Nabii Hebron: Unanichezea?
Nabii Hebron: Unanichezea?
Nabii Hebron: Hilo
jiwe mkononi ni ya nini?
Annastazia: Nimeokota
Nabii Hebron: Umeokota
wapi?
Nabii Hebron: Njoo
hapa
Nabii Hebron: Utanieleza
leo kila kitu
Nabii Hebron: Leta
hapa
Nabii Hebron: Aisee
unataka kupona?
Nabii Hebron: Niambie
ukweli
Nabii Hebron: Au
nikuache uchomwe na shetani?
Annastazia: Hapana
Nabii Hebron: Eeee?
Nabii Hebron: Niambie
ukweli, maana nakujua.
Nabii Hebron: Si
unanijua mimi?
Nabii Hebron: Jana
si nimekuchapa?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Nilikuchapaje
usiku?
Nabii Hebron: Usiogope,
sisi tunakupenda. Sawasawa? hata huyo unayekaa kwake hatakufukuza, usiogope.
Sisi tunakupenda. Sisi tunakupenda
Nabii Hebron: Si
nilikuchapa jana usiku?
Nabii Hebron: Nilikuchapa
saa ngapi?
Annastazia: Saa
nane usiku
Nabii Hebron: Ulikuwa
unafanyaje saa nane usiku?
Annastazia: Nilikuwa
nimekaa mlangoni
Nabii Hebron: Kwa
nani?
Annastazia: Kwa
mama
Nabii Hebron: Ulikuwa
unafanyaje mlangoni?
Annastazia: Sijui
ni vitu gani vilikuwa mlangoni
Nabii Hebron: Hujasema
ukweli, bado. Yale madini uliingia kwenye nyumba ya nani ukageuka tu mlango wa
nani mlango ukafunguka ukayatoa?
Nabii Hebron: Eeeee?
Annastazia: Sijui.
Nabii Hebron: Yaani
tumemkamata na madini. Yale madini yako wapi?
Nabii Hebron: Aliyekuja
na huyu mtoto yuko wapi? Yaani huyu mtoto akipita kwenye mlango akigeuka hivi,
mlango unafunguka anakomba madini yote. Akigeuka tu hivi, anachukua na hela.
lakini kwa watoto wangu “NO”. Hawa mimi nataka wapone bwana.
Nabii Hebron: Mama, huyu amebatizwa?
Mama: Ndio
amebatizwa.
Nabii Hebron: Huyu
mtoto mmempata wapi?
Nabii Hebron: Sasa
sema ukweli ili huyu mtoto hapa iwe ndio mwisho
Nabii Hebron: SItaki
huo uchawi
Waumini: Ameeeeen
Nabii Hebron: Ndio
maana watu wanafanya kazi benki, wanakuta wana shoti. Unafunga duka, unakuta
shoti.
Nabii Hebron: Majamaa
ndio hawa.
Nabii Hebron: Eeeeh....
Nabii Hebron: Aisee,
bibi alikuambiaje rafiki yangu? Unajua YESU alinituma kwa watu kama hawa.
Nabii Hebron: Lakini
mbona mnaogopa?
Nabii Hebron: Hilo
jiwe lina maana gani?
Annastazia: Nimeliokuta
mlangoni hata sijui maana yake.
Nabii Hebron: Hujui
maana yake hili jie?
Nabii Hebron: Mmmmmh.
Nabii Hebron: Haya,
litupe hapo chini haraka.
Nabii Hebron: Ile
madini uliiba wapi?
Nabii Hebron: Na
hajavunja hata solex; na watu wamelala, kawapita hapo hapo wanakoroma
tirrrrrrrrrrrrrr... kabeba. Kavunja na geti. Lina solex na security guard
(mlinzi) yuko hapo.
Nabii Hebron: Usiogope
mama.... Hizi ndio dili bwana. Hizi ndio nini?
Waumini: Dili?
Nabii Hebron: YESU
anataka atoke huko bwana.
