JE UNAONGOZWA NA ROHO MSAIDIZI WA MUNGU?
JE UNAONGOZWA NA ROHO MSAIDIZI WA SHETANI ?
JE UNAONGOZWA NA ROHO MSAIDIZI WA SHETANI ?
JE UNAJUA YUPO ROHO MSAIDIZI WA SHETANI?
YUKOJE?
BWANA YESU ASIFIWE, watu wote
wa mataifa yote ambao mmeumbwa na MUNGU na ambaye ndiye BABA yake YESU, na kwa
dini nyingine wanamwita yeye ni Nabii Issa, kipindi hiki amekaribia kurudi kwa
ajili ya unyakuo. Ukisoma katika kitabu cha Yohana 14:16-17 16 Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi
mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa Kweli; ambaye ulimwengu hauwezi
kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui. Bali ninyi mnamtambua, maana
anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”
Utaona hapa
YESU kabla ya kupaa aliwaahidi mitume wake atawatumia roho msaidizi kutoka
mbinguni na yeye atawaongoza awapeleke mahali alipo yeye mbinguni sababu hakuna
mwanadamu atakayeweza kujiongoza yeye peke yake afike mbinguni, njia
aliyetutumia YESU ni kupitia roho mtakatifu ambaye ndiye msaidizi wa YESU, na
roho huyu yeye huyasimamia yale tu ambayo YESU aliyaelekeza na katika neno la
MUNGU lifuatwe kama lilivyo bila kuchanganywa na uongo.
ROHO
MSAIDIZI WA SHETANI NI NANI?
Roho msaidizi
wa shetani ni roho ambaye katika biblia ya shetani na yeye alicopy hivyo hivyo
ila dunia imefungwa macho na kupigwa upofu ila wapo baadhi ya watumishi ambao
wanaenda kuonana na shetani uso kwa uso kama baba yao na huku duniani wakijifanya ni watumishi wanaomtumikia MUNGU
kumbe ni watumishi wa shetani kabisa na wanamipango ya kuangamiza nafsi za watu
ziende jehanamu. Kama nilivyoelekeza katika mafundisho yangu Nabii Hebron
nilisema yupo yesu wa uongo na huyu ni shina la shetani na yeye yupo kuzimu ila
ile siku ya mwisho na yeye atatoka kimwili kuwapokea wafuasi wake ambao ni
wakristo vile vile ambao hawakumfwata YESU wa kweli wa mbinguni sababu na YESU
wa kweli na yeye atakubalika na ile siku ya mwisho atawachukua wale walio
wakristo wa kweli sasa umeshaelezwa kuwa kama wewe ni mkristo wa uongo siku ile
ya mwisho utapokelewa na mkristo wa uongo na kama wewe ni mkristo wa kweli
utapokelewa na YESU wa kweli.
Huyu roho
msaidizi wa shetani alitumwa duniani kuwasaidia watumishi ambao ni wapinga
kristo na ambao wamemsaliti YESU ambao wapo kwa ajili ya kuwapoteza wanadamu
wasiende mbinguni. Roho huyu msaidizi ndiye ndiye anayewaongoza na ndipo
utashangaa mbona mtumishi anamtaja roho mtakatifu kanisani lakini hawaruhusu
kuokoka au wanamtaja YESU lakini hawabatizwi kama YESU au mtumishi anawaombea
watu kwa kuwachangisha watu pesa tofauti na neno la MUNGU lisemavyo “umepewa bure, toa bure” unapoona ni
tofauti basi sasa uelewe anaongozwa na roho msaidizi wa shetani na ndiyo sababu
biblia haifuatwi na umeshajiuliza ni kwa nini biblia inabebwa kanisani lakini
inafuatwa kwa kuchanganywa na uongo? Ni sababu huyu roho msaidizi wa shetani
yeye siyo mtakatifu ni muongo hiyo ndiyo dalili ya kujua ni roho msaidizi wa
shetani.
