PEPO
UPONYAJI YUKOJE?
Huyu ni pepo ambaye ni wa uponyaji kama vile wa mganga wa
kienyeji. Pepo huyu hufanya kazi kwa watumishi ambao wanaongozwa na shetani kwa
kupitia kanisa ili kuwateka wakristo waone ni nguvu za MUNGU zinatenda kazi, na
pepo huyu kwa lugha nyingine anaitwa pepo mchafu au roho mchafu ila kibinadamu
mtumishi hawezi kumwita roho mchafu atamtaja ROHO MTAKATIFU, ila wewe jinsi ya
kutambua chunguza hayo matendo yanayohubiriwa je yameendana na ya ROHO
MTAKATIFU au yanaendana na roho mchafu. Mfano ukikuta unaenda kwa mtumishi
yeyote yule na watu wanaponywa halafu wanachajiwa pesa za kufanyiwa maombi. Sasa
uelewe hapo unaenda kwa pepo wa shetani wa uponyaji na haujaenda kwa ROHO
MTAKATIFU akuponye.
Ukikuta unadaiwa pesa ndiyo uweze kuongea na mtumishi uelewe
unaenda kwa pepo uponyaji kwa sababu
yeye hatoi kitu chochote bila malipo ila kwa ROHO MTAKATIFU yeye huliangalia
neno la MUNGU na kulisimamia litimie; nimekupa bure, toa bure. Sasa pepo
uponyaji yeye hatoi bure na zaidi yeye hukipooza kwa muda lile tatizo na
baadaye akikuona wewe utaenda mbinguni, unampenda sana YESU kutoka katika moyo
wako basi hukurudishia hayo matatizo zaidi ili uangamie mapema na ndiyo sababu
watu wengi wanasafiri sehemu nyingi wakifuata maombezi na kufika wanachajiwa
gharama na matokeo yake wakirudi hali ndiyo inakuwa mbaya zaidi kuliko
mwanzoni, unawekewa pepo lingine ili udhoofike haraka ili usije ukakutana na
YESU wa kweli akakupata.
Nawatia moyo mliopita katika hayo msiogope, mtaponywa na
ROHO MTAKATIFU bure yeye hachaji watu pesa, yeye siyo mnyang’anyi, ila mahali
alipo pepo uponyaji ni lazima unyang’anywe uliyonavyo na YESU alishasema wapo
wanyang’anyi ndiyo hao hao. Sasa watu wote nawaeleza maneno haya ni ya YESU
siyo yangu mimi Hebron, kila ulipochajiwa pesa ili upate maombezi, nawaeleza
mlienda kwa mnyang’anyi, unaibiwa na vitu vingine vya kiroho, na baraka zako
ulizopewa na MUNGU na hiyo ndiyo njia shetani anatumia kuwaibia watu wengi hapa
ulimwenguni.
NOTE:
Zaidi kila maombezi au huduma yoyote ya kiroho katika
ulimwengu wote inayochaji pesa au gharama ili ufunguliwe au kubarikiwa au
kumwona mchungaji private, huduma hizo haziongozwi na roh mtakatifu hata kama
jina lake linatajwa bali zinaongozwa na roho mchafu, ikiwamo huduma za
kuchangia pesa kwa mpesa au kuweka benki kwa njia ya mtumishi kuomba na
kutangaza namba hizo ili watu waziwekee pesa ili wabarikiwe, hapo tayari watu
wanadaiwa gharama. Siyo vibaya kumtolea MUNGU ila usitengenezewe mazingira
hayo. Ikiwa umetoa kwa njia hiyo hujamtolea MUNGU bali umemtolea shetani pasipo
wewe kujua au kupenda, bali kiongozi anayesababisha hayo, yeye anajua
anaongozwa na roho mchafu na anamkufuru roho mtakatifu na kumwinua roho mchafu,
roho wa unyang’anyi.
Tubu sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote
uniokoe, unianidke jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele,
uniongoze wewe nisiende tena kwa pepo wa uponyaji. Amen.
NABII HEBRON.