Nabii Hebron: Amen
Nabii Hebron: (anauliza
waumini)Hata wewe si ulikuwa huko bwana? Hata wewe si ulikuwa huko bwana?
Waumini: Ameeen
Nabii Hebron: Tumetolewa
huko
Nabii Hebron: Tusijihehasabie
haki. Si ndio?
Waumini: Ameen.
Nabii Hebron: Au
sio jamani?
Nabii Hebron: Niambie,
bibi anakufanyia bwana?
Annastazia: Ananiambia....
Nabii Hebron: Ongea
basi. Usiogope basi.
Nabii Hebron: Hebu
leta hata maji anywe bwana. Hapa kuna faraja. Sawa sawa?
Waumini: Amen.
Nabii Hebron: Mmesikia?
Nabii Hebron: Lakini
nikikuonya usikie. Sawa sawa?
Nabii Hebron: Ameletwa
kufanya kazi mjini lakini sio kufanya kazi mjini, ni kitega uchumi nakuambia anaiba
pesa nyumba za watu malaki na hamjui zinakwenda wapi.
Nabii Hebron: Eeeh?!
Kunywa maji rafiki yangu, kunywa usiogope.
Nabii Hebron: YESU
alikaa na wachawi, sawa sawa? Na anawakumbatia, Mimi sijali hata kama amekwenda
na kuzimu huyu.
Nabii Hebron: Eeeeh..
Lakini mpaka uwe na YESU, kumkumbatia tu na ile... shindwa, unashindiliwa!...
Nabii Hebron: Bibi
alikufanyaje mpaka ukaingia kwenye hii mambo?
Nabii Hebron: Hapa
tumeshamuombea jamani, hakuwa hivi.
Annastazia: Alinipa
damu ya paka
Nabii Hebron: Alikupa
damu ya paka?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Eeeh,
Paka imechinjwa hapo akapewa.
Nabii Hebron: Ehe,
damu ya paka vipi? ikoje ulivyokunywa? Sasa nieleze vizuri kila kitu halafu
nikuombee. Si unataka kutoka?
Annastazia: Ndio
Nabii Hebron: Haya
nieleze. Hamna mtu atakufuata akupeleke polisi bwana. sawa sawa? Hata polisi
mimi nawapenda, nawaombea. Na wao
wanafurahi watu wanakuwa raia wema. Au siyo jamani?
Waumini: Ameeen.
Nabii Hebron: Hebu
niambie sasa, bibi alikunywesha damu ya paka?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Nieleze
kila kitu dakika mbili...
Annastazia: Alinikuta
nimelala usiku,
Nabii Hebron: Enhe,
Annastazia: Mama
alikuwa yuko chumbani kwake na baba.
Nabii Hebron: Enhe
Annastazia: Nilikuwa
niko peke yangu. Siku hiyo wadogo zangu hawakuwepo.
Annastazia: Mimi
nilikuwa sijui chochote. Akaingia, akaniita, nikagoma kutoka
Nabii Hebron: Usiogope,
zungumza.
Annastazia: Nikasimama
mlangoni nikajiuliza nani ananiita? Nikashindwa kuelewa. Nikarudi kwenda kulala. Wakaja wapo wengi.
Nabii Hebron: Usiku?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Wamevaa
nini?
Annastazia: Wamevaa
nguo zao nyeusi na yeye amejifunga nguo nyeupe.
Nabii Hebron: Bibi
huyo?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Ehe,
wakakufanyaje? Zungumza kwa kifupi.
Annastazia: Nilikuwa
nimelala siwaoni, lakini nikiwa kwenye ndoto nimelala nikamwona huyo hapo pembeni
yangu. Wakaninywesha damu ya nyau lita mbili.
Nabii Hebron: Nyau?
Nabii Hebron: Ndio
maana jamani na nyau zinakuwa kali kwa sababu ya wachawi.
Nabii Hebron: Aha.
Sasa kwenye nyumba unawezaje kuingia ukachukua hela?
