JE UPO NDANI YA YESU AU NJE YA YESU?
UTAJITAAMBUAJE?
SOMA
HAPA…
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE,
aliye hai, YESU anawapenda sana watoto wake pia anajua kuwa mnampenda sana
baadhi yenu na wengine hata hawataki kumsikia jina lake ila yeye bado anakupenda
tuu, na katika somo hili nitaelezea ili wewe unayempenda YESU ujue ukaekaaje
ili uwe ndani ya YESU sababu nilipokuwa naongea na YESU siku za nyuma,
aliniambia maneno haya YESU mwenyewe, watu wengi wanaona wapo sahihi na wapo na
mimi na kumbe hawapo na mimi kabisa na hawajui ila wapo baadhi yao wanaojua
kabisa wanajiita wao ni wakristo lakini mimi YESU sipo nao ila wapo nje yangu,
sasa nitakufundisha mwana wa MUNGU ili uelewe ukakaeje kuanzia sasa ili uwe
ndani ya YESU milele usikae tena nje ya
YESU.
Utasoma kitabu cha
Yohana(15:4-7) Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza
kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu,kadhalika nanyi msipokaa ndani
yangu. Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu name ndani yake, huyo
huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. Mtu asipo kaa
ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka, watu huyakusanya na kuyatupa
motoni yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani
yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
BWANA YESU wa Nazareti asifiwe,
hapa utaona YESU mwenyewe akielezea kuwa kaeni ndani yangu ili na mimi niishi
ndani yenu, na kama YESU asipokaa ndani yako basi na wewe utakatwa kama tawi siku
ile ya mwisho na utachomwa moto. Katika jambo hili watu wengi ni wakristo
baadhi yao wapo kweli ndani ya YESU ila wengi zaidi hawapo ndani ya YESU wapo
nje ya YESU japo hawaelewi, na mimi nabii Hebron nakuletea ujumbe huu ili
ujirekebishe sasa uingie ndani ya YESU ili katika siku ile ya mwisho usije
ukakatwa kama tawi la mti likanyauka likakatwa, shetani amewapiga watu wengi
upofu kupitia viongozi vipofu nao hawasemi kweli ipasavyo na kuwafanya waumini
wapotee pasipo wao kujua wala kupenda na jambo hili YESU analijua ndiyo sababu
amenituma YESU niwaeleze watu wote wa ulimwengu wote msome na muelewe na
mumrejee yeye YESU wa kweli kiimani na kimatendo ili uingie ndani ya YESU wa
kweli ili awe BABA yako na mwokozi wako.
a.)
Mkristo ukiwa ndani ya YESU upo hivi;
Ni
lazima uokoke na ubatizwe kwa ubatizo wa maji mengi yanayotembea ya mtoni,
utaishi maisha matakatifu, utaongozwa na mchungaji au mtumishi aliyeokoka na
aliyeitwa na MUNGU na hajamsaliti YESU, unatakiwa utimize haki zako zote za
kukufanya ukamilike kama mkristo au alivyoonyesha YESU njia ya kumfuata, mfano
alivyobatizwa, utajitenga na mahali ambapo pa ibada palipo kinyume na biblia au
neno la MUNGU la kweli ambalo halijachanganywa na uongo.
b.)
Mkristo akiwa nje ya YESU yupo hivi;
Kwanza kabisa kinachokufanya uwe mkristo feki au
kwa lugha nyingine upo nje ya YESU kwa kuwa umebatizwa kwa ubatizo ambao
hakubatizwa YESU, mfano ubatizo wa maji ya kikombe, kubatizwa kwenye maji ya
kisima au kubatizwa kwa jina la mchungaji, hii ni dalili ya kukufanya uelewe
upo nje ya YESU, haijalishi jina lake limetumika huo ni upofu ambao shetani
alilipiga kanisa upofu kwa sehemu kubwa sana 98% katika dunia yote japo wapo
watumishi baadhi yao ni viongozi wao wametumwa kabisa na shetani kupitia kristo
wa uongo wayasimamie haya ili shetani awateke watu na wasiingie ndani ya YESU
wa kweli, wapoteze muda wafe katika hali hiyo hiyo wakiwa nje ya YESU, na YESU
asiwapate watu sasa enyi mataifa yote mjielewe kama upo hivyo uelewe upo nje ya
YESU hata kanisa linalofanya hayo ambayo hayapo katika biblia tayari yapo
kinyume na MUNGU na hivyo kwa njia hiyo
hata hao waumini hawawezi kuingia ndani ya YESU wa kweli sababu huo ubatizo ni
wa uongo.
