BAADHI YA MITEGO ANAYOITUMIA SHETANI KUWATEGA WAKRISTO NA KUWA MAWINDO YAKE.
BWANA YESU ASIFIWE!
Karibu tena katika somo la Nabii Hebron ambapo katika somo
hili litawafungua mataifa yote na watu wengi zaidi waliowindwa na shetani au
tayari wameshategwa na shetani kuwa ni mawindo ya shetani pasipokujua au kupenda;
japo wapo baadhi yao wanajitambua kabisa wao ni mateka wa shetani. Ukisoma katika
kitabu cha Zaburi 91:3
“3Maana
yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji na katika tauni iharibuyo”
Mitego ya shetani ipo mingi lakini nitaelezea michache,
natumaini wengi mtapona na kutoka katika hiyo mitego ya shetani kwa sababu
MUNGU amesema atakuokoa na mitego hiyo. Uamuzi ni wako wewe kutoka katika
mitego either imeshakutega au inakufuatilia ikutege na ikikutega mwishowe
unamezwa na shetani. Mfano kila mwindaji anapowinda ni lazima anakuwa na lengo
la kufanya kuwa chakula na hivyo hivyo chakula cha shetani ni nyama za watu na
damu. Sasa ili akupate ni lazima akuwinde na akutege katika mitego soma Zaburi 35:
7 na akishakutega anakuwa amekupata na baadaye atakula nyama yako; unakuwa ni
chakula.
Mtego mkubwa ni kutenda dhambi ila nitaelezea mitego ambaye YESU
alinifundisha na uyajue; yale aliyonifundisha aliponitokea 2010 nikiwa
Serengeti National Park nchini Tanzania aliniambia “uwaeleze mataifa yote
wanirejee mimi, uwafundishe neno la kweli na siyo uongo. Wakristo wengi shetani
ameshawatega tayari na shetani anawasubiria ule mwisho awafanye chakula chake.”
Mitego nitaielezea michache;
1.
Kubatizwa kwa ubatizo wa maji ya kikombe, hapo
tayari umenaswa na mtego wa shetani katika ulimwengu wa roho na upo chini ya
himaya yake na anao uhalali na wewe kabisa.
2.
Kubatizwa kwenye kisima, kubatizwa kwa jina la
mchungaji na batizo nyingine zote ambazo ni tofauti na wa kwenye biblia. Unapozipokea
pasipo wewe kujua tayari umeshategwa na shetani na kwa njia hiyo tayari na wewe
upo katika mtego na ndiyo sababu ukisoma kitabu cha Ufunuo 22:18-19 MUNGU
alikataa neno lake lisiongezwe wala kubadilishwa. Inapokuwa hivyo tayari
mnategwa na shetani na baadaye unakuwa chakula cha shetani na yeye atakumeza.
3.
Upo utumishi ambao unaendeleza kazi ambazo sizo
za YESU na watu wengi hawaelewi wanafungwa fahamu zao na serikali ya kuzimu na
kupumbazwa wanaona wanaenda mbinguni kumbe wanaelekea Jehanamu. Wakati ni sasa,
hiyo mitego itoke kwako uje kwa YESU WA KWELI.
4.
Zipo nyumba za ibada ambazo zinatumia jina la
YESU lakini kinachofanyika ni tofauti na neno lilivyo; inachanganywa uongo na
ukweli. Hapo tayari panakuwa ni nyumba ya kuwatega watoto wa MUNGU wawe mateka
ya shetani. Mfano; kufanyika michango, harambee ndani ya kanisa, kubariki
watoto wakubwa, kubatiza watoto wadogo, kuandikiwa risiti ya malipo ya sadaka,
kanisa kukopa benki, kuchajiwa pesa za maombezi kama hospitali za kibinadamu,
kanisa kuongozwa na mashoga, kuongozwa na watumishi freemason na mengineyo mengi
zaidi. Endelea kusikiliza na YouTube ya Nabii Hebron yapo masomo mengi
yatakusaidia usitegwe na shetani tena, na unapoujua ukweli kwa usalama wako wa
kiroho usiingie tena mahali hapo omba MUNGU akuongoze palipo salama usije ukawa
chakula cha shetani.
5.
Madhabahu inayoabudu sanamu, kufanya ibada za
wafu hayo yote ndiyo mitego ambayo shetani ameingiza hapa ulimwenguni ili aweze
kuwatega na watu wengi wameshategwa. Mimi
nakueleza ukweli wala siweki neno langu. Ukweli ndiyo huo wewe umeshaelewa,
uamuzi ni wako, ila karibu upande wa YESU WA KWELI yeye hatakufanya chakula
chake, yeye hali watu bali yeye ndiye chakula cha watu wamfuatao kupitia neno
lake la kweli. Kula neno la kweli usile neno la uongo; hilo ni mtego
linakutega.
6.
Mafundisho ya mpinga kristo yote ni mitego ya
shetani. Unapojiita ni mkristo lakini wewe umebatizwa kwa ubatizo wa maji ya
kikombe, nakueleza ubadilike kama unataka kwenda mbinguni uondolewe huo mtego
wa shetani ukabatizwe upya katika maji yanayotembea mtoni na siyo ya kisima. Wengi
wanategwa na shetani, hata mimi nilitegwa kwa kupitia ubatizo wa maji ya
kikombe ila YESU ameniondolea huo mtego na yeye amenipata, sipo katika ngome ya
shetani kwenye ulimwengu wa roho na hata wa kimwili. Najua inashtua lakini
wacha ukweli niuseme na MUNGU afurahi na shetani anune kabisa, kwa sababu
kupitia ujumbe huu mtapona maelfu. Uwatumie na wengine popote, hakuna cha
kubisha, uamue kuwa mkristo wa kweli, usiwe wa uongo. Japo wengi mnapenda kuwa
wakristo wa kweli ila shetani akaleta mapokeo yake ya uongo yakasambazwa
dunaini zaidi, wakayaammini, yakachanganywa na uongo, hapo unatekwa. Soma Wagalatia
1:6.
SALA YA TOBA
BWANA YESU naomba unisamehe, uniandike jina langu katika
kitabu chako cha uzima wa kweli, uliondoe katika kitabu cha mauti ambacho nilitegwa
na shetani ili anifanye mawindo na chakula chake. Mimi sitaki. Asante YESU
nishike mkono, usiniache. Amen.
Ubarikiwe!
NABII HEBRON.