MAHUBIRI YA NABII HEBRON KUPITIA REDIO KUHUSU UBATIZO WA KWELI
2012.
Asante sana ndugu mtangazaji. MUNGU akubariki
Kwanza kabisa nitaomba kwa ajili ya wasikilizaji
wote wa kipindi hiki,
BABA yangu na MUNGU wangu uketie mahali pa juu,
nina libariki jina lako nakulitukuza, nakuinua juu sana, sana. Maana hakuna
kama wewe, wengine wote ni wa uongo, wewe ni MUNGU uliye hai, uliyeumba
ulimwengu mzima, hata huyu anayekusikiliza ni wewe umemuumba, pia mimi. BABA yangu
asante, ninawafungua wasikilizaji wako, natuma Malaika fahamu zao, akili zao.
Nina ondoa pamba kwenye masikio, nguvu zote za upinzani ndani yao, ili wasisikilize
hili jambo ambalo unaenda kuwafundisha
watoto wako lisiingie, lazima liingie kwa nguvu na mamlaka ya jina lako
ulilonipa, maana wewe ni MUNGU. Ukisema umesema, maana sasa ni wakati wa kila
mtu kujua ukweli ili wasiangamie, wewe ni kweli, na wewe unawapenda.
BABA yangu Asante, sifa na utukufu
na kurudishia wewe, asante kwa muda huu
Asante kwa Malaika wako walioshuka
mahali hapa kuyashuhudia haya sasa hivi akiwepo Malaika Gabriel.
Asante naomba uzidi kuwabariki sana.
Ndugu msikilizaji leo nina mambo
ambayo nitaelezea kwa undani zaidi ambayo ameniagiza Bwana YESU ambaye ndie
njia na uzima na kweli zaidi, tunayemuabudu na tunayemsubiri,
Katika mambo nitakayozungumzia zaidi ni kuhusu
Ubatizo ni nini? Kwanza
Jambo la pili ubatizo wa kweli ni nini?
Jambo la Tatu, faida ya ubatizo wa kweli
Jambo la Nne: hasara za kubatizwa kinyume na
mpango wa MUNGU
Jambo la Tano: jinsi MUNGU anavyotaka ubatizo
ufuatwe na ubatizo ambao ni mapenzi yake yeye mwenyewe alioanzisha mbinguni.
Jambo la Sita: mambo yanayokwenda kutokea
Tanzania.
BWANA YESU ASIFIWE sana,
Ndugu msikilizaji MUNGU akubariki mahali ulipo.
Nitaanza kuhusu ubatizo, ubatizo ni kiapo kati
ya mwanadamu na MUNGU aliye hai, aliyekuumba na aliyeumba ulimwengu pamoja na
wewe ndugu msikilizaji, ubatizo ni agano
lako kati yako wewe na MUNGU ya kwamba wewe ni wake wala si wa mwanadamu au
kitu chochote au dini.
Ubatizo chanzo chake ni MUNGU mwenyewe, ndiye aliyepanga
akiwa na maana nzuri na nia njema kwa ajili ya mwanadamu aliyemuumba kwa faida
yake yeye mwenyewe MUNGU.
Na sababu nyingine ya MUNGU kumuumba mwanadamu,
amemuumba ili amuabudu yeye tu na sio kitu kingine chochote sababu nyingine
atawale kila kitu, maana hivi viumbe vyote aliviumba ili mwanadamu avitawale.
Ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 1:26, baada ya anguko la mwanadamu,
shetani akavuruga ulimwengu na akijua ya
kwamba ndiyo ameshinda na atatawala ulimwengu, na wana wa adamu wote, baada ya
haya kukatokea ndipo MUNGU akaanzisha huduma ya ubatizo ili kuwasafisha na
kuwakomboa wanadamu kupitia maji, kwanza kabisa MUNGU alimtuma Yohana aje
ulimwenguni kuja kubatiza, Yohana ni mnadhiri wa MUNGU aliyetoka mbinguni ,
akiwa mbinguni alitumwa na BABA kuja kumtengenezea njia yaani YESU, ukisoma katika
kitabu cha Yohana 1:15-18 inaelezea kabla ya ujio wa YESU.
Yohana nabii alitabiri. Na juu ya nabii isaya
pia alitabiri ikatokea. Yohana akazaliwa na Elizabeth na YESU ilitabiriwa hivyo
hivyo ikatokea, hawa wote ukiangalia jinsi wazazi wao walivyopata ujauzito ni
kwa njia ya ROHO MTAKATIFU, hata ukisoma kitabu cha Mathayo 1:18-28 Luka 11:38
inaeleza vizuri kabisa au kwa njia ya mpango MUNGU mwenyewe wake ili kuukomboa
ulimwengu huu. Yohana akazaliwa na akatenda yale yote aliyoagizwa na MUNGU. Aje
ulimwenguni afanye yale yote alioagizwa
na akabatiza sawa sawa na MUNGU, huku ulimwenguni
na alifanya na alibatiza sawa sawa alivyoelezwa na MUNGU, Ukisoma
Mathayo 3:11; Yohana alibatiza kwa maji mengi ikiwa ina maana kusafisha.
BWANA YESU asifiwe
Ndugu msikilizaji natumaini mpaka sasa umeelewa
Ubatizo ni nini, na chanzo chake ya kuwa ni MUNGU mwenyewe ndiye mwanzilishi na
wakati Yohana akibatiza na yeye alikuwa akieleza habari ya YESU, yakuwa yeye ni
mkuu sana hata yeye Yohana alikiri sistahili kufunga kamba za viatu vyake.
