JE UNAJUA
KAZI YA FATHER CHRISTMAS KUZIMU?
Kama nilivyokuisha elezea katika makala za Nabii Hebron
kuhusu father Christmas au Santa Claus, kuwa baada ya Santa Claus au Saint
Nicholas kufa yeye hakuenda mbinguni yupo kuzimu na kuzimu anazo kazi alizopewa
ikiwemo ni kueneza injili ya mpinga kristo pamoja na kuitawala ile siku ya
Christmas watu waacha kumrudishia MUNGU utukufu mbinguni, wabakie na midoli ya
mizimu ya Saint Nicholas na kuwafanya mataifa wawe maadui wa YESU kwa kushiriki
kumuita yeye ndiye father Christmas, wakati hakuna anayestahili kuitwa father Christmas
katika ulimwengu huu. Hapa jiulize tu, je huyu mdoli unayempamba na kumuita yeye
ni father Christmas, je huo mdoli ndiye ahadi ya MUNGU kwa wanadamu? Au yeye
huyo father Christmas yeye ndio mkombozi wa ulimwengu? Na kama siyo yeye, je
umeshaona wapi mkombozi wa mahali popote haongei, hapumui, hali chakula,
amening’inizwa kama maiti? Mpaka hapo enyi mataifa sasa mnapata picha kuwa
mlidanganyika na kuingia katika kushiriki sanamu au ibada ya sanamu.
Unapoliweka ndani ya nyumba yako tu uelewe kwako panakuwa ni
madhabahu ya masanamu, iwe ni kanisani, hotelini au popote pale, japo najua
wengi hamuelewi na wengine hata wananishang’aa nasema nini. Huo ndio ukweli,
amenituma YESU niwaeleze ukweli mataifa yote mpate kupona, mtakaosikia mtapona
na hasira ya MUNGU, mtakao kaza shingo ile dhambi ya kuabudu sanamu ujue
unaishiriki na wewe. Leo utubu na uepuke, usije ukawa adui wa MUNGU kama siku
za nyuma, haya yangejulikana mara tu shetani alipo yabuni ila YESU aliniambia
kila alipowanyanyua watumishi walikuwa wanafika mahali wanamsaliti na kumfuata
shetani. Sasa amenituma kwa mataifa yote najua wengi hamjui na wewe watumie
wengine ujumbe huu ili wapone. Hakuna ushirika wowote kati ya father Christmas na
MUNGU bali upo ushirika na malango ya shetani kati ya father Christmas na
shetani ili awateke wanadamu ambao ni watoto wa MUNGU. Na sasa haitawezekana
katika jina la YESU WA NAZARETI, kwa wale ambao watatii maneno haya ambayo siyo
yangu mimi Hebron mimi ni chombo tu cha kupeleka ujumbe wa MUNGU.
Kazi nyingine anaifanya father Christmas kule kuzimu ipo
meli kubwa sana ambayo ukubwa wake ni kama 1,300,000 square kilomita. Meli hii
inaendeshwa na nahodha anaitwa father Christmas ambaye ndiye mzimu wa Saint
Nicholas, meli hii ilikuwa inapandwa na mtu mmoja tu ambaye alikuwa ni msaidizi
wa joka kuu namba tatu katika ufalme wa shetani ambaye ni mwanadamu anaitwa Maxwell,
kwa sasa anaitwa Isaya yupo katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE, nimemrudisha duniani kama alivyoniamuru YESU na kuubomoa ufalme
wa shetani na serikali yake na bado naendelea na kazi hiyo sababu siyo siri
wala sitaacha kumpiga joka kuu milele, aliwatesa watoto wa MUNGU na mataifa
yote. Meli hiyo kazi yake ilikuwa kusurvey kazi za mpinga kristo na kuwaletea
nguvu za kipepo ili makanisa ya uongo yashamiri kama ilivyo sasa 98% ya
makanisa yote katika ulimwengu wote waliyaanza na mengine yameanzishwa na
kuzimu kabisa 85% hayajaanzishwa na YESU hata kama wanalitaja jina la YESU, ni
ya mpinga kristo hii asilimia 15% ni ya YESU katika hii 15% ya YESU 13%
wamejiunga tena na shetani wakamsaliti YESU ikabakia 2% ulimwengu wote, ndiyo
iliyobakia na YESU wa kweli.
Ni ajabu na inatisha nilipoangalia nchi mbali mbali
nikiwa na malaika Gabriel katika
makanisa nchi nyingi sana hazikuwa ni kanisa la MUNGU wa kweli hata moja na
katika nchi nyingine unakuta ni kimoja na bado limefifia hakuna nguvu za YESU, na
sehemu nyingi makanisa yanaonekana ni giza tupu. Nikamuona na Maria Magdalena
na yeye yule ambaye alikuwa na YESU alipokuwa hapa ulimwenguni. Yaani anampenda
YESU sana na anampenda MUNGU sana, ukisoma katika habari zake ndivyo alivyo
hata sasa katika bidii yake na MUNGU. Akaniambia, Hebron mwanangu ifanye kazi
ya MUNGU kama ilivyo sasa. Sasa tunafurahi mbinguni sababu ilifika mahali hata
Malaika walishindwa kuja katika makanisa sababu yamechafuka ila sasa malaika
wanapanda na kushuka katika kanisa lako na tunashirikiana katika ibada zote na
wewe, akanishika mkono na kunieleza hayo, na mengine ambayo ni yangu peke yake
kwa ajili ya utukufu wa MUNGU.
Meli hii ndiyo iliyosmabaza roho za kuzimu kwa ulimwengu
wote na aliyetumika ni mwanadamu aliyetekwa na shetani aliyeitwa Maxwell
aliendeshwa na nahodha father Christmas, na meli hiyo ilikuwa na rangi saba na
kila moja ilikuwa ina maana yake. Soma katika makala ya kadi ya Krismasi
nimezielezea, ni kusambaza uharibifu. Meli niliilipua nikiwa na Malaika Mikaeli
na ilipokuwa inakuja duniani walikuwa na wenyeji wao ambao mmoja ni nabii
maarufu kutoka Afrika Magharibi na wengine wawili ni marais wastaafu katika
moja ya bara la magharibi, na kupitia hao watu wote walipewa nguvu za kipepo,
pamoja na nguvu za vyama vya illuminati na freemason, ila sasa njia hizo
alinituma YESU nimezibomoa. Sasa ni wakati wa YESU WA NAZARETI kutawala
ulimwengu wote, na MUNGU anawataka watoto wake ikiwemo na wewe umrejee.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote. Siabudu sanamu
tena wala kupamba father Christmas, nisamehe sikujua au nilikua, uniandike jina
langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Amen.
Zaidi ingia katika website ya www.prophethebron.org usome yapo mengi
yatakufungua na hautadanganyika tena na shetani wala watumishi wa uongo na
wanyang’anyi wa mali za watoto wa MUNGU. KARIBU Arusha, Tanzania katika kanisa
la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, utaombewa na kufunguliwa na utamjua
YESU wa kweli. Ubarikiwe!
NABII HEBRON.