Pages

Tuesday, March 10, 2015

UKRISTO WENYE ASILI YA MBINGUNI UPO HIVI…

BWANA YESU ASIFIWE, napenda kuwafundisha kuhusu ukristo wenye asili ya mbinguni ambao ndiyo tunatakiwa tuufuate ili siku moja na wewe ufike mbinguni ambapo ndipo penye asili ya ukristo wa mbinguni. Katika dunia hii kuna aina mbili za ukristo; upo ukristo wenye asili ya mbinguni na upo wenye asili ya kuzimu pia. YESU alishasema watakuja makristo wa uongo watatumia jina langu ili kuwateka wengi hata wateule lakini ninawaambia msiziamini kila roho bali zichunguzeni zimetokana na nini?

Uendelee kusoma makala ya Nabii Hebron utajifunza mengi na utazidi kuelewa ukweli na utakuwa mkristo mwenye asili ya mbinguni endapo utayapokea na ubadilike, ila ukigoma utakuwa umeamua kuwa mkristo mwenye asili ya kuzimu, na pia ni mkristo uliye adui na Kristo wa mbinguni.

Nitaelezea machache ili yakupe picha kuhusu ukristo wa mbinguni:
·        Lazima uokoke na ubatizwe kwa ubatizo wa maji mengi katika maji yanayotembea wala yasiwe ni ya kisima.

·        Hakuna kuabudu msalaba, wafu, sanamu, wala kubatizwa kwa maji ya kikombe.

·        Hakuna michango kanisani, huduma zote ni bure.

·        Kuishi maisha matakatifu siku zote.

·        Kufuata neno lilivyo bila kubadilishwa na kulitendea kazi.

·        Kanisa linaongozwa na huduma tano alizozianzisha YESU; Nabii, Mtume, Mchungaji, Mwinjilisti na Mwalimu tu, na siyo Askofu na nyinginezo. Yeye YESU hakuzianzisha hizo, na hata kama lina huduma hizo tano halafu inaongozwa na hiyo ya sita na kuendelea uelewe tayari pameharibika, umechanganywa ukristo wa uongo. Ni machukizo kwa MUNGU, ni dhambi.

·        Kanisa halinyang’anyi mali za watu au vitu vya waumini. Wala nyumba ya ibada siyo soko mahali pa harambee, ni mahali pa kumuabudu MUNGU tu, lakini inafanyika mambo tofauti na YESU alivyofanya.

Sema BWANA YESU naomba unisamehe, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima, nipokee ili niwe mkristo mwenye asili yako na siyo mkristo mwenye asili ya kuzimu tena. Nakataa ukristo wenye asili ya kuzimu kuanzia sasa, ulinipotezea muda. Nashukuru YESU sababu umeniondolea balaa kubwa.

NOTE:
Usishiriki tena katika kanisa au madhabahu iliyo tofauti na mbinguni na usirudi tena huko. Tokeni kati yao mkatengwe nao. Zaidi ingia katika website www.prophethebron.org, ingia katika blog utafunguka zaidi.


NABII HEBRON.