JE UNAJUA MAANA YA MSALABA KUWEKEWA TAJI LA MIBA KANISANI NI KUWAVALISHA WAUMINI NA MATESO KATIKA MAISHA YAO?
Kama alivyonituma YESU kwa watu wote niwaeleze ukweli,
utakayesikiliza utapona. Baada ya kanisa kutekwa na shetani akayaingiza
mafundisho yake ambayo hata katika biblia haijatuagiza hivyo wala kufanya. Inapokuwa
ni tofauti tu basi uelewe huyo ni shetani. Ila nitaelezea kwa ufupi kuhusu taji
la miba ambalo watu huliweka kanisani wakati wa kipindi cha pasaka wakifikiri
ni jambo zuri sababu hawaelewi, walipokea kwa njia ya mafunuo ya wamisionary
kwa njia ya mpinga kristo. Wote tunajua kuwa YESU ndiye akiyewekewa taji la
miba katika kichwa damu ikadondoka na alipata maumivu kwa ajili yetu. Alivalishwa
yeye kwa ajili yetu.
Sasa katika ulimwengu wa roho, kila taji la miba unapowekwa
katika msalaba na ni kanisani, kitendo hilo katika ulimwengu wa roho, kila
muumini anachomwa na ule mwiba katika kichwa chake na madahara yake, maisha ya
waumini hao roho ya mateso inakuwa inawafuatilia na kuwatesa sababu ya hilo
taji linalowekwa katika msalaba. YESU alishamaliza pale msalabani, akauwawa
katika msalaba uliokuwa unawaulia watu waliolaaniwa na sasa cha ajabu wakristo
wengi wao hawaelewi jambo hili hata wakafanya alama ya msalaba ndio ukristo. Alama
ya ukristo ni wokovu tu.
Nilipopelekwa mbinguni nilishangaa katika ofisi ya YESU
sikuona msalaba wala taji la miba. Ila nilipopelekwa na YESU katika ofisi ya
joka kuu nilikuta msalaba, taji la miba. Sasa funguka akili muujue ukweli; miba
na msalaba iliyomuulia YESU ilitokea kwa shetani. Cha ajabu makanisa yanaweka
product za shetani na hata kuzibusu baadhi yao. Hii haifai. Hatakuvaa msalaba
shingoni, unapovaa katika ulimwengu wa roho unahukumiwa wewe na ndio sababu
matatizo kwa wakristo hayaishi, hiyo ni sababu moja wapo mahali penye msalaba
siyo patakatifu, wala hakuna msalaba mtakatifu ni sababu haijatokea mbinguni.
Msalaba ni mzigo wako wa hayo maovu uyatendayo, watu tafsiri
wamekosea; sasa wanabeba msalaba
shingoni kimwili. Tupa usivae; mateso yatakuacha. Ingekuwa ni mtakatifu hakuna
pepo lingekufwata, usingekuwa na matatizo lakini cha ajabu wengi wao wanaovaa
ndiyo mashetani yanaishi ndani yao. Zaidi endelea kusoma vitabu vya Mtume na
Nabii Hebron, ingia katika YouTube, blog, website www.prophethebron.org. watumie na
wengine wapone utabarikiwa na YESU.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote,
uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Najivua misalaba
yote niliyoivaa na kuibusu sitaki tena sababu wewe haupo katika msalaba, umeshinda
upo mbinguni na uliteswa ili mimi nisihukumiwe tena, na damu yako ikamwagika
ili nipone. Asante kwa mafunuo yako uliyempa Nabii wako Hebron yameniponya. Amen.
NABII HEBRON.