Ndugu mskilizaji hapa hata Yohana aliyetoka mbinguni akatumwa
ulimwenguni anakiri YESU ni mfalme na yeye alibatiza kwa Roho na Moto, ukisoma katibu
cha Mathayo 3:11 na hata Yohana aliogopa
kumbatiza YESU kwa ajili ya ukuu wake
alionao, lakini YESU alimwambia Yohana kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo
itupasavyo kuitimiza haki yote, basi akakubali na YESU alipokwisha kubatizwa
mara akapanda kutoka majini, na tazama mbingu zikamfungukia akaona Roho wa
MUNGU akishuka kama Ua, akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikasema
huyu ndiye mwanangu mpendwa wangu niliyependezwa nae, imeandikwa katika kitabu
cha Mathayo 3:15-17 soma.
Ndugu msikilizaji Mtoto wa MUNGU tena unafanana
yeye, MUNGU azidi kukuinua na kukufungua ufahamu wako zaidi uelewe haya
ninayokueleza MUNGU akutengeneze zaidi na akusikilize. Na MUNGU azidi
kukufungua ufahamu wako ili uelewe zaidi kuhusu ubatizo alioagiza MUNGU, watu
wote wabatizwe. Ukisoma katika injili ya ubatizo wa Yohana utaona alifanya yote
aliyoagizwa na MUNGU ili tu ukombolewe maana pasipo kubatizwa hauendi Mbinguni.
Ukisoma katika kitabu cha Yohana 3:5-7 inaelezea vizuri bila kubatizwa hauendi
mbinguni, YESU alibatizwa kwa maji mengi, kwa maana ndivyo ilivyoagizwa na
akafanya kama yeye alivyotaka kufanya, na YESU alikuja ulimwenguni ili
kuukomboa na kwa sababu alikuja ulimwenguni, kwa njia ubatizo ilimbidi na yeye
abatizwe kupitia ubatizo aliobatizwa.
Na sisi sote tubatizwe kama yeye ambaye ndiye
tunaye mwamini na ni ndiye njia na uzima na kweli soma katika kitabu cha Yohana
14:16 kama YESU ndiye njia ya uzima na kweli inabidi tufuate yale yote
aliyoagiza, ndio njia ya kutupeleka sisi mahali alipo, na MUNGU alimtuma Yohana
kubatiza, hakusema awe na msimamizi mwanadamu, msimamizi wako ubatizo ni ROHO
MTAKATIFU.
Halleluya, inatia huruma sana yaani utaona baada
na hata kabla ya YESU kubatizwa hakukuwa na msimamizi mwanadamu msaidizi,
msimamizi.
Sasa mpaka hapa natumaini umezidi kuelewa kuwa
katika Ubatizo siyo mwanadamu msimamizi, ni ROHO MTAKATIFU na siyo mwanadamu,
angalia mfano YESU alivyobatizwa na Yohana na mpaka YESU alivyobatizwa. Na pia na wale mitume wa YESU, walivyo
batizwa, nao walivyowabatiza watu, bila wanadamu wasimamizi. Walivyobatizwa
walisimamiwa na ROHO MTAKATIFU tu, na ndio mpango wa MUNGU, na ubatizo unasimamiwa
na ROHO MTAKATIFU na siyo mwanadamu.
Lakini siku hizi agizo aliloagiza MUNGU
limeachwa, madhamini wako wa ubatizo ni mwanadamu tena lazima awe mwanamke au
mwanaume, huo sio mpango wa YESU ni mpango wa shetani, ili kuangamiza watu
wasiende mbinguni. Ameniambia YESU, waambie ulimwengu mzima hashiriki huo
ubatizo feki narudia tena, ubatizo huo ni feki haujatoka kwake, hajalishi
wanamtaja jina lake, baada ya ubatizo YESU alishukiwa na Ua ili kumshuhudia
huyu ni mwana wa MUNGU na baada ya kushukiwa ROHO MTAKATIFU hapo ndipo YESU
alipoanza kuongozwa na ROHO MTAKATIFU na huyo mdhamini ambaye anayeushirika na
MUNGU asilimia mia 100% akamuongoza
kuyashuhudia matendo ya MUNGU, kumtia nguvu mwana wa MUNGU. Hivi ndiyo
inavyotakiwa katika ubatizo, ROHO MTAKATIFU tu, siyo mtu asimamiwe na mtu.
Halleluya! BWANA YESU ASIFIWE,
Upate kufunguka na watu wajue ukweli maana
katika neno lake wa kwanza atakuwa wa mwisho, na wa mwisho atakuwa wa kwanza.
Haya yote yalianza kwa watu weupe nao wamepuuza, lakini sasa tokea Africa na
Tanzania Nchi yako. Itajulikana, watu wamjue MUNGU.
BWANA YESU ASIFIWE!
Ndugu msikilizaji naomba uendelee kusikiliza ni
kwa faida yako wewe, halleluya!
Mwana wa MUNGU hivi ndivyo inavyotakiwa katika
Ubatizo ni ROHO MTAKATIFU tu, siyo mtu anayesimamia.
