Kila mtu anampenda MUNGU na watu waliosikia habari za YESU
na kila anachokitaka kifuatwe ili uwe wakristo watu hupenda. Ila shetani
amewateka watu akishirikiana na mpinga kristo, sababu anajua ubatizo ni point
muhimu sana ya kufanya mtu awe kiungo kimoja na YESU wa kweli. Sasa ili avuruge
kusudi hili alichokifanya akabadili ufunuo huu kama ninavyoelezea. Kwanza biblia
inasema hivi Marko 16:16 “aaminiye na kubatizwa ataokoka na asiyeamini,
atahukumiwa.” Huu ni mfano halisi sasa tuje katika swali? Je mtoto mdogo na
mchanga je anaamini lolote au anajijua? Jibu haamini lolote. Je kama haamini je
atakuwa ameokoka? Jibu hajaokoka! Je hayo maji ya kumwagiwa kichwani ndiyo
kuzamishwa mwili wote? Jibu, siyo na kama siyo je hawa watoto wadogo wamebatizwa
au hawajabatizwa mpaka sasa jibu hawajabatizwa mpaka sasa, na kama
hawajabatizwa mpaka sasa basi siyo wakristo kabisa bali ni wakristo wa kujiita
kimajina wala YESU hawajui, na kama ulikuwa haujui sasa elewa na ubatizwe upya
sababu mpaka sasa wewe siyo mkristo na hata katika kanisa linalofanya haya
kinyume na biblia, hayo siyo makanisa ya YESU ni makanisa ya yesu wa uongo na
mpinga kristo yapo hapa ulimwenguni ili kuwazuia watu wasiwe mwili mmoja na
YESU ili wawe wakristo, haijalishi hata mtu atajiita yeye ni pastor, mtume,
mwinjilisti, mwalimu, nabii, kama hajabatizwa ubatizo wa maji mengi yeye siyo
mkristo.
Na pia wakati akibatiza ni lazima aokoke (huko ndipo
kuamini) na cha ajabu hata watu wazima wanabatizwa ubatizo wa kumwagiwa maji ya
kikombe, tena hata sala ya toba hakuna, haya yote ni njia ya shetani. Na kazi
zote za jinsi hii ya ubatizo nawaeleza MUNGU haujui, iwe ni maombi, injili,
hata kujenga haya makanisa, siyo ya YESU WA NAZARETI ni mapango ya mpinga
kristo, ni magereza ya kiroho. Hivyo kama ulibatizwa ubatizo huu na ukiwa mtoto
mdogo, nakueleza ukweli, wewe haujabatizwa na pia wewe siyo mkristo haijalishi
unajiita hivyo, fuata ukweli.
Amenituma YESU niwaeleze ukweli, karibu anarudi, na akija
kama haujaokoka na kubatizwa ubatizo wa maji mengi yanayotembea na kuishi
maisha matakatifu hautaenda mbinguni sababu wewe siyo mwili mmoja na yeye kiroho
na kimwili, hizo injili zote unazozifuata ni za uongo, point kubwa okoka,
uamini, ubatizwe kinyume na hapo utabakia kuwa mwanafunzi wa mpinga kristo
sababu moja ya kimwili ipo wazi haina ubishi. Je biblia inaruhusu ubatizo wa
watoto wadogo? Na je si mpaka uokoke umkiri kwanza YESU ndio tendo la ubatizo
lifuatwe, je umeokoka? Haiwezekani kupata ubatizo kama haujaokoka! tazama wengi
mmedanganywa haujaokoka halafu mnasema nyie ni wakristo, ipo neema yake. Tubu sasa
hivi; sema YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniokoe na uniandike jina
langu katika kitabu chako cha uzima wa milele niwe mwanafunzi wako na uniongoze
nikabatizwe kwa ubatizo wa kweli ili niwe ninaoushirika na wewe na nipate
kibali cha kuwa mkristo. Amen.
NABII HEBRON.