NINI
MAANA YA KUZALIWA MARA YA PILI KWA MBEGU IHARIBIKAYO??
BWANA
YESU WA NAZARETI ALIYE HAI ASIFIWE. Ukisoma
katika kitabu cha 1 Petro 1:23 inasema hivi kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili si
kwa mbegu iharibikayo bali kwa ile isiyoharibika kwa neno la MUNGU lenye uzima
lidumulo hata milele.
Kwanza
kabisa nataka uelewe kuwa kuzaliwa ninayoelezea mimi Nabii Hebron ni kuzaliwa
kwa njia ya ubatizo, huko ndipo kuzaliwa mara ya pili. Kuzaliwa mara ya kwanza
ni pale unapotoka katika tumbo la mama ukiwa kitoto kichanga, huko ndiko
kuzaliwa mara ya kwanza. Inatokea kimwili kabisa, na kuzaliwa mara ya pili ni
ukiwa mtu mzima unaelewa nini kinafanyika na unaokoka. Ukisoma mpaka ule mstari
wa 25, inaelezea vizuri, hapo utaona Yakobo akielezea kuzaliwa mara ya pili kwa
mbegu isiyoharibika, ambayo ndiyo mbegu ya MUNGU wa kweli yaani kama neno
lilivyoagizwa katika Ufunuo wa Yohana 22:18-19.
Mbegu
hii ya ubatizo wenye uhai na uzima ni ubatizo wa maji yanayotembea katika mto
na siyo popote pale. Tazama YESU mwenyewe aliifuata mbegu isiyoharibika katika
mto Yordani na Yohana mbatizaji na yeye alifundishwa na MUNGU na akafanya hivyo
hivyo wala hakupunguza wala kuongeza sababu yeye alitokea mbinguni na ndiyo
sababu imeandikwa ubatizo wa Yohana ulitokea mbinguni na hivyo alijulikana ni
Nabii wa MUNGU wa kweli mpaka leo.
MBEGU
HII YA KUMFANYA MTU AZALIWE MARA YA PILI KATIKA HALI YA KUHARIBIKA KIROHO NI
IPI?
Mbegu
hii ni batizo za aina zote ambazo hazipo
katika Biblia. Katika Biblia upo ubatizo mmoja tu ambao YESU na yeye alibatizwa
katika mto Yordani. Soma Yohana 3: 11-17, na usipozaliwa mara ya pili kama YESU
imeandikwa hauendi mbinguni, Yohana 3:5-7. Sasa shetani na malaika zake na
mpinga kristo walianzisha batizo zao na kuzaliwa mara ya pili, kama mbegu
iharibikayo ili utakapokubali kuzaliwa kwa jinsi hiyo mbaya basi unakuwa
umejifungia wewe kwenda mbinguni sababu ya kiapo ulicho kipokea wewe cha mbegu
mbaya iliyoharibika, neno “iliyoharibika” ina maana ni mbegu isiyofaa isiyo na
uhai wa milele, ni mbegu yenye mauti ya milele.
Hata
mimi nilishazaliwa katika mbegu iharibikayo ambayo ni ya ubatizo wa kikombe, ila
namshukuru mwenyezi MUNGU alinijulisha nikajua nikabatizwa tena na kupokea
mbegu idumuyo ya neno la MUNGU na ile ya kuharibika ikatolewa. Kabla ya hapo
nilijiona nimezaliwa mara ya pili kama MUNGU anavyotaka kumbe nilizaliwa mara
ya pili kwa njia ya mbegu iharibikayo na maisha yangu ya kiroho yaliharibika
ila neema yake ilinigusa nikakubali kubatizwa katika kijito cha utakaso.
YESU akaniambia,
Hebron hivi nikuulize swali, wewe umeshaona wapi mkulima mwenye akili timamu
akapanda shamba lake mbegu zilizoharibika? Au wewe ukachanganyiwa mbegu nzuri
na zilizoharibika, je utachukua zipi? Nikajibu nitachagua zile nzuri tu na
nitaziacha zile mbovu. Akaniambia hivyo ndivyo ilivyo na katika kuzaliwa mara
ya pili kizuri na kibaya mimi nitachukua mbegu za neno la MUNGU na siyo mbegu
za asiyejulikana aliyezileta yaani hizo batizo ndizo mbegu zilizoharibika
hazijatokea kwa BABA yangu mbinguni na ndivyo ilivyo katika ulimwengu wote
wengi wamezaliwa mara ya pili kwa mbegu iharibikayo ili wasiurithi ufalme wa
MUNGU. Ila ni wakati wako sasa uchukue hatua uwatumie na wengine injili hii ili
kuzaliwa mara ya pili kama YESU na siyo tofauti na YESU. Shetani aliuchezea
sana ukristo na wokovu kwa sehemu kubwa na akawateka wengi ikiwemo kuzaliwa kwa
mbegu mbovu mara ya pili.
Nitaelezea
baadhi ya mifano ya mbegu zilizoharibika za kuzaliwa mara ya pili. Kwanza ni ubatizo
wa kikombe, ubatizo wa kisima, ubatizo kwa jina la mchungaji, ubatizo wa watoto
wadogo (maji matone) na zaidi soma katika blog
ya Nabii Hebron na usome kitabu cha “UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE” (kilichoandikwa na Nabii Hebron),
utaelewa zaidi na majibu yako utayapata.
Huu ni
wakati wa ujio wa YESU mara ya pili, wapo watumishi wa MUNGU wa kweli na wapo
wa uongo, wachawi, freemason, watumishi wa mishahara na wa utapeli hivyo uwe
makini sana. Unaweza ukaenda jehanamu kwa kupelekwa na mtumishi anayekupa mbegu
iliyoharibika ukajikuta unazaliwa mara ya pili kiroho ukaingia mkataba wa mauti
kabisa pasipokujua japo wapo katika dunia hii wametumwa na shetani kuleta
batizo ambazo sio za MUNGU ni za miungu, unapozipokea na wewe unaangamia
kiroho. Mbegu hii mbovu ikatae na ujiulize kama mtumishi anaongozwa na ROHO
MTAKATIFU mbona hakuelezi batizo hizi hazijatokea mbinguni! Elewe unaongozwa na
roho mchafu, kiroho na kimwili.
Ambaye
unapenda kwenda mbinguni ubatizwe upya na ukatengwe nao ufuate njia nyingine ya
kweli na MUNGU wako atakuwa ni kweli na siyo uongo.
NABII
HEBRON.