Haya ni mapokeo ya mwanadamu ambao baada ya YESU
kupaa mbinguni shetani akawaingia wale ambao, hawakumtii ROHO MTAKATIFU na
kubadilisha mpango wa MUNGU katika Ubatizo, na walibadili ubatizo wa maji
mengi, baadhi yao wakaanza kubatiza kwa kutumia beseni au kikombe, kubatiza
tena vitone vya maji kichwani tu, nikuulize, Je wewe msikilizaji, je Yohana
ndiye aliyebatiza hivyo? jibu hapana.
Ndugu msikilizaji MUNGU akutie nguvu akuinue na upate
kuelewa ukweli, na kama jibu ni hapana na kwa MUNGU ni hapana. Yohana hakufanya
hivyo na hata mbinguni ubatizo huo haupo na kama haupo mbinguni, huo ubatizo
umetoka wapi? Jibu hapana kwa shetani
Haijalishi wana litaja jina la YESU, huo ni
ubatizo feki, ameniambia YESU niwaeleze ulimwengu wote, ikiwa ina maana mataifa
yote, watu wote, mabara yote, bila mipaka, makabila yote wamjue YESU.
Jina lake linatumiwa vibaya watoto wake
wanaangamia kwa ajili ya watu wanaobadilisha mpango wake MUNGU, akasema
mwanangu Hebron watoto wangu wananipenda sana ila hawaambiwi ukweli kuhusu
mimi 98% shetani ameliteka kanisa
ulimwengu wote imebakia asilimia 2% tu
ndiyo inajua, ndio sasa waeleze watabizwe ubatizo niliobatizwa mimi YESU, watu
wanajua kwamba mimi ni njia na uzima na kweli, na hakuna atakaye fika kwa Baba
pasipo mimi YESU.
Mimi YESU nilikuja ulimwengu ili nionyeshe njia
ya kwenda kwa Baba yangu hakuwa mjinga kuagiza ubatizo wa maji mengi yaani MUNGU
hakuwa mjinga kumwambia Yohana mtu akibatizwa asiwepo msimamizi, leo hii nafasi
ya ROHO MTAKATIFU imechukuliwa na mwanadamu.
Matokeo yake ni ubatizo batili, nakuuliza wewe
unayempenda YESU, Je YESU alivyobatizwa alikuwa na mdhamini.
Jibu ni hapana hivi ndivyo inavyotakiwa mdhamini
wako ni ROHO MTAKATIFU na ndiye atakaye kuongoza na kukuombea maishani mwako
na kukupeleka mbinguni nakuuliza swali,
Ndugu msikilizaji ili uzidi kufunguka ufahamu wako Je mwanadamu atakuongoza
wewe ufike mbinguni? Jibu hapana. Oohoo…MUNGU
tusaidie.
ROHO MTAKATIFU ndiye atakayekusaidia kufika
mbinguni na kukushindia hapa ulimwenguni. Kama YESU alivyoshinda. MUNGU
tusaidie kweli yako imeondoka, MUNGU kuwa mjinga kutupa ROHO MTAKATIFU au
mdhaimini katika ubatizo wake, yeye alijua kwamba ROHO MTAKATIFU ana umoja na
wewe au kwa Lugha nyingine rahisi ili uelewe ROHO MTAKATIFU ni mojawapo ya
nafsi ya MUNGU wajue kwamba zote zina umoja, BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU lilekusudi
na kiapo cha ubatizo walipanga wote hawa watatu ili kukupata wewe sasa na
kuuliza swali kama wewe haujadhaminiwa na ROHO MTAKATIFU utakwenda wapi? Jibu
jehanamu badilika ubatizwe kama YESU alivyobatizwa yeye ndiye njia ya uzima na
kweli, njia yake uifuate hakika hautapona Yohana 4:6 inasema usifuate mapokeo
ya dini. Fuata muongozo wa ubatizo ulioandikwa kwenye biblia, kitabu kitakatifu
cha MUNGU.
Safari yetu ya mbinguni na maelekezo ya mbinguni
yameandikwa ndani ya kitabu cha Ufunuo wa Yohana 22:18-19 ameonya ole wake
atakaye ongeza au kupunguza kitabu hiki cha unabii sehemu yake itaondolewa
katika ule mji mtakatifu, sasa ndugu msikilizaji embu chunguza kwenye biblia
kuanzia mwanzo mpaka sura ya kwanza mpaka mwisho nakuhakikishia 100% hakika
hautakuta ubatizo wa kikombe yaani wa kichwani. Pili hamna mdhamini katika
ubatizo, mwanadamu iwe mwanamke au mwanaume, wote mliofanya hivyo ni mapokeo,
haujatoka kwa MUNGU,na kama haujatoka kwa MUNGU na basi umebatizwa ubatizo wa
shetani, na wewe umeingia agano na shetani. Sasa hapo utaona kabisa ubatizo umeongezewa
mambo mengi na huu mpango wa shetani alioupanga ili wewe usiende mbinguni maana
tayari umeenda tofauti na yeye MUNGU lakini wewe hauna shida, shida waliokubatiza
na hao waliomsaliti MUNGU na neno lake, ndio wamekuwa vipofu maana hayapo kwa
MUNGU. Ni kuulize swali Je MUNGU ni mjinga aliposema kila mtu abatizwe kwenye
kijito cha utakaso na azamishwe mwili wote, Jibu ni hapana na Je embu fikiria
ufunguke ufahamu wako uwe huru, Je kwa nini ni kichwa tu kinamwagiwa maji tena
matone tu, Je MUNGU aliagiza hivyo kichwa kimwagiwe maji Jibu hapana, aliagiza
mwili mzima uzamishwe kwenye maji kama YESU alivyofanya. Kama wewe ni mkristo
kweli na unafuata ukweli ambaye ni YESU, tunamwamini tumfuate mahali alipo Je
hicho kichwa yeye alizamisha kwenye maji? Jibu hapana.
