JE UNAJUA
KUWA UKIBATIZWA UBATIZO TOFAUTI NA ALIOBATIZWA YESU UNAKUWA UMEBATIZWA NA PEPO
LINALOITWA HIDAN?
SOMA HAPA….
Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na ndiye
aliye mwana wa pekee wa MUNGU. Napenda kuwajulisha mataifa yote mnaompenda YESU
na YESU anawapenda nyie sana, ila shetani anawaonea wivu wanadamu sababu anajua
wataenda mbinguni siku moja mahali palipo pazuri sana alipofukuzwa yeye lusifa,
na baada ya hapo MUNGU akatengeneza njia ya agano la ubatizo wa maji mengi
yanayotembea kama Yohana mbatizaji alivyoonyehsa njia na YESU na yeye akabatizwa
ili kutuonyesha njia, na sisi wote ili tuwe na agano na MUNGU ni lazima tuokoke
na kubatizwa kama yeye. Ila sasa pia mpango huu ambao MUNGU aliuanisha ili
kuweka agano na wanadamu kwa njia ya ubatizo wa maji mengi kwa sasa shetani
amefanikiwa kulizuia hili agano la ubatizo wa maji mengi ili wanadamu wasiwe ni
wakristo wa kweli, wasiende mbinguni, na wasiwe wana wa MUNGU bali wabakie wana
wa shetani, hata wanadamu wasijielewe wametekwa na shetani.
Ila nawafunulia siri hii ili mpone sababu hata mimi Hebron
sikuyajua haya na nilifikiri nipo salama kumbe nilishatekwagwa. Ila neema ya
MUNGU iliniokoa na hata sasa MUNGU bado neema yake ipo hivyo, uchukue hatua leo
uokoke na ukabatizwe ubatizo wa maji mengi ambao upo katika biblia na
unajulikana na MUNGU. Sasa hizo batizo nyingine zote mfano ubatizo wa maji ya
kikombe, ubatizo wa maji ya kisima, kubatizwa kwa maji mengi kwa jina la
kiongozi wa dini au pastor au kwa jina la mtu yeyote yule, uelewe wewe
umebatizwa na pepo kiongozi anayeitwa HIDANI, yeye huyu ndiye aliyetumwa na
joka kuu kueneza aina hizi za batizo kwa wakristo ili wasiingie katika agano na
YESU bali waingie agano na shetani, haijalishi limetajwa jina la baba, mwana na
roho mtakatifu au la YESU.
Nataka uelewe kuzimu yupo mungu wao anayeitwa joka kuu, yupo
mwana wa pekee ambaye ndiye shetani, yupo roho mchafu ambaye anaitwa Maxwell. Hawa
wote ndio wanaoingia agano na hao wote ambao wanabatiza ubatizo ambao haujatokea
mbinguni bali ubatizo wa akili zao. Hii yote ni ili kuwapoteza wanadamu wajione
ni wakristo na wamekamilisha ahadi za kuwa wana wa MUNGU. Kumbe mpaka sasa ni
wana wa shetani hata ukristo wa jinsi hii ni ukristo wenye agano la shetani,
sababu tafuta katika biblia hakuna aina za ubatizo hizo. Na ukisoma katika
kitabu cha Ufunuo 22:18-19; ole wake aongezaye neno la MUNGU au kulipunguza. Sasa
hauoni hapa hii laana inamhusu kila aliyebatizwa na kubatiza tofauti na biblia
ina maana yeye ni adui wa YESU na kama ni adui wa YESU basi yeye ni rafiki wa
shetani. Zaidi ingia katika www.prophethebron.org;
ingia katika link ya blog, soma kitabu cha ubatizo wa kweli kwa ulimwengu wote
kilichoandikwa na Nabii Hebron utafunguka zaidi na utajua ni wapi ulitekwa, na
wewe ni rafiki wa YESU au rafiki wa shetani.
Najua hampendi urafiki na shetani, sasa utii ubatizwe kama
alivyobatizwa YESU uingie agano na yeye. Usikubali hata familia, rafiki zako na
wengineo wabatizwe ubatizo ambao unawafanya wawe adui na YESU na kuwafanya watu
wasiwe wakristo wa kweli bali ni wakristo waliopoteza direction ya mbinguni kwa
kuingia agano la pepo Hidani. Pepo huyu hukaa katika vichwa vya kila mtu
aliyebatizwa ubatizo tofauti na YESU, yeye hukaa katika paji la uso wa watu
kama ni alama huyu ni wa shetani. Hivyo katika ulimwengu wa roho unaonekana mtu
wewe ni wa shetani na umesaini hilo agano ulipobatizwa. Ili upone ubatizwe upya
hiyo saini ifutike na usiabudu katika mahali wanapobatiza watu tofauti na
biblia ilivyoagiza na pia utakaposhiriki tu uelewe utanajisika tena sababu hizo
madhabahu ni za miungu ya dunia hii hapo hayupo MUNGU wa mbinguni
Sasa rejea ili upone, uwe mkristo mwenye agano na MUNGU wa
mbinguni badala ya agano la miungu ukabatizwa ubatizo wa miungu, ukasali katika
ibada za miungu pasipokujua, ukijua wewe ni mkristo kumbe ni mkristo mfuasi wa
mpinga kristo. Moja ya sababu itakayo kuhakikishia wewe ni mpinga kristo bila
kubisha. Nikuulize swali, mbona umebatizwa ubatizo tofauti na YESU? Kivipi
hivi? YESU alibatizwa akiwa mtu mzima, wewe umebatizwa ukiwa mtoto mdogo. YESU
hakuwa na mama wa ubatizo wala baba wa ubatizo, alienda peke yake, ila wewe
ulienda nao. YESU aliokoka kwanza, wewe haujaokoka mpaka sasa. YESU alibatizwa
katika maji yatembeayo, wewe umebatizwa katika maji ya kisima. YESU alibatizwa
kwa jina la BABA, MWANA, NA ROHO MTAKATIFU, wewe umeongezewa na jina la
mchungaji. YESU alizamishwa kwenye maji mengi mwili wote, wewe umedanganywa na
hao waongo wakakumwagia maji matone
kichwani.
Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron mpaka sasa somo
umelielewa na wewe uwatumie na wengine makala hii na watapona na utabarikiwa
sababu watu wataenda mbinguni na kugombana na shetani. Sema BWANA YESU naomba
unisamehe dhambi zangu zote, niliingia agano la ubatizo wa shetani pasipokujua
au kwa kujua, naomba uniongoze kwa mtumishi unayemtumia wewe anibatize niingie
agano na wewe nifute saini zote za pepo Hidani. Akae katika paji langu la uso Roho
wako mtakatifu tu kama alama yako ujue mimi ni wako. Amen.
Zaidi ikishindikana karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA
MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, utabatizwa na uingie agano na YESU, uwe mkristo na
rafiki wa YESU sana.
NABII HEBRON.