MAKAFARA
BABA katika
jina la YESU ninakushukuru kwa muda na
wakati huu kwa ajili ya ujumbe na somo kwa mataifa yote. Ninakushukuru, ninakutukuza
MUNGU. Amen.
Katika
somo la leo nitakwenda kufundisha kuhusu “Makafara”
yanayofanyika na wakristo makanisani. Makafara haya yanakuwa yanawasaidia
kufanya kazi za kanisa au huduma zao zinaendelea lakini watu wanafikiri ni kazi
ya MUNGU. Pia nitaelezea makafara ambayo wanadamu wanayatumia ili wafanikiwe
lakini nitakwenda kuyaharibu dunia nzima katika jina la YESU. Kwa sababu kuna
watu pia wanakuwa wanateseka hawafanikiwi kwa sababu kuna watu wanawatolea
makafara kwa mashetani, labda damu za wanyama, kuuwa watu, damu za wadudu na kuzinenea
mambo mabaya ambayo ardhi iliyapokea kwa hiyo hawafanikiwi.
Nitasoma
katika kitabu cha Kutoka 22:20 “20Mtu atakayemchinjia sadaka mungu yeyote,
isipokuwa ni yeye BWANA peke yake na aangamizwe kabisa.” Na ukisoma katika
kitabu cha Mambo ya Walawi 19:26, 28 “26Msile kitu chochote pamoja
na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.”28 “Msichanje
chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama
miilini mwenu, mimi ndimi BWANA.”
BWANA
YESU ASIFIWE! Katika muda huu nitakwenda kufundisha, kuna mambo ambayo
yanawatesa dunia nzima, mambo ya makafara. Hapo zamani MUNGU alikuwa akichukua
sadaka za wanyama, baadae baada ya kumtoa mwana wake wa pekee; damu yake
kumwagika hayo mambo akayaacha na akakataza, Shetani ndiyo ameyachukua, damu ya
YESU inatunenea mambo mazuri; inatunenea amani, inatunenea furaha kwa wale
ambao wamempokea BWANA YESU. Lakini Shetani na yeye akaweka namna yake ya
kuwafanikisha watu wake kwa kupitia nyama na damu za wanyama au hata watu labda hata wewe. Kule
kuzimu ili mwanadamu labda abarikiwe anaambiwa labda atoe watu au aangushe
magari, aangushe meli, aangushe ndege ili damu inapomwagika ndipo wanapata cheo
au umaarufu na njia nyinginezo nyingi za kufanya damu zimwagike pasipo amri ya
MUNGU hizo damu anakunywa Shetani.
BWANA
YESU ASIFIWE! Nitazungumza katika pande mbili ila nitaanza upande wa kanisa. Makanisa
mengi yanafanya makafara na yanajiita makanisa ya YESU lakini siyo nguvu ya
YESU inayofanya kazi. Nafikiri wengi mmeshasikia wanazika watu kanisani, wanazika
na vichwa vya watu, hayo ni makafara. Wanaweka watu ndipo shetani anawaletea
watu kuja katika jengo hilo na wanakaa wanaendelea kupata pesa wale watu
wanachukuliwa nyota zao ,vitu vyao na wanafikiri wanakwenda mbinguni kumbe
wametekwa na shetani. Jambo lingine nitaeleza kwa ufupi makafara ambayo shetani
anayatoa, ni ubatizo wa kikombe, ubatizo wa maji mengi, ubatizo kwa jina la mchungaji.
Mchungaji anapofanya hivyo au hiyo huduma shetani anaiba nguvu ya kuongezeka kwa kusanyiko kubwa kwa sababu hilo
ni agano la shetani, hapo ndipo unakuta wanadamu wanatekwa na shetani pasipo wao
kujua kupitia hayo makafara. Ni watu wangapi wamefanyiwa makafara leo hii?
BWANA
YESU ASIFIWE! Makafara mengine ni michango makanisani, hayo ni makafara, lakini
wanadamu hawaelewi, nataka niwaeleze nyie wenyewe ni mashahidi. Utakuta labda
mfanya biashara ni mchawi au ni freemason lakini anakuja kujenga makanisa na wachungaji
wanamkumbatia, wanapokea misaada, nataka niwaeleze kwamba, anapotoa tu zile
pesa zake nyie kanisa pia mmefanywa kafara na waumini hivyo hivyo. Haya ni
mambo ambayo yalikuwa yamefichika sana lakini ni wakati wake wa kuwaeleza
watoto wa MUNGU sasa wapone. Yapo makafara ya mapete ya vyeo vya kitumishi, unaona
wanavaa yale mapete makubwa hayo ni makafara. Haleluya. Ninachotaka kukuambia
pete ya unabii au uaalimu ikiwa mtu ana pete ya cheo fulani hilo ni kafara
either anajua au hajui ina nguvu inayofanya hiyo kazi.
Unaweza kuta labda ni
mwanasiasa kwenye kampeni amevaa lipete likubwa sana yale ni makafara watu wana
wafuata wengi sana. Anakuwa ameshafanya kafara kubwa shetani anafurahi kwa hiyo
anawavutia watu, kwa sababu ni maagizo
anayopewa.Pia yapo makafara ya kuua watoto wa MUNGU, lakini hao hawajui hiyo ni
siri wanajua watumishi wenyewe. Mtu yeyote ulimwengu mzima ambaye amebatiwa kwa jina la Mchungaji ajue
kwamba Mchungaji amemtoa kafara kwa Shetani na hiyo ministry inaongozwa na
nguvu ya kafara kwa sababu wanapoenda kuzimu wanapewa katiba ya kufuata. Ukifuata
katiba ya MUNGU haijaeleza watu wabatizwe kwa jina la Mchungaji. Kafara lingine
ni kubatiza watu kwenye kisima. Hilo ni kafara la kuwazika, ndiyo maana kisima
kipo square hilo ni kaburi tayari, MUNGU hakuagiza watu wabatizwe kwenye kisima
bali katika mto. Haleluya.