BWANA YESU ASIFIWE.
Ooh MUNGU tusaidie
Ubatizo wa kuzama kwenye maji kama Yohana
mbatizaji umetimia na Je huu mwili umeingia kwenye maji wote Jibu ni kichwa tu,
kimemwagiwa maji.
Sasa ujumbe ameniambia YESU akanifundisha ukweli
niliogopa sana baada ya kujua ukweli maana mimi nilibatizwa hivyo, akaniambia
ameshasema na baadhi ya watumishi wangu waseme ukweli na waambie mataifa yote wamenisaliti
hawataki kusema ukweli baadhi, wananitaja kwa maji tu midomoni mwao baadhi yao
wanafiki.
Lakini ole wao mwisho wao umefika na sasa ni
wakati wangu baadhi yao hawasemi.
Mimi nataka mwili wako tu kama nilivyomtumia Paulo,
lazima watu wanirudie mimi kazi yake imeanza YESU mwenyewe tangu APRIL 2012
dunia nzima na njia ya kuzimu zote amenipa maelekezo namna ya kufunga kwa hilo
walikuwa wanategemea kuchukuwa nguvu hawana pia hawazipati tena, sasa hivi
masalia zimebaki baki vinaishia na wataporomoka mpaka ziro hasa watumishi
wanaotumia nguvu za giza hii ni kwa ulimwengu mzima tayari na wanajua mambo hayaendi.
Nchi zote mabara yote tayari wanajua mambo hayaendi.
Ndugu msikilizaji naomba sasa ujue ubatizo wa
kweli. Ubatizo wa kweli ambao MUNGU anaoutaka aliuandaa kwa ajili ya wewe upone
akishirikiana na ROHO MTAKATIFU. Mwana wa MUNGU ubatizo wa kweli ndio aliagiza
MUNGU ufuatwe, ni ubatizo aliobatiza Yohana, ni ubatizo aliobatizwa YESU tu huo
ndio ambao upo kwenye mafaili ya MUNGU na ndio unaotoka, na kama ubatizo uliopo
mbinguni basi ndio ufuatwe maana ndivyo anavyotaka aliuandaa kwa ajili yako.
Ili upone na sasa kama umekataa ubatizo anao utaka MUNGU na ukabatizwa ubatizo asioutaka
MUNGU, haijalishi jina lake linatajwa huo sio ubatizo. Ni ubatizo batili
haumuhusu yeye hayo ni mapokeo kutoka kwa waanzilishi waliomkufuru ROHO
MTAKATIFU na wapo kuzimu. Nilioneshwa na YESU,
tena ni adhabu kubwa sana, wamefungwa minyororo na YESU, ameniambia YESU
tayari hawa wameshakwisha kuhukumiwa hawataniona wana subiri moto siku ya
mwisho na wamekufuru ROHO MTAKATIFU na wanateseka sana, na walikataa kumtii
MUNGU wakamkufuru ROHO MTAKATIFU.
Sasa nakushangaa wewe unang’ang’ania dini unasema
uatakufa na dini ya wazazi wangu. Dini salama ni YESU tu kupitia wokovu na uwe
umeokoka, siyo unajiita mkristo halafu haujaokoka, wewe ni feki mbele za MUNGU,
mtegemee yeye tu na utapona,. Ubatizo wa kweli lazima taratibu zote alizozifuata
mwasisi wa kanisa zifuatwe Yaani YESU. Ikiwa na maana alichokifanya YESU ni
salama na ndio kweli na alifanya ili sisi tufuate njia aliotuonyesha.
Mtoto mdogo abarikiwe kwa kuwekwa wakfu kama
YESU, alivyowekwa wakfu na kubarikiwa akiwa Mtoto.
MUNGU aliandaa kumpa ujumbe mtumishi wake Simon,
ukisoma katika kitabu Luka 2:29 YESU alivyobarikiwa alikuwa mototo tena ajijui
na alivyokuwa mtu mzima anayo fahamu alibatizwa, na huo ndio mpango wa MUNGU wa
kweli uliopo mbinguni na hata Yohana alitimiza na YESU akafanya hivyo hivyo. Na
kama unataka kuwa mfuasi wa YESU ni lazima ufuate taratibu zote hapo utakuwa
kama yeye na utapokelewa na kufurahia nakufurahia na wazee 24 na malaika wake
na serikali yake yote ya mbinguni inafurahi.
Huo ubatizo mwingine hawafurahii kabisa na
ameniambia waambie wanangu wanielewe, nawapenda. Hayo hayajatoka kwangu maana
sasa naukomboa ulimwengu. Maana watumishi wengine vichwa ngumu, wamenisaliti,
wamenigeuka ndio maana ulimwengu unaangamia
FAIDA ZA UBATIZO WA
KWELI.
