JE
NI HALALI MBELE ZA MUNGU KWA SIKU YA IJUMAA KUU MTUMISHI KULALA MADHABAHUNI?
HII
NI DHAMBI…
BWANA YESU ASIFIWE, YESU
anawapenda watu wote, ni vizuri kila mtu ampende YESU na mwenyezi MUNGU
na kuokoka, hapo YESU atafurahia sana.
Katika makala hii nitaelezea
maana iliyofichika ambayo ni mapokeo ya wanadamu na siyo mpango wa MUNGU. Jambo
hili hufanyika katika maeneo mengi katika dunia hii katika siku ile ya ibada ya
Ijumaa Kuu, nitaelezea kuhusu
mtumishi anapolala madhabahuni akijifananisha amekufa na YESU na kufufuka na
YESU kwa njia ya ishara hiyo.
Kwanza nataka muelewe huo ni
upotevu na siyo maelekezo yaliyopo katika Biblia na wala YESU hakuwafundisha
wale mitume wake wa kwanza (12 Apostles). Jambo hili siyo halali wala
halimpendezi MUNGU. Wanawadanganya watu eti wanafuata neno la MUNGU linalosema,
“ishara hizi zitafuatana nao waaminio”.
Ndiyo, YESU alisema watatoa
mapepo na maana nyingine ni ya kiroho. Wewe uliyempokea YESU hata ukifa utaishi
utakuwa hai kama YESU na utafufuka, na utaenda mbinguni siku moja, ila siyo kwa
jambo hili la kulala madhabahuni eti ndiyo umekufa na YESU. Huo ni uongo na kujidanganya.
Neno la MUNGU ni kweli, na kama unataka hivyo, basi ufe, uzikwe kabisa halafu
ufufuke tuone hiyo ishara ya kuwa unafufuka kama YESU. Tunatakiwa tufuate
kiroho na siyo kimwili, sasa hauoni hapa ni kimwili kabisa? Ingekuwa ni kimwili
tunamwabudu YESU basi ingebidi aje kimwili katika ibada kila siku tuombe mbele
zake.
Dunia imepotezwa sana na
mafundisho ya uongo na hata kwa ishara za uongo. YESU ameshafufuka zaidi ya miaka
2000 iliyopita, yeye hayupo ardhini tena na zaidi basi kama wanasema na ishara
hizi zitafuatana na wanaomfuata YESU au watumishi wa MUNGU basi ingekuwa kila
ijumaa kuu watumishi ni lazima wasulubiwe msalabani na wakate roho wazikwe na
siku ya tatu wafufuke na baada ya siku 40 wapae kwenda mbinguni hivyo hivyo
kila mwaka. Nataka muelewe mambo mengine ni ya kumkufuru YESU na MUNGU.
MUNGU alimtoa Mwanaye kwa ajili
yetu lakini sasa bado watu wakafundishwa uongo wa elimu ya wanadamu na kufuata
ishara za uongo, Neno likabadilishwa. Nataka muelewe hata mnayoyafanya hayo kwa
kujua au kutokujua mrejeeni MUNGU, hiki ni kipindi cha neema bado. Ishara za
ijumaa kuu, hizo ishara zinazofanywa na wanadamu siku ambayo tunakumbuka YESU
alipokufa kwa ajili yetu hazitakiwi kufanywa kabisa, kwa kufanya hivyo unakuwa
unajisulubisha mwenyewe, unaenda kuzimu na kujiua kiroho na kujiunganisha na
kuzimu na hautatoka labda utubu leo na uokoke sasa, na hata waumini
wanaoshiriki katika tendo hilo na wao wanaunganishwa na kuhani katika ulimwengu
wa roho. Jinsi alivyo kuhani ndivyo na kondoo wake walivyo. Kama kuhani yupo
kuzimu na kondoo watakuwa huko, kama kuhani anamfuata MUNGU na Neno lake la
kweli na waumini watakuwa hivyo hivyo. Sasa wewe upo wapi? MUNGU
awafungue mataifa yote.
NABII HEBRON