ALIYONIELEZA
MUNGU KUHUSU UCHAGUZI WA TANZANIA WA 2020 KUHUSU URAIS, UBUNGE, UDIWANI.
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE!
Mnamo tarehe 9.4.2016 nilikuwa katika maombi na hata kuiombea nchi yangu ya
Tanzania na kuiombea dunia yote siku hiyo nilikuwa nchi ya Canada majira ya
mchana yapo mengi aliyonieleza kwa nchi mbali mbali ila mpaka wakati wake
akiniruhusu nitayasema. Aliniambia mengi ila hayo niliyopata kibali ndiyo
nitayasema kwa sasa.
Aliniambia “kama nilivyokueleza
nitamleta rais wala hatatokea katika mikono ya shetani, wala wachawi, wala
hatatokea kwa wanadamu kujipangia na ndivyo ilivyokuwa neno langu Hebron ni
lazima litimie sababu mimi ni MUNGU nisemaye ukweli hivyo kweli yangu lazima
utakuwa tu na ndivyo nitakavyotukuzwa mimi MUNGU katika nchi ambayo wewe Nabii
wangu upo. Mimi MUNGU ni amani nikiwepo katika nchi kupitia mtumishi wangu amani
itaonekana, ila uelewe pia wapo watumishi wa shetani wametawala nchi nyingi
wakisema ni Nabii wa MUNGU, jibu ni hapana ndiyo sababu machafuko yanawapata
baadhi yao.
Kama nilivyokuelezea
nitainyanyua Tanzania na mataifa watakuja kuponea hapa, ndivyo ilivyo na
imeshakuwa na siku zinavyoendelea mtayaona.
Kuhusu uchaguzi ujao rais wa sasa hatakuwa na upinzani japo watakuwepo
wagombea wengine na endapo rais huyu ataendelea kunisikiliza kama nimuongozavyo
mimi MUNGU na kuwa mwaminifu kwangu mimi niliyemuumba na kumweka awe rais wa
nchi hii atakuwa ameshapita katika uchaguzi ujao hivyo Hebron ombea mambo
mengine haya nimeshayajibu na ndivyo itakavyokuwa wala haitabadilika, na katika
kipindi kijacho akinitii mimi MUNGU itafika mahali hata wananchi wataomba
wenyewe kipengele cha uongozi aongezewe tena bila vurugu yeyote na itakuwa ni
kwa amani ya ajabu na furaha.”
Katika ubunge uchaguzi ujao
idadi kubwa ya wabunge watachaguliwa siyo kutokana na kupigiwa kura na vyama
vyao watapigiwa na watu wote hivyo katika ubunge ndipo patakuwa pana ushindani
mkubwa sana kuliko ushindani wa uchaguzi wa urais 2015 na katika udiwani
itakuwa hivyo hivyo na hata katika serikali za mitaa ushindani utakuwa ni
mkubwa sana. Mgombeaji ambaye atagombea ajipange sawa sawa. Ila na wengi
wataporomoka tu wapya kuingia.
Na kama nilivyoelezea miaka
miwili kabla ya uchaguzi kuhusu unabii wa Tanzania nilisema wakiibia pesa nchi
watakamatwa na mnayaona na mengi ukisoma makala ya Nabii Hebron utayaona. Yeye MUNGU
asemaye ukweli neno lake linatimia na haya yatatimia na yapo mengi MUNGU
atawaongoza watoto wake kupitia wanadamu watayafichua kila siku hata
yaliyoibiwa miaka ya nyuma. Nchi itaendelea kuinuliwa na rais huyu atakuwa ni
mfano wa kuigwa katika dunia hii. Ili nchi inyanyuliwe ni lazima rais
anyanyuliwe awe kioo na hiyo ndiyo dalili na hata uongozi utafuata spirit hiyo.
Wale watakaopinga hawatadumu katika uongozi na waliozoea uchawi nawaeleza
hamfanyikiwi tena katika nchi hii kwa sababu MUNGU yeye ndiye ameishika katika
mkono wake.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
NABII
HEBRON.