Ubatizo wa kweli ni
ubatizo wa MUNGU kwa hiyo unamamlaka, unashiriki ubatizo alioutaka MUNGU BABA muumba
wa vitu vyote ukiwemo na unashiriki kiapo kamili kama YESU kwa pendo hilo wewe
na YESU na wazee 24 wote wanashiriki na zaidi utajazwa ROHO MTAKATIFU kama YESU
alivyoshukiwa anakuwa kiongozi wako milele na atakaye kupeleka mahali alipo
MUNGU kama YESU alivyopelekwa tena, kwa kushiriki hatua alizozitaka yeye
mbinguni utakuwa wazi soma katika kitabu cha Yohana 3:5-7.
HASARA ZA KUBATIZWA
KINYUME NA MUNGU
Hasara moja wapo wewe unakuwa unashiriki jambo
ambalo halipo mbinguni na hata kitabu cha mwongozo wa kwenda mbinguni yaani
biblia.
Jambo lingine unakuwa unashiriki kuvunja Amri za
MUNGU soma katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:8-9 na Kumbukumbu la Torati
6:14 pia unabeba laana. Unamjaribu MUNGU maana unatumia jina lake na unafanya
kinyume na yeye anavyotaka na ukifanya kinyume na yeye tayari unaabudu miungu
mingine, kwa hiyo ubatizo ule ambao MUNGU hajauagiza hivyo unaabudu miungu, na
wewe ni mwana wa miungu wala si wa MUNGU kwa sababu hujapokea kiapo cha MUNGU
kupitia ubatizo wake wa maji mengi, bali umepokea ubatizo ambao haupo kwenye
biblia, hivyo ina maana ni ubatizo wa mungu asiyejulikana ambao ni miungu maana
haujatoka kwake.
Na usitegemee utaenda kwake sababu una chapa ya
miungu, na hao wanaofanya kazi hiyo hawafanyi kazi ya MUNGU kupitia neno lake,
bali wanafanya kazi ya kuwapoteza watoto wa MUNGU kupitia maneno ya miungu; kwa
mfano ya ubatizo huu wa maji ya kikombe na mengineyo.
Mtoto anapokuwa katika misingi isiyo ya MUNGU wa
kweli haijalishi jina la YESU limetajwa au kutumika, mtu huyu ataishi kwa
kushikiliwa na shetani na ndio maana mtoto mpaka awe mtu mzima, mpaka unajuta
kwa nini umemzaa anavuta bangi, anakuwa mwizi, mtukutu ni mtu wa ajabu hivi
vyote sababu ya kwenda kinyume na ubatizo alioutaka YESU, kwa sababu mtoto
alitakiwa apelekwe kanisani akiwa mdogo awekewe wakfu, sasa hajapelekwa kuwekwa
wakfu.
YESU alibarikiwa akiwa mtoto sasa siku hizi mtoto
anabatizwa kwanza halafu akiwa mtu mzima anabarikiwa Je huo ndio mpango wa
MUNGU Jibu ni Hapana, mtoto angekuwa amewekwa wakfu kama YESU haya mabaya yote
hayampati. Angeanza na baraka na ndio msingi wake MUNGU.
Shetani anakutengenezea kosa ili uangamie,
anakushitaki tena. Unaona jinsi alivyo mnafiki na shetani ni mbaya sana mkatae.
Anakutengenezea kitu halafu anakushitaki shetani ni mbaya sana mkatae.
Hasara nyingine hauendi mbinguni unakuwa
umeshiriki kiapo ambacho siyo kiapo amekitaka yeye MUNGU ili ukombolewe na kama
MUNGU hakubali kupokea kiapo ambacho yeye hajalitoa kwake, nikuulize swali Je
utakubali kusaini mkataba ambao wewe wenyewe kibinadamu haukuhusu wewe, Jibu
hausaini ndivyo ilivyo kama MUNGU. Hasaini wala hakubali.
Hasara nyingine ule wakati na wewe wa kubatizwa
ndio unapelekwa kubarikiwa ukiwa mtu mzima, hapo majira yako na baraka zako kwa
MUNGU kwako inakuwa imepitwa na wakati. Na MUNGU alikupangia hauendi na wakati
ndio maana kuna majira ya kupanda na kuvuna, kuna wakati wakulia, wakati wa kucheka.
Kwa hiyo haupati kitu kutoka kwake.
Hasara nyingine wewe unakuwa wa dini na wa
sheria tu, na hapa tunajua kabisa dini siyo mpango wa MUNGU na MUNGU anafuata
sheria na hapana jambo lingine.
Hasara ya kubatizwa ubatizo ambao si wa MUNGU,
unakuwa hutaki wokovu na unakuwa mgumu maana nafsi yako imeshikiliwa na mapokeo
ambayo hayajatoka kwa MUNGU, na kama hayajatoka kwa MUNGU, ni mpinga kristo,
haiwezekani wewe mkristo halafu unapinga wokovu. Soma katika kitabu cha Warumi
10:9-11 ina maana iko Roho ya mapokeo ya dini na mapokeo ya mwanadamu hayajui
yametoka wapi, ni ya shetani na ile roho haimtaki YESU.