Jambo hili ni
moja ya mambo ambaye alinifundisha YESU aliponipeleka mbinguni tokea 2010 ili
nijue ni jinsi gani shetani alivyoiteka ulimwengu na kufanya YESU akose watu
wengi wa kwenda mbinguni na shetani akawa ndiyo mwenye watu wengi 98% na YESU
akawa na 2% ya watu watakaoenda mbinguni. Hii idadi inatisha natumaini mnazidi
kuelewa na kuweza kumrejea YESU wa kweli na kumkataa na kumkana yesu wa uongo
hadharani pamoja na roho wake msaidizi aliyemtuma hapa ulimwenguni kote akaweka
mizizi yake, sasa ni wakati wake kuporomoka na ni serikali ya mbinguni itafanya
hiyo kazi na wataendelea mpaka atakapokuja YESU kulinyakua kanisa takatifu
yaani mkristo wa kweli. Kama ilivyo kazi za roho mtakatifu zilivyo na yeye roho
msaidizi wa shetani hufanya hivyo hivyo mfano kazi ya roho mtakatifu ni
kusimamia kweli ya neno la MUNGU lifuatwe, roho huyu wa shetani. Roho huyu wa
shetani hulipindua pindua mfano; tazama ubatizo aliobatizwa YESU katika mto je ndiyo batizo wakristo wanazofuata? Hapo
uelewe roho msaidizi wa shetani ndiye anayewaongoza na siku ile ya mwisho
atawakabidhi hao watu kwa shetani na watu hawajui jambo hili. Ameintuma YESU,
amenituma MUNGU, amenituma ROHO MTAKATIFU wa kweli, ninaeleza ukweli
utakayesikia na kugeuka utapona ila utakaye ng’ang’ana huyo roho msaidizi wa
shetani atakupeleka jehanamu; yeye kazi yake ni kuwapeleka watu jehanamu ndiyo
kazi aliyetumwa na shetani, ni jinsi gani utamjua au kumtambua kuwa ni roho
msaidizi wa shetani ndani ya kanisa au ndani ya mtumishi yeyote yule.
Jambo la
kwanza kabisa nataka uelewe haitwi kwa jina lake kuwa ni roho msaidizi wa
shetani yeye anatajwa kama roho mtakatifu ila utamjua kwa matendo anayoyaongoza
huyo anayeitwa roho mtakatifu. Utayaona ni kinyume na neno la MUNGU mfano wa
kufuata matendo baadhi yanayofanywa makanisani katika sehemu baadhi.
1.
Kubatizwa kwa maji
ya kikombe, kubatizwa katika kisima, kubatizwa kwa jina la mchungaji, kubatizwa
ubatizo tofauti na wa mtoni, maji tele
yanayotembea (hapa ni roho msaidizi wa shetani anayetia nguvu na watu humfuata.
Batizo hizo siyo za haki mbele za MUNGU na siku ile ya mwisho shetani
atamwambia MUNGU wewe ni wa haki je kwa nini wamepokea kinyume na neno lako? Sijui
utamjibuje MUNGU.
2.
Unapopewa huduma ya
maombezi halafu ukachajiwa pesa hapo uelewe siyo roho mtakatifu anayewaongoza
kabisa kabisa, bali ni roho msaidizi wa shetani anayempa nguvu hizo na pia
nataka uelewe roho huyu msaidizi na yeye ananena vile vile na hapo watu wengi
wamepigwa upofu wanaona ni MUNGU.
3.
Kuwa mkristo halafu
hataki kuokoka bali kung’ang’ania kujiita mkristo na hautaki wokovu, watu wa
namna hiyo wanashikiliwa na roho msaidizi wa shetani na ndiye anayewaongoza na
kuwapa mioyo migumu hata madhabahu za jinsi hiyo nataka uelewe zinaongozwa
na roho msaidizi wa shetani ili
awaongoze kwenda jehanamu sababu hata wewe soma katiba ya MUNGU yaani neno lake
hayo hayapo yamekatazwa ila katika katiba ya shetani yapo. Yametolewa katika
ulimwengu wa roho yafuatwe na yamefuatwa sana na jinsi unavyoyafuata ndivyo
unavyojiunganisha zaidi na safari ya kwenda jehanamu.
Upokee
wokovu sasa uikamate barabara ya kwenda mbinguni, ila nataka uelewe pia roho
huyu msaidizi wa shetani na yeye yupo katika makanisa ya dini ya wokovu baadhi
yake na kwa watumishi wengi zaidi na kama yupo ndani ya kuhani basi kanisa lote
litaongozwa na roho huyu msaidizi wa shetani pasipo watu kujua na kulipeleka
kanisa jehanamu na ndivyo ilivyo sasa kwa kupitia njia hii wakristo wengi
wanafikiri wapo salama kumbe tayari wameishika njia ya jehanamu pasipo kupenda
na wengine kujua.
