Pages

Sunday, December 7, 2014

JE UNAJUA TAA YA CHEMLI NI NYUMBA YA SHETANI (JOKA KUU).

BWANA YESU ASIFIWE, watu wote wa mataifa yote karibu sana katika makala ya Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo. Ufundishwe na upone na pia karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, Arusha, Tanzania. Ingia katika website www.prophethebron.org utakutana na habari za YESU alizonieleza kwa kinywa chake pia na katika YouTube.

Mwaka 2010 wakati bado ninafanya kazi ya professional driver guide, mara nyingi sana YESU alisema na mimi mara nyingi sana, alinifundisha na kunipa maagizo nimuaandalie kanisa lake la mwisho, akanichukua, akanipeleka kuzimu, nikaona mahali anapoishi Joka Kuu, yeye ambaye ndiye baba yake shetani. Nikaiona nyumba yake ilivyo na sasa ni miaka mine tokea YESU anijulishe hayo. Nyumba ya Joka Kuu ipo kama vile ilivyo ile chupa ya chemli ya kioo, nilishangaa, akaniambia angalia vizuri sana ila sikujua mimi maana yake. Ilipita miezi mitatu, karibu itimie miezi mine hivi akanifundisha maana yake niliogopa sana, na mimi akanionya nisitumie kabisa taa ya chemli sababu unapoitumia ina maana kuwa katika nyumba yako umeijenga nyumba ya Joka Kuu na hivyo yeye hupata mlango kupitia hiyo taa. Akaniambia aliwakamata wanadamu fahamu zao na wao hawajui lengo ni nini ila sasa Hebron wewe ndiye nimekufunulia mtumishi wangu

Sasa mimi naishi ndani yako na hayo yamefichika, niliowaita ili niwafunulie mambo yaliyofichika nao wamejiunga na Joka Kuu, ila kupitia wewe injili yangu itaenda mbele tu na watu watapona. Wale watakaokusikia watapona na wale watakao kaza shingo hawatapona. Akaniambia, unapoiwasha katika nyumba yako ule mwanga unakuwa ni mwanga wa joka kuu unamiliki maisha yako na balaa na mikosi na vifungo vinakumulika kila mahali na hata maisha yako. Akaniambia tumia mshumaa au torchi au taa ya umeme. Hata kama itakuwa ni taa ya bulb halafu ikawekewa chemli bado itakuwa tuu umeiweka nyumba ya joka kuu itawale hapo na maisha ya watu na kila unapotumia chemli unazidi kujengwa katika nyumba ya joka kuu na katika ulimwengu wa roho na wewe unakuwa unaishi katika nyumba ile ambayo nimekuonyesha ya joka kuu. Yapo madhara mengi ila nitayaelezea katika makala nyingine.

Ninakufunulia sasa uelewe na upone hayo ni maamuzi yako wewe kuacha sababu nimekujulisha asili yake na watu hawajui na ndio sababu watu ni ngumu kukaa katika utakatifu sababu shetani alibuni ni jinsi gani atamteka mwanadamu. Ni bora koroboi, ni salama. Wengi mtapona sasa. Mshukuru YESU WA NAZARETI anayenifundisha na MUNGU wa mbinguni na ROHO MTAKATIFU ili mtoke kwenye majengo ya  shetani. Miji yenu isiwe ni nyumba ya joka kuu ili MUNGU afanye makao katika nyumba zenu na awe ni BABA yenu. Utakapoacha kuitumia tu na kuitoa katika nyumba yako kitendo hicho tayari umeiondoa nyumba ya joka kuu na mikosi yake na kila kitu. YESU atakaribia katika nyumba yako na atakuwa ni mlinzi wako.

Zaidi soma makala ya Nabii Hebron utayajua mengi na utakuwa huru, nawakaribisheni mataifa yote katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, Arusha, Tanzania. Amen.

NABII HEBRON.