YESU aingie ndani yako, huu upofu ambao shetani
ametumia njia mojawapo kuliteka kanisa na wewe unayekataa wokovu sasa ufunguke
uokoke haiwezekani wewe ndugu msikilizaji unayesikiliza sasa hivi, unajiita mkristo
halafu unakataa wokovu umebatizwa huo huo tena zaidi ubatizo wa maji hayo hayo
ya kikombe na ubatizo wa maji ya kisima, na ubatizo wa kubatizwa kwa jina la
mchungaji. Na unaenda kanisani na umetoa sadaka wewe unampinga na unasema
hakuna wokovu hii ina maana kwamba ndani yako iko ile roho ya mpinga kristo,
ndio inazungumza na kukataa sasa, ili uokoke lazima hiyo roho ing’olewe,
inapoondoka ndio unaokoka na wewe, ukiokoka ndio maana baadaye ulikuwa
hauamini, ndio maana unasema haaa hivi nilikuwa wapi, funguka kupitia ubatizo
feki, aliyoniambia YESU anakula kiapo na dini na mapokeo yaani yeye ni wa dini
tu, siyo wangu na ndio maana mtu huyu hamtaki kabisa YESU ananiambia mtu huyu
ananikubali tu mpaka ili roho ya dini na mapokeo itoke maana ndani yake roho ya kuasi inamshikilia ndani, na ile kuasi ikiwa ndani yake, haijalishi ni
kwa watumishi au waumini.
Atashiriki pombe tena hata atazibariki atafanya
uchawi kuoa mke zaidi ya mmoja bila hofu ya MUNGU, na hata ubarikio na ubatizo,
na batizo zao watashiriki vitu vya shetani utashangaa mtu siku anabarikiwa na
kubatizwa pombe disco sana, sasa nikuulize YESU anashiriki pombe, YESU anashiriki disco, mapokeo ya nini
nikuulize Je YESU anashiriki hayo au ROHO MTAKATIFU anaruhusu disco kwenye
sherehe za ubatizo na ubarikio Jibu
Hapana, kwenye hizo sherehe mapepo na roho mchafu ndio huja kushiriki na
kufurahi ya kwamba mpango walioupanga kukuangamiza umetimia, wacha sherehe za
pombe, disco, haijalishi ni za harusi au nini. ROHO MTAKATIFU huondoka. Roho
mchafu huyo hapo..
BWANA YESU ASIFIWE
Tunakuja jambo lingine
Jinsi MUNGU anavyotaka ubatizo ufuatwe, mtoto
mdogo akizaliwa apelekwe awekwe wakfu tena iwe madhabahu ya ukweli iliyo hai
ambayo YESU anakaa hapo, mtu akiwa na ufahamu aokoke kwa hiari yake mwenyewe,
ndio abatizwe kwenye maji mengi tena yanayotembea kijito cha utakaso, siyo
kisima tayari imekuwa feki hapo mwili wote uzamishwe kwenye maji, kama YESU
alivyobatizwa siyo kichwa au kudondosha kichwani tayari hujatimiza angalia anaye kubatizwa
kweli ana roho wa MUNGU ndani yake,
maana kama roho wa shetani yuko ndani yake hawezi kushiriki ubatizo wa ROHO
MTAKATIFU hapo ni ubatizo feki, ubatizwe kwa jina la BABA, MWANA na ROHO
MTAKATIFU, usikubali kubatizwa kwa jina la mtu au kitu chochote tofauti na
YESU.
Usikubali kubatizwa na Nabii wa uongo, hapo
anakuwekea ma roho yake, mashetani aliye ndani yake ili kukunajisi usiende
mbinguni usitoe pesa zako kwa malipo ndio ubatizwe YESU hakutoa ili abatizwe na
wewe fanya hivyo hivyo usikubali ndugu msikilizaji mahali popote uliko, hii ni
kwa ajili ya watu wote ulimwengu mzima rangi zote aliniambia BABA yangu.
Nami natumika kama chombo tu nikueleze wewe,
utafikiri ni Hebron lakini ni MUNGU anasema na wewe umeyasikiliza tu, badilika
achana na mambo hayo tupa, badilika achana na mambo hayo mrudie MUNGU.
Ujumbe huu ameniambia YESU ni kwa wote ulimwengu
huu, na mtu yoyote ambaye amebatizwa kinyume na MUNGU alivyoagiza, waambie
hawaja batizwa na mimi YESU, siyo siri kabisa maana ubatizo huu haujatoka kwa BABA
yangu ni ubatizo wa mapokeo, haijalishi wanalitumia jina lake wanaofanya hivyo
hukumu inawasubiri, injili imebadiliswa na ndio maana watoto wangu hawanioni,
wamefungwa na shetani anayefanya kazi ya uongo kinyume nilivyoagiza anakuwa nabii wa uongo.
Mtu yeyote akiongoea neno langu au kupunguza
huyo ni muongo, sina furaha naye, hata BABA yangu na Malaika wa mbinguni wote
hawa hawafurahi na ubatizo wa kikombe, maji ya kichwani
Ole wao mwisho wao umefika, narudi kuchukua
ulimwengu na kuwakomboa watu wangu mwenyewe na Tanzania sasa ndio Eden, mimi
MUNGU nimeichagua, na mataifa yote yatakuja kuponea hapa na kunijua mimi YESU,
haya maneno aliyoniambia nimeyanukuu kama alivyoniambia sijaongeza, sijapunguza.
BWANA YESU ASIFIWE
Ooh MUNGU atusaidie sana, nimekuwa nikieleza
watu kuhusu ubatizo huu, sasa kuna jambo moja nitakuuliza, watu wengine
wanasema kuwa Ubatizo ni Imani yako, ndio imefanya upokee ubatizo ukiwa mtu
mzima wewe ulivyopelekwa kubatizwa ukiwa mtoto mdogo, kwanza ulikuwa na imani
wewe? Ulikuwa unajua kinachotendeka, Jibu wala hakuna Imani kwa hiyo ni feki.