BWANA
YESU ASIFIWE! Kafara lingine ni kuwanyima watu kuokoka na watu wamekubali
hawataki kuokoka, leo sema silitaki hili kafara nalikataa nina kutaka BWANA
YESU. Umeshawahi jiuliza nini kinakuzuia wewe usiokoke? Umeshajiuliza kwanini
unampinga YESU? Iko nguvu ya shetani ya makafara iliyokushikilia ni wakati wa
wewe kuokoka. Wako wengine, watumishi wana makafara kazi yao ni kuzini tu. Utashangaa
mtumishi anazini sana ,unasema ameanguka siyo kuangauka ni kafara anafanya amri
ili abarikiwe. Kuna makafara mengine utasikia mtu anajiita YESU, mwanadamu
anajiita YESU lile ni kafara aliloambiwa ili kazi iende ya kanisa la kishetani.
BWANA
YESU ASIFIWE! Nafikiri mnanielewa, kafara lingine kila mtu unapoona amejichanja
labda ni kwa mganga hilo ni kafara .Mtaona
waimbaji muziki, au wachezaji mpira, au watu maarufu wamejichora matatoo sana
huku mwilini yale ni makafara ya shetani lazima achore ili afanikiwe. Lakini
watu wanafikiri ni urembo wanajua wanafanya nini. Wapo wanaiga ni wachache
lakini asilimia kubwa wanajua kabisa wanachokifanya na shetani. Ili kutoka huko
ni ukabatizwe upya na kuoshwa na damu ya YESU ili hayo makafara yatoke. Watu wengi
wanasema hawajatoa makafara lakini ngoja nikuulize swali; unapoenda kwa mganga
unapeleka kuku, mbuzi ile ni kafara
unaenda kufanya.
Sasa zile damu unapozimwaga zinaendelea kunena mambo mabaya
sana juu yako na zimetesa watu wengi sana na kuna watu wanakaa na kutajirika
kwa sababu wanafanyia watu makafara hawafanikiwi, ninasema katika jina la YESU
ninaangusha makafara yote ni wakati wa damu ya YESU kunena mema kwa watu wote. Makafara
yamezungumza sana juu ya maisha ya watu na yakaharibika hata waende jehanamu. Kuna
watu wamepata uwaziri, uraisi, ubunge dunia nzima kwa njia ya makafara kupewa
na shetani, yawezekana na wewe pia ndugu mtazamaji, msikilizaji pia umeyafanya,tubu
uokoke ili ukapate kupona maana mwisho mtu yeyote anayefanya makafara
ataangamia tu. Vivyo na watoto wa MUNGU makanisani wanafanyiwa makafara kama
nilivyo kwisha kufundisha lakini wao hawaelewi ni mambo amabayo yamejificha
sana lakini nimekufunulia.
Mafundisho
ya uongo ni makafara pia.Haleluya. Mapokeo ya uongo yote ni makafara yanasababisha
watu wasisonge mbele, nataka damu ya YESU ikanene mema katika maisha yako na
ukombolewe na utakaswe, na hata sasa naona
kuna watu wanateseka kwa sababu wamefanyiwa makafara, hawapati watoto maisha
yameharibika, watu wamewaendea kwa waganga na kuwafanyia mafundo mbalimbali naamuru
yakatike kwa jina la YESU na hawa watu wanaotoa makafara ni waaminifu sana kwa
shetani, unakuta mtu labda ni msanii lakini unasikia labda kwenye kituo fulani
kapeleka msaada anaonyesha kwenye TV.
Wengi
ni wachawi ni makafara wanafanya kwa sababu ni amri. Kazi hizi zinasimamiwa na
waganga wakienyeji, washirikina na watumishi wa kipepo ndiyo wanasimamia
kupokea hizi sadaka huku duniani na
kuzipeleka kwa shetani na wao kuhakikisha watu wanaendelea kufanya mabaya. Unaweza
kukuta “hudi “au” ubani” unachomwa hayo ni makafara ukiwa dukani au kwenye nyumba
ya biashara ile ni makafara shetani anakaribishwa .
BWANA
YESU ASIFIWE! Maisha ya watu yamefungwa kupitia makafara. Nina amuru wote
waliokufanyia makafara nina vunja hiyo
nguvu kwa jina la YESU na bomoa .Ninaamuru dunia nzima makafara yote yateketee
angani, kuzimu kila mahali na wanaokwenda wasifanikiwe tena.
Sema
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote niliposhiriki kwenye makafara na
kutenda dhambi ,naomba uniokoe uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima
wa milele .Shetani sikutaki, makafara yako yote nayachoma moto katika jina la
YESU.Amen.
BABA ninavunja
makafara yote, ninachoma kwenye makaburi, ninachoma kwenye milima, ninachoma
kwenye maofisi, ninachoma kwenye madhabahu zote, ninachoma kwa mataifa yote. Ninapiga
kuzimu, ninapiga nguvu ya makafara ninachoma hiyo nguvu ya makafara zisifanye
kazi tena. Nimeamuru katika jina la YESU. Nimepiga muhuri duniani na mbinguni. Damu
ya YESU inene katika dunia nzima pande nne za dunia. Amen.
NABII HEBRON.