4.
Roho mtakatifu
aliyeletwa na YESU alituambia atatuombea yeye na kutuongoza tufike yeye alipo,
wala hatukuelezwa tuwataje malaika ndiyo watuombee. Tuliambiwa katika kuomba ni
watatu tu wapaswao kusujudiwa nao ni MUNGU BABA, MUNGU MWANA na ROHO MTAKATIFU
na zaidi yeye atatuombea. Sasa cha ajabu utashangaa anatajwa MUNGU, YESU, ROHO
MTAKATIFU hapo hapo utashangaa imani za watu zimepelekwa kumwomba Maria
atuombee, Petro atuombee au Musa au jina la mtume yeyote. Sasa nikuulize ni
wapi pameandikwa tuwafuate hao tuwaombe? Jibu hakuna na zaidi unapofanya hivyo
unakuwa umemfanya Maria, Petro na wengineo ndiyo miungu yako hivyo ndiyo roho
huyu msaidizi wa shetani alivyowateka watu wengi imani zao na wakifikiri
wanaenda mbinguni, sasa muelewe ukweli ndio huo, unaongozwa na roho msaidizi wa
shetani na ndiyo sababu unayafuata hayo. Na haikutosha MUNGU amekataa katika
neno lake watu wasiabudu sanamu na bado watu wanaabudu na zaidi anatajwa YESU
hapo mahali huyo siyo YESU wa kweli ni wa uongo na YESU wa mbinguni hawatambui
watu hao kabisa sababu wapo katika njia nyingine ya msaidizi wa shetani
5.
Maombi ya
kutengenezewa kamba zenye misalaba halafu unafanya kama ndiyo formula unataja
jina la mtakatifu yeyote kwa kuhesabu mafundo na kutaja mambo yako, hiyo pia
hayupo roho wa kweli huyo ni roho msaidizi wa shetani ndiye aliyeleta hiyo njia
kimwili ya kushika hiyo kamba na kuwekea msalaba. Sasa badala ya roho mtakatifu
wa kweli yeye akuombee hata pasipo wewe kujua nini anakuombea akaja roho
msaidizi wa shetani akaleta sheria yake ambayo biblia haijaruhusu tuombe kwa
kuhesabu vitu hapa mpaka pale na kuyataja majina ya mitume wake; hili ni kosa
ni dhambi na msitegemee kumwona roho mtakatifu akiwaongoza kwenda mbinguni bali
ni njia ya kwenda jehanamu, haya ni mapokeo ya wamisionari waliotumwa na
shetani yamesambaa na watu wameyashika, ili upone yakatae sasa, ndipo utakuwa
salama na YESU atakufurahia.
6.
Watumishi wote
wanaojiita wao ni YESU au wao ndiyo MUNGU wa majeshi hao wote wamepewa hayo
mafunuo na roho msaidizi wa shetani. Kila mtu anajua hakuna mtu anayeitwa MUNGU
au YESU au ROHO MTAKATIFU, Je hauoni huku ni kumkufuru Mwenyezi MUNGU?
7.
Kufanya harambee
makanisani, hapo siyo sokoni hayo ni makelele mbele za MUNGU bali ni roho wa
shetani hapo ndipo furaha yake na ni lazima aongoze ifanyike hivyo ili aujenge
ufalme wa shetani au mpinga kristo, aliitwa na shetani. Nyumba za ibada
zilizojengwa kwa jinsi hiyo ni mali za shetani wala msitegemee MUNGU aingie katika
jengo hilo sababu kama uhalali napo.
8.
Kukopa benki ili
kumjengea MUNGU kanisa- roho wa shetani.
9.
Kanisa kuwa na
benki, hayo ni mambo ya kaisari, MUNGU yeye hachaji riba, bali roho msaidizi wa
shetani ni lazima afanye hivyo yeye hana baraka.
10.
Watumishi wa
freemason wote wanaongozwa na roho msaidizi wa shetani.
11.
