SALAMU ZA
MWAKA MPYA 2015 KWA MATAIFA YOTE!
BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA NAZARETI aliye hai, nawasalimu
wote wa mataifa yote nikimaanisha nchi zote sababu nchi zote ni mali ya MUNGU
na siyo mali ya shetani. Katika mwaka huu 2015, nilipokuwa naongea na MUNGU
yapo aliyonieleza kama mimi mwenyewe Nabii Hebron kwa utukufu wake MUNGU
mwenyewe, na yapo ambayo ni ya kuwajulisheni watu wote, wote mjue MUNGU anataka
nini na hataki nini. Akaniambia, Hebron mimi sipendi miungu sababu miungu ni
shetani, waeleze watu ukweli sababu wengi wananipenda mimi lakini hawajielewi
wapo katika upande wa mungu yupi, na haya yote yanasababishwa na watumishi
waliomsaliti MUNGU wakawapeleka wanadamu katika ibada za miungu. Sasa nitakuelezea
ili uelewe miungu ni nani na MUNGU ni nani. Nitakuelezea kwa kiroho, kila
mtumishi anayebatiza ubatizo tofauti na wa maji mengi yanayotembea, tayari yeye
anaabudu miungu na hata hilo kanisa silo la MUNGU wa mbinguni bali ni la
miungu, haijalishi likatajwa jina la YESU wewe angalia je wanalitenda neno kazi
kama lilivyo au ni kinyume? Na utakapoona ni kinyume basi sasa elewa hapo ni
kwa miungu na wewe ufunguke ili uwe mwana wa MUNGU na siyo wa miungu.
A. KAMA
UNASHIRIKI YAFUATAYO UJIJUE WEWE UPO UPANDE WA MIUNGU NA SIYO KATIKA UPANDE WA
MUNGU WA IBRAHIM, ISAKA NA YAKOBO:
·
Kama haujaokoka na unajiita wewe ni mkristo,
bado upo katika miungu.
·
Kubatizwa ubatizo wa kisima, ubatizo wa kikombe,
kubatizwa kwa jina la mchungaji.
·
Kumuabudu mtumishi yeyote hata kumuita yeye ni
MUNGU.
·
Kubatiza watoto wadogo, kubariki watu wazima.
·
Kanisa lenye huduma sita badala ya tano
alizozianzisha YESU au kanisa lenye huduma zaidi ya tano na kuendelea ikiwemo
huduma ya Askofu. Hakuianzisha YESUna kama hakuianzisha YESU kaianzisha nani? Jibu,
miungu. Na unapoongozwa na mfumo huo na wewe unafanyika kuwa katika mpango wa
miungu kama ulikuwa hauelewi sasa uelewe. Amenituma MUNGU niwaeleze ukweli,
anayetaka kupona atapona, atakayekaza shingo Jehanamu palipoandaliwa moto wa
kuwachomea miungu na wewe usipowacha utaenda huko huko.
·
Kanisa linalofanya biashara, kuwa na benki,
kuchangisha pesa makanisani, kukopa pesa benki, hayo yote siyo makanisa ya
MUNGU wa kweli bali ni ya miungu, na waumini mnaosali hapo na nyie hufanyika
kuwa watoto wa miungu japo haupendi, sasa ufunguke. Ukisoma katika biblia ya
Neno la MUNGU aliyeiumba mbingu na dunia yeye anayekataa hayo katika neno lake.
Sasa endapo mtu ataivunja sheria ya MUNGU basi ajielewe ameipokea sheria ya
miungu na yeye yupo chini ya miungu katika ulimwengu wa roho. Sasa mfunguke
mataifa yote, mtoto wa MUNGU ambaye ni YESU WA NAZARETI, karibia anarudi kuja
kuwachukua wale ambao wapo katika upande wa MUNGU ambaye ndiye BABA yake yeye
hatamruhusu yeyote ambaye yupo katika upande wa miungu, nimekufunulia uelewe
jinsi ya kuielewa miungu inavyoliendesha kanisa na kulijenga kanisa lake katika
ulimwengu wote na kushika kasi katika nchi zote 98% ya ulimwengu wote,
madhabahu zote ni za miungu ya dunia hii.