Ulivyokuwa mtoto mdogo ulikuwa unajua unabatizwa,
haujijui sasa utaniambiaje ubatizo ni Imani yako? Hautaki kubatizwa kwa maji
mengi.
Ila roho ya dini imekushikilia.
Inakuzidishia kujua haujabatizwa kwa sababu
ulikuwa hauna Imani kwanza haujui.
Je hawa wasimamizi wako wa ubatizo mwanamke na
mwanaume hao ndio ROHO MTAKATIFU wako? Jibu hapana, kwanza unajilaani maana
Imani yako inasimamiwa na mwanadamu au kwa lugha nyingine unamtegemea na
kumwabudu mwanadamu.
Neno la MUNGU linasema amelaaniwa amtegemeaye
mwanadamu.
Amebarikiwa amtegemeaye MUNGU.
Hapo tayari umelaaniwa wacha mapokeo, kama
umesikiliza vizuri ujumbe huu wa siku ya leo alioniambia YESU hakuwa na
mdhamini wa ubatizo ni ROHO MTAKATIFU alimshukia YESU, sasa nikuulize swali huyo
mdhamini ndiye atakaye kuongoza kwenda mbinguni ?
Wewe huyo mwanadamu saa nyingine ni unakuta ni
uchafu hana hata MUNGU nakufungua tu, hapo anavuta sigara, anakunywa pombe,
bado anakushika mikono anakuwekea roho mchafu anapita hapo, Jibu hakuna rudi
ukabatizwe upya iwe mtumishi wa dini mahali hapo, sehemu yoyote ambayo hujabatizwa.
Ukisoma katika ufunuo ole wake aongezaye au
apunguzaye, sasa huu ubatizo umetoka wapi? Umeongezwa, wacha nikuulize swali
lingine ndugu msikilizaji hao wasimamizi wa ubatizo , mwanamke na mwanaume wapo
kwenye biblia? Ni mapokeo ya mwanadamu badilika fuata YESU acha mapokeo ya
wanadamu ni ya shetani.
BWANA YESU ASIFIWE
Ooh MUNGU tusaidie
Jambo lingine aliloniambia ni kuhusu mambo
yanayokwenda kutokea Tanzania
Kama nilivyokwisha kuwaeleza toka April 2012
YESU, ndiye kaikamata Tanzania, ameiandaa kama Eden. Mataifa yote yatakuja
kuponea Tanzania atainua kila kitu na yeye ameingia kwenye serikali, lakini
hatatumia watu, hakuna uovu uliofanyika ambao utaendelea tena.
Haijalishi walikuwa wanatumia uchawi, uchawi
haufanyi kazi tena,
Kuna mambo yanayoenda kutokea kwanza nitaanza na
uchumi.
Katika migodi ya Tanzania ya madini inaanza
kurudishwa Tanzania kwenye ulimwengu wa Roho Tayari na itarudishwa kabisa kwa
watanzania,
Shirika la ndege, reli na usafiri wa maji. YESU
anahudumia hayo ni maandalizi ya kunyanyua nchi kwenye miji ya hapa maana
ameumba yeye
Jambo lingine linaenda kutokea na mtaona
mabadiliko makubwa sana, nitaanza na Bunge la Tanzania litakuwa na mabadiliko
makubwa na baadhi wanashushwa vyeo, viongozi katika Bunge na wengine
watashitakiwa na haya yameshaanza na wakati wowote mtayaona kwa macho, YESU
anatengeneza nchi ameamua mwenyewe.
BWANA YESU ASIFIWE
Mabadiliko mengine yanayoenda kutokea, baadhi ya
mawaziri watatolewa kwa wakati wake. Wala msiseme ni mwanadamu ni MUNGU
mwenyewe, pia na wakuu wa mikoa wanaoenda vibaya hivyo hivyo itakuja kwa wakuu
wa wilaya hivyo hivyo kwa madiwani hivyo hivyo.
YESU ameamua mwenyewe anaendelea hatua kwa hatua.
Kwa hiyo mnayoyaona MUNGU ameamua
BWANA YESU ASIFIWE
Uchaguzi wowote katika nchi kuanzia mwenyekiti,
diwani, ubunge, uraisi atakaye tumia uchawi ili apate hicho cheo, hatapa
ameniambia YESU.
Mliokuwa mnamtegemea shetani kupata madaraka sasa
ni mwisho mtayaona YESU anasimamia mwenyewe chaguzi zote na haki mtaiona,
akaniambia hawa watu wote sisi mimi nimewaumba?
Nitawaonyesha na kuwabadilisha mioyo wakati wa
kupiga kura, yule anayetumia uchawi hata kama wanatoa hongo hawatapigiwa kura
na haitaibiwa, mimi nimesimama MUNGU mwenyewe.
BWANA YESU ASIFIWE
Na watumishi wanaotumia nguvu za giza
wataporomoka.
YESU mwenyewe ndio anafanya kazi hiyo, na yuko
tayari kazini anawashughulikia ni ulimwengu mzima.
Mabara yote anarudi sasa amechoka, anayepigana
na mimi anapigana na yeye, hawatakaa waniweze, mimi na songa mbele kama YESU,
alivyokuwa akipita hivyo hivyo na itadhihirika
MUNGU ameniambia kwa gharama yoyote ataukomboa ulimwengu, wanao kengeuka kiboko
cha kipo njiani na wengine tayari na wengine wanaotaka kukimbia nchi ya
Tanzania hawataweza huko waliko, Yona alikimbia huko huko alifuatwa na wengine
wako katika nchi hizo hizo za kwao huko huko, YESU anawashughulikia huko huko,
wataporomoka, YESU yupo kazini, lazima mliofanya uchawi yawarudie nyie nyie.
