Pages

Saturday, September 19, 2015

PEPO UBARIKIO

BWANA YESU ASIFIWE. Najua wengi mtashangaa ninaposema pepo ubarikio kwa sababu kitendo cha neno ubarikio ni tendo jema, lakini nataka uelewe kuwa hata shetani na yeye huwabarikia watu ambao wanaofuata masharti ya shetani na huo ndio ubarikio wa kipepo. Ila nataka kuelezea katika kanisa jinsi pepo ubarikio alivyoingia na kulitawala kanisa na hata watu pasipo kujua kuwa tayari hayupo tena ROHO MTAKATIFU abarikiye bali amebakia pepo barikio. Yapo mambo mengi ya baraka za kipepo ambazo watu wengi wanazipokea na hata wakajua kuwa wanapokea baraka za mwenyezi MUNGU kumbe wanapokea baraka za shetani.

Pepo barikio hili nilipepo ambalo linalosimamia kitendp cha kuvuruga mpango wa MUNGU watoto wadogo wasiwekwe wakfu wanapozaliwa tu kanisani na badala yake na kubadilisha wawekwe wakfu wakiwa watu wazima na ile nafasi ya ubatizo ambayo walitakiwa wabatizwe wakiwa watu wazima akaibadilisha wabatizwe  wakiwa wadogo. Na watoto wakiwa watu wazima ndiyo sasa hili pepo linashiriki kuja kumtawala mtu kwa kukabidhiwa kwa dunia na kumtenga na utakatifu na wokovu na kumpatanisha na dhambi na maovu. Hivyo hata mimi Hebron nilifanywa hivyo hivyo nilibarikiwa ubarikio wa kipepo na mimi sikujua na hata wazazi wangu kwa sababu waliyarithi mapokeo ya wanadamu, mpaka nilipoujua ukweli nikafunguliwa vifungo hivyo vya mateso, kwa sababu nilipiga magoti kanisani na kuwekewa mikono nikijua nabarikiwa na ROHO MTAKATIFU kumbe nilibarikiwa na pepo.

Nilipoyajua haya niliogopa sana nilikuwa sitting room nyumbani kwangu nikasikia sauti kutoka mbinguni ikinieleza haya niliogop sana ila nilimshukuru YESU. Akaniambia uwaeleze watu wote wale walio wangu watayapokea na kubatizwa upya na wale wa dunia hii hawatayakubali, akaniambia hata mimi YESU kipindi changu nilipokuwepo hapa ulimwenguni na hata ukisoma katika vitabu vya nyaraka utaona wapo walionikubali na wapo walionikataa, haya yatakuwepo tu ila peleka ujumbe wangu, atakayetii atapona. Watu wamepotoshwa na mpinga kristo, waeleze mimi YESU sifanyi kazi na mpinga kristo wala ROHO MTAKATIFU wala BABA yangu wa mbinguni, bali wanaye baba yao wa uwongo, roho mchafu na yesu wa uwongo. Mnirejee mimi YESU nawapenda wanangu, muda wa unyakuo umefika. Tubu sasa sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote ikiwemo ya kubarikiwa nikiwa mtu mzima kwa sababu neno lako halijaandika hivyo, nimekwenda tofauti na neno lako kwa kujua au kutokujua. Uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele. Amen.

KARIBUNI KATIKA KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. MBARIKIWE.


NABII HEBRON.