Na ubatizo ni moja ya kiapo cha kuwa mkristo sasa ukila kiapo cha
ubatizo wa uongo uelewe kabisa na wewe ni mkristo wa uongo, inawezekana haujui
au haupendi ila kwa njia hii watu wengi wametekwa na hawajijui
wanaona wapo kweli katika upande wa YESU kumbe wapo nje ya YESU, na ikiwa wapo
nje ya YESU basi uelewe jehanam inakusubiri au inawasubiri, sasa uelewe na
ufanye maamuzi ili shetani asikupate au kwa maana nyingine kama umebatizwa kwa
ubatizo wa uongo basi wewe ni mkristo wa uongo na ili uwe mkristo wa kweli ni
lazima upate ubatizo kama aliobatizwa YESU ambao umeandikwa katika Biblia wa
mtoni.
·
Unakuwa haujaokoka na unajiita wewe ni mkristo.
·
Unachajiwa pesa za kufanyiwa huduma ya kiroho
uelewe upo kwa mtumishi ambaye yeye yupo nje ya YESU au upande wa mpinga kristo
na wewe unaenda kwa mpinga kristo kabisa.
·
Utasali katika kanisa linalochangisha pesa,
kuabudu sanamu, kuchangisha partners, lisilo na wokovu na hata kama lina wokovu
chunguza kama kuna michango, au matabaka ya kuwekewa viti maalum vya wale wenye
pesa au wale wanaotoaga zaidi uelewe hapo ni nje ya YESU na hata nguvu itendayo
kazi hapo siyo ya mbinguni ambako alipo YESU wa kweli.
·
Kanisa ambalo watu wanajaza form za kiasi cha
pesa unazozitoaga sadaka na kupewa risiti wakati biblia inasema utoapo sadaka
ni siri yako hapo uelewe ni madhabahu iliyopo nje ya YESU, shetani ndiye
anayeabuduwa ila watu hawajui siri hii, au ukute kanisa linawasoma watu majina ya wale watu
waliotoa fungu la kumi na kuwasoma majina wale ambao hawajatoa, mahali hapo
sipo kwa YESU ni nje ya YESU hata hizo sadaka haujamtolea YESU umezitoa katika
ufalme mwingine pasipo wewe kujua japo na wengine wanajua kabisa. Mambo hayo au
katika biblia hayapo na YESU aliyakataza sasa iwapo kanisa linayafanya hayo
basi hauwezi kupinga kuwa kanisa hilo
linampinga YESU na limeamua kukaa nje ya YESU na kuwaingiza na waumini
wanaompenda YESU wawe matawi ya shetani.
· Inawezekana kanisa linaitwa labda la YESU, la
MUNGU, la Roho Mtakatifu, ni la wokovu, chunguza sana usiangalie jina la kanisa
tuu ukafikiria kweli yupo YESU wa kweli hapo ukiona matendo ni tofauti , mfano
mnakunywa pombe, na hata mchungaji mwenyewe anakunywa au kukukaribisha kabisa
uelewe hiyo madhabahu ipo nje ya YESU na mengineyo machafu. Zaidi soma kitabu
cha jinsi kanisa lilivyotekwa na shetani, kilichoandikwa na Nabii Hebron na
vinginevyo utakuwa huru utaelewa mambo mengi na wewe utakuwa ni mwisho wako wa
wewe kuteseka na uingie ndani ya YESU.
NOTE:
Watu wengi katika nchi nyingi
YESU anajua mnampenda ila mpo nje ya YESU idada kubwa na ndiyo sababu hamjibiwi
na mnaona kama vile YESU hayupo, ni kweli ukiwa nje ya YESU usitazamie utamwona YESU
hata kama upo unasoma biblia, unaomba,
unatoa sadaka, mambo yote hayo ni bure unapoteza muda wako kabisa sasa ipo
neema ya YESU fanya maamuzi uokoke nausishiriki tena katika madhabahu zilizopo
nje ya YESU, ninakujulisha utazijuaje zaidi endelea kusoma makala ya Nabii
Hebron na uingie katika website yangu www.prophethebron.org
ingia katika link ya youtube yapo mafundisho mengi kwa ajili yako ulikata tama
, umefika mahali unaona maisha yako basi, hii ni sababu ulitekwa katika
ulimwengu wa roho ukawekwa nje ya YESU kupitia watumishi ambao wame mwakilisha
shetani wakitumia jina la YESU ili kuwapoteza watu. Amenituma YESU kwa kila mtu
anabisha hodi mfungulie mlango ili aingie ndani yako, awe baba yako, awe
kiongozi wako na mwokozi wako.
Sema, BWANA YESU wa Nazareti,
naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike jina langu katika kitabu chako
cha uzima wa milele, na sasa YESU uingie ndani yangu, nimeamua kutoka nje ya
YESU na kuingia ndani ya YESU. Amen.
Nabii Hebron.