Ibada za wafu-
zimeongozwa na roho msaidizi wa shetani, twajua katika neno la MUNGU, yeye siyo
MUNGU wa wafu.
12.
Watumishi wote
wanaoomba pesa za tv, radio na michango mbali mbali kwa ajili ya kazi ya
kanisa, neno linasema msijisumbue watumishi wangu nitafanya nini sasa hao
wanaongozwa na roho msaidizi wa shetani ni lazima wafanye hivyo sababu baba yao
ni masikini na wanapofanya hivyo unafikiri wanajenga ufalme wa YESU wa kweli
bali ni kujenga ufalme wa shetani ndiyo sababu utashangaa hawana aibu kabisa
kuomba pesa, ni sababu yule roho msaidizi wa shetani ndiye anayewatia nguvu
hiyo na wale watumishi wa MUNGU wenye roho mtakatifu wa kweli wao hutiwa nguvu
na roho mtakatifu na kumtegemea MUNGU na yeye hufanya.
IPO SIKU YA PENTEKOSTE YA MSAIDIZI WA SHETANI.
Kama ilivyo ipo siku ya
pentekoste ya roho mtakatifu wa kweli na katika siku hiyo hiyo na yeye
hujiadhimisha katika makanisa yake na kwa watumishi wake, japo utaelezwa
pokeeni roho mtakatifu katika kinywa bali katika ulimwengu wa roho ni kumpokea
roho msaidizi wa shetani. Nikuulize swali je iweje roho mtakatifu aongoze
wakristo wasiokoke? Utaona ni roho wa
shetani, au iweje wachungaji ni mashoga na wanamtaja roho mtakatifu je jiulize
ni roho mtakatifu anayewatia nguvu ya kuwa mashoga? Jibu siyo roho mtakatifu
huyo ndiye yule roho msaidizi wa shetani aliyetumwa kuongoza kanisa la mpinga
kristo wenye ufahamu na wafahamu zaidi.
Wapo watu siku ya pentekoste
wanapigwa makofi na wachungaji, kuingiliwa kimwili, kutemewa mate, kupigwa busu
eti ndio njia ya kumpokea roho mtakatifu,
hapo mmepokea roho msaidizi wa shetani.
Ukiona unachajiwa pesa ndio
uonane na Nabii au mtumishi yeyote, ninakusihi usiende, unaenda kuonana na
shetani uso kwa uso aliyopo ndani yake.
Ukikutana na mtumishi
ukamweleza matatizo yako ya ndoa halafu akakuambia akusaidie kwa kukutana na
wewe kimwili huyo ni pepo, kimbia kabisa. Huyo anaongozwa na roho msaidizi wa
shetani kuendeleza uovu wa shetani.
Kapu la mama mchungaji- hili ni
pepo.
Kulazimishwa kutoa sadaka na
kupangiwa kiasi- pepo hilo.
Kwa leo watu wote wa mataifa
yote mjifunze haya na mliokuwa mmepotea njia sasa tubuni maana hata sasa
ninavyoandika ujumbe huu nasikia sauti ya MUNGU ikiniambia katika ulimwengu
wote hakuna aliyemfunulia siri hii ailete duniani hivyo muishike sana na
mumkatae roho msaidizi wa shetani mumfuate roho mtakatifu wa kweli wengi mmelia
mmemtolea MUNGU na mmefilisika angalia neno lake katika Malaki 3 sasa kwa nini
iwe ni uongo. Jibu roho wa kweli hakuhusika na sadaka zako bali ni roho
msaidizi wa shetani yeye ni muongo. Tubu BWANA YESU naomba unisamehe dhambi
zangu zote nilizozifanya kwa kujua au kutokujua. Naomba uiandike jina langu
katika kitabu chako, ulitoe katika kitabu cha yesu wa uongo kupitia roho wake
msaidizi wa shetani, nami namkana kabisa. Sirudi tena kwenye madhabahu zake ili
asinipate tena. Niongoze YESU mahali ulipo wewe wa kweli na roho wako mtakatifu
wa kweli. Amen.
Mbarikiwe! Zaidi karibu katika
kanisa langu lililopo popote. YESU anarudi nyakati hizi ni za hatari amenieleza
yeye mwenyewe, uyasikie na uyatumie, watumie na wengine blog hii.
NABII HEBRON.