Annastazia: Mimi
hata sijui, nikifika hapo mlangoni wenyewe wanaugusa mlango unafunguka wenyewe.
Ndipo nikiingia hawanionyeshi sehemu yoyote. Napita tu pale walipokuwa
wanapoweka hela nachukua. Lakini hii juzi nimepotea na hata sijui nimepotea
poteaje. Japo nilisema nimeshafuta nikasema sitarudia tena.
Annastazia: Nikaenda
kubatizwa,
Nabii Hebron: Usijali
Annastazia: nikarudi.
Nabii Hebron: Anavyozungumza
hivi ndiio anafuta maagano
Nabii Hebron: Na
yale madini uliibaje?
Annastazia: Nilitoka
nayo nyumbani.
Nabii Hebron: Enhe,
Annastazia: wakati
nakuja mjini nikapitia kwa bibi. Nilivyopitia kwa bibi
Nabii Hebron: enhe
Annastazia: Akanipa
hirizi, pete tatu na maji yaliyochanganywa na damu ya paka lita mbili, nikawa
nakunywa njiani.
Nabii Hebron: Enhe.
Annastazia: Nakunywa
tu lakini sijielewi elewi
Nabii Hebron: Enhe
Annastazia: Nilipokuwa
kwenye gari, gari ilitaka kupinduka.
Nabii Hebron: Enhe
Annastazia: Yule
bibi akanisogelea, akaniambia sitaki ufe, wewe ndio ninayekutegemea, hautatoboa
siri yangu.
Nabii Hebron: Hutatoboa
siri?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Siri
gani hizo?
Annastazia: Alizokuwa
anazifanya kwa watu.
Nabii Hebron: Kama
nini?
Annastazia: Wanaenda
wanaua watu
Nabii Hebron: Wewe
ulishaua?
Annastazia: Hapana.
Nabii Hebron: Sasa
kwenye nyumba ya watu unaingiaje mpaka unachukua hela bila kuvunja hata mlango?
Annastazia: Nilikuwa
naingia kwa njia ya kwenye kona
Nabii Hebron: Hebu
onyesha kwa mfano ulikuwa unaingiaje mfano, onyesha tu. Usiogope wewe rafiki
yangu bwana. (Ananyanyua na kukuja mguu kwenye goti kuelekea nyuma)
Nabii Hebron: Ukishafanya
hivyo halafu inakuwaje?
Annastazia: Ninapotea
Nabii Hebron: Mlango
unafunguka?
Annastazia: Haufunguki.
Unaingia kwenye njia ya ukutani
Nabii Hebron: Enhe...
Annastazia: Niliingia
nyumbani kwa mama yangu kabisa alifunga mlango, akaenda kwenye msiba. Aliporudi
akakuta laki tatu hazipo.
Nabii Hebron: Laki
tatu hazipo!!!
Annastazia: Akaniuliza
hela nikamwambia mama sijui wewe si ulifunga mlango wako ukaondoka na ufunguo?
Nabii Hebron: Hata
anayekaa naye asimchukie, aliwekewa robot. Sawasawa?.
Nabii Hebron: Mmesikia
jamani? Unatumikishwa...
Nabii Hebron: Lakini
sasa umesema, hii kuongea ndio anafuta maagano.
Waumini: Ameen
Nabii Hebron: Damu
ya paka! watu mnaua? Watu mnaibiwa mapesa. ndio maana unakuta kuna watu
wanacheza bao tu, hawataki kufanya kazi. Kumbe wana hizi eee? (anakunja mguu)
Nabii Hebron: Eeee?!
Nabii Hebron: Si
unaona kuna watu wanacheza bao tu hawataki kulima wala kufanya kazi?
Waumini: Ndio.
Nabii Hebron: Kazi
yao ni ...(anakunja mguu)
Nabii Hebron: Nyumba
zenu haziingiliwi kwa damu ya YESU.
Waumini: Ameen.