·
Mahali popote ambapo watu wanaenda kutoa sadaka
zao kwa vinyago makanisani au katika kanisa ukaona sanamu ya aina yeyote, hapa
uelewe ni madhabahu ya miungu na ndiyo iliyowateka watu hao wasiende mbinguni
na bila kutoka hapo uelewe wewe ni adui wa MUNGUwa kweli na unabakia kuwa
rafiki wa miungu. Sasa uelewe na ufunguke ufahamu wako (soma katika kitabu cha
Kumbukumbu la Torati 5: 7-9) hiyo ni miungu yenyewe na sasa inayatumia makanisa
mengi katika ulimwengu wote na kuwapoteza watoto wa MUNGU kama ilivyo sasa hata
wewe fikiria upate picha hizo sanamu ni za nini katika nyumba za ibada? Je kama
huyu MUNGU wa kweli yeye anaonya hataki sanamu, je nikuulize swali je anavifurahia
viwepo katika madhabahu yake? Jibu, MUNGU aliyeziumba mbingu na dunia yeye siyo
MUNGU wa vinyago au sanamu, bali miungu ndiyo inayoshirikiana na vinyago au
sanamu katika makanisa au madhabahu
Mahali pa jinsi hiyo uelewe ni
kwa miungu. Shetani alitumia ujanja mwingi ili kuwapofusha wanadamu wasijielewe
akawateka kama ilivyo wote wanaoshiriki mambo hayo tayari wao ni watoto wa
miungu na wametekwa na miungu. Amenituma MUNGU na serikali yake niwafungue
macho muelewe ili mpone. Mtoto wake ambaye ndiye YESU WA NAZARETI muda wowote,
siku yeyote isiyojulikana hii ni siri yake MUNGU peke yake.
·
Kanisa ambalo kiongozi wake ni mchawi au
anatumia nguvu za giza au yeye ni freemason au mwanachama wa illuminati, kanisa
lote pamoja na waumini wote wanakuwa chini ya miungu yake huyo kuhani, sababu
jinsi alivyo kuhani ndivyo na kondoo wake walivyo.
·
Kanisa linaloongozwa na mchungaji halafu bado
yeye ni mwanasiasa au anamtumikia kaisari, huyo ajielewe yeye yupo kwa Kaisari
na siyo kwa MUNGU. Hawezi kuwatumikia mabwana wawili, kama ni MUNGU basi ni
yeye tu na siyo kujiita mchungaji halafu upo katika siasa wewe haufai mbele za
MUNGU. Kila alivyo hivyo yeye siyo mtumishi wa MUNGU bali yeye ni wa miungu.
(Kumbukumbu la Torati 6:13-15 soma).
·
Ibada za misalaba, ibada za wafu, kubusu sanamu,
kubusu misalaba, hayo yote uelewe ni mambo ya miungu.
NOTE:
Nimeelezea kwa ufupi mpate kuelewa ni jinsi gani miungu
ilivyowashikilia watu wengi na hata watumishi baadhi yao hawajui wanaabudu
miungu tayari na tayari wameshatekwa na shetani. Katika salamu za mwaka mpya wa
2015 kutoka kwa Nabii Hebron, ikatae miungu ili upone na uchukue maamuzi kutoka
katika moyo wako na usishiriki katika makanisa ya miungu, wewe chunguza hayo
niliyokueleza na zaidi endelea kusoma katika makala ya Nabii Hebron utaujua
ukweli zaidi na utakuwa huru.
Watu wengi wanaona wapo sahihi na hata wameokoka kumbe wapo
kwa miungu. Na haya yote ni shetani anaungana na watumishi waliomuasi MUNGU
sasa wanatumia jina la YESU kuwapotezea watu na kumbe siri wanaijua.
Sema BWANA YESU WA NAZARETI naomba unisamehe dhambi zangu
zote unitoe kwa miungu uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele. Miungu
siwataki katika maisha yangu pamoja na madhabahu zenu kimwili na kiroho. Amen.
Karibuni katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE mkutane na MUNGU aliyeiumba mbingu na nchi pamoja na wewe na awe
MUNGU wako sasa.
NABII HEBRON.