JE UTALIJUAJE KANISA AU MADHABAHU ILIYOPO NJE YA
YESU?
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE,
Katika makala hii nitaelezea
jinsi ya kulijua kanisa au madhabahu ambayo inatumia jina la YESU lakini haipo
ndani ya YESU au YESU hayupo kabisa.
Kwanza kabisa kanisa hilo
linakuwa na misingi ya dini , sababu dini zilikuwepo tokea zamani na YESU
alipokuja alizikuta na zilimpinga kupitia mafarisayo na masadukayo, zamani
ilikuwa ni kimwili ila sasa hivi YESU anapigwa kupitia neno lake linabadilishwa
au kuchanganywa kweli na uongo.
1. Ukikuta
kanisa linachangisha pesa kanisani uelewe lipo nje ya YESU
2. Ubatizo
tofauti na ule wa maji mengi tena ya mtoni yanayotembea uelewe hapo ni batili
haijalishi jina la YESU linatajwa na hao wafuasi na wao wanaunganishwa na huo
uovu tena pasipo kupenda ila sasa mfunguke mataifa yote.
3. Kanisa
linalofungisha ndoa za mashoga au jinsia moja.
4. Linalo
abudu sanamu, au watoto wa MUNGU wanadamu kama wewe.
5. Kushiriki
ibada za wafu
6. Kuruhusu
pombe au hata kubariki pombe na watumishi wanakunywa vile vile mfano wine, na vinginevyo
vileo vyote.
7. Katika
kanisa au kwa mtumishi anayechaji watu pesa ndiyo afanye nao maongezi au
kuwasikiliza shida zao na kama haja toa pesa hakusikilizi na wengine kwanza
hata wanao kabisa cashier unalipa kwanza unapewa risiti ndiyo unapangiwa
appointment, hao watumishi siyo wa YESU wapo nje ya YESU ndiyo sababu
wanayatenda hayo.
Na hata
wengine huweka kiwango pale ambapo muumini ataomba apunguziwe bei ya kumwona
mtumishi wakiona umeomba sana unayo pesa kidogo tena bila aibu utaelezwa , haya
basi kiwango kimepunguka haya leta hicho kiasi Fulani, hao ni majangili wa
injili wapo kumchafua YESU na mwenyezi MUNGU,na kumwinua shetani.
8. Kanisa
linalozuia watu wasiokoke au wanasema hakuna wokovu, jiulize swali, je
YESU alileta nini? Jibu ni wokovu, sasa
why wanamnyima mtu asiokoke? Kinyume chake wanawatengenezea watu njia ya
jehanam na ndivyo ilivyo.
9. Mtumishi
wake ataomba pesa za michango hata kwenye redio, youtube, TV, huku ni
kumuabisha YESU, wengekuwa ndani ya YESU, yeye angefungua njia ila mtumishi au kanisa likiwa nje ya YESU
linakuwa ni omba omba na hata hao wanaotoaga hawatabarikiwa kabisa ni mnatupa
jalalani pesa zenu, ni bora mkafanye maendeleo yenu. Shetani amebuni njia ya
kuwafilisi wanadamu katika kanisa kwa kutumia njia hiyo.
NOTE:
Yapo mambo mengi sana
yakukujulisha vizuri zaidi wewe ingia katika website ya www.prophet hebron.org
ingia katika linki ya youtube, na blog yapo masomo mengi ya kukufundisha, kukufungua uelewe zaidi
kuhusu madhabahu au kanisa lililopo nje ya YESU na itakusaidia utakuwa huru na
utajiepusha nayo usije ukatekwa hapo akija YESU katika unyakuo ukabaki
ukiteseka na ukijuta majuto yasiyo na mwisho haya yote kanituma YESU kwa watu
wote muelewe na mumjue YESU wa kweli aliye
hai.
Sema, BWANA YESU,naomba unisamehe
dhambi zangu zote, uniokoe YESU uniandike jina langu katika kitabu chako cha
uzima wa milele, unitoe katika madhabahu ambayo ipo nje yako, uniongoze katika
madhabahu au kwa mtumishi ambaye wewe YESU upo ndani yake ili uniongoze sasa.
Amen.
Karibu sana kanisani kwangu
shida yeyote au mengine uliyokosa majibu wewe karibu YESU atakuweka huru na
ataingia ndani yako na atatembea na wewe na ataondoa mapando yote ya madhabahu
zilizojengeka ndani yako za nje ya YESU, au za yesu wa uongo.
NABII HEBRON.