUNGU na kumlazimisha MUNGU akubali yale ambayo
hayajatoka katika kinywa chake ndio yafuatwe kama vile yeye MUNGU hajui kazi
yake aliyoipanga au mwanadamu kutaka kumfundisha MUNGU wakati ni kitu ambacho
hakiwezekani kabisa? Hivyo basi yakupasa uelewe kuwa ubatizo wowote ambao ni
tofauti na ule ambao alibatizwa YESU, yaani mtoni, ni batili (fake)
na kama umebatizwa hivyo utakuwa umepokea ubatizo ambao MUNGU hajautaja na
unapoupokea basi umebatizwa na miungu au mungu asiyejulikana na kukufanya kuwa
mkristo asiye na MUNGU anayejulikana na hatimaye safari ya maisha ya mtu
huishia kwa mungu asiyejulikana. Hivyo basi yakupasa kubatizwa kama YESU na kwa
kufuata Kitabu chake na Sheria yake na siyo kwa kuleta sheria za kuwaongozea
watu ambazo haziko katika Biblia Takatifu.
2.
MUNGU anasema msiwatoze watu pesa mnapowaombea, soma Mathayo10: 7- 8. Lakini
bado watu wanatozwa pesa za maombezi, unapo ona hayo uelewa kuwa ipo nguvu ya
shetani ndani ya mtumishi huyo aidha ni wakala wa shetani anajificha kwa kutumia
jina la YESU. Hebu muulize ni kwa nini unatoza pesa? Je! Ndivyo Neno lenye
pumzi linavyosema? Hatakuwa na jibu!
3.
Imeandikwa msiabudu sanamu, lakini utashangaa wakristo na baadhi ya watu wana
abudu sanamu, sasa kuabudu sanamu sio neno aliloliamuru MUNGU, bali
analikataa, ila watu wamekuwa na vichwa vigumu hawataki kumsikiliza MUNGU
anavyotaka bali hupenda kufuata yale ambayo hayaja amriwa na MUNGU.
4.
Imeandikwa nyumba ya MUNGU ni mahali pa sala tu, lakini utakuta inaitwa nyumba
ya MUNGU ila ni mahali pa harambee, michango, matambiko, na baadhi ni sehemu za
malango ya wachawi na shetani na kufanyia maagano ya makafara.
5.
Kwa watumishi imeandikwa msijisumbukie, bali mniulize Mimi nami nitafanya,
lakini wako baadhi ya watumishi huwalazimisha watoto wa MUNGU kutoa tena kwa
lazima, na sadaka yako inakuwa ni deni na utafuatwa mpaka nyumbani au kazini.
Hebu jiulize wewe unatoa sadaka au unalipa deni? Je! MUNGU wetu sisi ni MUNGU
wa madeni au ni MUNGU mnyang’anyi? Jibu ni HAPANA. Yampasa mtumishi amuombe
MUNGU na MUNGU atatenda, ila kwa wale watumishi waliojiita au kumwacha MUNGU au
kujitengenezea utumishi kwa njia ya uganga, hao ni lazima wafanye hayo ya
michango kupitia katika TV au radio au popote pale. Hebu muulize si imeandikwa
msijisumbukie maana nyie ni bora kuliko maua na mbona wanafanya hivyo na hilo
sio neno lenye pumzi ya MUNGU? Hawatakua na jibu!
Ukiwa
msomaji mzuri wa Biblia, utajua mambo mengi yanayofanywa na baadhi ya makanisa
au baadhi ya watumishi katika dunia hii kwa kiwango kikubwa utafahamu ya kuwa
MUNGU anachukiwa na wala haheshimiwi bali shetani anatukuzwa sana kwa
maandiko yake yasio na pumzi ambayo yanatumika katika baadhi ya makanisa,
lakini nataka uelewe kuwa sio kila kanisa au kila mtumishi anayetumia jina la
YESU ni wa kweli au ni makanisa ya kweli. Makanisa au watumishi wa kweli
wamebaki wachache sana, wengi wao aidha mmoja mmoja au kwa umoja wao wako kipesa
au kibiashara na wengine wametumwa na shetani kuangamiza roho za wanadamu ili
unapowafuata au unapofuata elimu yao, yenye michanganyo na uongo basi unakuwa
umepotea, jinsi alivyo kuhani ndivyo walivyo na kondoo wake.
Zaidi fuatilia YouTube za Prophet
Hebron kupitia www.prophethebron.org, utajifunza
mengi na kuokolewa, ni wakati sasa wa kila mtu ambaye anampenda MUNGU akatae
kabisa kupokea maandiko yasiyo na pumzi ya MUNGU, unapoyapokea tu unakuwa
umekufa kiroho, ila sasa ipo neema, pokea na kufuata Neno lenye pumzi ya MUNGU,
uchukue hatua ili ufufuke, sababu ulikuwa umekufa kiroho na katika ulimwengu wa
roho, MUNGU hakujui japo wewe utaona kuwa unampenda ila ulikuwa umepotezwa
ukaletewa mapokeo ya wanadamu, soma Mathayo
15:6-9.
Sema: Bwana YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote ikiwemo na dhambi ya
kupokea mafundisho yasiyo na pumzi yako, namkataa shetani na mafundisho yake na
kazi zake, naomba uandike jina langu katika Kitabu chako cha Uzima wa Milele na
naomba Neema ya kupokea mafundisho yenye pumzi Yako. AMEN.
NABII HEBRON.