BWANA YESU ASIFIWE
Ooh MUNGU tusaidie
Jambo aliloniambia niendelee kuwaambia watoto
wangu, hiki nikidonda sugu wazidi kuendelea kufunguka mahali popote wanataja
jina langu na kuna michango mimi sipo ni shetani yuko hapo, haijalishi mimi
wananitaja, maana siyataki haya. Nilikwishaingia kwenye madhabahu nilipokuwa
ulimwenguni enzi zangu niliya bomoa bomoa na kuyakataa, sasa yamerudishwa sipo
hapo, mnachanga michango mnaita sadaka hiyo siyo sadaka, huo ni unyang’anyi, makanisa
yanayo kopa benki, mimi sipo nimesema kwamba msikope wala msidai riba , mimi
YESU nimeshakwisha kukataa. Leo imerudishwa roho ya mpinga kristo hiyo. Kanisa
linaloabudu sanamu na mnanitaja mimi sipo, au kuabudu watakatifu mimi sipo,
nimewaumba mimi nina wivu, nimesema kisiabuduwe chochote nilichokiumba, sasa
hata niliowaumba mnawaabudu mimi sipo. Mahali wanapokuwa na ibada ya wafu nimekwisha
sema tengeneza maisha yako hapa wewe unaacha kutengeneza maisha yako hapa
unategemea kwamba ukifa utafanyiwa ibada ya wafu, ukisha kata kauli tu, ndio
mwisho wako mwana wa MUNGU.
Ooh MUNGU tusaidie, funguka mwana wa MUNGU,
kubali kwenda mbinguni usipoteze muda wako hapa, ukisubiri kwamba ukifa
utaombewa hii ni usanii tu.
Soma katika kitabu cha Waebrania 7:20 kwa kuwa
haikuwa pasipo kiapo Waebrania 9:27.
BWANA YESU ASIFIWE
Anasema kwamba na kama vile watu wanavyowekewa
kufa mara moja baada ya kifo ni hukumu ooh funguka mwana wa MUNGU, ukisha kufa
tu pap, hukumu hiyo yale yote uliyoyapanda ndiyo hayo hayo utavuna hayo,
funguka tengeneza maisha yako.
BWANA YESU ASIFIWE
Funguka funguka kabisa, usikubali kabisa “BWANA YESU
ASIFIWE”
Jambo lingine hii kwa kanisa lolote linalonyang’anya
mali, kusema mimi mnanyang’anya mali zao kwa kutumia jina langu, mimi si
mnyang’anyi au mtumishi anayenyang’anya mali kwa kutumia jina lake, huyo sio
mtumishi wangu yeye hakutuma watumishi wanyang’anyi, hakutuma watumishi
kukusanya pesa , hakutuma kuzini na kondoo, hakutuma kufanya kazi hiyo,
inamaana mtumishi wa YESU ndani yake ndiye YESU anayekaa, sasa kama YESU anakaa
ndani yake, Je YESU atazini na kondoo? YESU atakunyang’anya mali zako? Je YESU
atasema hili ni kaburi, Kaburi la kuzini hapa?
Ooh ninakwambia ameniambia tena ufunuo mwingine
hata kaburi alilozikwa halifai kwenda kuabudu pale hilo kaburi, kulisujudia ni
yeye peke yake anatakakiwa watu wengine wanatembeza makaburi wanasema YESU
hapa, hakuna, hataki acheni hata kuabudu kaburi la YESU hataki liabudiwe ni
MUNGU peke yake. MUNGU wa Ibrahimu na Isaka.
Jambo lingine
akaniambia mwanangu hivi kuna mtu anaweza kununua nguvu zangu, nikabaki
nikiduaa nikamwambia hapana akaniambia hivi leo hii watu wanaambiwa upako wangu
unauzwa ukisikia mtumishi anasema upako
unauzwa huo ni upako wa shetani.
Nikuulize wewe kuna
mtu anaweza kununua nguvu ya MUNGU. Jibu ni Hapana,
Nikuulize wewe kuna
watumishi wanaponya kwa kutumia nguvu za mapepo Je? MUNGU anaponya kwa kutumia
mapepo? Funguka ufahamu kaniambia siku hizi mimi mwenyewe nakataa ushoga lakini
wameibuka watu ambao wanatumia Jina langu wanasema ndoa za mashoga, sasa
nikuulize swali wewe YESU anaruhusu ndoa za ushoga.
Ameniambia YESU huko
hayupo na msitegemee akuongoze, nyakati hizi ni mbaya mwana wa MUNGU.
MUNGU akubariki
sana.
SALA YA TOBA
BWANA YESU naomba unisamehe
dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua au kutokujua namkataa shetani na kazi
zake zote, naomba uniandike jina langu ndani ya kitabu chako nishike mkono
uniongoze wewe mwenyewe, nisipotee tena wewe ndiye salama. Amen.
Nakufunika kwa damu
ya YESU WA NAZARETI.
Karibu katika
kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.
Visit www.prophethebron.org na YouTube ya
Prophet Hebron.
NABII HEBRON.